Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 40,017
- 51,157
how do you explain, mtu mwenye salary ya laki tisa pale TRA kumiliki vogue na international schools??Nimeeleza vizuri sana kwa ufupi profile ya Janeth mama yao.
Unaelewa kwamba kial mtu ana vipaumbele vyake katika maisha? Kwa kazi za Janeth, zilimpa kipato kizuri na alitumia kusomesha watoto. Pengine mwingine mwenye kipato hicho alitumia kwenye ulevi na nyumba ndogo. Mwingine alinunua magari ya kifahari mengi mengi yakuonyeshea mitaani. Mwingine atitumia kwa likizo zake kupumzikia Ulaya n.k.
Na ninategemea kama hujaelewa hata nilichokisema kuhusu huyu binti ni kwa sababu pengine muda wako wa kuelewa bado. Ila usidhani matokeo ya matumizi ya fedha unazopata wewe yatakuwa sawa na matokeo ya matumizi ya mtu mwingine asiyewaza kama wewe. Sasa mmoja hapo akifanikiwa, kwa ufahamumdogo na wivu, asiyefanikiwa aanze kusema alilyefanikiwa ni mwizi kwa kuw ayeye hajafanikiwa. Ridiculous!.
Au naomba ujibu swali hili kichwani mwako. Hivi watu wote Tanzania wanaelimu sawa na uwezo sawa wa kufanya kazi ama kuzalisha? Na kama hawako sawa, hiyo tofauti ni uvunjaji wa katiba au sheria ya nchi?
Je watu wote wenye elimu sawa, au wanaofanya kazi sehemu moja wanapata malipo sawa? Yanapotofautiana kunakuwa na sheria gani ya nchi imevunjwa?
Watu wanaopata fedha za kufanana kwa kiwango wana matumizi na vipaumbele sawa? Wakitofautiana wanakuwa wamevunja sheria gani ya nchi?
Matokeo ya matumizi ya fedha kwa wanaopata viwango sawa vya mishahara yanalingana? Yakitofautiana inakuwa imevunjwa sheria gani ya nchi?
Kwa nini uelewe kwamba kila anayefanikiwa ni mwizi wakati unaona kabisa njia za kila mtu za maisha ni tofauti na za mwingine?
Wewe hujasoma kama Janeth, leo unataka mlingane. Wapi na wapi kijana wangu?
Wewe umeridhika na kazi unayoifanya, nayo unaifanya kwa majungu, manung'uniko na kutegea wakati Janeth amekuwa akitafuta kazi anazoona zitakidhi mahitaji yake ya kufanya kazi na zina mlipa. Sasa yeye kapata zaidi yako unamwita mwizi. Ni nini hicho kijana wangu?
Mwenziyo Janeth, anatazama maisha kwa mtazamo mpana wa kusomesha watoto tena kwa ufahamu na malengo. Wewe unatumia ffedha zako kubadilisha magari na starehe. Sasa Janeth kasomesha watoto elimu safi, unasema kaiba. Si kweli kijana wangu.
Janeth kasoma shule nzuri na kazi nzuri na mshahara wake halai mzuri na marupurupu mengine halali mazuri, kaseomesha watoto vizuri. Wewe hujasoma kama yeye hata mkiitwa kwenye interview na yeye wewe atakushinda ka sababu huna uwezo kama yeye. Kwa kuwa anakuzidi, anapata kpato kizuri kinamletea matokeo mazuri maishani lakni wewe unataka matokeo ya maisha yake yawe kama ya kwako na akikuzidi kaiba!. Dunia ya wapi hiyo kijana?
Hata Mbinguni kuna Ujira kila mtu na kazi yake.
HAPA TUELEWANE JAMBO MOJA. TUNAPOSEMA NI ADUI, TUN AMAANA AMETUMIA FURSA AMA MAPATO YA AIBU KUSABABISHA HASRA KWA WATANZANIA WANYONGE NA YEYE KUJINUFAISHA, LAKINI HATUNA VITA NA WANAOFANIKIWA KWA MISINGI YA HAKI.
KAMA VITA HIVI MTAVIGEUZA VIWE NI VITA VYA MASKINI KINYUME CHA WALIFANIKIWA, MTABAKI PEKE YENU KWA SABABU WENYE AKILI TIMAMU HATUTASHIRIKI. ILA TUTAPIGANA BEGA KWA BEGA KINYUME NA ANAYETHIBITIKA KUJINUFAISHA KWA GHARAMA YA JASHO LETU. HAO TUTAKULA NAO SAHANI MOJA.
LAKINI PIA VITA HII HAITAISHIA HAPO. TUTAHITAJI KUPIGANA NAN WAZEMBE WASIOTUMIA FURSA NA RASLIMALI VIZURI KWA MAENDELEO YAO NA TAIFA. NI LAZIMA KILA MTU AFANYE KAZI NA AMBAYO KWA KUWA TUTAKUWA TUMEONDOA UFISADI, LAZIMA ITAMLIPA KWA VIGEZO NA SIFA ZA UTENDAJI WAKE KWA NAFASI YAKE.
MAWAZO KWAMBA TUKIPIGANA NA UFISADI BASI MAISH AYATAKUWA MAZURI BILA JUHUDI HAKUNA. TUNAHITAJI KUWA NA MFUMO SAHIHI LAKIN MFUMO BILA KUUTENDEA KAZI HAULETI MAFANIKIO. NI JAMBO LA KILA MTU KUWAJIBIKA MAHALA ALIPO.