help please-forming a company | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

help please-forming a company

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by carmel, Feb 4, 2010.

 1. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dear members, naombeni msaada urgently. Mtu akitaka kuanzisha kampuni inayodeal na variety of things kama viwili vitau inakuwaje? Naikia inabidi iandikishwe wizara ya viwanda na biashara, lakini am not sure ndo maana nauliza. implication ya tax ikoje? Nataka kujua pprocess nzima, i will appreciate.
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Iam very shallow on this,lakini nijuavyo mimi,Kuna taasisi inaitwa Brela ndio inahusika kusajili makampuni.Nadhani ungeenda kuwaona wakupatie mchakato mzima.
  Hongera kwa malengo ya kuanzisha kampuni.
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  mm nimefungua juzi,nenda brella utapata mahitaji yako yote ya maswali na majibu
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
 5. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,539
  Likes Received: 2,056
  Trophy Points: 280
  kama umefungua juzi why dont u give an insight of the story....anyway..kwa uelewa wangu

  ...kuna kampuni za aina mbili..a LIMITED and SOLE proprietorship companies..sasa inategemeana na ipi unayotaka kuanzisha...

  kwa LTD....taraibu ni sawa na ya sole ila tuu..unahitaji kuwa na memorandum of understanding/association kwakuwa utakuwa na more than 1 directors ambao watakuwea na liabilities kwenye kampuni...

  nenda brella submit 3 company name ..ili wafanye name search...ukipata jina tayari unapeleka Memorandum 3 copies...wanaipitia then unapewa certificate of registration ya company....

  kisha unaenda TRA unapata TIN...kisha unaenda municipal husika unachukua business licence ...then unaenda bank kufungua account ya kampuni kwa taratibu na masharti ya bank husika...

  kama unafanya biashara inayodeal na vitu ambavyo vina-boards zinazogovern that business ...inafika wakati unahitaji pia ku-register na hizo boards ili uweze kupata registration ya board husika...say unataka kuuza madawa...inabidi pia upate kibali/registration ya TFDA...kwa mama sigonda...etc

  kuhusu ku-run 3 business kwa kampuni moja ni rahisi tu..maana ulivyokuwa unasubmitt brella ile memorandum uliandika objectives za kampuni ..kwa hiyo inakuwa ni rahisi kukata leseni ya biashara zote tatu na kuzifanya kwa jina moja na possible 1 bank account ila utakuwa na usajili tofauti kwa kila governing board......

  ni maoni tuu..na uelewa wangu binafsi
   
 6. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  So sorry am in a bad situation cant advise at the moment,hope she understand,real sorry.
   
 7. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Thanks dears, i have just opened that website ya brela (thanks charity), naona its very useful for now. Lakini haina maana kwamba sitaki ideas zingine.
   
 8. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,539
  Likes Received: 2,056
  Trophy Points: 280
  pole sana mamaa....pole pia kama nimekuumiza
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,118
  Likes Received: 2,415
  Trophy Points: 280
  Si mara zote ni lazima kuanzisha kampuni. Kama lengo ni kufanya biashara una weza pia kufanya kama mtu binafsi (sole propriatorship) au kwa kushirikiana na wengine (Partnership). ubaya wa kampuni, inakuwa na compliance requirements nyingi amabazo in some cases zinaweza kukudistract.

  Kwa kusaidia kujibu swali lako. Cha kwanza ni kuisajiri (incorporation) hiyo kampuni BRELA (www.brela-tz.org). Katika hiyo process utatakiwa kuandaa Memorandum of Association (katiba inayoelezea umiliki na wamiliki wa kampuni, madhumuni ya kampuni na ukomo wa wajibu) na kama ukitaka Articles of Association (taratibu za kuendesha kampuni).

  Baada ya hapo utatakiwa kuisajili kampuni kama kama mlipa kodi (TRA watakupa TIN). Na pia utatakiwa kuomba leseni (inaweza kuwa zaidi ya moja) kuendana na aina ya biashara kampuni itataka kufanya.
   
 10. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  I understand dia, and hope you feel better.
   
 12. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  At least now,thx
   
 13. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  what if ni biashara ya mtu mmoja, i mean labda niwe kidogo wazi ili nipate insight. Nataka kuanzisha biashara (peke yangu) ambayo inatahusisha mimi kudeal na kampuni mabalimbali nikimaanisha tender etc, lakini cha msingi ambacho kinanisukuma kuanzisha kampuni ni ili nipate account bank itakayoniwezesha kufanya transactions. Hii pia inahitaji MoU?
   
 14. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tHANKS WHOCARES, Lakini do i need an MoU kama ni SOLE proprietorship company? TRA TIN unalipia sh ngapi kwa business isiyozidi 5m?
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,090
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Inategemea unaanzanisha aina gani ya Kampuni. Chini ya Sheria ya Makampuni (The Companies Act, cap, 212) kuna aina mbili tatu za makampuni (i) Private (ii) Public akwa zo zinaweza kuwa "limited liabilty (limited by shares), unlimited Companies" au Companies limited by guarantee. Lakini nyingi binafsi zinakuwa " Private Limited" au LTD" (haziruhusiwe kuuza hisa kwa umma kama "Public Limited Comapanies "PLC".

  Kwa kuwa umekwishaelekezwa kwenye tovuti ya brela, mengi utajua hapo ningekushauri haya:

  Kwanza kabla ya kwenda kusajili kampuni, ni vizuri ujue aina ya kampuni unayotaka, Jina la kampuni, wamiliki wake, itafanya kazi gani, na pengine unaweza kufikiria wadau wake, na pia nani atakuwa "Company Secretary".

  Baada ya hapo unaandika kwa Msajili wa Makampuni (Registrar of Companies) kuaomba kupata "Name clarance" (yaani uthibitisho wa jina unaotaka kutumia.Jina ni lazima liwe "unique" ambalo halipo kwenye regista (yaani halijawahi kutumika na kampuni nyingine).

  Baada ya kupata "name clarance" omba msaada wa Wanasheria wakuandalie "MEMARTS" (Memorundum and Articles of Association) na kuwasilisha sambamba na fomu maalumu utakazopata hapo BLERA na malipo kulingana na "fee structure" ambayo utaelekezwa BRELA au na Mwanasheria nayefahamu taratibu za kusajili.

  Katika "Memorundum of Association" ndimo ambapo malengo (objectives) ya kampuni unayoianzisha yatakuwepo. Kisheria unaruhusiwa kuweka kadiri uwezavyo yale ya moja kwa moja/Malengo makuu (main objectives) na yale yenye mwelekeo au uhusiano wa karibu (incidentals to the main objectives )..Kwani kisheria kampuni hairuhusiwi kufanya yale yaliyo nje ya malengo ya kuanzishwa kwake.

  Katika "Articles of Associations" ndimo muuundo wa Kampuni unaelezwa ni Katiba ya Kampuni (Constitution)

  "Memorundum and Articles of Associations" unaweza kuziandaa mwenyewe au kwa kuwa ni nyaraka za kisheria, ni vyema unasaidiwa na wenye hiyo taaluma. Hizi zinapaswa kuidhinishwa na Mwanasheria (attestation) kwenye sahihi za wamiliki (shareholders/Directors) samabamba na hizo fomu za kuwasilishia nyaraka hizi kwa Msajii wa Makampuni. Msajili akiridhia, utapewa cheti (Registration/ Certificate of Incorporation) ambacho kisheria ndio uthibitisho wa usajili wa hiy kampuni wa kukuwezesha pia kuwasilisha TRA na mamlaka nyingine kwa ajili ya kuendelea na biashara.

  Huu ni mwongozo tu!.

  Ikiwa id
   
 16. t

  tony25 Member

  #16
  Feb 4, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ok. inategemea

  Kama nataka kufungua company inabbidi uandae memorandum and articles of Association. Kabla ya kufanya hivyo inakubidi ufanyie kitu kinachoitwa search of company name. Hapa unaandika barua kwa mkurugenzi wa brella ukimention majina ambayo unataka kuipa kampuni yako. Hii inasaidia kwenye kuaandaa memorandum of association ili jina la kampuni yako lisije likafanana na la mtu mwingine ambaye ameshafungua kwa jina hilo. Hii inachukua only three working days kupata jibu. Thereafter unaendelea na process za kuandaa memeorandu,ukishamaliza unazipeleka pale brella (Jengo la Ushirika) ghorofa ya tatu. Pale wataangalia ukubwa wa memorandum kwani wanachaji kwa kile page mara copy ulizo nazo plus registration fee. Hapa watakupa form ambazo utajaza your personal details and of the like then zinabecertified na mwanasheria. Hapo ukimaliza unazirudisha brella wao watazipitia, hapo hakuna specific time yakusubiri but normally kuanzia wk 1. Thereafter kama kutakuwa hamna marekebisho kwenye memorandum then wanakupa certificate of incoorporation. Nadhani nimeeleweka.
   
 17. m

  majogajo JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ngoja waje..........
   
 18. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,778
  Likes Received: 1,317
  Trophy Points: 280
  msaada hapa tafadhali je memorandum of association ndio sawa na business plan??
   
 19. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #19
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,350
  Likes Received: 2,529
  Trophy Points: 280
  MKUUKUNA KAMPUNI ZA AINA TATU TU
  1,Private Company- kampuni kam Mohamed entreprises na kazalika

  2. PublicCompany- TBL, CRDB, NBC, TWIGA CEMENT

  3.Private company isiyo kuwa na share zinatumiwa sana na NGOs


  kablahujasajiri kampuni Tafuta watu ambao mtafanya nao hiyo kazi means madirecta nahakikisha yafuatayo

  1. Waweni watu ambao mna lengo moja

  2. Wawetiyali kujitolea kwa muda wao na hata fedha ili kukuza kampuni,

  3. Uweunafaham Historical back ground yao/yake

  4. Kamikibidi wewe muanzilishi wa wazo inabidi uwe na share 51% yaani kati ya sharezote wewe umiliki 51% YA HISA ZOTE
  - Hiiitakusaidia kulinda aidea yako na hawataweza kukupindua kamwe kama wana niambaya
  - Ukiwana 40% mwenzako 30% mwingine 10% mwingine 10% na mwingine 10%
  Hawa 30%
  10%
  10%
  10%
  Wanawezaunganisha share zao na ikala kwako mazima so make sure unakua na 51% na hizo49% ndo wacheze nazo hao wengine

   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...