Hii dhana kwamba walimu hawazeeki ina ukweli wowote?

Hii dhana kwamba walimu hawazeeki ina ukweli wowote?

Labda mazoezi wanayofanya walimu kila siku yanawapa uimara na kuwafanya wasichoke mapema.

kusimama zaidi ya saa 2 kwa siku 5 mpaka uku wakitembea tembea darasani wakati wanafundisha,kuongea kwa zaidi ya masaa mawili kwa siku 5 mpaka 6 sio mchezo ni mazoezi tosha.
Inawezekana inawasaidia wawe na afya njema lakini sio kama inavyoelezwa
 
nafikiri huo msemo una ukweli ndani yake, kwa maana ukiangalia kwa undani utaona kwamba zamani walimu ndiyo moja kati watanzagiza wachache waliokuwa na ajira ya uhakika i.e ambao walikuwa na uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi na wengi walikuwa huko wilayani wengine vijijini sasa huko wilayani kulipwa mshahara kila mwezi wa uhakika ina maana una weza ku-afford vingi ambavyo wananchi wengi ambao hawana kipato cha uhakika kila mwisho wa mwezi hawawezi.

unaweza kula vizuri au kubadilisha menu kununua vipodozi sasa hii yote inawafanya walimu waishi maisha bora klk wazazi wa watoto wanaowafundisha, hivyo kuna ukweli waliosema walimu walikuwa hawazeeki ...
 
Inategemea na lifestyle yako, kuna kijana wa miaka 20 ila ukimuona kama ana 45
Na hili ndio jibu. Walimu hasa miaka ya zamani wakati tunasoma walikuwa na simple stress-free lifestyle ambayo ilisababisha wasizeeke haraka.
Kuzeeka sio umri tu, mnaweza kuwa wote mko 50yrs lakini mmoja akaonekana kama ana 60 kwasababu ya mambo ya kimaisha.
 
nafikiri huo msemo una ukweli ndani yake, kwa maana ukiangalia kwa undani utaona kwamba zamani walimu ndiyo moja kati watanzagiza wachache waliokuwa na ajira ya uhakika i.e ambao walikuwa na uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi na wengi walikuwa huko wilayani wengine vijijini sasa huko wilayani kulipwa mshahara kila mwezi wa uhakika ina maana una weza ku-afford vingi ambayo wananchi wengi ambao hawana kipato cha uhakika kila mwisho wa mwezi hawawezi, unaweza kula vizuri au kubadilisha menu kununua vipodozi sasa hii yote inawafanya walimu waishi maisha bora klk wazazi wa watoto wanaowafundisha, hivyo kuna ukweli waliosema walimu walikuwa hawazeeki ...
nakwede97 pale juu kasema wanaishi kwa nidhamu sana kwa sababu wana kipato kidogo na wewe hapa unasema hawaonekani kuzeeka kwa sababu ya kipato cha uhakika. Jibu sahihi ni lipi?
 
Na hili ndio jibu. Walimu hasa miaka ya zamani wakati tunasoma walikuwa na simple stress-free lifestyle ambayo ilisababisha wasizeeke haraka.
Kuzeeka sio umri tu, mnaweza kuwa wote mko 50yrs lakini mmoja akaonekana kama ana 60 kwasababu ya mambo ya kimaisha.
Mimi nadhani hii inawahusu watu wote wa zamani na sio walimu pekee.
 
Nature ya kazi yao unaweza kuwafanya wasizeeke au kuchoka mapema, kusimama muda mrefu, kutembea kwa miguu sana...na activities kama zingine zinazohusisha movements
Nadhani hii inawahusu pia watu wa afya pia hasa wauguzi maana nao kazi zao zinahusisha kutembeatembea, watu wa kwenye majeshi pia walitakiwa ndio wawe wanaongoza kwa 'kutokuzeeka'. Kwa nini walimu tu?
 
Wale waalimu wa kweli kweli. Hata akistaafu, wanakua na nuru hawachoki na kuchakaa kama sekta zingine. Nafikiri ile kazi ina baraka zake na haina stress.

Hawa wa siku hizi siwezi kutia neno.
Mimi nilifikiri walimu wa sasa ndio hasa wenye wito, maana kuna taaluma kibao za kuchagua hivyo mtu akichagua ualimu anakuwa amependa kweli tofauti na zamani mtu anapangiwa tu kwa kwenda 🤣
 
Back
Top Bottom