Hemed Kivuyo wa ITV acha ushamba

Hemed Kivuyo wa ITV acha ushamba

Yeye ni mwandishi anayejiamini, unapojaribu kumpangia ndio unaharibu kabisa..mimi nasema chapa kazi Kivuyo, chapa kazi.

Sio lazima kila mtu akupendeze,anaweza akaamua kukupendeza wewe kumbe anawakera zaidi ya watu mia!
 
Unataka kumpangia sauti na jinsi ya kuongea..!! Kwani wakati anasomea uandishi wa habari ulimpa hata mia ya Adaa.. Achaa upuuzi wewe....
 
Mauza uza ya baadhi ya wabongo kulalamika tu mtangazaji anatumia sekunde kadhaa kati ya masaa 24 wewe imekua kero katangaze na wewe kama kipaji unacho
 
Ni kweli kunao identity kama ya joji maratu na hata mimi naipenda ila tatizo la Hemedi kivuyo ni kwamba anayo maneno mengi na mashairi mpaka yanaboa yani, maneno Mengi kweli, naungana na mleta Mada, inabidi kivuyo abadilike habari ikiripotiwa na yeye inakua haina mvuto tena.
 
ujue kutofautisha unatuletea na anakuletea

kama wewe humpendi nenda ITV mikocheni kuna sanduku la maoni

vitu vingine sio mpaka upost vile umehamisha chaneli nyingine inatosha

kama Kivuyo anakuboa basi hata list itakuwa inakuboa pia

  • Dokta Panjuan
    Salim Kikeke
    Harris Kapiga
    Tbway360
    Sam Mahela
    Mauleed Kitenge
hawa wote wana mbwembwe katika utangazaji wao je washawahi kukuboa

mcheza kwao hutunzwa
unajua maana ya uniqueness?
Tbway, mahela kivuyo na kapiga mimi wananikera sana, ndio maana siku hizi nachek azam TV tu, watangazaji wako serious kweli yani
 
Acha ushamba na wewe, kila mtu ana aina yake ya maisha (life style)!
 
Ukweli ni kwamba anaiga wazungu kuanza kama kutoa intro ya kitu, ubaya ni kwamba swagga hizo zinafanyakazi vizuri kwa kiingereza lakini sio kwa kiswahili...
 
Mimi binafsi huyu mtangazaji wa habari za michezo ananikera utangazaji wake! kiasi kwamba akianza kutangaza tu nahamisha stesheni, kwani hizo mbwembwe zote zina umuhimu gani,

Unaleta madoido ya kizamani, mbona ukifanya mazungumzo ya kawaida sauti yako ni ya kawaida hadi unapotangaza ndo unatuletea mbwembwe! Acha hizo ni ushamba tu huo kama hujui, au unataka umaarufu?
Sasa mimi ndio napenda hayo madoido yake sio wengine wanaboa, Taarifa za Michezo kama taarifa ya habari?!? Hapana inabidi ziwe na mbwembwe. Ho Kivuyo go!
 
Kivuyo Chapa kazi nimeangalia ni 10% tu ndio wanamuunga mtoa mada. Tanzania hatupendi watu creative, hilo ndio tatizo kubwa sana! Anachangamsha kwa kweli kaza buti! Kuna mtangazaji mmoja wa TBC Somebody Omari jamani alienaga wapi?
 
Mimi nampenda sana Kivuyo na mashairi yake ni bonge la mtangazaji kwangu mno.... Sasa sam Mahela utasema je?
 
Back
Top Bottom