Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Binafsi sielewi na bado sijawahi kuielewa reasoning yetu Waafrika hata siku moja. Huko nchini AK kumezuka fujo kubwa iliyopelekea wanafunzi kuchoma na kuharibu Miundo mbinu ya Chuo Kikuu wanachosomea, sasa kisa ni nini?
Ni kwamba Wanafunzi Waafrika (weusi) hawataki kufundishwa kwa lugha ya Kiafrikaans ambayo ni lugha rasmi ya Makaburu wanasema kwamba ni lugha ya Kikoloni na ya ukandamizaji na wanataka Vyuo vyao vifundishwe kwa kutumia Kiingereza, hapo ndipo nilipochoka ningeelewa kama wangegoma kufundishwa Kiafrikans na kutaka wafundishwe Kizulu, Xhosa , Kitwsana au hata Kiswahili kama shida ni lugha ya Kikoloni lkn wanataka Kiingereza sasa Kiingereza ni lugha ya nani?
Unakataaje Kiafrikaans kwa kigezo kwamba ya Kikoloni halafu unataka Kiingereza?
Inanikumbusha Raisi Kagame wa Rwanda alipoondoa Kifaransa kama Lugha ya Taifa na kuweka Kiingereza kwa nini asingeweka Kirundi/Kinyarwanda? Au Raisi Mugabe wa Zimbambwe anatukana Wazungu na kuwakebehi lkn kwa Kiingereza na nchi yake anatumia Kiingereza kwa nini siyo Kishona?
Kwa mambo kama haya Waafrika hatuwezi kuheshika Duniani kamwe kwani watu wa nje wanatuona hatuna akili, Dunia nzima binadamu hufanya Mapinduzi na kuweka lugha zao sasa tuko tayari kuharibu Miundo mbinu yetu kupigania Kiingereza, sasa Kiingereza kina tofauti gani na Kiafrikaans? Zote si ni lugha za Kikoloni pia!
Hata hapa nyumbani watu wengi wanaona na kuamini kwamba Kiswahili chetu ndiyo adui wa Maendeleo yetu nina uhakika ukifanya kura ya maoni ya kama Kiswahili kifutwe TanZania na kuwekwa Kiingereza au Kifaransa au hata Kireno zaidi ya asilimia 60 wataataka Kiswahili chetu kifutwe, na kama siyo kuwa Sera ya CCM Kiswahili kingekuwa kimeshafutwa kwani kwenye manifesto ya chadema walikwishakiondoa na kubakia somo tu!
Hii ni Afrika kwetu tu hakuna sehemu nyingine Duniani kuna binadamu wa aina kama yetu!
Hata Afrika Kaskazini hawako hivyo Gadafi mpaka anakufa anaongea Lugha yake!
Chini ni Uharibifu uliofanywa na Wanafunzi kwa kuchoma majengo ya Chuo chao kupinga Kiafrikaans na kutaka Kiingereza!
SABC News - UP student’s Afrikaans protest grows:Friday 19 February 2016