Ulifanya ACSEE ukapita vizuri. Maths ukapata Aπ
Kwa sababu wewe na hesabu mlikuwa kama mapacha waliozaliwa siku moja, ukaamua kuingia university uchukue Statistics, Pure Mathematics na kila course yenye namba ndani yake. π
Ukasema:
βMimi si fala bana. Dunia inahitaji kujua uwezo wangu.β π
Semester ya kwanza ikaenda vizuri tu.
Semester ya pili ndiyo Mungu akaanza kukufundisha humility. π₯²
Kijana wa wenyewe akaanza kunywa dawa za ulcers. π₯΅
Usingizi ukawa unaupata kwa msaada wa sleeping pills. π
Ukikaa anawaza derivatives.
Ukioga anawaza probability.
Ukilala anaota matrices. ππ
SECOND YEAR:
Hapo sasa ndipo degree inaanza kukutengeneza upya. π
Lecturer anaingia class, anaanza kuongea kama ana-communicate na viumbe wa sayari nyingine. π½
Unaangalia boardβ¦
Unaangalia lecturerβ¦
Unaangalia notesβ¦
Unaangalia rafiki yakoβ¦
Kila mtu ana uso wa:
"Broβ¦ tunaelewa kweli?β ππ
Unaamua kuuliza swali.
Lecturer anakasirika:
βI have already explained this!β π€
Na moyoni unasema:
βProfessor, hata wewe sijui kama umeelewa unachotufundisha.β π
Nilipofanya ACSEE nilikuwa na A ya Maths, nikaingia university nikachukua kila kitu kilichokuwa na hesabu ndani yake kwa sababu nilijiona mimi ndiye BABA WA MATHEMATICS. ππ
Mwaka wa kwanza haujaishaβ¦
Miwani tayari.
Machoni unaona equation hata ukiangalia kuku.
Na ukifika Level 3 Calculusβ¦
Hapo sasa siyo tena education. Ni spiritual warfare. ππ
Calculus Level 3 inaweza kukufanya uanze kufikiria:
βLabda nilizaliwa kwa ajili ya kilimo.β ππ
Probability nayo usiichezee.
Inaweza kukufanya upungue kilo bila hata kwenda gym. ππ
Nadhani wanafunzi wa Engineering nyinyi mliona mengi kwenye lecture halls. ππ
Ukisikia mtu anasema:
βNinateseka na SMA 401β¦β
Usimcheke, mwangalie kwa huruma. π
Kwa sababu huyo amebaki kidogo tu
Mabingwa wa hesabu hali ilikuaje huko?
Matatizo ya kusoma kikoloni haya, siku hizi kila kitu cha Stanford na MIT kiko Youtube na zaidi preprint papers zipo
www.arxivx.org , unajifunza huku una pause unavyotaka.
Mfano, calculus si ngumu hivyo, ila kuna hesabu kama za factoring, function, trig identities etc, usipozijua, halafu ukalazimishwa kukariri derivative na integral bila kuelewa ni nini, kuelewa calculus ni vigumu.
Tatizo Tanzania kuna watu wanasoma calculus mwanzo mpaka mwisho, ukimuuliza hizi hesabu ni za nini, nielezee kwa lugha nyepesi hata kwa Kiswahili tu, hawawezi kukuelezea. Hawajaelewa, wanakariri.
Tatizo ukiwa unasoma huku una majukumu ya familia hesabu huwezi kuzielewa.
Ukisoma huku unafukuzia wanawali huwezi kuzielewa.
Ukisoma huku unafakamia pombe huwezi kuelewa.
Ukisomeshwa na ma profesa wanaotaka kukukomesha huwezi kuelewa hesabu wala somo lolote.
Ukisoma huku una njaa hujui mlo utatoka wapi, huwezi kuelewa.
Ukisoma kwa kupanda daladala vikumbo vya watu tu vinaondoa ulivjojifunza.
Hesabu zinataka utulivu, kazi yako iwe shule tu, ikibidi uwe kama mfungwa fulani wa hesabu unajiondoa akili kama Grigori Perelman.
Yani wenzako wanaangalia mpira huko, wanafukuzia mademu, wewe una solve ma Riemann Zeta function.
Unakuwa mtawa wa dini ya hesabu.
Wengi hawawezi nidhamu hiyo.