Hii mnaionaje, inaniboa sana

Hii mnaionaje, inaniboa sana

Sal

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2008
Posts
498
Reaction score
228
Unakuta mtu unaingia kwenye ofisi ya watu. kuko kimya kama maji ya mtungi maana people a busy working. Umekaribishwa kiti ili umsubiri mwenyeji wako. ghafla simu yako ya kiganjani inaita. Sauti kubwa, mziki wa ajabu, kwaya fulani ya Rose Mhando au taarabu ya Mzee Yusuf, hupokei mapema unaaiangalia kwa muda wakati inaitwa halafu unapokea.

kwa vile huna nidhamu, huwezi kudhani ofisi ya watu iko kimya na watu wako kazini, unapayuka bila aibu, hakuna la maana unaloongea zaidi ya jinsi mlivyolewa previous night.

Receptionist anakuomba samahani utoke ukaongelee nje, lakini bado unafanya kiburi hutaki kuelewa.
Huu ni ushamba, ulimbukeni au kitu gani jamani? Inaniboa sana kusema kweli.

Ni lazima uongee kwa sauti ukipokea simu mpaka kusumbua wengine?
 
pole sana wewe ni sekretare/resepshenisti wa ofisi gani?
 
Lol! Afu ukute simu ya mchina na wimbo wenyewe 'umelala huo, umelala dorooo'
Hivi simu za mchina hazina mute button?
 
Lol! Afu ukute simu ya mchina na wimbo wenyewe 'umelala huo, umelala dorooo'
Hivi simu za mchina hazina mute button?

hazinaga mwaya...
kama hii yanagu saa ingine tu ikiita inaweza hata isiwezekane kupokea unabonyeza weeee, wapi
 
sometimes wamuanglia mwenye simu... na simu inavopiga kelele kufananisha
ustaarabu wa muonekana na matendo... Then watikisha kichwa kwa masikitiko....
 
simu ya kichina haina ustaarabu kabisa. Ukisema uizime ndio itapiga kelele kuliko kelele ya mwanzo. Mi nikitaka kuizima kama nipo eneo lenye utulivu nachomoa betri.
 
Ha ha ha ha, mbavu zangu jamani
Mchina juu juu zaidi
 
pole sana ila na wewe punguza jazba mkuu!!!!!!!!!!
real inakera sana sana lakini you should have to learn different behaviours with refference to people
 
....yaani kama ulikuwepo last week; deadline ya report ili tupate ofa ya mapumziko ya mwisho wa mwaka; then mswahili wa ujiji na mchina wake....

Nisivyopenda kelele; mimi Simu yangu ni vibration 24/7
 
Kuna watu hawana kazi mjini hapa kazi ni kuzunguka maofisini mwa watu kupiga umbea. Anaondoka nyumbani mapemaaa as if anawahi kazini na kajikwatua utafikiri mfanya kazi, utaona naye yuko stand anasubiri magari ya posta. Kama huna kazi kwa nini usitafute shughuli nyingine ya kufanya? unafanya hivyo mpaka lini?
 
simu ya kichina haina ustaarabu kabisa. Ukisema uizime ndio itapiga kelele kuliko kelele ya mwanzo. Mi nikitaka kuizima kama nipo eneo lenye utulivu nachomoa betri.

Umenivunja mbavu mkuu
 
Inakera kweli, hasa sehem za C/service, simu ya mtu m1 inaweza kufanya walokuepo wote wasielewane. Sio ustaarabu hata kdg, binafsi nachukia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom