Hii imezidi

Jun 10, 2011
20
0
Kuna kaka nilikutana naye facebook, tukapeana namba za simu tukawa tunawasiliana vizuri mpaka sasa tumefikisha mwaka mmoja. Wakati nikitafakari undani wa upendo wetu ikaonesha ya kuwa mkaka hana mapenzi yakweli kwani alinipatia information za uongo.​
1. hakuwa mpenzi name kuwa chaguo lake la pekee,​
2. eti anaishi Kenya, mfanya biashara,​
3. Familia niya elite group.​
Kwa sababu hizo tukaamua kushirikiana kwa kila jambo japokuwa tuko mbali from each other mwaka ujao tulipanga tukatambulishane kwa wazazi.​
MWISHO WA SIKU….nikagundua kuwa kaka anampenzi wake na wanasoma chuo kimoja mwaka wa pili, yuko Tanzania chuo kikuu cha Dodoma​
Je nifanyeje?​
 
Pole sana,kwa wakati wote ambao mlikuwa mkiwasiliana hamkuwahi kukutana?
Jiepushe na mapenzi ya kwenye simu au ya mtandaoni maana huwezi kujua yupi ni mkweli na yupi ni muongo.
 
Una mapungufu makubwa kwani kwa mtoto wa kike nina imani kuna vijana wanaongea na wewe ana kwa ana juu ya mapenzi ikiwemo pengine kukutaka urafiki wa milele yaani uwe mke na yeye mume yawezekana uanakataa unababaika na huyo unayewasliana naye kwenye simu toka nje ambaye umjui hata sura yake labda kupitia mtandao mtandao wa uhakika wa maisha yako ni macho yako kuona Live kusikia mwenyewe kile unachoambaiwa:lock1:
 
umevuna ulichopanda...tokea lini lini mchumba akatafutwa kwa dizani hiyo ka yako au ndio ulimbukeni wa utandawazi!
 
usi date mtu uliyekutana nae facebook au kwenye hii mitandao...wengi wao ni matapeli tu
 
tafuta mpenzi live....achana na hao wa mitandaoni......
preta mbona maneno kuntu?? mbona mi nimempenda 'M' Na ni wahapahapa!! sa unataka hisia zangu niziweke pending, wakati ndani mwangu naumia, preta acha tu nidanganywe, sio steel wire kusema ikisugua sana sufuria itakwisha! nitamuonjesha akija kunijua wallah japo kiduchu tu, aweke chata kwenye moyo wangu, kuwa na ye alipita!
 
nimeipenda hii......kudadeki......
we usione sooo....kama vipi....mwambie....akikubali....mtumie....akiganda mgandie....akisepa mpotezee.....
sio steel wool bana.......

Jamani mdada, mtandaoni kweli? Kwani kwa kipindi chote cha uhai wako hukakutana na wa ana kwa ana? Sasa kilichokuvutia wewe zaidi ni hiyo CV yake aliyokuwa ameambatanisha, ambayo obvious ataipamba ili apate kazi! Hebu njoo kwe nye maisha halisi ndugu, huyo mbuzi wa kwenye gunia mwache apite na gunia lake....
 
nimeipenda hii......kudadeki......
we usione sooo....kama vipi....mwambie....akikubali....mtumie....akiganda mgandie....akisepa mpotezee.....
sio steel wool bana.......

Huu mpasho lazima niutungie mwimbo kwenye bendi yangu ya Kiduku!.
 
dah, huu utandawazi utatupeleka pabaya... yaani mkatambulishane home wakati hata kuonana ana kwa ana pengine bado?
 
Kuna kaka nilikutana naye facebook, tukapeana namba za simu tukawa tunawasiliana vizuri mpaka sasa tumefikisha mwaka mmoja. Wakati nikitafakari undani wa upendo wetu ikaonesha ya kuwa mkaka hana mapenzi yakweli kwani alinipatia information za uongo.​
1. hakuwa mpenzi name kuwa chaguo lake la pekee,​
2. eti anaishi Kenya, mfanya biashara,​
3. Familia niya elite group.​
Kwa sababu hizo tukaamua kushirikiana kwa kila jambo japokuwa tuko mbali from each other mwaka ujao tulipanga tukatambulishane kwa wazazi.​
MWISHO WA SIKU….nikagundua kuwa kaka anampenzi wake na wanasoma chuo kimoja mwaka wa pili, yuko Tanzania chuo kikuu cha Dodoma​
Je nifanyeje?​

Tatizo kupenda "Ghost" huko> Hebu penda mtu unayemuona na kuwasiliana nae uso kwa uso!
 
Back
Top Bottom