Nature ya kazi zangu imenifanya kuzunguka mikoa mingi hapa nchini, karibia 80%, na hasa vijijini. Nimefanya kazi Lindi na Mtawara about 7 yrs ndo maana nimeizungumzia mazingira magumu waliyonayo wananchi hawa. Kuna vijiji unaenda unaweza kuhesabu nyumba za bati, ukionyeshwa maji ya kunywa hutaweza kuamini kama ni maji ya kunywa mwanadamu. Vijumba vingine milango ni ya makuti tuu na imeegeshwa , habari ya choo ndo usiseme,. Ninakwambia haya kwani nimeshiriki kazi za TASAF 1 kuibua miradi, Miradi ya mazingira n.k kwa hiyo tumezunguka sana kwenye vijiji hivi. Huwezi ukalinganisha Kijiji kilichopo Mtwara au Lindi na vijiji vya mikoa kama Morogoro.
sasa hivi ninapoandika kuna watu wamekwama kilometer chache baada ya daraja la Mkapa na watalala hapo kama hawatakwamuliwa.........watu wanaitukana serikali yao sikivu ile mbaya...........alafu wewe unasema @ work Nyambafu......"ukawa @ work"
Ulishaenda vijiji vya Dodoma? Tena hata sio mbali jaribu tu kwenda pale kijiji kilichopo mjini kabisa Kule Ng'ong'ona jirani na chuo kikuu cha dodoma kitivo cha elimu ndo utajua maji ni uhai ama sio na ndo utajua vijiji vyenyeshida viko Lindi na Mtwara tu au la.
Nilikuwa huko mwaka jana (Vijiji vya Dodoma, Singida na Manyara) sawa tatizo la maji pia ni kubwa, but generally ukiangalia kiwango cha umasikini wagogo hawa wana nafuu maana wana vimbuzi, ving'ombe, wanalima sana mtama n.k Nyumba zao za tembe though full suti ni afadhali kuliko baadhi ya vibanda nilivyoona kusini. Kuna kipindi miaka ya nyuma nilikuwa Lindi, wilaya ya Kilwa Kijiji kimoja mbele ya Nainokwe nilishuhudia tukio la simba akichomoa mtu kutoka kwenye kibanda na kuondoka naye. Baada ya kusikia makelele kulifika sehemu ya tukio na kwa kweli huwezi kusema mtu alikuwa ndani kwani ukuta ni wa majani.
Kwani wale wa Pwani ambao wengi wao ni wavuvi hawana uhakika wachakula kwao?? Mbona hata makazi wengine ni nafuu maana kuna vijiji sio vyote hadi nyumba wanajenga kwa tofali za kuchoma sikuiz na Dodoma mmh bora tu nikae kimya ila hali ya vijiji tz ni kote tu shida huko manyara wengi wao hata makazi hawana kutokana na nature yao ya ufugaji ila still hali zao duni
habar mkuu?. mi nataka kwenda kuishi mtwara au lindi hasa kijijin ili niweze kujishuhurisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji na kilimo kwaajili ya chakula. Nimefanya tafiti ili niweze kuona kijiji kipi niende nikapata majibu:Nature ya kazi zangu imenifanya kuzunguka mikoa mingi hapa nchini, karibia 80%, na hasa vijijini. Nimefanya kazi Lindi na Mtawara about 7 yrs ndo maana nimeizungumzia mazingira magumu waliyonayo wananchi hawa. Kuna vijiji unaenda unaweza kuhesabu nyumba za bati, ukionyeshwa maji ya kunywa hutaweza kuamini kama ni maji ya kunywa mwanadamu. Vijumba vingine milango ni ya makuti tuu na imeegeshwa , habari ya choo ndo usiseme,. Ninakwambia haya kwani nimeshiriki kazi za TASAF 1 kuibua miradi, Miradi ya mazingira n.k kwa hiyo tumezunguka sana kwenye vijiji hivi. Huwezi ukalinganisha Kijiji kilichopo Mtwara au Lindi na vijiji vya mikoa kama Morogoro.