Hii kauli ya Magufuli "Polisi ueni Majambazi", imenitisha sana

Magufuli anaonekana kuwa na jazba sana katika hotuba zake kipindi hiki, ni wazi anahofu ya kitu fulani,

Nimeota kuwa uchaguzi wa kumpata mgombea ndani ya CCM bado haujaisha na hivyo huenda kura zisipigwe tarehe 25 kwani nimeota utasogezwa mbele.. Nimeota kuna kitu kitampata mgombea na hivyo kuna chama kitapewa fursa ya kuchagua mgombea mwingine na hivyo kupeleka mgombea wamtakae.
Ndoto nyingine ni mbaya sana na zinatisha mbaya.
 
kisheria kosa la ujambazi likithibitishwa bila kuacha shaka mbele ya mahakama adhabu yake iliyo kubwa kabisa sii kifo.

kura yangu nitampa Lowasa na nitailinda mpaka ipewe thamani niliyoikusudia.
 
Safi sana, kama wewe sio muathirika wa matukio ya majambazi utaendelea kupiga kelele za haki za binadamu!! Tena kama polisi wasipowaua, raia tunawavalisha tairi kisha kiberiti
 
Watu kila siku wanauawa na majambazi!wauawe tu na wao,safi sana Magufuri
 
Km kawaida ccm wamekuwa chama cha kupanic kwa muda mrefu sana
 
Magufuli anaonekana kuwa na jazba sana katika hotuba zake kipindi hiki, ni wazi anahofu ya kitu fulani,

Hii kauli haina tofauti na ile ya Pinda,Piga tuuuuuu,CCM utawala wa sheria siyo jadi yao.Kama jambazi amemgeuzia mgong unamua ili nini?Je akijisalimisha naye atauawa?
 
Hivi hao unao watetea huwa wanasubiri mahakama kabla ya kuuwa polisi wetu? Ukiwa jambazi ukavamia kituo na silaha hakuna huruma ni kuuwawa tuu! Hivi haki ya polisi wetu haipo?

Ni upotoshaji kusema kuwa kuna sheria inakataza polisi kuua majambazi yanayovamia vituo vya polisi. Hio sio kweli. Eleza ni wapi na lini askari polisi walichukuliwa hatua kwa kumuua jambazi aliyevamia kituo chao? Mbona kule Stakishari jambazi mmoja walimuua na hawajachukuliwa hatua zaidi ya kupongezwa. Makomeo anataka kutudanganya. Ukweli ni kuwa kauli yake inaweza kuongeza visa vya watu wengine ambao huwa wanauawa kwa kusingiziwa kuwa majambazi, kuongezeka.

Hata wewe unaweza kudhaniwa kuwa jambazi. Maana ikiwa mtu aliyekuwa anayefahamika kama alivyokuwa Amran Kombe alipigwa risasi kwa kudhaniwa jambazi, wewe utaponea wapi?

Majambazi kutokupora vituo vya jeshi kamwe haitokani tu na sheria kuwa wanajeshi watawaua majambazi (maana hata polisi wanafanya hivyo) bali ushupavu wa askari wa jeshi dhidi ya ulegevu na udhaifu wa jeshi la polisi. Kingine ni wingi wa siasa katika jeshi la polisi, kitu ambacho angalau kina ahueni jeshini.

Kwa kipimo chochote, alichosema Makomeo ni kauli mbaya kabisa kutoka kwa mtu ambaye anaweza kuwa rais wa nchi hii.
 
Unamjuaje jambazi kwa kumuona tu?
Huo siyo utawala bora kuua tu arafu utatawala nini? Huyo hafai.
Hiyo ni kweli mkuu, kuna mtu anaweza kuwa anapita na akawa traped kwenye tukio au kuna baadhi ya majambazi wanateka civilian na kuwatumia kama ngao n.k. hawa wote wataathirika bure.
 
Nilipost kipindi cha nyuma na kumfananisha Magufuli na Nduli Idd Amini Dadaa..!! Kwa kauli na maamuzi yake yenye kutumia nguvu ni hatari sana kwa maisha tunayo ishi kwa sasa. Magufuli sio mwanasiasa ndugu zangu. Magufuli kazi zake ni kujenga madaraja kwa kufoji na kula fedha za umma. Huyu bwana atatuletea vita na mauaji hapa.
 
Kavunja katiba... Hana haki ya kusema au kutoa kauli kama hiyo.... Yeye kazi yake ni kutoa mafunzo, ueledi na kuwapa ujuzi askari wake ili wapambane na majamambazi sawasawa...

Hivi mbona unajitoa ufahamu kwamakusudi?!ina maana hukumsikiliza vizuri au ndio ushabiki tu kwa lowassa?!nani haoni madhara ya majambazi hapa mjini?

Polisi wanaogopa kuua majambazi kwasababu ya sheria zinawabana sio kwamba wanakosa nafasi!na ndio maana magufuri amesema hivyo,mtu amevamia kituo na SMG au PISTOL na akataka kuua polisi halafu wewe unataka asipigwe risasi kwa wakati huo huo ili Kuokoa maisha ya wengine?!

Msilete siasa na ushabiki wa kampeni kwenye uhai wa mtu
 
Polisi atauaje mtanzania, ? . speech kama hizi hupata tafsiri mbaya sana. Mara nyingi wakati polisi na majambazi wakijibizana risasi za moto hapo kwa kweli jambazi akiuawa ni sawa kwa sababu ilikuwa kwenye harakati za mapambano. Polisi hawezi kusimama tumbo nje na siraha yake wakati jambazi akimtupia risasi, lazima ajitetee.

Lakini Kusema hadharani "UENI" ni mbaya. Hutafsiriwa vibaya na mapolisi sasa wataua kila mbaya wao kwa kisingizio ni jambazi. Ukigombania demu na njagu basi anakulisha chamoto kisha anatoa taarifa kituoni kwamba jamaa alikuwa jambazi.

Hizi kauli za kuropokaropoka zina madhara sana. Utawala Wa sheria mbona uko imara ukikarabatiwa?

Kwa polisi wanaouawa kila siku sio watanzania?!mbona hawavamii vituo vya Jeshi?Magufuri ameeleweka vizuri sana!hizo propaganda zenu za kugeuza maana ili Magufuri aonekane hafai tumeshazishtukia siku nyingi!
 

Kuteuliwa kuwa mgombea urais haimanishi ni rais, sasa anajipa madaraka kabla hajachagualiwa anajiona kama ndio rais tayari. Hatari kweli kweli

Propaganda zenu hazina mashiko tena!munageuza maana makusudi ili aonekane Magufuri hafai wakati unajua hajasema hivyo!

Alisema endapo "nikichaguliwa kuingia madarakani"sasa hayo madaraka amejipa wapi?
 
sasa na wewe mengi ametoka wapi kwenye ihi story? Wakazkazini wamewakosea nini ccm?

Kwani wa kazkazini sio watanzania? Sasa mnatuaminisha kwamba tuhuma zote kwa ndugu. Lowassa kisa ni mkazkazini?

Jamani watu wa ccm mchunge sana ulimi wenu mtalipua nchi ihi kwa kupandikiza chuki za ukabila na ukanda.

Mkuu wakaskazini sio watanzania wala hawana haki ya kugombania nafasi za nchi hii ,,,hii nchi wataipasua vipande vipande wanaoleta propaganda zao za ukanda ,
Hivi ikitokea magufuli akashinda na wakaskazini wakataa ,au Lowassa akashinda na hao Wa kanda nyingine wakakataa ,mchawi atakua Nani ??
 
Mm na kwambia Hapo akuna raisi siai wananchi tuambiwa tusiuwe she ria ifate mkondo wake police wanaambiwa wauwe je ni sawa Hapo afaiiii kuwa president uyoo magufuli@ Hapa ni lowassa tu October rest in peace Ccm
 
Jamani hiyokauri niyakulaani kwamtu yeyote anayefikili vizuri. Nyie mnaoishabikia inawezekana mnatumia kile kiungo alichowaambia Masabuli kwamba mnakitumia kufikili badala yakichwa.

Hivi leo ukiwaambia Polisi ueni majambazi kwa akili yenu mnadhani watauliwa majambazi tu?! Visasi tu vyamtaani kati yaraia na Polisi vitatosha kusababisha mauaji, then wanasema tu alikuwa jambazi. Mnashabikia tu hiyo kauri ila hamjui madhara yautekelezaji wake. Vigezo vyakwamba nijambazi ama siyo jambazi kwahiyo waachiwe Polisi ndo waamue?

Mmesahau enzi za Mahita nakina Zombe? Niraia wangapi waliuawa enzi hizo bila hatia tukiaminishwa walikuwa majambazi kumbe niwafanya biashara au raia tu kama mimi nawewe?
Jamani msitake kushabikia mambo bilakuyatafakari kwakina. Kazi aliyofanya Kikwete ktk kuliweka sawa jeshi la Polisi nikubwa mno sematu watu hamjui. Tulishafika pabaya enzi hizo jamani kama mnataka turudi huko, mimi nawaambia mtalia.
Siku akiuliwa mwanao, babako, kakako, mjomba, Mkwe nk, ukaambiwa alikua jambazi wkt sikweli bali alikuwa nahela zake akienda kwenye mahangaiko ya bishara zake nk, ndo mtakapojua mnachoshabikia kwamba nimauti.

Namimi naomba Mungu atuweke tu nahiyo kauri iannze kutekelezwa kama mlivoshabikia, na naomba yaanzie kwenu nafamilia zenu nawatu wanao wahusu sisitunaotoa angalizo Mungu atuepushie hayo maadhura.

Tumeshamuelewa Dkt Magufuri na hakuna wa kutuongezea maneno
 
Kwa polisi wanaouawa kila siku sio watanzania?!mbona hawavamii vituo vya Jeshi?Magufuri ameeleweka vizuri sana!hizo propaganda zenu za kugeuza maana ili Magufuri aonekane hafai tumeshazishtukia siku nyingi!
Kwa utaratibu huo kuna haja ya kuwa na mahakama kweli kama tutatoa madaraka kwa polisi kujichukulia sheria mikononi ?!!
 
Mimi mwenyewe nilikuwepo na amesema na tumuunga mkono kwakuwa majambazi hayana huruma kwa polisi kwanini waonewe huruma?

Kwanini hizo haki za binadamu haziangalii hatari ya polisi wetu kuuwawa kila siku tena kisa haki za binadamu!

Hivi hayo majambazi leo hii wanaliliwa kuliko polisi wetu? Magufuli kasema atatoa ruhusa kwa polisi kuwauwa wanapo vamia vituo vya polisi!
Tena aliuliza kwanini tuwaonee huruma wakati wao hawana huruma?

Hakika Magufuli amenena na hakuna kuonea huruma watu wasio na huruma...

Watu wakisikia majambazi watu uwawa wanaanza kuwaonea huruma na kuwasahau polisi wetu....

Ujambazi haulipi wauwawe tuu...

Polisi hawa hawa waliomuua mwandishi wa Chanel ten?? Au wengine
 
Back
Top Bottom