Sielewi kama mimi ndio nina matatizo ama vipi, maana hivi vitu watu wanafanya siku hizi vinanichanganya
Unakuta mtu ana miaka 25+ anaishi nyumbani kwao, hata rent ya miezi miwili hawezi kujilipia lkn ukija kwenye status yake unakuta yy ni bingwa wa kuandika historia ya mabilioni ya Jeff Bezos, Jack Ma na kina Patrice Motsepe
Mtu huyo huyo hafanyi chochote kbs, akishashiba chakula cha mama anakuja IG anaandika "Dear haters, the more you hate me the more I become successful" Ni kama vile kuwa na haters ni fashion inayoTrend
Watu wa aina hii ukimuuliza bruh mishe zinaendaje,kwanza lazima akujibu kwa kingereza,utasikia "Patience bruh, you know patience is bitter, but it's fruit is sweet". Sasa mimi najiuliza hivi tatizo ni kuwa na elimu au kutokuwa na elimu. Maana watu wa namna hii huwa wanasoma vitabu kweli kweli, cashflow quadrant yote ipo kichwani
Kukaa nyumbani kufikiria kuwa milionea ni utoto sana na hii michezo ya kujifanya wasomi na wachambuzi haitatufikisha popote pale. Mtu anajua matoleo yote ya Range Rover lkn bado nauli ya daladala mpk aombe kwa mtu
Sisemi kuwa watu wasiwe na ndoto kubwa, hapana! lkn kabla ya kutamani kuwa bilionea fikiria kwanza jinsi utakavyofanikisha kuhamia kwako. Kama una degree ya BaEd na hauna ajira, nunua mabenchi fundisha watoto twisheni jioni, 25,000 kwa mwezi, anza na watoto 10, hiyo ni 250,000... hapo unaweza kuanzisha baby care ya wanafunzi 40, kila mmoja ada 30,000 kwa mwezi una milioni yako. Asubuhi baby care, jioni twisheni, weekend mitihani
Muhimu sana ukaepuka kuwaambia watu shida zako, coz kila mtu ana shida zake kibao na hkn anayeshtushwa na shida zako. Km una ndoto sahau mtu kuinvest hela yake kwenye ndoto yako wkt ww haujainvest hata mia. Komaa invest hela yako then push, mtu akitaka kukujoin akukute kati kati, ht ukimwambia inahitajika mil 20 at least inaelezeka hiyo hela itatumika wapi. Sio uniombe mil 5 wkt unalala kwa mama'ko, hapo nitajua tu huyu jamaa hela yng atalipia kodi....#NIMEIKUTA MAHALI WADAU#