Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Bora angeendelea kuandika articles zake magazetini lakini sio kutaka kutuongopea eti yeye yuko kama sisi

Kivipi? Mtu anavaa suti ya dola elfu 7 atajua kweli shida zetu huyu?

Nyie mamburula kweli!Nani kama ninyi miongoni mwa watia nia wote?Mnalingana na Lowasa na team yake Rostam,Mengi,Sabodo,Karamagi,Mgenja,Tıbaijuka??Si afadhali hata Mahiga?Wanaojua shda zenu wamewasaidia nini?Hata hvyo mimi namuunga mkono Prof.Muhongo.
 
Naona sasa mmeanza kumchafua jamaa, baada ya kuona huenda ndiye mtu aliyekuwa anasubiriwa au bado kuna mwingine? Huenda sio yeye, ngoja tusubiri kwanza. Tuliambiwa huyo mtu atakuwa wa mwisho kuchukua form. Huenda akawa ni Yohana Mbatizaji anatengeneza tu njia , chonde chonde acheni kumchafua. Hii ni TeamLowassa au TeamMembe? Ila TeamLowassa ndio wachafua wengine ili FISADI achukue nchi
Kuna watu nawasubiria kwa hamu Sana 2016 wkaianza kulalamikia serikali,Mara baada ya kuchagua hovyo.wataniona mbaya humu ndani.

2005 baada ya kushibishwa na hongo za wana mtandao walikuwa bize kumtukana Dr.Salim,waliposhinda wakamuangukia awe beacon YAO ya uhusiano na china.ambayo in fact ndio ime bank roll serikali yetu kwa miaka 10 iliyopita.kwa sampuli za mleta madam MTU kama mahiga hafai kuwa raising wake,he deserves the type kama lowassa hivi au wasira.waongo waongo wadi na vision wala weledi sahihi.wakichaguliwa waliokuwepo wanalalamika ndio haohao miaka nenda rudi,wakiletewa walio nje ya serikali wenye uwezo sahihi wanaanza vioja.

Sasa MTU kaishi nje miaka 30 unataka Watoto wake wasome wapi?wewe unayeishi dar watoto wako wanasoma kijijini kwenu ulikozaliwa?
Hawa Watoto ndio wataongoza nchi?

Kazi tunayo watanzania.toendelee kuchagua hovyo halafu tuje kulalamika hovyo.
 
Mahinga ndo nani?hebu tugusieni na sisi tujuwe kuwa kazaliwa wapi?kasomea wapi?kafanya kazi wapi nachojuwa ni kuwa aliwahi kuwa balozi huko UN
Dk Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945 huko Tosamanganga, Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa (atatimiza miaka 70 ifikapo Agosti mwaka huu). Amesoma elimu ya msingi katika shule za Serikali enzi ya mkoloni na alihitimu darasa la VIII muda mfupi baada ya uhuru. Safari ya elimu ya Dk Mahiga ilikuwa ya umaskini uliopitiliza, alishindwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa kutokuwa na fedha za kulipia mashuka na mablanketi hadi aliposaidiwa na msamaria mwema kutoka Shirika la Kennedy wakati huo.

Aliendelea na masomo ya sekondari hapahapa nchini na mwaka 1968, alijiunga katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye elimu mwaka 1971.
Mwaka huohuo, Dk Mahiga alipata ufadhili na kuendelea na masomo ya juu nchini Canada katika Chuo Kikuu cha Toronto ambako alihitimu Shahada ya Uzamili. Aliendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika chuo hichohicho akijikita katika Uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1975.
Mwaka huohuo 1975 (akiwa na miaka 30), Dk Mahiga alirejea nchini akiwa daktari wa falsafa kitaaluma na alipangiwa kazi ya kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mhadhiri katika Idara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kikanda. Alifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977 alipohamishiwa katika Ofisi ya Rais kuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo na alidumu hapo akifanya kazi pamoja na Mwalimu Julius Nyerere hadi mwaka 1980.

Kati ya mwaka 1980 hadi 1983, Dk Mahiga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Nafasi hii aliitumikia kwa weledi mkubwa katika historia ya watu waliowahi kuitumikia, aliweza kuifahamu nchi vizuri na mifumo yake kwa mtizamo wa ndani na nje.
Mwaka 1989 hadi 1992, aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Kimataifa akifanyia kazi Geneva – Uswisi na mwaka 1992 hadi 1994, Balozi Mahiga aliteuliwa kuwa Kiongozi (Mwakilishi) wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) mjini Monrovia, Liberia na huu ndiyo wakati aliponusurika kuuawa na Majeshi ya Rais Charles Taylor, kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kuna wakati akiwa katikati ya operesheni ya wakimbizi hapo Monrovia, Serikali ya Tanzania ilimteua kuwa Balozi na kumuongezea jukumu jingine zito.

Mwaka 1994–1998, Balozi Mahiga alihudumu akiwa Mratibu na Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni ya Dharura ya Ukanda wa Maziwa Makuu akifanyia kazi hiyo kutokea Geneva–Uswisi na kati ya mwaka 1998 – 2002 aliteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu (Mwakilishi) wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) huko mjini Delhi India kabla ya kuteuliwa tena kuwa mwakilishi wa shirika hilo katika nchi za Italia, Malta na Jamhuri ya San Marino kati ya mwaka 2002 – 2003.

Balozi Mahiga amepata pia kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2010 na alishiriki kikamilifu katika mipango ya kimataifa pamoja na kusimamia mazungumzo ya kuanzishwa kwa Kamisheni ya Ujenzi wa Amani (mwaka 2005). Pia kushiriki kwenye masuala ya maingiliano ya serikali mbalimbali na makundi yanayofanya kazi zisizo rasmi, maendeleo, amani, usalama na ujenzi wa ushirikiano wa uhakika kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Balozi Mahiga alirejesha heshima ya Tanzania hadi kuwa mojawapo ya nchi zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi yetu ilipopata heshima hiyo, yeye aliteuliwa kuwa mkuu wa ujumbe wa Tanzania katika Baraza hilo, hii ilikuwa ni mwaka 2005.
Dk Mahiga ameoa na ana watoto watatu.
 
Mleta mada huna maana alafu unaonekana kuwa mshamba.Matatizo ya Watanzania wanayajua Marekani iweje Mahiga asijue.Yawezekana Mahiga hana uwezo wa kupendekezwa lakn hoja yako inanipa picha yako kuwa utakuwa mshamba hv na mwenye uelewe mdogo sana wa mambo lakn umri wako upo juu ya 40.Dunia ya sasa unaweza sema diplomat gani asijue shda zenu duniani humu?
 
Wanaukumbi.

Kwa wale wasiyomjua Mahinga.

ALIYEKUWA Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk. -Augustine Mahiga ametangaza nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es salaam leo.Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mahiga amesema maadili yamemomonyoka na kufanya kuwepo kwa rushwa na ufisadi.Mahiga amesema ubadhirifu na ufisadi katika taifa kunahitajika kuwepo kwa mwelekeo katika kuweza kupambana na vitu hivyo ili maendeleo yapatikane kwa wananchi.

"Nikipata nafasi hii nitatumikia watu katika kuujenga uchumi imara kwa kila mwananchi kutokana na kuwepo kwa dira na kuondoa matabaka yanayotokana na ubadhirifu wa mali za umma"amesema Mahiga.Amesema CCM itoe fursa, isifikie utawala wa watu wenye pesa hiyo sio dhamira ya CCM, na watu wanaotoa msaada uwe na kikomo chake.Mahiga amesema katika kuweza kufikia uchumi wa kati kunatakiwa kupambana na rushwa na ufisadi, bila kufanya hivyo uchumi huo hautafikiwa.
 
Mkuu ondoa hizi Videos kabla ya Wema Sepetu hajamtafuta huyo dogo (Andrew Mahiga-25).

Ki uhalisia haishi kitanzania!!
Teh teh teh hizo videos za 2011 jamaa mkubwa saizi kasoma Marekani.

Andrew Mahiga (B.A. International Studies) serves as the Managing Director of-Maanisha! Limited.Andrew's involvement in media began as a hobby while in university in New York City. He interned at a Men's Lifestyle Magazine (Complex Magazine) where he wrote online articles for the fashion department and assisted in the marketing and advertising departments.

He also conducted online marketing for a urban-wear clothing store has been involved with event planning/promoting and fundraising for both for-profit and non-profit organisations both in the United States and Tanzania. After his studies Andrew worked for a Media Monitoring company in Tanzania and appeared on a few progrms on MTV Base, Capital TV, Choice FM, Clouds FM and EATV."
 
Ila kuna kuna humu jamiiforum kuna mambo, watu wanahitaji kuwa na weledi Sana katika kuchambua threads na hoja za watu, coz ukiwa bendera unapotea.

Humu kuna #Team kibao....kila mmoja anakuja la kwake with 2 things kumjenga mtangaza nia wake na kuwabomoa wengine.

Mengi yatatokea kwa kuwa huku tuna
1. Team Lowassa
2. team membe
3. Team Wasira
4. Team mahiga
5. Team mwigulu
6. Team makamba
7. Team mwandosya
8. Team magufuli
9. Team sitta
10 .Team makongoro
11. Team Nyalandu
12. Mizengo pinda
13. Ukawa- Hapa kuna
# mbatia
# Dr silaa. mbatia na makaidi na wengine.
14. Team Gharib Bilal
15 . Team mkulima wa kasulu.


Team kibaooo km nimesahau weka hapa tuzijue,

My take; Tutegemee mengi ila tuwe wajanja wa kuyachambua...
 
janeth.jpg


mkewe (Janeth Mbene).
Mkuu mkewe ni mama Elizabeth Mahiga kama sijakosea, au kuna ufafanuzi juu ya huyu mhe. uliyemuweka hapa kwenye picha???
 
Back
Top Bottom