Hii Mikoa Nani Kailoga?

Hii Mikoa Nani Kailoga?

Habari za majukumu wana-Jf,.

Hapa nazungumzia mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara,.

Siyo jambo la siri mikoa hii ipo nyuma sana kimaendeleo au naweza kusema imesahaulika katika sura ya nchi yetu,.

Huwezi kulinganisha mikoa hii na mikoa mingine Tanzania kama Kilimanjaro, Mbeya na mingine ambayo imepiga hatua katika suala la maendeleo, uchumi na hata elimu,.

Nalitaka kujua kulikoni kwa hii mikoa kuwa nyuma katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo,.

Lengo la huu uzi siyo lingine zaidi ya kufahamu sababu za hii mikoa kuwa nyuma kwa hiyo mizaha na matusi hayatakuwa na tija katika kujuzana.

Ongeza Tabora
 
Huko ni kujidanganya!! Tulitegemea shinyanga ingekuwa tajiri mno kutokana na almas lakini waapi!! Iko wapi tanzanite ya arusha? Hivi uranium ina mchango gani kwa taifa? Hebu tulia kwanza, usije ukaongeza mke kwa ajili eti gas imegundulika mtwara!!

Asante.....Kumbe mambo yakichanganya unaongeza mke?
 
ongeza na Mara
Kwa sie ma-Vasco Da Gama mkoa wa Mara una afadhali aisee maana unafikika kiurahisi sehemu kubwa ya eneo lake ukilinganisha na maeneo mengine (wilaya karibu zote zipo along main road except Serengeti ambayo imejitenga pembezoni but gari za kwenda Musoma, Tarime na Bunda ambako kuna main road za kuunganisha na miji mingine zipo kibao (kuna sehemu likikuacha gari imekula kwako).
 
Tz hakuna sehemu ambako ni hafadhari ndo mana ktk majiji 200 bora hakuna jiji 1 la Tz musijipe moyo na dar,arusha na mwanza yote ni hovyohovyo tembeeni muone miji watu ilivyo
Mleta uzi chakii ameleta mada kutokana na hali ya kimaisha kwa kulinganisha mkoa mmoja na mwingine kwa vigezo vyetu vya kibongo maana hata ukienda kijijini kwenye nyumba za nyasi kijiji kizima huwa wana vigezo vyao vya familia gani ina unafuu wa maisha (hata kama mikoa yote ni chokest ila kuna maeneo mengine kazi ya ziada inahitajika)
 
Last edited by a moderator:
Mikoa inaendelezwa na serikali na kuuwawa na serikali,kwani Dodoma ilikuwaje miaka7 iliyopita ?? ilikuwa hivi ilivyo leo? na unaweza kusema kuna chochote wenyeji wamefanya kuubadilisha mkoa wao zaidi ya serikali? lakini si unaona leo kunapendeza,hata hiyo mikoa unayoisema ni serikali ndo imeifanya iwe hapo ilipo zaidi ya hapa fatilia mwenyewe ...kuna sababu ya kijiografia pia kama mlima Kilimanjaro umechangia sana kuwepo kwa maendeleo eneo husika kupitia nafasi za utalii,fikiria hule mlima uko Lindi
 
Hapo mtwara tandahimba kuna dogo langu lilichaguliwa form five.. Likashndwa na maisha...
 
Na hizo ni takwimu sahihi! Mimi namshukuru Mungu nimetembea mikoa mingi Tanzania isipokuwa Kigoma. Lakini makao makuu ya wilaya nyingi almost zinafana. Wilaya ambazo miji yake ni mikubwa ni Tarime-Mara, Masasi- Mtwara, Njombe- Iringa( kwa wakati ule), Korogwe- Tanga, Nzega-Tabora, Kahama-Shinyanga. Nyingi ya zilizobaki ni ndogo kabisa.
Mikoa ambayo makao makuu yake ni miji mikubwa kwa maana ya Level ya Jiji, Manispaa na Miji ni kama ifuatayo:-
Mwanza
Arusha
Mbeya
Tanga
Moshi
Morogoro
Dodoma
Tabora
Mtwara
Musoma
Iringa
Kigoma. Mingine yote ni miji midogo sana japokuwa ni Manispaa pia. Lakini pia fungua website ya TRA halafu google: Tanzania Domestic Revenue Collection Regionalwise, Mtwara bado iko juu kimaendeleo! Wilaya ya Tandahimba kwa mfano, moja ya wilaya tajiri kabisa nchini Tanzania. Mkoa wa Mtwara kila kitu kitakwimu ni duni sana katika wilaya moja, nayo ni Mtwara Vijijini, ni.duni kielimu, kiuchumi, kimiundombinu, vifo vya watoto na akinamama, na hii ndo pekee hushusha hadhi ya mkoa mzima, lakini kwingineko, Mtwara ni bora sana ukilinganisha na maeneo mengi ya Tanzania
Salute kwako umetoa tathimini nzuri ila ongezea kwa wilaya ambazo miji yake mikubwa Karatu (Manyara), Arumeru mashariki na magharibi (Tengeru mpaka Usariver), Bariadi (kwa zamani sasa hivi ni makao makuu ya mkoa), Geita, Chato pia kwa Njombe japo hata kwa wakati ule kama ulivosema lakini bado Makambako na Njombe mjini zote zilikuwa zinatisha though zipo kwa karibu wa umbali wa 60km. Pia kuna wilaya zingine ambazo zinakuja kwa kasi (Karagwe, Mafinga/Mufindi, Bunda na hata Mugumu - Serengeti) plus centre zinazokuwa kwa kasi Lamadi kipindi kile ipo wilaya ya Magu ilikuwa ina shughuli nyingi za kiuchumi inaikimbilia Magu. Kiujumla tathimini nyingine ya kuona kama sehemu kuna afadhali angalia wilaya ambayo ina bank zaidi ya moja yaani ukikuta kuna bank zaidi ya NMB na Posta Bank ujue hapo pana intervention za kiuchumi. Wilaya zote ulizozitaja hapo na hizi nilizoongezea kuna bank za biashara zimetia timu hapo kama Njombe hata kabla ya kuwa mkoa kulikuwa kuna NBC, CRDB tena ina ATM machine tatu na NMB pia hata Makambako ambako ilikuwa ni sehemu ya Njombe just 60km from Njombe ilikuwa na NBC na NMB
 
Mikoa inaendelezwa na serikali na kuuwawa na serikali,kwani Dodoma ilikuwaje miaka7 iliyopita ?? ilikuwa hivi ilivyo leo? na unaweza kusema kuna chochote wenyeji wamefanya kuubadilisha mkoa wao zaidi ya serikali? lakini si unaona leo kunapendeza,hata hiyo mikoa unayoisema ni serikali ndo imeifanya iwe hapo ilipo zaidi ya hapa fatilia mwenyewe ...kuna sababu ya kijiografia pia kama mlima Kilimanjaro umechangia sana kuwepo kwa maendeleo eneo husika kupitia nafasi za utalii,fikiria hule mlima uko Lindi
Mkuu observation yako nzuri hata mie nimekaa Dodoma, ni kweli mikoa inaendelezwa na serikali na kuuwawa, Dodoma ya leo ni tofauti na Dodoma ya miaka iliyopita kabisa ila kwa upande mwingine kuna mikoa mingine ilisahaulika lakini kwa namna moja ama nyingine ilijibeba kutokana na nguvu za halmashauri zao mfano mzuri, mikoa kama Mara, Mwanza, kwenda Geita mpaka Kagera kwa muda mrefu imekuwa imesahaulika lakini wakati serikali imeibuka kutoa support inakuwa kama inaongezea na kuongeza kasi zaidi ya ukuaji. (though pia inachangiwa na sababu za kijiografia na watu kuwa na utamaduni wa kupenda kwao kwani kuna sehemu zingine mtu akichomoka harudi na akipata hela anachomoka) Mikoa yote ingepata support kama ya Dodoma nadhani kuna mikoa mingine ingekua juu zaidi sema Dodoma napo ni kama pamelogwa pamoja na kwamba pamesogea kidogo lakini ukilinganisha na investment iliyowekwa tangu those days ilitakiwa pawe zaidi ya hapo)
 
"mjenga nchi ni mwananchi na bidii yake binafsi"
Wewe ndio umenena, mbona Mwanza yetu pamoja na kwamba tulifungwa kimawasiliano lakini watu walikuwa by any means wanajitutumua kutoka mpaka leo hii serikali imekumbuka lake zone imekuta watu wamejiandaa kupokea maendeleo. Kwanza ni wananchi wa eneo husika kujikubali na kuwa proud na kwao then maendeleo yanakuja, kuna watani zangu flani wao huwa wanapenda kujitambulisha kama Wakaguru yaani wewe ukimuuliza wewe kabila lako hili atakuambia "aah mie Mkaguru" kwa mtaji huu mtu wa namna hii anaweza kurudi kwa kwenda kujenga nchi in case maisha yamemshinda
 
Salute kwako umetoa tathimini nzuri ila ongezea kwa wilaya ambazo miji yake mikubwa Karatu (Manyara), Arumeru mashariki na magharibi (Tengeru mpaka Usariver), Bariadi (kwa zamani sasa hivi ni makao makuu ya mkoa), Geita, Chato pia kwa Njombe japo hata kwa wakati ule kama ulivosema lakini bado Makambako na Njombe mjini zote zilikuwa zinatisha though zipo kwa karibu wa umbali wa 60km. Pia kuna wilaya zingine ambazo zinakuja kwa kasi (Karagwe, Mafinga/Mufindi, Bunda na hata Mugumu - Serengeti) plus centre zinazokuwa kwa kasi Lamadi kipindi kile ipo wilaya ya Magu ilikuwa ina shughuli nyingi za kiuchumi inaikimbilia Magu. Kiujumla tathimini nyingine ya kuona kama sehemu kuna afadhali angalia wilaya ambayo ina bank zaidi ya moja yaani ukikuta kuna bank zaidi ya NMB na Posta Bank ujue hapo pana intervention za kiuchumi. Wilaya zote ulizozitaja hapo na hizi nilizoongezea kuna bank za biashara zimetia timu hapo kama Njombe hata kabla ya kuwa mkoa kulikuwa kuna NBC, CRDB tena ina ATM machine tatu na NMB pia hata Makambako ambako ilikuwa ni sehemu ya Njombe just 60km from Njombe ilikuwa na NBC na NMB

Yap, umenikumbusha Geita, nilipitiwa! Lakini centre zingine za ukweli ni Tunduma pale jirani na Nakonde, Makambako iko poa! Kuhusu Arumeru sikuitaja kwa kuwa tayari inaangukia Arusha jiji, ndo maana hata Dar sikuitaja kwa makusudi, pia nimeacha Manispaa zote.za jiji la Mwanza makusudi. So mtu kugeneralize tu kuwa sehemu fulani pako vibaya, kwa kigezo gani, je ni eneo lote au? Umefika au umeambiwa. Kwa mimi ambae nimeshatembea miji na mikoa mbalimbali huwezi kunidanganya kiurahisi, unakuta mtu anatoka mkoa wa kawaida kabisa, ambao makao makuu ya mkoa wake ni wa kawaida, halafu unakuta anabeza mikoa na miji ya wenzake! Kuna mtu mmoja alinichekesha, anabeza Mtwara halafu yeye kwao ni Kibaha Mail1, nikamuuliza, hivi mail1 kuna jambo lolote? Bandar,Uwanja wa ndege, mji na kila kitu, hata kwa taasis nyingi Mtwara iko juu, lakini mtu hajafika anambiwa stori za vijiweni yeye anakurupuka tu!
 
Kigoma mbona imepiga hatua sana msiiweke katka hilo kundi hata vijiji vingi vya kigoma vimepiga hatua sana tuwapongeze
 
Yap, umenikumbusha Geita, nilipitiwa! Lakini centre zingine za ukweli ni Tunduma pale jirani na Nakonde, Makambako iko poa! Kuhusu Arumeru sikuitaja kwa kuwa tayari inaangukia Arusha jiji, ndo maana hata Dar sikuitaja kwa makusudi, pia nimeacha Manispaa zote.za jiji la Mwanza makusudi. So mtu kugeneralize tu kuwa sehemu fulani pako vibaya, kwa kigezo gani, je ni eneo lote au? Umefika au umeambiwa. Kwa mimi ambae nimeshatembea miji na mikoa mbalimbali huwezi kunidanganya kiurahisi, unakuta mtu anatoka mkoa wa kawaida kabisa, ambao makao makuu ya mkoa wake ni wa kawaida, halafu unakuta anabeza mikoa na miji ya wenzake! Kuna mtu mmoja alinichekesha, anabeza Mtwara halafu yeye kwao ni Kibaha Mail1, nikamuuliza, hivi mail1 kuna jambo lolote? Bandar,Uwanja wa ndege, mji na kila kitu, hata kwa taasis nyingi Mtwara iko juu, lakini mtu hajafika anambiwa stori za vijiweni yeye anakurupuka tu!
Kumbe na Arumeru imeingia upande wa jiji nilidhani wameiacha kama zamani, asikudanganye mtu hakuna kitu kizuri kama kuzunguuka nchini kwako kuna mambo mengi ya kujifunza pia mambo mengi si kama watu wanavyodhani, namshukuru mungu hata mie nimezunguuka mjini na vijijini, kuna watu huwa nawatania mie ni mtanzania halisi maana nimezunguuka miji mikubwa yote na midogo midogo plus mpaka vijijini na niliwahi kufika mpaka Karagwe kijiji cha mwisho kabisa cha Chamchuzi maeneo Nyabiyonza nikalala guest house ya 1000 na Solar ipo
 
Jaribu kufananisha vijiji vya mkoa wa dodoma na vile vya Ruvuma.Ruvuma iko mbali sana au mnaangalia mjini tuu.Ukienda dodoma vijijini utalia.
 
Jaribu kufananisha vijiji vya mkoa wa dodoma na vile vya Ruvuma.Ruvuma iko mbali sana au mnaangalia mjini tuu.Ukienda dodoma vijijini utalia.

Kwa Dodoma vijijin kuko ovyo, ila Kondoa hasa ule upande kama unaelekea Babati kuko poa!
 
Kwa Dodoma vijijin kuko ovyo, ila Kondoa hasa ule upande kama unaelekea Babati kuko poa!
Kondoa napo sio pabaya sana nilikuta chemichemi moja ya Mparangwi kuna mifereji imechimbwa mpaka katikati ya mji watu wanachota (zamani sana nilifika), watu wa Kondoa (warangi wengi ni wajasiamari hata ukienda Dar na sehemu nyingine ukikuta mrangi wa kondoa ni mfanyabiashara)
 
mimi tz nimetembea mikoa yote na karibia wilaya nyingi nimefika usiiponde lindi ukaisifia tabora umefika mtwara mjini au tandahimba au kilwa masoko au masasi mjini ama kule nanjingwea hadi tunduru unarudi hadi ruangwa mjini unashindanisha na wapi kyela au tukuyu au babati au uvinza au mtukula ama loliondo wapi namtumbo ama nzega au iramba wapi sasa kiomboi au ngorongoro au lushoto sema muheza au pangani au kule njombe we vp rufiji au kisalawe au hai ama same rukwa hadi ukerewe sengerema au simiyu au karagwe kabla ya kutoa mada kama hizi hebu katembee kwanza au wewe ndo wale wasioenda sehemu kama hana ndugu
kwa hapa Tz mikoa hii bado ipo nyuma mkuu ukilinganisha na mingine,.
 
Back
Top Bottom