Heri ya mwaka mpya 2013! Nawashukuru, Nawaomba radhi!

Status
Not open for further replies.
Hongera sana mh heri ya mwaka mpya na wewe pia naomba tuanze mwaka mpya kwa kusameheana kwa kila tulipokosea mwaka 2013 uwe ni wa kujenga chama kujiandaa na uchaguzi wa 2015
 
Mkuu umetumia busara kuomba msamaha, binafsi ulinikera sana kwa kuanzisha mjadala wa urais ndani ya chama chetu wakati ambao kwetu mjadala huo haukuwa kipaumbele kabisa.

Mimi ni mwanachama niliye na shughuli zangu nje kabisa ya siasa, lakini kwa uzalendo wangu naliona tumaini jipya laTanzania niitakayo ndani ya CHADEMA. siyo kwamba chama hiki hakina kasoro ila kwa sababu kimejiweka kwa namna ambayo kinaitika matakwa ya umma. Ni kwa msingi huu basi kila anayeonekana msaliti ndani ya chama hiki namuona kama adui namba moja wa nchi yangu na ni lazima huyo pia atakuwa adui yangu.

Nina ukubali msamaha wako kwa masharti makuu mawili;

1) Anza sasa kuzunguka nchi nzima na makamanda wengine kukijenga chama kupitia M4C (na tafadhali usithubutu kuitumia M4C kurudia makosa yaliyopita (kutangaza kugombea urais.katika hili sina tatizo na wewe kugombea nafasi hiyo lakini kwa hakika kwa sasa hili litatugawa zaidi ya kutuleta pamoja kama chama.nafikiri utakuwa umeiona impact yake ilivyo mbaya haishii kutugawa kama chama lakini pia inaenda mbali zaidi kwa kuzua hisia za ukanda/umkoa (kigoma Vs mikoa mingine) na udini pia.

2) Nieleze kwa nini wakati wa kampeni za mwaka 2010 watu tukiwa busy kumkampenia mgombea urais aliyepitishwa na chama wewe ulitoa kauli za kuutaka urais 2015. Je, hii haikulenga kuwakatisha tamaa wananchi kwamba tuna uhakika wa kutokushinda nafasi hiyo? (Katika hili hata baada ya kujibu ushauri wangu kwako uko hivi; wakati wa shughuli inayotuhusu wanachama wote toa kauli inayunga mkono kile kinachofanyika na chama kwa wakati huo, then hayo mambo binafsi yakifika wakati wake kwa baraka za chama tutakuunga mkono.

NB: NATEGEMEA MABADILIKO MAKUBWA BAADA YA MSAMAHA HUU. HERI YA MWAKA MPYA KWAKO PIA KAKA.

HERI YA MWAKA MPYA KWA WAZALENDO WOTE (HATA WASIO NA VYAMA) KWA PAMOJA TULIJENGE TAIFA LETU KILA MTU KWA NAFASI ALIYONAYO.
 
Mh. zitto,

Kwa kweli, mimi ni miongoni mwa watanzania wengi - makumi, mamia, maelfu, malaki, mamilioni - ambao tulikuwa tunakerwa na wewe. Ulitukera kwa mengi, lakini machache ni ile hali ya ukinyonga wako. Ukigeugeu katika mambo mengi. Leo kusema hivi, na kesho kusema vile (rejea post iliyowekwa hapa siku za karibuni ikinukuu mmsimamo na mtazamo wako juu ya Kafulila, Umiliki wa magari n.k.). Pia namna ulivyoshindwa kuwakemea wale vijana waliokuwa wanatumia jina lako vibaya; huku wakishambulia wazee wa chama.

Yaliyopita si ndwele.

Kama kweli radhi hii unaiomba kutoka katika uvungu wa moyo wako, mimi nimekusamehe. Na wengi wamekusamehe.

Badilika. Mwaka 2013 na kuelendelea tuko ki-dijitali zaidi; tuachane na analojia; tuachane na kusifiwa na kupewa kichwa na wana Analojia : Ritz, zomba, chama na akina Taswira, WABHEJASANA etc.

Heri ya Mwaka Mpya 2013 Mheshimiwa..!
 
Last edited by a moderator:
umerudisha imani yngu kwako!! naomba 2013 msituchanganye tena. kep movng zitto 4 chadema en al tanzanian pple

happy new year!!!!
 
I see, wanasiasa wachache wa kuandika hivi! Kuna sehemu ulinikera kweli, apology accepted!

Happy New Year 2013
Hata mimi nimefurahishwa na maneno ya Zitto na kweli nimemsamehe....

Kwa vile amesema kuwa kajifunza mengi, namwomba adhamirie kubadilika kweli na mwaka 2013 apunguze mambo ambayo anajua au kuhisi kuwa yatakera watu.....

Kila la heri ndugu yangu Zitto.
 
Zitto Apology Accepted. Tuanze mwaka mpya kwa mapatano mema.

Hata hivyo niseme kilicho ndani ya moyo wangu kwamba hakikisha unashirikiana na Chama kuangamiza kundi la wahuni na waasi wanaokula njama kukivuruga chama na uongozi wa juu.

But all in all Heri ya mwaka mpya 2013.
 
Zitto

Shukrani KAMANDA!!! Nilikereka na sasa umeuweka moyo wangu kuwa SAFI. Nimekusamehe na nimesahau kila kitu. Ni wachache sana wanao weza kukubali walipo teleza (nikiwepo mimi), ila wewe umekuwa mfano.

Tuijenge CHADEMA imara na kusahau yote yaliyo pita. Machache umeaandika lakini naamini vitendo vitakuwa vingi. NAKUAMINIA MPIGANAJI.

Mungu akujaze nguvu na uvumilivu, ili tupiganie haki, usawa na maslahi ya kila mTanzania.

Mwaka 2013 uwe mwema kwako na pia kwa chama chetu CHADEMA. Changamoto za 2012 ziwe chachu ya kukuongezea kasi katika kuikomboa Tanzania kutoka mikononi mwa mkoloni mweusi. UBARIKIWE SANA KAMANDA ZUBERI ZITTO KABWE.
 
Last edited by a moderator:
Ume kosea wapi?
Mbona umeomba radhi kwa mitego namna hii?
Naona umeendelea kuwa mjanja!
Kuomba radhi ni njia ya kukubali makosa!
Bado sijajua ni makosa yapi? Wewe ni mwana siasa na tunajua kabisa hii kauli inaweza ikawa na maana kubwa lakini ikawa ni mtego pia!
.........................................................................
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
Nakutakia mwaka 2013 mwema na ushiriki kikamilifu JF kwa kauli yako JF ni kila kitu unasoma, unasomesha na kusomeshwa
 
aitwe tuntemeke,
yericko nyerere,
ben saa nane,
shonza,
kitila mkumbo,
waje tuupokee msamaha huu na turekebishane kwa maslahi ya chama na kuingamiza ccm,
waitwe waje hapa
 
Mkuu Zitto pole sana na maandalizi ya kuingia kwenye mwaka mpya,na hongera kwa kumaliza mwaka 2012.

Nasema hivyo kwa sababu Mwaka tunaokwenda kuuanza muda mfupi unaokuja ni mwaka ambao utakuwa umejaa kila aina ya matatizo,na ni imani yangu kwamba yawezekana utakenda kuwaudhi wengi zaidi,kwa sababu katika mapambano ya kuitafuta amani tena na ile kweli kuna misukosuko mingi sana ikiwa ni pamoja na kuwaudhi wengi sana.

Kama mwaka 2012 ambao unagawanyika bila utata yalijitokeza hayo ambayo umeyasema na kuyaombea msamaha ni wazi kwamba huu mwaka unaokuja ambao haugawanyiki kutakua na matukio hayo uliyoyaombea msamaha mengi sana kwa sababu mwaka wenyewe unajionesha kama unavyosomeka.

Langu ni moja tu kwamba vyovyote vile itakavyokua ni lazima tufike sehemu tuseme yaliyopita sio ndwele Tugange yanayokuja,nakupa Bigup sana tuko pamoja na mapambano bado yanaendelea katika kuhakikisha kwamba amani ya kweli inapatikana ili upendo uweze kudumu milele,WABHEJASANA MWANAWANE.
 
Mkuu kama hawajaingia kwenye kuikaribisha mwaka mpya basi watakuwa bado wanatafakari na kujipanga,lakini naamini kwamba wao ni binadamu wenye damu,maji na nyama kama wengine wataukubali msamaha huu na mambo yatakwenda vizuri.

aitwe tuntemeke,
yericko nyerere,
ben saa nane,
shonza,
kitila mkumbo,
waje tuupokee msamaha huu na turekebishane kwa maslahi ya chama na kuingamiza ccm,
waitwe waje hapa
 
Happy New Year 2013; Tukaache Usaliti na Utafutaji maslahi binafsi TUKAJENGE CHAMA chetu
 
Huu ni ukomavu wa kisiasa :clap2::clap2:

We nae kwa unafiki! Watu hapa wakati wanatoa michango yao kumrekebisha ZZK wewe na wenzio mlikuwa mnampa kichwa kwa kumjaza maneno yenu ya uchonganishi. Leo kaja hapa baada ya kuregain senses unajifanya kumsifu eti UKOMAVU wa kisiasa. Acheni tabia hizi. Viongozi wetu ni binadamu kama sisi, wanapokosea kwa dhahiri kabisa tunatakiwa kuwarudisha kwenye mstari ili waendelee kutuongoza vyema. Msiwe kila kitu mnakibeba kishabiki tu as if kuwa na itikadi na imani tofauti ni uadui. Tubadilike!
 
Mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wenye changamoto nyingi, mafanikio makubwa ya kisiasa kama vile kushinda uchaguzi mdogo Arumeru na chaguzi kadhaa za Udiwani Kwa upande wa chama. Bungeni ulikuwa mwaka wenye rekodi za kujivunia ikiwemo hoja ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu iliyopelekea mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri, hoja binafsi za Mkonge, ugawaji Ardhi na utoroshwaji wa Fedha nje ya nchi. Sheria ya kulinda kazi wasanii, Sheria ya "capital gains tax", Sheria ya kulinda viwanda vya maziwa vya ndani na viwanda vya nguo na Sheria kufutwa Kwa msamaha wa VAT Kwa kampuni za madini.

Hata hivyo kuna changamoto kadhaa zimejitokeza. Muhimu kuliko yote ni kwamba Kwa njia moja ama nyingine nitakuwa nimewakera, kuwaudhi au kuwakatisha tamaa. Mimi ni binaadam, sijakamilika. Naomba radhi Kwa mapungufu yangu yote.
Hongera sana ndg zitto kwa kazi kubwa unayofanya kulijenga taifa. Wewe ni mfano bora wa kuigwa kwa wabunge vijana. Mwaka 2013 uwe mwaka wa mafanikio zaidi kwako. Wewe ni ROLE MODEL WANGU. I salute you.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom