Lakini hapo ndipo Ujinga wetu Waafrika ulipo, kwa maana hapa ukiangalia Kiafrikaans ni lugha ya Wazungu Makaburu unaweza hata kukiita Kiholanzi na Wazungu hawa hawataki kuiacha lugha yao na kuchukuwa English ingawaje wewe unasema ni lugha ya Dunia lkn Mwafrika mweusi anapigania na yuko tayari kuharibu Miundo mbinu ya Chuo Kikuu iliyojengwa kwa fedha nyingi ili Kiingereza kifundishwe!
Sasa ni kwa nini Mzungu anapigania Kiafrikaans chake tena ndani ya Afrika lkn Mwafrika mweusi yuko tayari kufa kupigania Kiingereza na siyo Kizulu chake?
Kumbuka Wazungu (ukiondoa machotara/coloreds) wanaoongea Kiafrikaans kama lugha yao asili hawazidi milioni 2 wkt Kizulu kinaongewa na Watu milioni 11 au asilimia 22 (22%) ya wananchi wa AK, sasa kwa nini nguvu zao Waafrika weusi wasizielekeze hapa kwenye Kizulu badala ya Kiingereza?
Afrikaner si lugha ya Kiafrika. Ni lugha ya makaburu. Makaburu kwa jina jingine huitwa Afrikaners