HESABU kitu cha ajabu

Duhh ulikasirishwa na kitu gani?

Huyu mdogo wangu hawezi ni mstaarabu huwezi amini nilikuwa nikipika ataosha vyombo, na nyumba anadeki! Kwa mziki wa mama yangu sidhani kama atathubutu! Hizo hekaheka tunaziweza mimi na anayenifuata ndio tulikuwa wa moto! Ila huyu hawezi bana..

Hapa tu nimemwambia afikie kwangu naona anasitasita, anaulizia tu hostel za chuo😊
 
Masoma siyo magumu ila yanafanywa kuwa magumu makusudi na walimu.

Siku ya kwanza mwalimu akiingia lecture room anawaambia kabisa atawakamata nusu ya darasa.
Mwl anaona sifa kufelisha
Shetani ana mawakala wake kila sehemu!
 
Elimu ya bongo jau; kuna kipindi wakaweka Physics na Chemistry kuwa somo moja, inasikitisha sana bongo hii.
unified science hiyo..mambo ya Joseph Mungai😅😅😅😅Ukiniwekea hesabu kwenye somo lolote basi ujue nimefeli. Sijawahi kujua hesabu na ilifika kipindi nikakubaliana na hali na nikaliweka pembeni kabisa. Nikawa nalamba miswaki tu mpaka Necta.
 
Bora akae hostel.
Alikuwa anapendaga kunionea, na hiyo siku nilikuwa nimeamka vibaya.
 
Kufika tu Kwanza chuoni nakuta watu wanakimbia hovyo kwenye korido wanaenda darasani, usiku naona mbona taa watu hawazimi Kila nikishtuka nakuta watu wanasoma na Ku solve tu, nikaona huu ujinga, nikahama chumba, nilihama vyumba kama vitatu hivi, mwisho nikapata chumba na room mate wa kufanana nao.

Tulikuwa watatu chumba kimoja, Mimi nlikuwa nikisoma Sana ni lisaa limoja tena ni Kati ya Saa moja Hadi mbili usiku na vipindi vikiwa vinaendelea Hadi huo muda basi ndio sisomi tena had kesho, wale Jamaa zangu wawili mmoja akitoka class anaenda kushinda kanisani anaimba sijui kwaya mara mkesha, akirudi kachoka basi analala tu na mwingine yeye anavutaga bangi chooni (bafuni) au nyuma ya bweni akimaliza anarudi kulala.

Maisha yalikuwa ni hayo, tulikuwa tuna share masomo ya hesabu lakini hakuna hata siku tuliokaa tuka solve pamoja. Jirani zetu walikuwa watu wa kanda ya ziwa, nafkir ni wasukuma au watu wa mara na niliwavulia kofia, wale Jamaa hata ukiamka Saa nane usiku Wana solve tu Hadi siku nikawaibia taa na switch maana walikuwa na kelele vibaya mno usiku...

Hakuna hata mmoja Kati yetu aliyewahi kufeli japokuwa Yule mwenzetu mmoja mvuta bangi (Martin) baadae kwenye harakati za maisha alichanganyikiwa sijui walimfanya nini huko kwao Machame but he was one of the best ever, akishika kalamu jua haitui chini, akiweka kalamu chini Jua kamaliza mtihani, he was very fast kwenye paper hasa hesabu, huwezi kuamini ukioneshwa huyu alishapataga A's, kawa kichaa kabisa.
 
🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…