Hii bahati au mkosi?

Given Edward

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
850
202
Mida ya saa 12 jioni jamaa kahangaikia gari(daladala) hadi kapata. Kaingia ndani na 500 tu mfukoni halafu ndani wamebanana kiasi kwamba hata kunyanyua mkono wala kujikuna mtu hauwezi.Unaona bwana!
Konda kapita kaanza kudai nauli.Jamaa kaingiza mkono mfukoni, katoka na 10,000.Jamaa kashangaa wee lakini kamshukuru MUNGU kwa baraka hiyo.
KUMBE JAMAA KAINGIZA MKONO KWENYE MFUKO WA MTU MWINGINE!!!!
:embarrassed:

Konda kamrudishia chenji yake jamaa bado anamshukuru MUNGU tu halafu akashuka haraka haraka kwenye kituo hata sio chake. Ile kujisachi jamaa kajikuta na jero lake lile lile!
KUMBE KWENYE KURUDISHA MFUKONI KARUDISHA KWENYE MFUKO WA MTU MWINGINE!!!
 
hahahahah hii kali,bora lakini alivyoikosa hata kama atakuwa hajairudisha kwa muhusika:coffee:
 
si ndo hapo sasa,unajua alipaswa aupate utamu pale ambapo angekuta na yakwake imechenjiwa
 
Madam mia tano yake bado ilikuwepo basi hiyo ni bahati, kwa maana alijilipia nauli kwa kutumia pesa ambayo si ya kwake....

Ila simpatii picha mwenye elfu kumi (kama pesa ilirudishwa mfukoni mwake), anaweza kudhani kuna vibaka wamemwibia hela halafu wakamrudishia chenji.....:bump:
 
Hehehe tamu hiyo!Bora angebaki afike alipokua anaenda angesevu 500 yake ila sasa hapo lazima ilimbidi kuitumia ili afike alipokua anaenda!
 
Hahaha sijui tuiiteje mana lazima mia 5 yake itatumia kwakuwa ameshuka kituo si chake afu yaonekana jamaa hakuwa na nia njema(Mwivi) mana alitegemea hela iingeingia kwenye mifuko yake kwa mazingaombwe
 
hahahahaa.., jamaa hakutoa machozi kweli? maana alishajihakikisha :popcorn::popcorn: kwa week nzima
 
hahahaa! Sasa ingependeza na yy akute jamaa alikosea mfuko akachukua jero yake na kurudisha chenji.
 
Madam mia tano yake bado ilikuwepo basi hiyo ni bahati, kwa maana alijilipia nauli kwa kutumia pesa ambayo si ya kwake....

Ila simpatii picha mwenye elfu kumi (kama pesa ilirudishwa mfukoni mwake), anaweza kudhani kuna vibaka wamemwibia hela halafu wakamrudishia chenji.....:bump:
hahahahahahaha nimecheka sana Mkuu Tanmo
 
Eee bwana eeh, Amejifunza asiwe anatumia kisicho chake, alichotakiwa kufanya ilikuwa kuirudisha ile shs. 10,000/= mfukoni na kutoa shs. 500/= lazima asingekosea tena, ingekuwa riziki mintashaara!!! Jibu ni kwamba alipata bahati halafu ukafuata mkosi.
 
Aiseee hiyo kali lakini kama ni mimi siwezi kujilaumu kwa mkosi huo bali nitajua nimesafiri bure tu kwa route hiyo!
 
Du bora hapo alipofika atembee kwa mguu km karibu au aishikilie hiyo 500 mkononi, ni balaa na si bahati siku iyo kwake
 
hiii kali aisee, mi sipati picha yule jamaa aliyechenchiwa akifika akakuta chenchi wakati kulikuwa na buku kumi kamili, atawaza sana asipate jibu!
 
Back
Top Bottom