Hii hapa namba yangu.

Hii hapa namba yangu.

Joseph Isaack

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2011
Posts
450
Reaction score
89
Wana Jf habarini za asabuhi! Najuwa wote hm mmeamka vema kwa ajili ya mishemishe za j3. Nipo kwenye daladala muda natokea Mwanzacity naelekea Magu na nimekaa kiti cha nyuma kabisa. Pembeni yangu kuna bwana mmoja mtu mzima kakaa siti ya dirishani na yupo na mwanafunzi mmoja ametinga uniform anaenda shule na anaonekana kama si form one basi ni form two. Huyu bwana yuko anamsaundisha huyo dent na mazungumzo yapo hivi,.... Jamaa...vipi unaenda shule? ..dent...ndiyo! Jamaa... Unasoma wapi?...dent....Kandawe sec. Mara jamaa akaandika namba ya cm kwenye tiketi na kumkabidhi dent...namba yangu hii nitafute tuongee zaidi...dent..mi sina cm. Jamaa...aah si utaazima hata kwa rafiki yako...dent..wote hawana cm . ...jamaa...basi unaonaje tukapitiliza tukashuke magu na nitakupa nauli ya kurudia kwani mimi naenda magu...dent kainamia siti bila kutoa jibu. Mazungumzo yao yanaendelea ngoja nitawajuza kitakachotokea kama dent a tapitiliza au la,
 
SASA WEWE SI UCHUKUE HATUA? ninani unataka achukue hatua kama siyosisi twaweza
 
lijibaba lililo sahau akili maliwatoni ndo lilivyo na dent naye akili zake zaelekea huko huko bila kujali nini kitatokea mbeleni
 
SASA WEWE SI UCHUKUE HATUA? ninani unataka achukue hatua kama siyosisi twaweza

mkuu ngnja nisome kwanza misimamo ya watoto wetu, bint bado kainamia siti na jamaa badn anaendelea kumshawishi na sasa kamuahidi k umnunulia cm.
 
Daaaah!Navuta picha ya mzazi wake anavyohangaika kumtafutia hela ya kaunta buuku!

Yaani unaweza piga mtu risasi
 
Hilo toto la shule limekosa malezi bora toka kwa wazazi wake, ana kiherere.
 
Wakuu mtoto kakubali kupitiliza kituo cha shuleni kwao hebu mnishauri nifanyeje, mana wanashukia mwisho wa gari nami ndo nashukia hapohapo.
 
Mfuate huyo baba ongea naye angalau umfahamu ni nani na anafanya kazi wapi, muhakikishie umeona kila kitu kinachoendelea. mtafadhalishe amrudishe mtoto kituo cha shuleni kwao la sivyo utamripoti katika vyombo vya sheria mara moja.
 
Ungemoa za uso huyo fataki. Kwani wewe huangalii matangazo ya tv ya twaweza? Change ni wewe!
 
Mfuate huyo baba ongea naye angalau umfahamu ni nani na anafanya kazi wapi, muhakikishie umeona kila kitu kinachoendelea. mtafadhalishe amrudishe mtoto kituo cha shuleni kwao la sivyo utamripoti katika vyombo vya sheria mara moja.

Vema ngoja nifanye hivyo , lakini pale stand ya magari magu kuna kituo kidogo cha polisi, sijui niwaunganishe na mchongo huo au nyinyi mnasemaje wakuu?
 
Vema ngoja nifanye hivyo , lakini pale stand ya magari magu kuna kituo kidogo cha polisi, sijui niwaunganishe na mchongo huo au nyinyi mnasemaje wakuu?

Sawa sawa kabisa,ukifanikiwa hilo ni wazi utakuwa umeingia kwenye shindano la umemfanyia nini mtoto mwaka huu 2013. Hongera sana mkuu.
 
Change ni mimi na wewe...ebu badilika na chukua hatua fasta kuokoa mimba za utotoni et cetera.
 
Vema ngoja nifanye hivyo , lakini pale stand ya magari magu kuna kituo kidogo cha polisi, sijui niwaunganishe na mchongo huo au nyinyi mnasemaje wakuu?

Mkuu hilo ndo jibu sahihi. Ila uwe makini anaweza kuruka na maadam dent kakubali anaweza kukuruka na kusema mjomba huyo!
 
Wakuu tumeshuka hapa stand , jamaa amemchukua yule mtoto ameenda nayo kwenye kiduka fulani cha M-pesa sijui ndo anadroo pesa ya guest au vipi na mimi ndo naingia hapa polisi post huku nikiwacheck wasije nitoroka.,.nitawajuza kitakachofuata.
 
Utakua umemsaidia sana huyo bint, na wazazi wanaomsomesha, ila inasikitisha sana.
 
ww kama una muda mbona ungefuatilia ukijua waenda gesti basi ukimbie na kuchukua askari waje kuvunja mlango na kuwakamata he
 
Good move! Hongera.

Back
Top Bottom