Heshima kitu cha bure tumheshimu Raisi wetu

Heshima kitu cha bure tumheshimu Raisi wetu

mafurikoyamoto

Senior Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
160
Reaction score
53
Nimelazimika kuanzisha hii thread baada ya kuona watu wamesahau kuwa rais ni kiongozi mkuu kuliko wote katika nchi yoyote hapa duniani.

HIVYO basi tuna wa jibu si tu kumheshimu ila pia kumsaidia kulinda heshima yake daima.

Hakuna asiye juwa kuwa sisi wenyewe ndio tulimchagua kikwete kwa Kura nyingi huku tukiwa na akili timamu na bila kushawishiwa na mtu yeyote iwe kwa fedha au maneno.

Sasa kama tulikosea aibu ni yetu sisi wenyewe na haina maana sasa kuanza kumdharau kumkejeli au kumkosea heshima prof. Kikwete.

Mbona marekani china na nchi mbali mbali anaheshimika ? Mbona vyuo mbali mbali vinamtunuku shahada kila kukicha?

Sasa iweye sisi tusimheshimu?

Hili ni kosa pia ni dhambi kwa kuwa hata biblia inasisitiza tuwaheshimu viongozi wetu.

Pia tuache kumwita rais majina yasio faa

Mfano

Mh.tezi dume

Prof. Wa kichina

Naomba tubadilike.
 
angekuwa anataka apate heshima asingelea wezi wa EPA,RICHMOND,Escrow,Rada,ndege ya rais
wakurugenzi wa mikoa kama mwanza wameiba 43 Bl na anacheka cheka tu!!?
siwezi kumuheshimu kikwete!!
 
angekuwa anataka apate heshima asingelea wezi wa EPA,RICHMOND,Escrow,Rada,ndege ya rais
wakurugenzi wa mikoa kama mwanza wameiba 43 Bl na anacheka cheka tu!!?
siwezi kumuheshimu kikwete!!
Nchi inaongozwa kwa misingi ya demokrasia. Kama mnaona wana makosa muwapeleke mahakamani
 
Moja ya PHD alizonazo Mr. Kikwete ni ya Uhusiano wa kimataifa aliyoipata Faith University ya Uturuki but nadhani huyu bwana anatambulika kimataifa kuliko kwenye nchi yake,

kwa maneno machache unaweza kusema Kikwete ni Rais wa Kimataifa,ukienda mbali zaidi unaweza kuona ni Rais asiye na mipaka ya Utawala...Yes! Anaongoza taifa gani?
 
Heshima inaanzia kwako kabla watu hawajakuheshimu. Kwa tanayoendelea nchini huwezi kutegemea watu wamuheshimu JK. Wale wanafiki na wanaofaidika na madhambi yake ndo wanamuheshimu.

Ni Siku gani JK amesimama km baba mwenye nyumba na kutoa maagizo ambayo taifa lilitikisika kwa kweli mzee kasema? Ni hakuna. Na madhambi mengi yanaendelea nchini alafu huyo ndo aheshimiwe?
 
Kama unampenda sana mwambie aje mwenyewe,sio kujificha nyuma ya wazee.sidhani kama anajiheshimu asingeweza kumwambia Tundu Lisu ni mzandiki
 
Kumbe kumheshimu mtu ni kutomwambia ukweli!!!?
 
Haaaaaaahhh alikuwa Dr..and now he is Prof....!!! Kwangu hainuhusu kabisa labda aishie huko2 anakopewa hizo title...and hate green colour
 
Ni changamoto sana kuheshimika na jamii kama utashindwa kuilinda heshima,kama kuwa mtovu wa maadili au mwizi wa mali za umma.
 
Akijeheshimu, ataheshimiwa. Ametufikisha mahali tunaona aibu kujiita watanzania.
Heshima si zawadi hupatikana kwa kuifanyia kazi.
 
Mi sijui bana........kama namheshimu au simheshimu........nitajua zaidi 2015 October huko..........
 
Back
Top Bottom