Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Smirna na Mhabarishaji... Naona wewe ndo una mashaka na pesa alizonazo Kakobe na unazitolea macho na udenda... Unafurahii akiwa maskini eeh... Basi mwacheni awe MASKINI maana na yeye amekubali kuwa hivyo.... Anafikiri akiendelea kukaa hivyo atapewa Zawadi ya Nyumbani na Watanzania... Kamwe hawawezi kuacha kumsema .... Mpaka anaingia Kaburini... Hivyo kujitesa kwake kwa kuishi hapo "kibandani" sijui itakuwa imemsaidia nini Askofu wangu... Nampenda sana Kakobe ila kumbe sio jasiri kama nilivyokuwa nadhani....
 
Dawa ya waongo na wazushi ni ukweli kuwekwa hadharani! Waongo Wamedanganya sana na wengi kudanganyika lakini kila kitu sasa kimewekwa wazi na kila mmoja popote pale alipo alete ushahidi kukanusha hii taarifa, naona mpaka sasa hakuna aliyeleta!na hawezi kupatikana maana yote yaliyokuwa yanazungumzwa yalikuwa ni uongo na uzushi. Tuache kuuamini uongo na uzushi.Askofu Kakobe ni Mtumishi wa kweli wa Mungu.

Ni Mtumishi wa Kweli kwa sababu ni Maskini?? Hebu kwendraaaa.... Ndio maana wapentekoste tunadharaulika sana... GBBS kaone thread humu JF zinazowasifu Watumishi kama Mwingira na Lusekelo kwa utajiri wao...!! Wale ndo Washirika au Waumini wa ukweli...
 
Kulikuwa na kipindi cha Mkasi alihojiwa Mch. Lusekelo akasema kuhusu utajiri wake wa Magari na Majumba bila kujificha... Na akasema hana biashara... Maana yake pesa zinazotumika ni za Kanisa au Waumini... Lakini hakuwa na hofu kusema hivyo na wala Kanisa lake halijasambaratika... Watu wanaenda kanisani pale kwa hiari na kutoa kwa hiari...
 
Mtu anawekwa huru kwa kuifahamu kweli.Wengi wamekuwa wakipotosha jamii kwa uongo.Lengo la hii ni kumfanya kila mtu aelewe ukweli kuhusu nyumba pekee ya Askofu Kakobe na kuwa mbali na kudanganywa kwamba Kakobe ana majumba mengi ya kifahari wakati siyo kweli!
 
Endelea kusema ngonjera huku mkeo akivishwa viremba chakavu kila kukicha na wewe ukiwa mlinzi pale nje bila malipo kweli tuna wa tz mzigo isee

Vielelezo vinajibiwa kwa vielelezo, siyo blabla kama hizi, Njia ya mwongo ni fupi!
 
Kulikuwa na kipindi cha Mkasi alihojiwa Mch. Lusekelo akasema kuhusu utajiri wake wa Magari na Majumba bila kujificha... Na akasema hana biashara... Maana yake pesa zinazotumika ni za Kanisa au Waumini... Lakini hakuwa na hofu kusema hivyo na wala Kanisa lake halijasambaratika... Watu wanaenda kanisani pale kwa hiari na kutoa kwa hiari...

Lusekelo ni Lusekelo, na Kakobe ni Kakobe!
 
Smirna, mhabarishaji na GBSS ni washirika wanafiki wa Kakobe... mmekazana kusema kwamba watu wanasema kuhusu Kakobe kumbe ni ninyi mnaofurahia Maisha magumu ya Mchungaji wenu.... Mungu awasamehe. ..
 
Lusekelo ni Lusekelo, na Kakobe ni Kakobe!
Sawa. Mimi nilikuwa nataka kujua kwanini mnajivunia umasikini wa Mchungaji wenu? Na kwa kuwa masikini Askofu wetu, ninyi
Imewasaidia nini kama washirika so kama Kanisa? Mimi nampenda sana Askofu Kakobe. Mungu amuepushie mbali na hawa waumini waovu. .. Mungu mbariki Kakobe.
 
Ishara maajabu na miujiza, siyo alama kuu ya uwepo wa Mungu juu ya Mtumishi wa Mungu. Yohana Mbatizaji alikuwa Mtumishi wa Mungu, wa kipekee sana, na Yesu anasema juu yake katika MATHAYO 11:11,"Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; ....." Hata hivyo, Yohana Mbatizaji hakuwahi kutoa pepo hata mmoja, au kufanya hizo ishara, maajabu na miujiza!
Mkuu, acha kwenda nje ya mada iliyowekwa na mleta uzi, turudi kwenye mada
.
Halafu unaponiambia nirudi kwenye MADA na kuniletea mistari ya kwenye Biblia ndio sikuelewi kabisa ni
NANI ALIYETOKA kwenye MADA mm na wewe?
mbona mnatudanganya hana nyumba wakati ana mahekalu kwa kukusanya sadaka na vidani vya kina-Mama?
\
Vielelezo vinajibiwa kwa vielelezo, siyo blabla kama hizi, Njia ya mwongo ni fupi!
Soma Isaya 42;1-4 kuhusu Mtumishi wa MUNGU
Isaya 42;2 Hatalia wala kupiga kelele wala hatapaza sauti yake barabarani

au Mathayo 12;15-21 Mtumishi mteule wa MUNGU
Mathayo 15;18Tazama Mtumishi wangu niliyemteua .......................nitaiweka Roho yangu juu yakenaye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote
Mathayo 15;19 hatakuwa na ubishi wala kupiga kelele wala sauti yake haitasikika barabarani


(Kakobe hana sifa hizo asilani kwani ni mropokaji na ni mtu anayeshindana na Dola (Ikulu, Siasa, Tanesco, Uchangzi kumpigia debe Mrema)

ASKOFU KAKOBE AKIMBIA NCHI - Global Publishers

Hili Jengo ni mali ya nani?
na ni kwanini alilibadilisha jina na ninyi Waumini wake (Walokole wa FGBH
) na kuliita "Bishop Zacharia Kakobe International Ministry"
Acheni kutudanganya ana kajumba kamoja

Exposed From The Source.....Askofu Kakobe Kuhamia America? | Sam Sasali Ze Blogger
Weekend hii Blog ikiwa katika Kukamilisha habari zake za Kichunguzi Ilibaini Mabango yaliyokuwa yameandikwa "Kama Unapenda Ukweli Unakaribishwa" yaliyokuwa Mbele ya kanisa hilo lenye Matawi zaidi ya 400 nchini Tanzania, yamebadilishwa na kuandikwa Maneno mengine yenye kutambulisha Address ya Kanisa Hilo.
Mabango Yaliyokuwa Yamewekwa Malongoni Kabla Hayajabadilishwa juzi juzi


Ndipo Blog Ikaingia katika Kusaka chanzo cha Kubadilishwa kwa Mabango hayo, Katika Kutafuta habari hizo Blog ilibadilisha mwelekeo Baada ya Kubaini Askofu Zacharia Kakobe Amefungua huduma yake "Binafsi" yenye jina la "Bishop Zacharia Kakobe International Ministry" nchini Marekani.
 
attachment.php


attachment.php



Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.


Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.


Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.


Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".


Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.


Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.

Denis Msacky akiwa gazeti la Mwananchi alitumia vijana wake waka kaa hapo kwenye nyumba hiyo wakitaka kumpiga picha Askof Kakobe lakini mda wote Kakobe alikuwa kwenye maombi ya faragha ndipo walipokuja na habari ya uongo kuwa Kakobe ametoroka na habari hiyo ikaenea nchi nzima na kuwafurahisha sana watawala .

Kwa ufupi Denis amekuwa akitumiwa na watawala wa CCM kumuhujumu Kakobe na gazeti hilo limekuwa la Kwanza kumuchafua Kakobe.

Uchafu huo umepungua baada ya Denis Kuonda Mwananchi.

Kiukweli nymba hiyo ipo moja tu na jambo hili linawashangaza watawala kwa kuwa Kakobe hana personal account Benk, isipokuwa Akaunt ya Kanisa tu.
Nyumba hiyo inafahamika na hakuna nyumba nyingine.

Hata ukiangalia nyumba hiyo ni ya chini kuliko hata nyumba za waumini wake pia.
Huwezi ukamgusa Kakobe katika masuala ya maadili na uongozi harafu ukamshinda!!

Nawapa Changamoto watawala waonyeshe hadharani nyumba anayomiliki Kakobe tofauti na hii na ushahidi wake!!
 
Mara nyingi hawa watumishi feki wanaweka pesa zao ndani,wanachimba chini kisha wanatunza madola tu.Nadhani Kakobe atakuwa na dola bilioni 1.Msanii Gwajima atakuwa na dola bilioni 2 kwa maana yeye sadaka zote anatia kwapani,hataki hata kununua eneo ajenge.mama rwakatare atakuwa na bilioni 3,Yule mwenye bank atakuwa na bilioni 5,lusekelo nae yuko nyuma yao na anawakimbiza kwa hasira atakuwa na milioni 7.Waacheni wajinga waliwe,hawajazimishwa.

Mtu aliyezoe kusema uongo hawezi kuwa mkweli, mtu aliyezoea kujilimbizia mali haweli kuamini wengine !!
Ukizoea kuibiba humwani mtu hata mmoja sasa kama wewe una ushahidi wa hayo unayosema basi tuambie hapa. Na siyo kufanya propagada ukitaja dola bilioni na kwa jinsi serikali wanavyomchukia kakobe angekuwa amekamatwa lakini hawana njinsi ndio maana wanakudanganya.
 
Ujue waumini wamepungua sana kwa KAKOBE kwahiyo promo lazima.
Mahubiri ya kakobe yamerushwa sana kwenye TV yeye hana mchezo na watu wanaocheza na dhambi neno la pale halijachakachuliwa na ndo maana watawala wanafiki hawaendi pale!!

Fuatilia sana LOWASA ameweza kugusa na kuhonga makanisa mengi lakini si makanisa ya Kakobe hapo kuna msimamo wa neno la kweli!!
 
Mara nyingi hawa watumishi feki wanaweka pesa zao ndani,wanachimba chini kisha wanatunza madola tu.Nadhani Kakobe atakuwa na dola bilioni 1.Msanii Gwajima atakuwa na dola bilioni 2 kwa maana yeye sadaka zote anatia kwapani,hataki hata kununua eneo ajenge.mama rwakatare atakuwa na bilioni 3,Yule mwenye bank atakuwa na bilioni 5,lusekelo nae yuko nyuma yao na anawakimbiza kwa hasira atakuwa na milioni 7.Waacheni wajinga waliwe,hawajazimishwa.
Kakobe angekuwa Mtumishi feki watawala wasinge yumba!
 
Back
Top Bottom