Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Mkuu GRAND MUFTI, sina uhakika kama umekuja JF kwa ajili ya kuwachafua wenzio lakini andiko lako limenigusa sana. Kuna baadhi ya watu wana uwezo lakini kwa matatizo ya Tanzania ni ngumu.
Andiko lako limenifanya nifikirie mara mbili mbili kama Mzee augustine Mrema angeliweza kuwa rais mzuri kwa level ya uelewa wake kuliko hawa tuliowajaribu. Yaani ni sawa na kumleta Jose Mourinho leo kufundisha Taifa Stars au Yanga kwa kudhania kuwa Mkwasa au Kibadeni hawawezi!
 
Umesema sahihi kijana wangu. Sasa hapa tushauriane. Janeth alisoma shule vizuri, amefanya kazi katika banking industry, na international Organizations mbali mbali na NGOs hapa nyumbani. Na bahati nzuri kwa ajili ya elimu yake na ufanisi wake kazini, vimempa uwezo wa kushika nafasi nzuri zenye malipo mazuri yanayokubalika kisheria kwa mujibu wa mikataba yake ya kazi. Ametumia mapato yake hayo katika kujenga maisha yake na kusomesha watoto wake. Kosa lake kijana wangu ni lipi?

Janeth amepata wapi mapato ya aibu hata tumhukumu kwamba ameiibia serikali au kafaidika na serikali kinyume cha utaratibu hadi kasomesha watoto? Mimi sidhani kama tukiipeleka vita hii kwa mtazamo wa kuwatenga waliofanikiwa kwamba ndio wamefanya sisi tusifanikiwe bila kuwa na scientific analysis tutakuwa tuko salama na sahihi.

Ninapinga sana wizi, ufisadi, forgery, favoritism, na unyanyasaji wa maskini unaofanywa na ccm na serikali yake. Katika hili wanufaika na watengenezaji wa mazingira haya kwangu wote wanakaa sehemu moja kwamba ni adui wa taifa na wanatakiwa kupigwa vita hadi watokomezwe. Na hawa ndio Ccm. Lakini si kila mwana ccm anaangukia hapo. Wapo wanaojifungulia sehemu nzuri kama ulivyosema kwa sababu ya uharamia huo ambao unawafanya wengine wajifungulie sehemu mbaya ambao ni watu wa chini bila kujali ni wana ccm ama la.

Janeth Mbene, ameanza lini harakati za siasa? Watot wake walisoma lini? Amehusikaje katika uharamia ninao usema hapo? Amenufaikaje na mfumo badhirifu katika kupata uwezo wa kusomesha watoto? Janeth kuna wakti nilikuwa naye Marekani na niliona alivyokuwa makini kwenye suala la kusave na matumizi. Alinunua kile alichokihitaji tu lakini si alichokitaka. Muda wote alikuwa akiviongelea vijukuu vyangu vi modesta hivi vikiwa shule za msingi.

Niliona hakuwa tofauti na Marehemu Baba yake kwa ukomavu wa akili. Alikuwa na nidhamu sana ya fedha na maongezi yake mara nyingi akiwa na wenyeji wake, alipenda kudadisi masuala mbali mbali ya maendeleo. Kusema kwamba amesomesha watoto kwa kuhujumu wengine, hilo siliamini labda kama una taarifa zake ambazo mimi sizijui nitashukuru ukiniambia.

Ninaomba unielewe. Bidii ya kutafuta elimu na maarifa, kufanya kazi kwa bidii na maarifa, mipango safi na matumizi mazuri ya raslimali, kuishi kwa malengo na kuomba Mungu, vinaweza kuleta mafanikio hata bila kuiba. Siamini kwamba kila aliyefanikiwa ni adui wa Watanzania kwa sababu sikila mafanikio yamehujumu haki za wengine.

Tusije kupoteza vita kwa kuwapiga waliofanikiwa kisha tukawaacha wanaotuibia na kutuharibia maisha hata kama hawafanikiwi kwa kuwa hawana akili za kuona mbali.

Kama una taarifa za uhusika wa Janeth kwenye wizi, hujuma au unufaika wa mfumo fisadi kwamba ndio umemuwezesha kufanikiwa na kusomesha watoto wake, ulete hapa tutajadiliana kwa uhuru tu. Tunachotakiwa ni kuhakikisha mifumo yote inayotumiwa na ccm kutuharibia maisha tunaifunga na kuwafundisha hawa wezi adabu.

Hapa narudi tena. Kama Janeth naye amesomesha watoto kwa kuhujumu taifa, bila shaka atakuwa miongoni mwa maadui zetu. Lakini kwa kuwa ninamfahamu, sikumbuki kama amewahi kuwa na access na mfumo wowote wa kuibia serikali au kujipatia mali kwa njia haramu ambazo si haki yake na hivyo kusomesha watoto wake kwa kunyima haki wengine. Na ndiyo maana ninasimama kusema hili na hata kama kuna mwingine atakuwa accused wrongly kama ninafahamu habari zake sahihi, nitasimama kuzisema ili vita vyetu na ufisadi visiathiri wasiohusika. Ni watanzania wenzetu hata kama ni ccm maadamu ni waadilifu. Hawa tuungane nao kupigana na mfumo haramu wa chama chao.

Ni vizuri tukawatuhumu watu kwa makosa halisi na si kujumulisha tu kila anayefnikiwa ni mwizi. Si kweli.

Pole kwa kushikwa pabaya mzee. . . . .Ila huwezi mshauri mtu aichukie CCM halafu awapende waliofaidika na mfumo huo kama unataka kuita spade ni spade basi kubali ichukiwe CCM na yatokanayo na mfumo mzima, tatizo nchii hii hata baadhi ya wazee kama wewe sasa hivi mnashindwa kuwa wakweli na wawazi na ndio maana tunakwama. . . . . . . . Unapoamua kuwa mkweli kuwa mkweli hata kama baadhi ya watu wako wataumia na ukweli husika!!!!!

Class based hatred huwezi iongea na kuiondoa kama unavyoiweka wewe. . . Mtu kazalia njiani kwa kukosa huduma labda na mtoto kapoteza uje umwambie muache X salama na umoende wakati huyo X hajui hata usafiri wa jumuia ukoje (labda) na huyi muathirika anajua wazi kuwa mfumo uliosababisha yeye kujifungulia njiani ndio huo uliosababisha X kujifungulia sehemu nzuri na kisomesha watoto. . . . . .,

kama kweli u mtu mzima basi ongea dhati ya moyo wako kwa ku adress source ya tatizo kuliko kuwa buffer na kuongea suoerficially. . . . . Nchi yetu wote watu wasipoona faida ya umoja basi chuki kama hizi za kwenye uzi huu huwezi ziondoa kwa kuhadithia historia ya mtu mmoja mmoja
 
mtoa mada naona ana stress zake, na labda hasa ana WIVU juu ya watoto wa mahiga hasa hawa wawili ambao wanaonekana sana kwenye media. Haiwezekani mgombea awe baba yao yeye alete video za watoto, inahuu?
Haya some corrections:
1. Hivi mtu anaitwaje 'posh boy' wakati historia yake inaonyesha alizaliwa katika umaskini uliokithiri kiasi cha kushindwa ku-afford michango ya mablanketi sijui na makorokoro gani huko enzi za mwalimu na akasomeshwa kwa michango ya kanisa? Huyu ni wale watu typical ambao walikuwa wanataniwa 'wanasomeshwa na kijiji'! Leo hii mtoa mada anasema huyu naye ni silver spooner? Hizi ni chuki tu.

2. Mke wake ni huyu hapa kama alivyokuja naye kuchukua form na sio Janet Mbene.
IMG_6943.JPG

3. Wabongo sijui kwa nini wanachukia watu wenye mafanikio bila sababu. Utadhani Mahiga huko UN alikuwa anafanya dili zake na sio za serikali. ARRRRRGh!
Huyu Mahiga ana approach 70 years lakini naona hana mvi daah!!! au mambo ya super black.
 
1. Mzee Tabby tatizo ni mfumo ndio ulioleta hiyo "chuki" unayoiona. . . . .mfumo uliaminisha watu kuwa na mali nyingi ni uhujumu ni nani alikuja kuondoa hiyo dhana kwa vitendo kama ilivyoingizwa??!!

2. Kumbuka hao watoto hawatajwi kwa adress ya mama humu ila mzee wao. . . .Lakini wewe unageuza mada kuwa ya mama wa watoto. . . .. The linking thread ni aliyetangaza nia hiyo ndio focus it be right or wrong. . . I see wewe ndio unamuongelea sana huyu mama sijui kwa nini. . . .Na unaposisistiza kawalea hivi na vile another person will ask mchango wa baba yao katika hayo malezi. . . .Will you respond to that??!! Muache huyo mama mtoto wa rafiki yako please. . . . .

3. Unapokuwa na nchi iliyogawanyika kimatabaka struggle huwezi iondoa ja struggle inaenda mpaka kuchafuana, kuungana, ili tu anayehitaji apate lake. . . . Sasa soft targets haziwezi kuachwa free. . .Lazima ziguswe then hisotria itahukumu. . . Hili hatuwezi zuia

4. Huyu mzee inawezekana kabisa anaweza kuwa good candidate lakini ji mfumo huo huo ninaousemea haujaweka mazingira ya watu wenye uwezo kuwa independent mfumo uko in such a way ili uonekane lazima
uwe na mahusiano na watu au makundi fulani ukiruhusu hii basi lazima uhasama uwepo "in those struggling
classes". . . . . Katiba ndio suluhisho la hizi fujo cha ajabu hawa wagombea hawazungumzii hiyo habari na wakati iko hot wote walijificha wasioneshe misimamo yao. . . . . .. Hii tafsiri yake nini??!!!

Uwezo anao ila system hii iliyoko. . . . . .. . anyway the race should continue
 
Last edited by a moderator:
hata mumchafui vipi mahiga hapati hata harufu ya ufisadi na rais hajaguliwi na wadau wa jf anapitishwa na ccm

Sawa lakini nakuhakikishia hatatoboza hata kwenye tano bora (take my words)..... CCM ni zaidi ya uijuavyo
 
All I know hatufai, hachakuliki hata kuwa mjumbe wa nyumba 10 let alone kuwa rais wa watu milioni 50 na hatumtaki

nashauri aende akacheze GOLF na walevi wenzake pale Kawe.

Talk for yourself!!

Hivi kweli unafikiri Presidential material anasifa za kuwa mjumbe au balozi wa nyumba 10!! Kama ndiyo hivyo unavyofikiria basi hujui ni Rais wa namna gani Tanzania inamuhitaji. Hicho unachokisema ni kama kusema Professor hana sifa za kufundisha Kindergarten au First Graders, which is True!!

Tanzania kwa sasa inahitaji mtu ambaye na uwezo na exposure ya kutosha. Hii biashara ya Mtu kasoma Local Universities, kafanya kazi locally throughout his live then President, same mentality!!
 
sidhani kama wananchi wengi wanamfahamu huyu mtu let alone kuwa na fikra kama anaweza kuwa kiongozi wao, anatakiwa kufanya investment bado ya popularity aweze kushinda akili za watu kabla ya kuwa mshindani wa kweli, kama hii ni mbinu ya kufahamika sawa ila sidhani kama ni mshindani wa kweli na hao waliopo.
 
mtabaki kutumiwa nao kama dekio,kusafishia watu ulaji
 
Mkuu, nimemtetea Mama kutokana na wachangia mada wa mwanzo kabisa kumhusisha pamoja na watoto kwenye muamala wa Dr.Mahiga, isivyo halali kwa kuwa ninamfahamu personally tangu akiwa binti mdogo sana. Baba yake Janeth na mimi tulikuwa tunakaribiana ingawa mimi nilikuwa mkubwa kwake.

Ukiniuliza mchango wa baba kwa watoto, ninaweza kusema zaidi ya kutengeneza hao watoto. Lakini sihitaji kuyaongelea hapa kwa kuwa ni mambo ya watu binafsi na siyo public agenda.

Mkuu, mifumo yote inatengenezwa na kuwa propagated na watu na marekebisho ya mifumo pia hufanywa na watu kwa kutoa relevant facts zitakazotoa concept za wazi zenye maana na mwelekeo sahihi.

Kama watu wengi walikaririshwa kwamba mtu akiwa na mali ni mwizi na kwamba utanzania sahihi ni umaskini na ujinga, ni ujinga uliokithiri ambao unatakiwa kuwa replaced kama idea kwamba dunia ni kama meza inakingo badala yake ikawekwa bayana kwamba dunia ni tufe, lenye rough surface area.

Sasa tulitegemea kwamba Tanzania ingekuwa na wasomi wenye uelewa sahihi wengi lakin bahati mbaya wajinga wasiojielewa ndio wengi.

Lakini si jambo la kuendekeza, kuwaacha watu waamini kwamba ni umasikini ndio utanzania bora. Kunahitajika tafsiri sahihi kati ya mafanikio halali na mafanikio haramu, lakini pia tafsiri ya maendeleo kwa uhusiano na mafanikio.

Na kama lengo la nchi ni kuelendelea, basi tuhamasishe maendeleo halali huku tukiharibu kila nyanja inayotoa nafasi ya maendeleo haram. Na hili litafanikiwa ikiwa litaanzia kwenye ubongo wa watu ili watengeneze katiba safi na mipango bora yenye kulinda utashi na malengo yataifa.

Siamini katiba bila ufahamu kwa watu italeta transformation. Mentality na knowledge sahihi kwa watu ili watengeneze na kusimamia katiba safi. Tumeona juzi zoezi la katiba lilivyogeuka kuwa kama ngoma za wachawi kwa sababu ya kuwa na mijitu mijinga mijinga isyokuwa na ufahamu wala malengo.

Ki msingi nina ungana na wewe lakini tunahitaji transformation vichwani mwa watu ili watengeneze katiba na mifumo sahihi itakayolinda maslahi mapana ya Tanzania na watu wake. Bila kuwa na brains sahihi, tutaishia kutengenezewa midundiko kwenye katiba ya taifa kwa sababu watengenezaji watakuwa wale wale majuha wenye wrong attitudes, poor mindsets and Ill educational backgrounds.

LAKINI HAYA TU YATAFANIKIWA MARA MOJA CCM IKIONDOKA MADARAKANI MAANA NDYO INAYOENDESHA UJINGA UJINGA HAPA TANZANIA.

1. Mzee Tabby tatizo ni mfumo ndio ulioleta hiyo "chuki" unayoiona. . . . .mfumo uliaminisha watu kuwa na mali nyingi ni uhujumu ni nani alikuja kuondoa hiyo dhana kwa vitendo kama ilivyoingizwa??!!

2. Kumbuka hao watoto hawatajwi kwa adress ya mama humu ila mzee wao. . . .Lakini wewe unageuza mada kuwa ya mama wa watoto. . . .. The linking thread ni aliyetangaza nia hiyo ndio focus it be right or wrong. . . I see wewe ndio unamuongelea sana huyu mama sijui kwa nini. . . .Na unaposisistiza kawalea hivi na vile another person will ask mchango wa baba yao katika hayo malezi. . . .Will you respond to that??!! Muache huyo mama mtoto wa rafiki yako please. . . . .

3. Unapokuwa na nchi iliyogawanyika kimatabaka struggle huwezi iondoa ja struggle inaenda mpaka kuchafuana, kuungana, ili tu anayehitaji apate lake. . . . Sasa soft targets haziwezi kuachwa free. . .Lazima ziguswe then hisotria itahukumu. . . Hili hatuwezi zuia

4. Huyu mzee inawezekana kabisa anaweza kuwa good candidate lakini ji mfumo huo huo ninaousemea haujaweka mazingira ya watu wenye uwezo kuwa independent mfumo uko in such a way ili uonekane lazima
uwe na mahusiano na watu au makundi fulani ukiruhusu hii basi lazima uhasama uwepo "in those struggling
classes". . . . . Katiba ndio suluhisho la hizi fujo cha ajabu hawa wagombea hawazungumzii hiyo habari na wakati iko hot wote walijificha wasioneshe misimamo yao. . . . . .. Hii tafsiri yake nini??!!!

Uwezo anao ila system hii iliyoko. . . . . .. . anyway the race should continue
 
Mkuu, nimemtetea Mama kutokana na wachangia mada wa mwanzo kabisa kumhusisha pamoja na watoto kwenye muamala wa Dr.Mahiga, isivyo halali kwa kuwa ninamfahamu personally tangu akiwa binti mdogo sana. Baba yake Janeth na mimi tulikuwa tunakaribiana ingawa mimi nilikuwa mkubwa kwake.

Mkuu, mifumo yote inatengenezwa na kuwa propagated na watu na marekebisho ya mifumo pia hufanywa na watu kwa kutoa relevant facts zitakazotoa concept za wazi zenye maana na mwelekeo sahihi.

Kama watu wengi walikaririshwa kwamba mtu akiwa na mali ni mwizi na kwamba utanzania sahihi ni umaskini na ujinga, ni ujinga uliokithiri ambao unatakiwa kuwa replaced kama idea kwamba dunia ni kama meza inakingo badala yake ikawekwa bayana kwamba dunia ni tufe, lenye rough surface area.

Sasa tulitegemea kwamba Tanzania ingekuwa na wasomi wenye uelewa sahihi wengi lakin bahati mbaya wajinga wasiojielewa ndio wengi.

Lakini si jambo la kuendekeza, kuwaacha watu waamini kwamba ni umasikini ndio utanzania bora. Kunahitajika tafsiri sahihi kati ya mafanikio halali na mafanikio haramu, lakini pia tafsiri ya maendeleo kwa uhusiano na mafanikio.

Na kama lengo la nchi ni kuelendelea, basi tuhamasishe maendeleo halali huku tukiharibu kila nyanja inayotoa nafasi ya maendeleo haram. Na hili litafanikiwa ikiwa litaanzia kwenye ubongo wa watu ili watengeneze katiba safi na mipango bora yenye kulinda utashi na malengo yataifa.

Siamini katiba bila ufahamu kwa watu italeta transformation. Mentality na knowledge sahihi kwa watu ili watengeneze na kusimamia katiba safi. Tumeona juzi zoezi la katiba lilivyogeuka kuwa kama ngoma za wachawi kwa sababu ya kuwa na mijitu mijinga mijinga isyokuwa na ufahamu wala malengo.

Ki msingi nina ungana na wewe lakini tunahitaji transformation vichwani mwa watu ili watengeneze katiba na mifumo sahihi itakayolinda maslahi mapana ya Tanzania na watu wake. Bila kuwa na brains sahihi, tutaishia kutengenezewa midundiko kwenye katiba ya taifa kwa sababu watengenezaji watakuwa wale wale majuha wenye wrong attitudes, poor mindsets and Ill educational backgrounds.

LAKINI HAYA TU YATAFANIKIWA MARA MOJA CCM IKIONDOKA MADARAKANI MAANA NDYO INAYOENDESHA UJINGA UJINGA HAPA TANZANIA.
mfumo uliopo tanzania hauruhusu mafanikio halali bila wizi, ndio maana hatuamini kwamba kuna waliofanikiwa bila kuiba....
 
Hivi huyu angekuwa Muislam ingekuwaje?

Halafu kwa nini kuna watu hawataki kutuambia Mahusiano yake na waziri Janeth Mbene?

Nahisi kama vile wa Ghala wanafanya jitihada za ziada kumsafisha mtu wao lakini hasafishiki. Iweje balozi na maofisa wa balozi zetu nchini Burundi na Comoros na Malaysia na kwingineko wakose mishahara miezi 7 huyu awe anatumia dola elf10 kununua suti moja?
 
mfumo uliopo tanzania hauruhusu mafanikio halali bila wizi, ndio maana hatuamini kwamba kuna waliofanikiwa bila kuiba....

jamani mbona mbowe na ndesamburo wamefanikiwa hapahapa bongo! Watoto wa mbowe wanasoma afrika ya kusini wala hamna shida, mkamwana wa ndesamburo ni mbunge machachari pamoja na dada yake lissu, big up sana.
 
Hivi huyu angekuwa Muislam ingekuwaje?

Halafu kwa nini kuna watu hawataki kutuambia Mahusiano yake na waziri Janeth Mbene?

Nahisi kama vile wa Ghala wanafanya jitihada za ziada kumsafisha mtu wao lakini hasafishiki. Iweje balozi na maofisa wa balozi zetu nchini Burundi na Comoros na Malaysia na kwingineko wakose mishahara miezi 7 huyu awe anatumia dola elf10 kununua suti moja?

mkuu haya majungu yanakusaidia nini? Mtoto wa kishua wacha hizo.
 
Nimeeleza vizuri sana kwa ufupi profile ya Janeth mama yao.

Unaelewa kwamba kial mtu ana vipaumbele vyake katika maisha? Kwa kazi za Janeth, zilimpa kipato kizuri na alitumia kusomesha watoto. Pengine mwingine mwenye kipato hicho alitumia kwenye ulevi na nyumba ndogo. Mwingine alinunua magari ya kifahari mengi mengi yakuonyeshea mitaani. Mwingine atitumia kwa likizo zake kupumzikia Ulaya n.k.

Na ninategemea kama hujaelewa hata nilichokisema kuhusu huyu binti ni kwa sababu pengine muda wako wa kuelewa bado. Ila usidhani matokeo ya matumizi ya fedha unazopata wewe yatakuwa sawa na matokeo ya matumizi ya mtu mwingine asiyewaza kama wewe. Sasa mmoja hapo akifanikiwa, kwa ufahamumdogo na wivu, asiyefanikiwa aanze kusema alilyefanikiwa ni mwizi kwa kuw ayeye hajafanikiwa. Ridiculous!.

Au naomba ujibu swali hili kichwani mwako. Hivi watu wote Tanzania wanaelimu sawa na uwezo sawa wa kufanya kazi ama kuzalisha? Na kama hawako sawa, hiyo tofauti ni uvunjaji wa katiba au sheria ya nchi?

Je watu wote wenye elimu sawa, au wanaofanya kazi sehemu moja wanapata malipo sawa? Yanapotofautiana kunakuwa na sheria gani ya nchi imevunjwa?

Watu wanaopata fedha za kufanana kwa kiwango wana matumizi na vipaumbele sawa? Wakitofautiana wanakuwa wamevunja sheria gani ya nchi?

Matokeo ya matumizi ya fedha kwa wanaopata viwango sawa vya mishahara yanalingana? Yakitofautiana inakuwa imevunjwa sheria gani ya nchi?

Kwa nini uelewe kwamba kila anayefanikiwa ni mwizi wakati unaona kabisa njia za kila mtu za maisha ni tofauti na za mwingine?

Wewe hujasoma kama Janeth, leo unataka mlingane. Wapi na wapi kijana wangu?

Wewe umeridhika na kazi unayoifanya, nayo unaifanya kwa majungu, manung'uniko na kutegea wakati Janeth amekuwa akitafuta kazi anazoona zitakidhi mahitaji yake ya kufanya kazi na zina mlipa. Sasa yeye kapata zaidi yako unamwita mwizi. Ni nini hicho kijana wangu?

Mwenziyo Janeth, anatazama maisha kwa mtazamo mpana wa kusomesha watoto tena kwa ufahamu na malengo. Wewe unatumia ffedha zako kubadilisha magari na starehe. Sasa Janeth kasomesha watoto elimu safi, unasema kaiba. Si kweli kijana wangu.

Janeth kasoma shule nzuri na kazi nzuri na mshahara wake halai mzuri na marupurupu mengine halali mazuri, kaseomesha watoto vizuri. Wewe hujasoma kama yeye hata mkiitwa kwenye interview na yeye wewe atakushinda ka sababu huna uwezo kama yeye. Kwa kuwa anakuzidi, anapata kpato kizuri kinamletea matokeo mazuri maishani lakni wewe unataka matokeo ya maisha yake yawe kama ya kwako na akikuzidi kaiba!. Dunia ya wapi hiyo kijana?

Hata Mbinguni kuna Ujira kila mtu na kazi yake.

HAPA TUELEWANE JAMBO MOJA. TUNAPOSEMA NI ADUI, TUN AMAANA AMETUMIA FURSA AMA MAPATO YA AIBU KUSABABISHA HASRA KWA WATANZANIA WANYONGE NA YEYE KUJINUFAISHA, LAKINI HATUNA VITA NA WANAOFANIKIWA KWA MISINGI YA HAKI.

KAMA VITA HIVI MTAVIGEUZA VIWE NI VITA VYA MASKINI KINYUME CHA WALIFANIKIWA, MTABAKI PEKE YENU KWA SABABU WENYE AKILI TIMAMU HATUTASHIRIKI. ILA TUTAPIGANA BEGA KWA BEGA KINYUME NA ANAYETHIBITIKA KUJINUFAISHA KWA GHARAMA YA JASHO LETU. HAO TUTAKULA NAO SAHANI MOJA.

LAKINI PIA VITA HII HAITAISHIA HAPO. TUTAHITAJI KUPIGANA NAN WAZEMBE WASIOTUMIA FURSA NA RASLIMALI VIZURI KWA MAENDELEO YAO NA TAIFA. NI LAZIMA KILA MTU AFANYE KAZI NA AMBAYO KWA KUWA TUTAKUWA TUMEONDOA UFISADI, LAZIMA ITAMLIPA KWA VIGEZO NA SIFA ZA UTENDAJI WAKE KWA NAFASI YAKE.

MAWAZO KWAMBA TUKIPIGANA NA UFISADI BASI MAISH AYATAKUWA MAZURI BILA JUHUDI HAKUNA. TUNAHITAJI KUWA NA MFUMO SAHIHI LAKIN MFUMO BILA KUUTENDEA KAZI HAULETI MAFANIKIO. NI JAMBO LA KILA MTU KUWAJIBIKA MAHALA ALIPO.

mfumo uliopo tanzania hauruhusu mafanikio halali bila wizi, ndio maana hatuamini kwamba kuna waliofanikiwa bila kuiba....
 
hawa ndio wanatudhulumu sisi watoto wa maskini

tukisema tunaambiwa ohhhh bas nyie kila wakati mwalalama tuuuuu

suti dola elf 10 sasa huyu atakuwa kweli hana akaunti uswisi kweli?
 
Hivi huyu angekuwa Muislam ingekuwaje?

Halafu kwa nini kuna watu hawataki kutuambia Mahusiano yake na waziri Janeth Mbene?

Nahisi kama vile wa Ghala wanafanya jitihada za ziada kumsafisha mtu wao lakini hasafishiki. Iweje balozi na maofisa wa balozi zetu nchini Burundi na Comoros na Malaysia na kwingineko wakose mishahara miezi 7 huyu awe anatumia dola elf10 kununua suti moja?

Umeambiwa tu katumia dola elfu kumi kununua suti moja ukaumeza uongo huo huo bila hata kuuliza huyu Mahiga ana itikadi gani, historia gani, kwao kukoje, ndugu zake wakoje, ana vitegauchumi gani etc.

Usifanye maamuzi makubwa kama kum dismiss mtu kwahabariambazo zimetungwa bila mpangilio.
 
Mkuu unataka jamaa atoke NY aje kua Rais huku mavumbini??? Unaamini hilo linawezekana? je kuna muingiliano wa maisha ya ny na namtumbo??? Umri umemtupa tunashukuru kwa uwakilishi wake mzuri huko alikokua, labda ainvest sasa kwa watoto wake lakini sio yeye
 
Back
Top Bottom