Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Kama ilivyo kwenye sheria za bofi ya mikopo, kila mnufaika atapewa kiasi kinachoendana na siku alizokaa chuoni.
Hapo awali kabla ya Corona, boom moja ilikuwa 505,000 hadi 520,000 lakini kwa mfumo huu itakuwa pungufu.
Je, kama boom limepunguzwa, vipi kuhusu ada na direct cost? Vilipunguzwa kulingana na siku za masomo?
======
Soma ufafanuzi uliotolew na Bodi ya Mikopo:
= > HESLB: Hatujapunguza mikopo ya Wanafunzi. Tunatoa fedha za kujikimu kulingana na siku za masomo
Hapo awali kabla ya Corona, boom moja ilikuwa 505,000 hadi 520,000 lakini kwa mfumo huu itakuwa pungufu.
Je, kama boom limepunguzwa, vipi kuhusu ada na direct cost? Vilipunguzwa kulingana na siku za masomo?
Soma ufafanuzi uliotolew na Bodi ya Mikopo:
= > HESLB: Hatujapunguza mikopo ya Wanafunzi. Tunatoa fedha za kujikimu kulingana na siku za masomo
Baadhi ya Michango ya Wanachama Waliochangia huu Mjadala
HESLB wamesema sababu ya kupunguza boom ni kwamba eti muda wa masomo kwa semista hii ni mdogo sana
Je, kama boom limepunguzwa, vipi kuhusu ada na direct cost? Vilipunguzwa kulingana na siku za masomo?
Kama ndo hivyo serikali inakwama wapi kutoa muongozo kwa vyuo kwamba wanafunzi wapunguziwe ada Mfano wanasema semista hii ni fupi sana hata miezi mitatu haifiki sasa kwanini na ada isipunguzwe?Kwanini watu wapunguziwe maboom lakini pia wasipunguziwe kiasi cha ada kwa muhula huu?
Mimi naona kama wanafunzi wamepunguziwa boom kisa ufupi wa semista basi na ada ipunguzwe maana unakuta chuo ada milioni 3 sasa nusu muula ni milioni 1.5 sasa kwanini mtu alipe 1.5 kama nusu muhula wakati muhula ni mdogo wa miezi 2 na siku chache tu?
Kama wamepunguziwa boom la muhula huu basi na ada ipunguzwe tu maana nina uhakika kuna wanafunzi wengi tu ambao wanatumia boom lao kulipia ada maana sio wote wana asilimia mia moja
Mkuu Kuna sehemu gani kwenye mkataba pameandikwa kuwa pesa ya chakula italipwa kwa semester? Nayo imekuwa Ada?
Mkataba upo wazi kabisa kuwa pesa ya chakula na malazi italipwa kwa Siku ambazo mwanafunzi atakapokuwa masomoni, Sasa Kama mtu anaondoka chuoni August mwishoni unataka apewe pesa ya kujikimu Hadi ya mwezi wa kumi wakati hayupo chuoni kimasomo?
Kuhusu kupewa taarifa ilishatolewa zamani Sana kwenye mkataba Kama mtu alisoma mkataba vizuri na kuuelewa kabla ya kuomba mkopo hawezi shangazwa na mabadiliko haya.
Halfu hajaandikwa kwenye mkataba kuwa pesa ya chakula itatumika kulipa ada Bali hayo Ni matumizi ya mtu binafsi Ila matumizi elekezi ya hiyo pesa Ni chakula na maladhi tu. Ukiitumia kulipia ada, usafiri, kununulia viwalo, kuhonga na n.k hiyo Ni juu yako na Wala siyo wao.
fafanua na ulipaji wa hilo deni... na ile jumla ya pesa wanazoonyesha kwenye account ya muhusika...
je kama kwenye account inaonyesha una jumla ya 3459000 na jumla ya pesa ya kula ikiwemo...
na kwa situation iliyotokea hilo deni linakuwa hivyo hivyo kamili ama kunakuwa na deduction ya hiyo pesa walioipungiza..????
Sent using Jamii Forums mobile app
Naona kitendo cha bodi kimeamsha ari ya wanafunzi vyuoni na vyuo vingine hadi washaanza kupanga maandamano ya amani
Picha ya kwanza ni chuo cha uhasibu Arusha ambapo wanafunzi wanapanga kuandamana
Sio hivyo tu kuna vyuo vingi sana wamepanga maandamano yaanze na hii yote ni kwasababu ya ya mambo ya ajabu yanayofanywa na bodi ya mikopo
Wanafunzi wengine wamepewa laki 1 tu eti ndo boom la kujikimu na sio laki 5 tena halaf siku za kurejesha mkataba unawaforce warejeshe laki 5
Nimeattach na video ya wanafunzi wa udsm pia wakijiandaa kwa maandamano ya amani
Maandamano ya amani ni haki yao ya msingi kama litahitajika kufanyika hivyo
View attachment 1514540View attachment 1514547
View attachment 1514551