melxkb
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 206
- 56
Ndg ZZ Kabwe,
Asante sana kwa kutupa furaha na amani kwa mananeno machache yenye ujumbe mzito. Hakika ni faraja kwetu wote wapenda mabadiliko hasa wana-CHADEMA, nakuomba sana ujitahidi kujitambua nafasi yako uliyo nayo hasa katika kuhakikisha ustawi wa CHADEMA ambacho hakika ni chama mbadala wetu tunaonyonywa na na kuibiwa tena kwa jeuri na serikali ya kikoloni ya CCM.
Jitahidi kuepusha rapsha rapsha katika chama na sasa uungane na wenzako kuimarisha M4C na mengineyo, penye utata ebu ongea na wenzako vizuri kama kiongozi ukijua kuwa nao na binadamu na wote mnaongoza mapambano kwa pamoja. Ni kweli kaka yetu Zitto mioyo ya wengi hasa vijana uliiumiza sana lakini sasa ni kweli tumeukubali ustaarab wako wa kukiri kutukwaza na kuomba msamaha hadharani lakini naomba ujue kwamba bado unahitaji kututhibitishia kiutendaji ili tuweze kurejesha imani yetu kwako kivitendo pia bila kusitasita ili yasiwe maneno tu.
Mwisho nakuomba utusamehe na sisi pia maana peenye manunguniko pana kujibizana na kufokeana, hivyo kuna wakati na sisi tulikukosea na kukukwaza, UTUSAMEHE KAKAETU. Bila shaka unajua mtu akikuamini halafu akaona kama unamsaliti hulalamika na kunungunika sana.
Hongera na asante kwa muhtasari wa kazi za 2012 na ufafanuzi wa mikakati ya 2013 - TUKO PAMOJA.