Hii kero ya matrafiki Arusha imezidi

Hii kero ya matrafiki Arusha imezidi

jembe afrika

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
7,602
Reaction score
3,781
Wakuu naandika hii maada nikiwa na hasira isiyozuilika.

Hata kama Ni usalama wa barabarani sasa huu ni upumbavu.Rushwa imekuwa logo yao ya kazi hata kama unakila kitu kwenye gari.Imefikia hatua kama huna hela Arusha kamwe hutaendesha gari hata kama gari lingekuwa jipya hutothubutu.Mbaya zaidi kama unatokea kisongo unaenda Kia imekula kwako kila mita 600wapo.

Anzia uwanjani Kisongo wapo,TANAPA,kona Mbauda,mataa ya Esso,kona ya TCA,Mianzini,Sanawari,kwa Mrefu,Daraja la Nduruma,,shamba la mbegu,Kilala,Makumira university,Usa River ,Maji ya Chai,Kikatiti,Funga kazi Ni King'ori kuna kadada kana miguu kama vibua kapenda rushwa mbaya na kengine kana matege kapo Arusha mjini hako ndo kiboko,nafikiri Arusha inaongoza Kwa kuwa na matrafiki wengi kuliko maaskari wa kawaida.

Kilichobaki ni kuwalipua kwenye vyombo vya habari au kuchukuwa hatua mkononi tu,tumechoka.Siku hizi mimi huwa sisimami kabisa.Haya matrafiki yana njaa kama dumuzi.

Sasa wanajamvi tuwachukulie hatua gani zingine za ziada kukomesha upuuzi huu maana mimi naweza kuja vunja mtu miguu.

Nina hasira sana.
 
Kweli ni kero sena. Sasa hivi nimepita maeneo ya raskazoni wamejazana kama ishirini hivi. Wanasababisha trafic jam mchana huu
 
Ndio pesa zinazoendesha jeshi la polisi ndugu yangu. Wako watumiaji wa barabara ambao ni maafisa wa takukuru na usalama wa taifa na wanashuhudia vitendo hivyo. Ni kero kweli kweli hasa lile kundi kubwa utafikiri ni pride of lion.
 
Wanashindwa kushika madawa ya kulevya wanahangaika na magari
 
Kuwapa rushwa tunataka wenyewe...
Hakikisha gari lako halina kasoro yeyote...
Na ukiendesha fuata sheria za barabarani, hakuna trafic atakayekugusa...
 
Msome vizuri mleta mada! Amesema hata kama gari lako liko vizuri jamaa hawaelewi!
 
Kosa kubwa limefanywa na serikali,hawa trafiki kama walivyo watumishi wengine wa umma wanatakiwwa kupewa uhamisho wa kituo cha kazi kila baada muda fulani kuepuka kuzoeana raia.
 
Kuwapa rushwa tunataka wenyewe...
Hakikisha gari lako halina kasoro yeyote...
Na ukiendesha fuata sheria za barabarani, hakuna trafic atakayekugusa...
Huwajui vizuri Trafiki wa Arusha wewe eeh?,watakugusa tu,labda uwe na mkonge tu ndo hutasumbuliwa,otherwise,watakushambulia wote na wanataka pesa yako kwa ulazima,hata kama ni kubambikiziwa kakitu.
 
Kosa kubwa limefanywa na serikali,hawa trafiki kama walivyo watumishi wengine wa umma wanatakiwwa kupewa uhamisho wa kituo cha kazi kila baada muda fulani kuepuka kuzoeana raia.
Mkuu nasikia huwa wanahonga hela nyingi ili wabaki hapa Arusha na unaambiwa Traffic akihamishwa kwenda mkoa mwingine kama sio Dar/Mwanza/Moshi/Arusha na akapangiwa mkoa mwingine lazima afe kutokana na kuwa huko hakuna hela!
 
Kunasiku mmoja wao alinisimamisha na baada ya kuanza kuniuliza maswali ya Kingese nikamuuliza hivi nini maana ya Sticker ya nenda kwausalama barabarani? akashindwa kunijibu nikamwambia ngoja nikufundishe, nikamwambia ili nipate Sticker ya nenda kwausalama barabarani ni kuwa inanibidi nilipeleke gari langu likakaguliwe na Vehicle Inspector halafu mtakapo ridhika ndipo mnanipatia hiyo Stiker tena kwa malipo, sasa wewe haya maswali yakuniuliza Leseni/Fire Extinguisher/Road License/Insurance yanatoka wapi?? akaniambia basi nenda!

Narudia tena naapa lazima nigonge mmoja wao!
 
Nimeyapita mengine hapa sanawari cedha yanatoa macho kama mademu wa mrina
 
Kuna hawa wanaokaa maeneo ya Triple A kuanzia asubuhi hadi jioni kunasiku nimewasikia wakiadidhiana eti mmoja anamwambia mwenzake usipojenga na kununua gari Arusha nenda katambikie!
Aisee kama hao wanakaa tripple A asubuhi mchana wanahamia TCA ni kero sana, hii nchi haina serikali? Hii nchi haina takukuru? Mbona wanajiachia sana na rushwa za wazi kuanzia asubuhi mpaka jioni? Yaan ntakuja mkanyaga mmoja amwage uharo we ngoja tu. Kero sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom