Acha Hofu ya Watu: Timiza Ndoto Zako

Acha Hofu ya Watu: Timiza Ndoto Zako

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,095
Reaction score
869
"Hofu ya watu watanionaje"

imewachelewesha watu wengi sana kutimiza ndoto zao za thamani.

Watu wengi wana ndoto kubwa,mawazo makubwa,vipaji na uwezo wa kufanya mambo makubwa sana.

Lakini wanashindwa kuanza kwasababu wanaogopa na kuhofia kuwa watachekwa,watakosolewa au kuonekana tofauti na watu wengine.

Inawezekana una ndoto ya kuanzisha biashara,kuongeza Elimu au kuanzisha mradi mpya n.k

Acha kuendelea kupoteza muda kwasababu hao watu unaowahofia kuwa watakuonaje hawana msaada wala mchango wowote kwenye maisha yako🤷

"Usiruhusu maoni ya mtu mwingine kuhusu wewe yawe uhalisia wa maisha yako"
Alisema LES BROWN mwandishi na mtaalamu wa masuala ya mafanikio na maendeleo binafsi.

Sijajua ni mara ngapi au nikwa kiasi gani umecheleweshwa na hofu ya kuogopa watu watakuonaje.

Lakini leo amua kwa dhati na uanze kufanya bila kujali watu watasema nini kuhusu wewe,ipo siku watakuelewa tu.

-The Power Is Within You-

_Dr.Zack✍️
 
Back
Top Bottom