Hii inakera sana

Unique Flower

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
12,714
24,888
Jamani mtu akiolewa kaolewa na ukoo mtu anakuja na familia nzima .

Yaani wazazi wote wawili , dada , kaka na wadogo zake ndani yanyumba halafu hawana hata haya yakukaa na wao ndio wamefika. Hata wakitafutiwa kazi wapo hapo hapo na chakusikitisha hawachangii chochote sio luku au chakula wala kodi au nini kila kitu ni shemeji kama mpo huku acheni hii tabia mnakera ipo siku mtampomza dada yenu ataachika.

Wifi alijifungua akaniita nikamsalimie kufika nyumba ya jirani yake hadi aibu yaani wamemganda shemeji yao hadi aibu . Na hadi kuoga , chakula na kuishi kwa ujumla inaboa inasikitisha mtu hana raha.

Mimi na wifi yangu tukicheka ile siku mtu na ndugu yake wanakimbizana kisa mtu kala pajaa. Kama mpo huku acheni ujinga na roho ya unafiki nendeni kwenu.

Kwa wifi yangu sijawahi hata kuona ndugu zake. Hata kuwaona ila kama anaumwa au anaboreka ndio unawaona na sio hawana shida ila wanaheshima .

Kama mpo humu acheni uroho wakwanini.

Mnaboa mtu amezeeka kwa shemeji yake . Hadi mvii sio freshi wakuu.
 
Hii niliwahi kuiona kisongo Arusha,Jamaa na mkewe wote walikuwa wanafanya kazi A to Z kiwandani wamepanga chumba na sebure

Siku moja wakapata ugeni kutoka singida ndugu zake na mke wa jamaa walikuwa watatu(mama mkwe na vijana wawili wa kiume wadogo zake na mke wa jamaa),walikuja kwa ajili ya kuuza mafuta ya alizeti lakini hata mafuta yalipoisha hawakuondoka wakawa wakaaji,mama mkwe analala sebuleni wale vijana jamaa kawaombea kwa mpangaji mwenzie,nakwambia ilikuwa ni fujo hiyo ndoa ilikosa amani kabisa,asubuhi wanaomba matumizi utazani jamaa aliwaita waje Arusha,jamaa alikoma
 
Nawe jitahidi usikae Sana hapo,hawaongeagi kuwa wamekuchoka huumia ndani Kwa ndani.Jaman,watu wakioana waacheni nao watengeneze familia Yao,siyo kuwaanzishia kulea familia ndugu😠
Mie sikaagi kwa sababu ni aibu aisee.
Narudigi home tu .
Ila siwezi hata kukaa 2 weeks nakuwaga sina amani.
 
Choyo kimezidi katika jamii, kila mtu ana rizki yake kutoka kwa Allah ,Qaumu nyingi zimeangamizwa kwa kupenda choyo, napenda ndugu wa mke wangu, sisi ni wapemba tunapenda kujazana nyumba moja, its part and percel y traditional yetu
 
Alichokosea jamaa ni kuwaombea kwa mpangaji angeacha wabanane hapo hapo sebuleni wangewahi kuondoka
Hii niliwahi kuiona kisongo Arusha,Jamaa na mkewe wote walikuwa wanafanya kazi A to Z kiwandani wamepanga chumba na sebure

Siku moja wakapata ugeni kutoka singida ndugu zake na mke wa jamaa walikuwa watatu(mama mkwe na vijana wawili wa kiume wadogo zake na mke wa jamaa),walikuja kwa ajili ya kuuza mafuta ya alizeti lakini hata mafuta yalipoisha hawakuondoka wakawa wakaaji,mama mkwe analala sebuleni wale vijana jamaa kawaombea kwa mpangaji mwenzie,nakwambia ilikuwa ni fujo hiyo ndoa ilikosa amani kabisa,asubuhi wanaomba matumizi utazani jamaa aliwaita waje Arusha,jamaa alikoma
 
Hii niliwahi kuiona kisongo Arusha,Jamaa na mkewe wote walikuwa wanafanya kazi A to Z kiwandani wamepanga chumba na sebure

Siku moja wakapata ugeni kutoka singida ndugu zake na mke wa jamaa walikuwa watatu(mama mkwe na vijana wawili wa kiume wadogo zake na mke wa jamaa),walikuja kwa ajili ya kuuza mafuta ya alizeti lakini hata mafuta yalipoisha hawakuondoka wakawa wakaaji,mama mkwe analala sebuleni wale vijana jamaa kawaombea kwa mpangaji mwenzie,nakwambia ilikuwa ni fujo hiyo ndoa ilikosa amani kabisa,asubuhi wanaomba matumizi utazani jamaa aliwaita waje Arusha,jamaa alikoma
Wanayaturu hao,hatari sana.Nina ya kuongea kuhusu hao ila wacha nikae kimya
 
Back
Top Bottom