Wana Jf habarini za asabuhi! Najuwa wote hm mmeamka vema kwa ajili ya mishemishe za j3. Nipo kwenye daladala muda natokea Mwanzacity naelekea Magu na nimekaa kiti cha nyuma kabisa. Pembeni yangu kuna bwana mmoja mtu mzima kakaa siti ya dirishani na yupo na mwanafunzi mmoja ametinga uniform anaenda shule na anaonekana kama si form one basi ni form two. Huyu bwana yuko anamsaundisha huyo dent na mazungumzo yapo hivi,.... Jamaa...vipi unaenda shule? ..dent...ndiyo! Jamaa... Unasoma wapi?...dent....Kandawe sec. Mara jamaa akaandika namba ya cm kwenye tiketi na kumkabidhi dent...namba yangu hii nitafute tuongee zaidi...dent..mi sina cm. Jamaa...aah si utaazima hata kwa rafiki yako...dent..wote hawana cm . ...jamaa...basi unaonaje tukapitiliza tukashuke magu na nitakupa nauli ya kurudia kwani mimi naenda magu...dent kainamia siti bila kutoa jibu. Mazungumzo yao yanaendelea ngoja nitawajuza kitakachotokea kama dent a tapitiliza au la,