Vijana wa namba 9, “Wazee wa chombezo kichuo chuo”

Vijana wa namba 9, “Wazee wa chombezo kichuo chuo”

Man Middo tz

Senior Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
182
Reaction score
280
STORI: VIJANA WA NAMBA WA NAMBA 9
“Wazee wa chombezo kichuo chuo”
SEHEMU YA KWANZA (01)
INSTARAM @middotz_
Whatstapp: +255 655 969 973

Chombezo ni moja ya vitu wafikiriavyo vijana wengi chuoni, hii ni kutokana na uwepo wa wadada wazuri chuoni. Kama ni hivyo basi hapa tunakutana na vijana wa tano wanaishi katika chumba namba 9.

Chumba hiki kina matukio ya utamu wa kitanda hadi kikabatizwa jina la chumba kidogo cha upasuaji.

Chumba namba 9 ni miongoni mwa vyumba 30 vilivyopo katika bweni la Serengeti.

Wanafunzi wengi hupenda kupaita kwa wanyama, jina hilo limetokana na historia ya kupendwa na wadada sana. Katika chuo kile cha social works imekua kawaida kwa wadada kuuliza jina la bweni pale atongozwapo na kama akitajiwa jina tofauti na Serengeti basi jua kabisa ni ngumu kukubaliwa.

Sifa za bweni lile maarufu kama mbugani, kwa wanyama nk zilipelekea vigori wengi haswa wale wenye uchu na chombezo kulipenda sana lile bweni.

Sifa moja wapo ni kuwa katika bweni hilo hakuna taa za nje, sifa hiyo iliwafanya wale wenye viaibu aibu kwenda kwa urahisi zaidi haswa nyakati za usiku. Pili katika bweni lile 90% wote wanamademu zao hivyo hakuna kufuatiliana, pia katika bweni hilo unambiwa hawakai wale viongozi wa dini kwasababu huko kunanuka chombezo tu.

Kiufupi bweni hilo lilikua na sifa nyingi kuhusu tamu lakini sifa kubwa ni kuwa msichana akifika hawezi kutoka salama.
Basi katika chumba namba 9 ( Wazee wa chombezo) wenyewe hupaita ofisini au wadau wengine hupaita chumba kidogo cha upasuaji. Vijana waliongoza kazi hapo alikuepo
Fred au Daktari kwa jina la utani,
kuna Denis (Msukuma)
Shaban Mkush ,
Saimon (Chuga Boy) pamoja na
Muhsin (Bichwa tango) hao vijana watano ndio walikua wanaishi hapo namba 9 au ofisini.

Vijana wao walipendana sana hadi wengi wakizani wametokea mkoa mmoja na shule moja lakini kumbe wote wamekutana hapo hapo bwenini.

Kutokana na upendo walionao ndipo wakajibatiza jina la wakush na baadae ikaja WAKUSH CLASSIC OFFICE (W.C.O) na hii ni kutokana na kuendana kitabia haswa katika mambo yetu.

Sifa zao za kutembeza bakora silipenya chini chini katika kona za chuo kile na kujikuta wakijizolea umaarufu kwa kazi ile ambayo sio iliyowapeleka pale chuoni. Siku moja usiku wakiwa wamelala wakanza kupiga stori za hapa na pale, tena muda huo ni kipindi ambacho wameanza mwaka mpya wamasomo. Basi bwana Denis aingiza mada nyingine

“Wazee tuache utani hilo kontena waliloshusha lina watoto wa kali balaa, hivi Fred umewaona?”

Denis aliuliza huku akinuka na kukaa katika kitanda chake huku akimuangalia Fred ambae yupo deka ya juu. Basi Fred nae kumbe amewaona hao watoto wazuri asemao mr msukuma, Fred akasema

“Mwanangu nikajua nimeona peke yangu kumbe ata wewe msukuma”

Fred alimjibu kwa kuchomekea utani hadi washkaj wengine wakaanza kucheka. Kama ilivyo wasukuma huwa wanataniwa sana kwa mambo ya hovyo haswa na watani zao watu wa ukanda wa Pwani. Basi wakiwa wanacheka Bichwa Tango akaanza utani akisema

“Kwaiyo bwana Fred unamaana msukuma kaona watoto wa kali”

Sasa mada ikawa juu ya kujadili msukuma wakimtania kama vile kuona watoto wa kali ni jambo la ajabu sana. Shaban mkush akasema

“Oya Fred eeh unajua jamaa juzi nilimkuta anapiga show humu ndani cha ajabu yeye ndio analia hahahah… yani wasukuma bhna Mnafeli wapi”

Daah! Mkushi aliwacha hoi watu wote kwa kicheko mle ndani, Room ile kwa kawaida huwa hawalai mapema kutokana na mada zao za ajabu ajabu za utani.

Baada ya kucheka sana pale lakini bado Msukuma alikua amang’ang’ania ile mada yake akasema

“Tuacheni utani kikuweli kuna mtoto nimuona aisee lazima nimpate, anakaa Dorm la meru, Fred kesho utanisindikiza mwanangu nikakuonyeshe kwanza wewe si Dokta wa haya mambo”

Fred (Dokta) akashtuka kusikia hivyo kwasababu sio kawaida ya Mr Msukuma kushadadia jambo hivyo.

“Huyo mtoto atakua kweli mkali hadi wewe unataka kunionyesha, kwanza umemuona wapi” Fred alimuliza msukuma

“Nimemuona Lecture 1 wakati najisomea, yani Fred huyo mtoto ukimuona mwenyewe utakubali”

Siamon (Chuga boy) muda wote wenzake wanamtania msukuma yeye alikua kimya lakin safari hii akaja na lake jambo hadi akamtisha kidogo Msukuma.

“Wewe Denis unaenda kumuonyesha Demu Fred umesahau kuwa huyo anatokea Tanga hee! Yani huyo unaeda kumpa demu na sio kumtambulisha hahahah! Hembu muulize Dani kilichomtokea asee”

Chuga boy aliongea kwa lafudhi yake ya kaskazin kwa mkazo kabisa lakini Fred akamtatisha chap.

“Oya chuga acha kumzingua Chalii, ukaacha asinitambulishe shemeji. Oya Denis asikudanganye huyu mmeru kwanza nitambulishe ndio vizuri maana usiponitambulisha siku nikimuona afu sijui kuwa ni wako ndio napita nae kwanza mi mwenyewe napenda vitu vizuri”

“Aah! Mi siogopi wala nini kesho nakutambulisha hivyo hivyo”

Denis Msukuma alijibu huku akionyesha kujiamini ingawa alitishika kidogo.

Mara Bichwa tango nae “Oya wadogo zangu zima taa ni muda wa kulala saa nne saiv”

“ aaah! usituzingue bhn kama unalala lala tu”

wakashkaji zake wote walijikuta wakimjibu kwa pamoja. Muda huo huo Mkushi akaingiza utani kwake

“Oya Msimlaumu sana unajua hawa watu wa kibiti waliathirika kidogo na yale matukio, yani saivi huwezi amini hawa jamaa hawajawahi kukwich kwich kwa miezi yote ile, hapo alipo msukuma kataja tu kakutana na demu mkali yeye kadindisha hahahahah!”

basi baada ya utani ule wengine waliendelea na stori za hapa na pale hata muda wa kulala haukujulikana walikuja kustuka tu ni ile asubuhi.


Basi walivyoamka tu wakastuana wote kwa pamoja wakaamka wakanza kwenda kuoga maana siku hiyo ilikua ni siku ya kuanza masomo.

Lengo alao siku hiyo wawahi mapema kuingia Lecture ili kila demu mkali atakae ingia wathaminishe wenyewe, kwani Chombezo ndio ilikua kazi yao.

Kweli wakawahi kufika wakawakuta washikaji wawili na wao wakawa 7.

Walichokifanya wakatulia zao nyuma ili kuwapimia, Aloo dakika mbili sio nyingi wakanza kuingia.

Sasa wazee wa chombezo wakawa wanakodoa tu macho kusoma vichenchede vipyaa.

Baada ya lecture kujaa akaingia Lecturer mmoja hivi anaitwa Dkt Makulile pindi la PPM likaendelea lilipoisha tu ikatoka hapo hapo Assignement

“Assingment hii ni ya kuchapa Limit 4 pages plus refecence n cover page, sawa”
ilikua ni sauti ya Dkt Makulile akasema

“CR after three days nikute kazi yangu ofisini”

Basi baada ya kutolewa ile assignment wazee wachombezo wakatazamana kisha wakatabasamu. walijua hiyo ni fursa kwani wanafunzi wengi wapya hawana PC [emoji335] na computer lab kunakua na jam mnoo hivyo ni lazima watawapata tu.

Sasa Fred akiwa ametulia zake kwa pembeni kulikua na dada mmoja hivi mzuri mweupee, yule dada akamstua ile kugeuka anakumbana na sauti nzuri.

“ Hi! Sorry kaka eti hii kazi inachapwa kwa PC?”

“Ndio kwa PC, mbona kama unahofu hivi nin shida?” Fred alimuliza yule mrembo

“Ndio ninahofu kwakua sijawahi kutumia PC kufanyia kazi, unajua form six hatutumiagi kabisa, hivyo kazi tunafanya kwa mkono tu, nimeona unayo PC kwa begi yako naomba unielekeze tunaiadinkaje na mpaka upate reference”

(Moyoni Fred akajisemea ‘Fred leo nimeapata zali’) ooh! Basi Hapo hapo Kichwani mwa Fred kulikuja wimbo wa Proffessa Jay ft Juma nature ujulikanao kama zali la mentali. Basi akampanga mtoto akamwambia

“chukua namba yangu coz lazima tuelekezane sehemu iliyotulia kidogo, kwanza unakaa dorm gan?” akasema

“Meru namba 9”

“waooh! Namba za vyumba zinafanana, mi nakaa Serengeti namba 9, so unaweza kunicheki mida ya saa 10 ukafika kule room, andika namba yangu 655 969 973” mtoto akasema

“Sawa nashukuru sana”

Fred akacheka na kushangilia kimya kimya maana huyo atakua ameisha iyo….ITAENDELEA.

UNAJUA KITAKACHOTOKEA HIYO SAA 10? TWENDE PAMOJA UKAONE SHUGHULI YA CHUMBA NAMBA 9.

NUKUU “Maisha ya chuo yapo yatofauti tofauti wengi wao bila kutarajia wakifika chuo hujikuta wanaishi maisha kama ya hawa vijana wa namba 9 wajiitao Wakush, utaburudika na utajifunza pia”
MAJUTO NI MJUKU.

@middotz_
UTACHEKA NA KUFURAHI, UTAJIFUNZA PIA, JARIBU KUFUATILIA.
1671625298973.jpg
 
Jitahd ukiandika story yako,,
Malizia kabisa tuwe huru kuchangia pande zote za Uzi wako, mwanzo,Kati na mwisho.

Ukiandika "itaendelea" afu story imeishia katkati, tunashindwa kuelewa lengo la Uzi wako Ni Nini na uko utakakoendelea kutakua na Nini.

Utazua maswali,kejeli na matus yasio kua na msingi kwny Uzi wako.

Humu Jf tumetofautiana sn jins ya mapokeo na response kwenye nyuz mbalimbali zinazoenda kinyume na hobbies zetu au matarajio yetu.

(Ni ushaur TU, No offense intended [emoji4][emoji120])
 
Jitahd ukiandika story yako,,
Malizia kabisa tuwe huru kuchangia pande zote za Uzi wako, mwanzo,Kati na mwisho.

Ukiandika "itaendelea" afu story imeishia katkati, tunashindwa kuelewa lengo la Uzi wako Ni Nini na uko utakakoendelea kutakua na Nini.

(Ni ushaur TU, No offense intended [emoji4][emoji120])
Pamoja
 
Back
Top Bottom