Hii itawauma wengi

Hii itawauma wengi

Tena watu kama hao unakuta anapata tubinti tuzuri tu na unakuta ana watoto hata watatu au wanne kila mmoja ana mama yake, unabaki unashangaa wewe mchapa kazi mpaka miaka 30 bado huna mtoto hata mmoja na hujapata hata rafiki wa maana
Mkuu hata ndoa za watu! hawa jamaa baadhi ni waharibufu sana hasa kwa wale ambao Mungu kawajalia wazazi wao kujenga nyumba za wapangaji na wanishi nao kwenye compound moja!
 
Kuishi home sio utoto kama hujaoa , na wazazi wako hawaishi hapo.kuna familia zingine wana nyumba nyingi so mleta mada acha chuki,tuache tukae home
 
Sielewi kama mimi ndio nina matatizo ama vipi, maana hivi vitu watu wanafanya siku hizi vinanichanganya

Unakuta mtu ana miaka 25+ anaishi nyumbani kwao, hata rent ya miezi miwili hawezi kujilipia lkn ukija kwenye status yake unakuta yy ni bingwa wa kuandika historia ya mabilioni ya Jeff Bezos, Jack Ma na kina Patrice Motsepe

Mtu huyo huyo hafanyi chochote kbs, akishashiba chakula cha mama anakuja IG anaandika "Dear haters, the more you hate me the more I become successful" Ni kama vile kuwa na haters ni fashion inayoTrend

Watu wa aina hii ukimuuliza bruh mishe zinaendaje,kwanza lazima akujibu kwa kingereza,utasikia "Patience bruh, you know patience is bitter, but it's fruit is sweet". Sasa mimi najiuliza hivi tatizo ni kuwa na elimu au kutokuwa na elimu. Maana watu wa namna hii huwa wanasoma vitabu kweli kweli, cashflow quadrant yote ipo kichwani

Kukaa nyumbani kufikiria kuwa milionea ni utoto sana na hii michezo ya kujifanya wasomi na wachambuzi haitatufikisha popote pale. Mtu anajua matoleo yote ya Range Rover lkn bado nauli ya daladala mpk aombe kwa mtu

Sisemi kuwa watu wasiwe na ndoto kubwa, hapana! lkn kabla ya kutamani kuwa bilionea fikiria kwanza jinsi utakavyofanikisha kuhamia kwako. Kama una degree ya BaEd na hauna ajira, nunua mabenchi fundisha watoto twisheni jioni, 25,000 kwa mwezi, anza na watoto 10, hiyo ni 250,000... hapo unaweza kuanzisha baby care ya wanafunzi 40, kila mmoja ada 30,000 kwa mwezi una milioni yako. Asubuhi baby care, jioni twisheni, weekend mitihani

Muhimu sana ukaepuka kuwaambia watu shida zako, coz kila mtu ana shida zake kibao na hkn anayeshtushwa na shida zako. Km una ndoto sahau mtu kuinvest hela yake kwenye ndoto yako wkt ww haujainvest hata mia. Komaa invest hela yako then push, mtu akitaka kukujoin akukute kati kati, ht ukimwambia inahitajika mil 20 at least inaelezeka hiyo hela itatumika wapi. Sio uniombe mil 5 wkt unalala kwa mama'ko, hapo nitajua tu huyu jamaa hela yng atalipia kodi....#NIMEIKUTA MAHALI WADAU#
Nilitamani ungeacknowledge the source. Nimeisoma mahali. Ni nzuri.
 
Yeye kukaa kwao na kula hela za Wazazi wake wewe unaumizwa na nini?

Waafrika tuache tabia za kimaskini za kuona anayeishi nyumbani kwao hana malengo yoyote.
Si ndio hapa sasa, hata ray anaishi kwao na ni moja ya vijana wenye mafanikio tu,mimi nitaondoka home nikiwa 35 hapo ndio nitaoa, mleta mada asitupangie
 
Dah, wakati mwingine wazazi huwaandalia masiaha mwanao, so Kosa. Mie sasa sitaivwanangu watabike km Mimi nilivyopitia, kukaa ka ndugu kwa shida nk. Unalazimika kulish KUKU na nguruwe ili TUWEZE kula. Sasa km home anaweza akfany shughuli hizo huku akiikadiria vocha navuhakika wa kula mchana na usiku, kulala pazuri, kuongea na marafiki nk. Sio dhambi, siku ikifika wataondoka kwa amani na,wataishi vizuri.
 
Si ndio hapa sasa, hata ray anaishi kwao na ni moja ya vijana wenye mafanikio tu,mimi nitaondoka home nikiwa 35 hapo ndio nitaoa, mleta mada asitupangie
Hahah mtu akiona amepata Kaelfu 50 anaondoka anaenda kupanga , hii yote ni kutafuta gheto la kugongea "mademu" hakuna lingine.
 
"Patience bruh, you know patience is bitter, but it's fruit is sweet".😀😀
 
Hilo Mleta mada hataki kulisikia ndio maana nikatolea mfano wa Wahindi na Waarabu na hata Wazungu je hii nayo haifai?

Hao wanaolisha familia kidogo wana tu aibu aibu kidogo!, ila wote ni wale wale kwani ukiwa na kwako kuhudumia familia ya kwenu itashindikana vipi?

Mtu kuishi kwao wala sidhambi pia akuna ubaya wowote tuache mambo ya kizamani jamani. mathalani nyumbani kwenu kuna nafasi au vyumba vya kutosha miundo mbinu mizuri ya maji na umeme na wewe unakazi ambayo inakuingizia kipato kizuri na wewe bado ni bachela, sasa yanini kwenda kwenye nyumba za kupanga sibora ukae kwenu wakati huo nawewe unachangia gharama za matumizi .kwa kukaa nyumbani utapata unafuu kiasi Fulani katika kujipanga vizuri tena bila kuathiri uchumi wa wazazi wako kwa sababu unachotumia nyumbani kinatokana na mchango wako.
Mtu kama kapata bahati kuwa karibu na kwao na mazingira ni rafiki anaweza kuishi kwao kwa mazingira niliyoelezea hapo juu wala asione tatizo labda kiuchumi anajimudu ana viwanja, usafiri na kuhusu kujenga nitaratibutaratibu ujenzi hautaki haraka kwa wale wanauchumi wanalijua hili, labda atahama kwao atakapofikia wakati ambao yeye anaona ni sahihi kuhama baada ya kupata mchumba wa kuishinae.
Faida za kuishi nyumbani .
  • unapunguza gharama ambazo zingapotea bure tu kwenda kwa mwenye nyumba umeme na maji
  • unaachana na mambo ya kula migahawani kula migahawani sikuzuri sana kiafya hata kiuchumi
  • unaokoa muda mwingi sana badala ya kukaa na kuwaza vikazi vidogovidog lakini nyumbuni kuna wadogo zako wanakupa kampani
  • pia nyumbani kunakufanya kudumisha maadili mema zaidi kwasababu uwezi kujiingiza kwenye mambo ya kishenzi wakati upo kwenu na wazazi
  • unapoumwa au kupata matatizo msaada unoupata ni wa uhakika na kwaurahisi kwa kutoka kwa wazizi na ndugu
  • zipo faida nyingi za kiuchumi,kijamii nk
lakini pia hata kwa wale ambao hawana kipato bado sivibaya kukaa kwao kama kuna msaada kwanini asikae kwao ili ajipange vizuri kwani ni nani katika maisha haya asiye saidiwa, tena huyu anasadiwa na wazazi wake. Jambo baya ambalo naliona hapa ni mtu kuamua kuishi nyumbani kwao bila kuwa najitihada zozote za namna ya kujikwamua na kuwa mtegemezi wengine hadi anaoa akiwa kwao na mke anakuja kuishi hapohapokwao. Mtu wa hivyo kwa kweli ni hamnazo .
mwisho tusiforce kuyafanya maisha kuwa magumu tukiamini ni upambanaji ukipata fursa ya kurahisisha maisha utumie ili ufanikiwe haraka. Angalieni wazungu,wahindi na waraabu wala hawapitii msoto kiivo lakini wao ndio wanafanikiwa zaidi kuliko sisi manguvu mengi wavulia umande.
Excuses.
 
Mkuu kiuhalisia maisha hayapo hivyo aisee,wewe pambana tu na hali yako,hautakiwi kuishi kwa ajili ya watu wengine,ishi kwa ajili yako na utafanikiwa,kukaa na kuumiza kichwa juu ya nani anaishi wapi na anafanya nini wakati wote mnapambania ku`survive,huo nao ni ujinga kama ujinga mwingine,utacheleweshwa sana ukianza kuumiza kichwa kwa ajili ya watu wengine wanavyoishi,pole sana!
Toka kwenu aisee nenda kajitegemee
Wazazi wako wanashindwa kujiachia kwa sababu ya uwepo wako.. Wacha kutafuta defence mechanism
 
Yeye kukaa kwao na kula hela za Wazazi wake wewe unaumizwa na nini?

Waafrika tuache tabia za kimaskini za kuona anayeishi nyumbani kwao hana malengo yoyote.
Toka kwenu katafute hela zako
Mwishoe wazazi wahisi unawaombea kifo
Ili uzitafune vzr
 
Kuna kitu kinaitwa udhubutu. Vijana wengi wa kibongo hatuna hii kitu..
Yaan kudhubutu kutoka kwenu na kufanya kaz fulani...
Kudhubutu kutoka kwenu na kwenda kufanya kufanya shughul japo uingize chochote..

Kinacho waponza watu ni ile hali ya kuwa nitaonekanaje na usomi wangu huu nikianza kufanya kaz fulani.
kudhubutu kuacha kazi na kujiajir....ha ha haaa fupa hili wameshindwa wabongo wengi
 
Back
Top Bottom