ilisha juniour
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 714
- 220
Siku ya leo nimekuwa mpweke sana,nahangaika na kazi kwa muda mref sasa sijapata,nikichek mwaka unaisha, umri unazidi kwenda,hakuna la maana lolote nililofanya zaidi ya kuwa na afya njema tu aliyonijalia mungu,sina kipato,sina msaada,maisha ni magumu sana,nyumbani nako majirani kila kukicha masimango hayaishi,kodi ya nyumba inaisha,umeme nadaiwa,bill ya maji sijalipa,eeeh mungu nakuomba kama kuna uwezekano unifungulie njia nipate kuepuka kikombe hiki,pia nawaomba ndugu zangu humu jamvini mnipe japo neno tu la kunifanya niendelee kutamani kuishi,sina mtu yoyote wa karibu mda huu wa kunifarij hata usingizi sina!!