Hela ya Tanzania yazidi kuporomoka!

Hela ya Tanzania yazidi kuporomoka!

Naona hapa tayari tumepoteza muelekeo na kama kawaida yetu JF kila mada lazima iwe twisted ili ichukuwe sura ya kisiasa. Inaaibisha.

Mada hii ni juu ya kupungua kwa thamani ya dola ya Tz katika kipindi husika. Inachekesha kwamba wachangiaji wanadai kwamba kuporomoka kwa shilingi yetu katika kipindi husika ni kutokana na kutotilia mkazo elimu.

Wote tunajuwa kwamba matunda ya elimu yanatokea in long-term wakati fractuations za inflation na thamani ya shiling vs US$ vinatokea na kurekodiwa in short/medium-term. Madhara ya kupungua kwa thamani ya ela yetu, na madhara ya inflation yanatokea leo, na yanahitaji measures zitakazo zaa matunda siku za karibuni. Na ndio maana tuna BoT kama naodha wa kudhibiti hali hii mara inapotokea.

With all due respect kwa wachangiaji waliosema tatizo la kupungua kwa ela yetu linatokana na kutotilia mkazo elimu, kuhusisha short-term/medium term inflation and depreciation phenomena ni sawa na kulazimisha panya awe ngamia. Tumeona dola ya Marekani ikishuka thamani kabla ya global economic crisis, je tuseme USA walishindwa kutilia manani elimu? Hivi leo dola ya Canada imepungua thamani na inflation ya Canada imeongezeka, je tuseme nao hawana mikakati ya elimu? Tangu lini elimu ikawa a direct input ya equation inayo determine inflation na kupanda au kushuka kwa thamani ya ela ya nchi? Au elimu inaingia tu kwenye equation tunapo analyze ela ya Tz!!

Inflation na depreciation zinasababishwa na factor nyingi, zikiwamo internal na external. Katika uchumi wa gulio factors zinazochangia depreciation au inflation ni short-term au medium term. Kwanini? Kwasababu inflation and depreciation vinarekodiwa in short-term au medium term. Kwa siku moja au dakika moja stock market zinaweza kusababisha depreciation, bei ya siku moja ya pamba yetu inaweza kusababisha depreciation, kampeni za uchaguzi za miezi 3 zinaweza kusababisha inflation instantly, mabilion ya kikwete yakitolewa kwa kipindi cha wiki moja yaweza kusababisha inflation na depreciation; kadhalika ukame na uvivu kazini kwa mwezi moja.

Elimu ni human capital ambayo inachukuwa karne au miongo kadhaa ku-materialize. Kuhusisha elimu na inflation na depreciation ni 100% ze comedy.
 
Tumeona dola ya Marekani ikishuka thamani kabla ya global economic crisis, je tuseme USA walishindwa kutilia manani elimu? Hivi leo dola ya Canada imepungua thamani na inflation ya Canada imeongezeka, je tuseme nao hawana mikakati ya elimu? Tangu lini elimu ikawa a direct input ya equation inayo determine inflation na kupanda au kushuka kwa thamani ya ela ya nchi? Au elimu inaingia tu kwenye equation tunapo analyze ela ya Tz!!.

Kaka uko sahihi, hii maada haitaweza endelea bila kuangalia inputs nyingi

Kama tuna wasomi walio wengi kwenye uchumi mkuu, na bado tunayumba tatizo ni nini?? elimu yao ndogo au finyu au wako partial?? basi tukijua tatizo ni elimu tutaelezea elinmu

Tukiamini kuwa tatizo si wataalamu tulio nao amabao wengi wamekuzidi elimi yako ya uchumi uliyonayo(ashakum si matusi) na tukajua kuwa chanzo cha wao kutoperofm ni tatizo la viongozi tutazungumzia viongozi katu hatutawakwepa wanasiasa!

Tukijua majirani zetu wana viongozi bomu , may be kupita sisi na still wanafanya vizrui fedha yao inapanda thamani, tutaangalia kitu gani kinawafanya wao waendelee!

tukijua kuwa kenya ina raia wengi nje ya nchi, na pato la fedha ya kigeni kwa mwaka nchini kenya ni kikubwa mno, tutaangalia what made them to be in that way! tukifikia kujua elimu imesababisha hayo tutasema elimu kaka

Yes there is no direct input katika equation ya inflation, lakini equation yeyyote inajengwa na assumptions , ina kuwa na factors,

mfano.

A of circle=pi* radius* radius, inputs ni radius, pi ni constant

lakini katika equations zingine constant inabadilika kutokana na tatizo lenyewe, au inputs nayo inaconditions zake, what if unapima radius na unapokandamiza na vernier calliper basi radius inapungua? what if kifaa unachopimia radius ni kibovu hakijawa calibrated?? what if mpimaji ana matatizo ya macho au hajui vipimo?? what if calculator ina matatizo?

siyo mtaalamau wa uchumi , lakini naamini kama equation ya inflation haiendani na mazingira, wakati, hali halisi basi kuna tatizo, uchumi unabadilika sana!

formula iko pale , ili iperform inahitaji factors nyingi!
 
Waberoya,
Kama inflation na depreciation zinazotokea kila mara katika nchi zilizoendelea zinasababishwa na elimu yao kuwa duni nitafika tamati na kukubaliana na wewe 100%.

Kama kuna nchi zilizotilia mkazo elimu (mfano USA na Canada) na bado ela za nchi hizo zinateremka na kupanda na bado wanatatizo la inflation, sisi tutakuwa vichekesho kusema tatizo letu ni elimu (ambayo tunailazimisha iwe kwenye equation ya depreciation). Ela ya mjapani imekuwa chini ya US$ kwa miaka kadhaa, ela ya Canada imekuwa chini ya US$ kwa miaka kadhaa, US$ imekuwa chini ya pound kwa miaka kadhaa. Nchi hizi zote zinakumbwa na misukosuko ya inflation na kupanda na kushuka kwa ela zao na bado nchi hizi zimpepiga hatua kielimu.

Kusingizia elimu katika depreciation na inflation ni sawa na mgonjwa anayesumbuliwa na kwikwi na daktari akamwambia kwamba dawa ni kula vizuri na kuwa msafi.....kwikwi ni short-term na effects za kula vizuri na usafi ni long-term....mgonjwa wa kwikwi anatakiwa apewe dawa ya kwikwi, then ashauriwe kula vizuri na usafi....ukimshauri bila dawa kwikwi itaendelea na itachukuwa muda hadi apone kutokana na ula vizuri na usafi, wakati huo tayari madhara ya kwikwi katika shughuli zake za kila siku zitakuwa maradufu.
 
Kaka uko sahihi, hii maada haitaweza endelea bila kuangalia inputs nyingi

Kama tuna wasomi walio wengi kwenye uchumi mkuu, na bado tunayumba tatizo ni nini?? elimu yao ndogo au finyu au wako partial?? basi tukijua tatizo ni elimu tutaelezea elinmu

Tukiamini kuwa tatizo si wataalamu tulio nao amabao wengi wamekuzidi elimi yako ya uchumi uliyonayo(ashakum si matusi) na tukajua kuwa chanzo cha wao kutoperofm ni tatizo la viongozi tutazungumzia viongozi katu hatutawakwepa wanasiasa!

Tukijua majirani zetu wana viongozi bomu , may be kupita sisi na still wanafanya vizrui fedha yao inapanda thamani, tutaangalia kitu gani kinawafanya wao waendelee!

tukijua kuwa kenya ina raia wengi nje ya nchi, na pato la fedha ya kigeni kwa mwaka nchini kenya ni kikubwa mno, tutaangalia what made them to be in that way! tukifikia kujua elimu imesababisha hayo tutasema elimu kaka

Yes there is no direct input katika equation ya inflation, lakini equation yeyyote inajengwa na assumptions , ina kuwa na factors,

mfano.

A of circle=pi* radius* radius, inputs ni radius, pi ni constant

lakini katika equations zingine constant inabadilika kutokana na tatizo lenyewe, au inputs nayo inaconditions zake, what if unapima radius na unapokandamiza na vernier calliper basi radius inapungua? what if kifaa unachopimia radius ni kibovu hakijawa calibrated?? what if mpimaji ana matatizo ya macho au hajui vipimo?? what if calculator ina matatizo?

siyo mtaalamau wa uchumi , lakini naamini kama equation ya inflation haiendani na mazingira, wakati, hali halisi basi kuna tatizo, uchumi unabadilika sana!

formula iko pale , ili iperform inahitaji factors nyingi!

Waberoya:

Umetoa mifano mizuri sana. Tanzania ni nchi kubwa na ina wakazi 40 millioni. Zaidi ya hapo tuna diversity ya resources na matatizo. Hivyo hatuwezi kuwa na silver bullet au panacea ya ufumbuzi wa matatizo yetu. Ni lazima tutumie combination ya vitu vingi kutatua matatizo yetu.

Katika majadiliano mengi ya maendeleo, kwa mawazo yangu watanzania tuko irrational. Na irrationality inatokana na ukweli kuwa tunazo resources nyingi lakini bado tupo nyuma kimaendeleo na tunategemea misaada.

Mtu akifikiri kuwa Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa inaweza kulisha nchi nzima kwanini basi tunategemea misaada ya chakula? Kwanini Kenya wanapata mara tatu katika utalii wakati tunazo mbuga nyingi na nzuri?

Tukirudi kwenye mada kuhusu inflation. Miezi michache kabla Balali hajaacha nafasi ya ugavana, inflation ilipanda kwenye 7%. Na akatoa matamshi kuwa watanzania waanze kufanya kazi wasiwe wavivu.

Muda si mrefu akasema inflation hiko kwenye 5% hivi. Na muda huohuo maskendo ya EPA yakaanza kujitokeza. Baadaye ikafahamika kuwa alimrubuni Waziri kutia saini hundi ya dollar 30 Millioni.

Kama ninavyoelewa, government statistics ikiwemo inflation can be cooked. Mtu anayewaibia dollar 30 Million, kwanini aaminiwe kuwa anachosema ni kweli.

Na nikirudi kwenye mifano uliyotoa. Ninachoamini ni kuwa uchumi na maendeleo ya jamii yana variables nyingi na zingine unknown. Kwa mfano

Alan Greenspan ni mchumi mahiri sana. Na katika fani yake ya econometrix aliamini kabisa kupunguza interest rates kunasaidia uchumi kukua kwa sababu watu watakopa na kutumia pesa katika shughuli za maendeleo. Lakini vilevile hakuelewa kuwa kutakuwepo na ambao watashindwa kulipa mikopo yao na kusababisha sub-prime financial crisis.

Kwa kumalizia tu. Nchi yoyote ni lazima ikabiliwe na matatizo ya kiuchumi. Inflation au GDP itashuka na kupanda. Na sababu za kushuka na kupanda zitakuwa tofauti kwa vipindi tofauti. Lakini nchi itakayofanikiwa ni ile yenye misingi mizuri ya maendeleo. Na misingi ya maendeleo haijengwi kwa miaka michache.
 
Nipo na wewe kwa asilimia 100%.

Tukiwa tunajadiri juu ya inflation na depreciation ni bora tukajizuia kuchanganya mambo matatu ambayo yanajitegemea, ingawa yanawiana kimalengo. Mambo haya ni economic dynamics, economic growth, na human development.

Inflation na depreciation ni miongoni mwa economic dynamics (mienendo ya shughuli za kiuchumi ya kila siku), economic growth ni period-specific end-product za shughuli za kiuchumi (kama inavyopimwa na GDP), human development ni theoretical (some would say practical) benefits za kukuwa kwa GDP.

Sasa elimu, afya, miundombinu, sera za mgawanyo pato la taifa ni vichocheo vya maendeleo vyenye lengo la kupanua amendeleo ya kiuchumi na ku translate economic growth kuwa maendeleo ya watu. Hivi ni vichocheo vinavyochukuwa muda kuleta athari zinazokusudiwa. Tusichanganye, hivi si vichocheo ya kudhibiti viashiria mienendo ya shughuli za uchumi ya kila siku (economic dynamics) kama inflation na depreciation.
 
Waberoya:
Kwa kumalizia tu. Nchi yoyote ni lazima ikabiliwe na matatizo ya kiuchumi. Inflation au GDP itashuka na kupanda. Na sababu za kushuka na kupanda zitakuwa tofauti kwa vipindi tofauti. Lakini nchi itakayofanikiwa ni ile yenye misingi mizuri ya maendeleo. Na misingi ya maendeleo haijengwi kwa miaka michache.

Na ndiyo kosa kubwa tunalolifanya watanzania tunajadili vitu kujilingaisha na USA, CANADA, UK. USA wameishi hali hii miaka ya 1700! kuzungumzia inflationa kwa nchi amabayo inategemea export za malighafi , na importation za products , ni kutojijua tuko wapi!

Do we have compentent personell in economics? the answer could be yes we have, kwa sababu hatuna coiche, nchi yenye competion kubwa za human resources zina maendelea makubwa. SASA tunapozungumzia kuwa baada ya USA kutetereka kiuchumu bsi dunia nzima ikiwemo Tanzania tunayumba, hapa kuna tatizo?? tatizo hili si kutoa mifano mbona nchi fulani nayo imeyumba!!

In other words, hatuna hela yetu Tanzania?? hatuna nguvu,hauna wataalamu, tunapangiwa mambo.Je nafikiri ni rahisi hawa jamaa wakakubali leo hii nchi yetu iwe shilingi moja sawa na dola moja?? juzi tu miaka ya 90,Botswana dollar ilikuwa sawa na US dola, leo hii nadhani imeshuka. Hawako radhi.

Nilikubaliana na waliosema elimu, kama tutafanikiwa malighafi zetu ziwe processed humuhumu ndani, na products ziuzwe humuhumu ndani, basi hatutaathirika sana na hizi crisis,jamni is so simple we can only reach that kama tuna wataalamu, na tunawatumia na viongozi wenye vision.

Kuzungumzia Tanzania ya sasa na inflation hazitakwepeka, even if we have good economists, kama uchumi wetu ni tegemezi, misaada, na kuhamisha malighafi forget!!!!!!!! ishu ya inflation it will be Normal, as we are not the one we are controlling our economy other people outside somewhere they are doing for us!

fellas lets open up our minds
 
Na ndiyo kosa kubwa tunalolifanya watanzania tunajadili vitu kujilingaisha na USA, CANADA, UK. USA wameishi hali hii miaka ya 1700! kuzungumzia inflationa kwa nchi amabayo inategemea export za malighafi , na importation za products , ni kutojijua tuko wapi!

Do we have compentent personell in economics? the answer could be yes we have, kwa sababu hatuna coiche, nchi yenye competion kubwa za human resources zina maendelea makubwa. SASA tunapozungumzia kuwa baada ya USA kutetereka kiuchumu bsi dunia nzima ikiwemo Tanzania tunayumba, hapa kuna tatizo?? tatizo hili si kutoa mifano mbona nchi fulani nayo imeyumba!!

In other words, hatuna hela yetu Tanzania?? hatuna nguvu,hauna leo hii nchi yetu iwe shilingi moja sawa na dola moja?? juzi tu miaka ya 90wataalamu, tunapangiwa mambo.Je nafikiri ni rahisi hawa jamaa wakakubali ,Botswana dollar ilikuwa sawa na US dola, leo hii nadhani imeshuka. Hawako radhi.

Nilikubaliana na waliosema elimu, kama tutafanikiwa malighafi zetu ziwe processed humuhumu ndani, na products ziuzwe humuhumu ndani, basi hatutaathirika sana na hizi crisis,jamni is so simple we can only reach that kama tuna wataalamu, na tunawatumia na viongozi wenye vision.

Kuzungumzia Tanzania ya sasa na inflation hazitakwepeka, even if we have good economists, kama uchumi wetu ni tegemezi, misaada, na kuhamisha malighafi forget!!!!!!!! ishu ya inflation it will be Normal, as we are not the one we are controlling our economy other people outside somewhere they are doing for us!

fellas lets open up our minds

Waberoya:

Kwa maoni yangu binafsi wataalamu wapo wa kutosha Tanzania lakini kuna uwezekano mkuwa hatuna expertise wa kutosha katika soko huria. Kwa sababu katika kipindi cha zaidi ya miaka 25 hatukuamini kuwa tunaweza kuendelea kwa kutumia soko huria na tulijaribu njia zetu mpya.

Tunaishi katika information age. Miaka 1700, 1800 na Mwanzoni mwa 1900 ilikuwa taabu kwa maarifa kusambaa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ata kwa zile nchi zilizopo kwenye continent moja.

Sasa hivi dunia imeunganika na impacts ya mambo yanayotokea dunia ni lazima yasikike Tanzania.

Miaka ya 1960 mpika vitumbua DSM alitegemea mchele kutoka bonde la Msimbazi na mafuta ya kukaanga vitumbua kutoka katika minazi ambayo leo ni eneo la chuo kikuu cha DSM. Kwa maana nyingine alijitosheleza katika mazingira yake na kuna uwezekano mkubwa kuwa impact ya vita vya Vietname au kati ya waarabu na waIsrael havikufanya bei ya vitumbua DSM ipande.

Leo hii mpika vitumbua mwenye kutumia ingredients zilezile zilizotumika mwaka 1960 ana watu zaidi ya 100 anaowategemea kutengeneza kitumbua kimoja. Kwanza inabidi apate mchele kutoka Mbeya au Thailand ambao unasafirishwa kwa gari lilotengenezwa japan linalotumia mafuta kutoka Saudi Arabia. Hivyo ongezeko la bei ya mafuta pekee yake, ambalo linaweza kutokea kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu, linaweza kusababisha ongezeko la bei ya vitumbua.

Ongezeko hili la bei ya vitumbua halina sababu ya kuwa nchi ina wasomi wachache au wengi. Na vilevile wasomi waliopo na kufanya kazi nje ya nchi hawataweza kusaidia kuondoa tatizo hili. Pamoja na hayo, kuna tools za kiuchumi ambazo nchi inaweza kuzitumia kupunguza bei au kufanya watu waweze kumudu ongezeko hilo la bei.

Suala la sisi kutumia elimu na wataalamu wetu ni muhimu. Lakini wengi wetu wanasahau kuwa Tanzania imefanya U turn mbili. Mara ya kwanza kutoka katika uchumi unategemea private sector kwenda kwenye ujamaa. Na mara ya pili ni kutoka ujamaa kwenda kwenye private sector.

Na katika U-turn zetu tumepoteza expertise ya kutosha katika masuala ya uchumi na biashara. Kwa mfano katika miaka 60,70,80 utalii uliendeshwa na mashirika ya umma. Wakati huohuo utalii Kenya unaendeshwa na sekta binafsi. Leo tumeingia katika soko huria tunataka mara moja pato letu liwe sawa na Kenya bila kuonyesha expertise ya namna yoyote.

Watu wawili waliomaliza chuo kikuu cha EA miaka ya 60. Na mmoja kufanya kazi shirika la umma Tanzania. Na mwingine sekta binafasi Kenya, ni watu wawili tofauti japokuwa wamemaliza shule moja na kupata digrii moja. Expertise walizopata kutokana na nafasi zao za kazi, zimewafanya wawe watu wenye mitazamo tofauti ya kile walichosomea.

Hivyo elimu pekee yake sio Silver Bullet.
 
Wadau nimefaidika sana na majadiliano yanayoendelea juu ya kushuka kwa thamani ya fedha ya Kitanzania.
Ni vyema tuka toka kwenye ku analyse the situation na kupendekeza hatua za kuondoa hali hii, hata kama hazitachukuliwa hatua hizo.
Ni ukweli usiopingika kuwa bei za vyakula zimeongezeka sana miaka ya karibuni, hivyo kuchangia inflation.
Dola nayo haikamatiki na sasa hatuelezwi tufanye nini ili kuikwamua hali hii.Kama alivyosema Obama , "YEs We Can", hata sisi twaweza badilisha hali hii.
 
Lole gwakisa,
Direction ya mjadala huu inaweka mazingira magumu kutoa suluhisho la nini kifanyike.

Kuna baadhi ya wachangiaji wanaona maada hii kuwa ni suala la maendeleo (human development) na sio suala la inflation na depreciation kama kilivyo kichwa cha mada hii. Hawa suluhisho lao ni ELIMU.

Kuna wachangiaji kama mimi, ninayeona kwamba kinachozungumziwa hapa sio maendeleo, bali ni viashiria au indicators (short/medium term) za shughuli za kila siku za kiuchumi. Kwangu mimi suluhisho ni kama ifuatavyo:

1). Kwasababu depreciation inasababishwa na factors za ndani na nje ya uwezo wetu. Tunaweza kupunguza magnitude ya athari zake kwa kurekebisha factors za ndani ya uwezo wetu. Tunaweza kufanya hivi kwa (a) kuthibiti mahitaji ya US$ kwa kuhakikisha kwamba shughuli zote za kibihashara za ndani ya nchi hazifanyiki in US$ (mfano bei za vitu vyote viwe in Tz shillings);(b) kudhibiti mahitaji au utumiaji wa bidhaa za nje (imports) zisizo za lazima au bidhaa ambazo sisi wenyewe tunazalisha kwa kiwango kinachojitosheleza; (c) kuongeza uzalishaji wa mazao tunayotegemea kutuletea US$ na kuendeleza jitihada za kuwavutia watalii ili kuongeza supply ya US$ na hivyo kuipandisha shillingi yetu.

2). Kusifanyike chochote kudhibiti inflation kwa sasa, isipokuwa tu serikali iwe makini katika kukusanya kodi. Nina wasiwasi kwamba inflation inayotokea sasa kwa kiasi kikubwa inasababishwa na kuwapo kwa fedha nyingi zisizowiana na uzalishaji. Mabilion ya JK, malipo ya wastaafu wa EA na malipo ya malimbikizo ya walimu, marejesho ya fedha za EPA, kampeni za uchaguzi wa viti vya ubunge vilivyoachwa wazi, matumizi makubwa ya serikali, n.k. Kwa maoni yangu binafsi, katika jitihada za kuongeza shughuli za uchumi transitory inflation haikwepeki hata siku moja; tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba fedha hizi zinaongeza uzalishaji katika viwango vilivyokusudiwa ili ku-offset inflation. Policies za kuzuia inflation kwa sasa hazifai na zitadidimiza uchumi ambao tayari umeangamizwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia....kinachotakiwa sasa ni policies za kuongeza uzalishaji.

Nionye tu kwamba suluhisho zote nilizotoa zina faida na hasara, pia utekelezaji wa baadhi ya suluhisho waweza kuwa mgumu. Pia nionye kwamba suluhisho nilizoshauri ni suluhisho za kupambana na inflation na depreciation, sio suluhisho za kuinua maendeleo ya kiuchumi au maendeleo ya watu.
 
Lole G:

To be honest, sina solution yoyote kwa sababu niliondoka Tanzania miaka mingi. Na vilevile siamini kuwa kuna Silver Bullet ya kutatua matatizo kwa sababu tunacho-deal nacho sasa kipo ndani ya dynamic system ambacho kina inputs (variables) nyingi ambazo zinaeleweka na zingine hazieleweki kabisa.

Hila kuna kitu ambacho ningependa kuwashauri watanzania wenzangu kuwa toka tumepata uhuru hatujawahi kuona matatizo makubwa ya kiuchumi katika nchi zilizoendelea kama yaliopo sasa. Na kwa mtaji huu, tulijenga sababu mbalimbali kwanini wao wanaendelea. Kuna watu wanafikiri kuwa elimu imewasaidia, kuna wanaofikiri ukoloni wao, kuna wanaofikiri kuwa ni demokrasi.

Kwa maoni yangu kipindi hiki ndio cha kujifunza na kupata expertise. Kwa mara ya kwanza tunaona mataifa makubwa yakitumia tools za kiuchumi katika massive scale. Kuna tofauti kubwa ya kujifunza mashuleni na vilevile kumuona master at work.
 
Kwa wenye kumbukumbu nzuri: Kuanzia miaka ya themanini, kuna mwaka ambao thamani ya hela yetu ilipanda kulinganisha na dola ya marekani?

Au hata miaka hii ya 2000s, kuna mwaka wowote ambao Tzs ilitunisha misuli versus US$?

Kama jibu ni siyo, basi tusisingizie global economic downturn kama sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu. Kwanza katika hiyo inayoitwa global economy, sidhani kama sisi tumo. Nina maana kwamba ule mzunguko wa uchumi katika sekta mbalimbali: growth, boom, maturity, downturn, recession, depression, recovery, etc, hautuhusu sana sisi wa dunia ya mkiani (ya nne). Tuna mauza uza yetu mengine.
 
Mkuu Invicible,
Aidha swali hili haliko sahihi, ama unachanganya mambo mawili tofauti hapa: (a) kupanda kwa thamani ya shilingi na (b) shilingi ya Tz kuwa na thamani zaidi ya USA.

Kama ulitaka kuuliza endapo shilingi ya Tz imewahi kupanda (ku appreaciate) vs US$, jibu ni NDIYO IMESHAWAHI KUPANDA, tena mara kadhaa...na kama unakumbuka ni mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, shilingi yetu ilipanda.

Kama ulitaka kuuliza endapo thamani ya shilingi ya Tz imeshawahi kupita thamani ya US$ katika kipindi husika jibu ni HAPANA. Kama ulikuwa na maana hii, isikupe taabu mana ela ya Japan, Canada, na nchi nyingine kadhaa zimekuwa na thamani pungufu ya US$ kwa karne na karne, na wachumi watakueleza kwamba haijalishi kwani hii haionyeshi depreciation trends wala appreciation trends bali ni levels tu za thamani. Ubaya ni pale kunapotokea depreciation (au sometimes excessive appreciation); kwa maana pale shilingi yetu inapoacha kubaki katika position yake dhidi ya US$.

Kuhusu link yetu na global economy, ndio uchumi wetu huko so vunerable na global economy. Kukiwa na global economic crisis, exports zetu haziuziki (manake imports za bidhaa adimu na muhimu kwa uchumi wetu zinapunbgua), watalii wanaacha kuja, wawekezaji wa nje wanaishia zao, donors waliohaidi kutoa misaada wanakacha, kadhalika shughuli za uchumi zinadumaa.
 
Mkuu naomba shule zaidi hapa.
Swali langu ni hilo la kwanza nililoweka rangi nyekundu. Huko kupanda unakozungumzia mimi napata kizunguzungu. Ebu angalia timeline kwa mfano miaka kumi iliyopita halafu uone net result ya kupanda kwa Tsh yetu.

Kuna nchi moja inayotumia currency ya Kroner. Mwaka 2000, 1 US$ ilibadilishwa kwa Kroner 8.2 hivi. Baadaye ikabadilika mpaka 8.5. Ikaanza kushuka kwenye 7 point something; 6 point something. Mwaka huu mwanzoni ilishuka mpaka 5.xxx. Lakini kwa sasa exchange rate ni 1:7. Wachumi wa nchi hiyo wanasema mwaka huu dollar iliteremka sana (1:5.xxx) kulinganishwa na kroner. Ni rekodi iliyowahi kutokea mwaka 1982.

Huku ndiko kupanda kwa kroner ninakokuelewa mimi. Hii ya Tanzania haijanielea vema. Kama ningechora graph au skatter diagram, basi mwelekeo wa shilingi yetu versus dollar ni downward, haijalishi kama kuna miezi miwili mitatu fedha yetu ilipanda. Hiyo inaonekana zaidi kama outlier kwenye graph. Lakini graph ya dollar versus kroner itaonekana na sura tofauti kabisa.

Pia suala la sisi kuwa sehemu ya global economy, bado nahitaji maelezo ya kunisadikisha. Sisi uchumi wetu umedorora na maisha ya wananchi yameendelea kuwa magumu katika kipindi cha miaka karibu thelathini iliyopita. Katika kipindi hicho hicho uchumi wa dunia ulikuwa katika hali bora(boom). Sasa mbona hatukupata hiyo trickle-down effect ya misaada, watalii, na kuongeza mauzo nje?
 
Direction ya mjadala huu inaweka mazingira magumu kutoa suluhisho la nini kifanyike.

Kuna baadhi ya wachangiaji wanaona maada hii kuwa ni suala la maendeleo (human development) na sio suala la inflation na depreciation kama kilivyo kichwa cha mada hii. Hawa suluhisho lao ni ELIMU.

Kuna wachangiaji kama mimi, ninayeona kwamba kinachozungumziwa hapa sio maendeleo, bali ni viashiria au indicators (short/medium term) za shughuli za kila siku za kiuchumi. Kwangu mimi suluhisho ni kama ifuatavyo:

1). Kwasababu depreciation inasababishwa na factors za ndani na nje ya uwezo wetu. Tunaweza kupunguza magnitude ya athari zake kwa kurekebisha factors za ndani ya uwezo wetu. Tunaweza kufanya hivi kwa (a) kuthibiti mahitaji ya US$ kwa kuhakikisha kwamba shughuli zote za kibihashara za ndani ya nchi hazifanyiki in US$ (mfano bei za vitu vyote viwe in Tz shillings);(b) kudhibiti mahitaji au utumiaji wa bidhaa za nje (imports) zisizo za lazima au bidhaa ambazo sisi wenyewe tunazalisha kwa kiwango kinachojitosheleza; (c) kuongeza uzalishaji wa mazao tunayotegemea kutuletea US$ na kuendeleza jitihada za kuwavutia watalii ili kuongeza supply ya US$ na hivyo kuipandisha shillingi yetu.

2). Kusifanyike chochote kudhibiti inflation kwa sasa, isipokuwa tu serikali iwe makini katika kukusanya kodi. Nina wasiwasi kwamba inflation inayotokea sasa kwa kiasi kikubwa inasababishwa na kuwapo kwa fedha nyingi zisizowiana na uzalishaji. Mabilion ya JK, malipo ya wastaafu wa EA na malipo ya malimbikizo ya walimu, marejesho ya fedha za EPA, kampeni za uchaguzi wa viti vya ubunge vilivyoachwa wazi, matumizi makubwa ya serikali, n.k. Kwa maoni yangu binafsi, katika jitihada za kuongeza shughuli za uchumi transitory inflation haikwepeki hata siku moja; tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba fedha hizi zinaongeza uzalishaji katika viwango vilivyokusudiwa ili ku-offset inflation. Policies za kuzuia inflation kwa sasa hazifai na zitadidimiza uchumi ambao tayari umeangamizwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia....kinachotakiwa sasa ni policies za kuongeza uzalishaji.

Nionye tu kwamba suluhisho zote nilizotoa zina faida na hasara, pia utekelezaji wa baadhi ya suluhisho waweza kuwa mgumu. Pia nionye kwamba suluhisho nilizoshauri ni suluhisho za kupambana na inflation na depreciation, sio suluhisho za kuinua maendeleo ya kiuchumi au maendeleo ya watu.

3) Tuache bajeti tegemezi, tuache kutegemea wafadhili

4) Tufungue viwanda vingi sisi wenyewe, tujifunze ku-export ready made material, na siyo rawa materials,

5) Wananchi wanunue bidhaa za ndani , zilizotengenezwa humu humu, baada ya point ya nne kufanyika. viwanda vya ndani vitengenezewe mazingira mazuri ya kushindana na vya nje, to my surprise serikali wanapigana usiku na mchana kuweka mazingira mazuri kwa wageni!

6) point ya 4,5 ikishafikiwa, tuhamasishe matumizi ya fdha yetu ambayo inacirculate humu humu, kiasi ambacho itaongeza thamani ya fedha nje ya nchi.

Kuhusu link yetu na global economy, ndio uchumi wetu huko so vunerable na global economy. Kukiwa na global economic crisis, exports zetu haziuziki (manake imports za bidhaa adimu na muhimu kwa uchumi wetu zinapunbgua), watalii wanaacha kuja, wawekezaji wa nje wanaishia zao, donors waliohaidi kutoa misaada wanakacha, kadhalika shughuli za uchumi zinadumaa.

inatokana na kuwa we have no say about our economy! piga ua!

when you talk about donors, katika nchi yenye kila sababu ya kuendelea yenye, maliasili za kumwaga, when you talk about them, you are confirming that, all these issues of inflation, or whatever may be Tanzania is not a country to talk about! we are exporting raw materials mkuu, thats wrong very very wrong.

waberoya
 
Mkuu naomba shule zaidi hapa.
Swali langu ni hilo la kwanza nililoweka rangi nyekundu. Huko kupanda unakozungumzia mimi napata kizunguzungu. Ebu angalia timeline kwa mfano miaka kumi iliyopita halafu uone net result ya kupanda kwa Tsh yetu.

Mkuu, swali lako la mwanzo halikugusia NET results ya kupanda kwa shilingi yetu. Wewe uliuliza kama ifuatavyo:

Invincible said:
Kwa wenye kumbukumbu nzuri: Kuanzia miaka ya themanini, kuna mwaka ambao thamani ya hela yetu ilipanda kulinganisha na dola ya marekani?.

Hata hivyo kutumia NET results kama indicator ya kupanda kwa thamani ya Tz ni makosa kiufundi na kutoitendea haki Tz Shilling, kwa sababu Tz shilling inapanda na kushuka kutegemea na fractuations za US$ (you can't hold US$ constant and record net depreciation ya Tz shilling, kwa sababu thamani ya US$ haiko constant). Net results ingekuwa meaningful indicator endapo Tz shillings haiyumbi kufuatana na US$.

Kuna nchi moja inayotumia currency ya Kroner. Mwaka 2000, 1 US$ ilibadilishwa kwa Kroner 8.2 hivi. Baadaye ikabadilika mpaka 8.5. Ikaanza kushuka kwenye 7 point something; 6 point something. Mwaka huu mwanzoni ilishuka mpaka 5.xxx. Lakini kwa sasa exchange rate ni 1:7. Wachumi wa nchi hiyo wanasema mwaka huu dollar iliteremka sana (1:5.xxx) kulinganishwa na kroner. Ni rekodi iliyowahi kutokea mwaka 1982.

Wachumi wa Sweeden wako sahihi, na hii haikutokea Sweeden tu bali katika nchi kadhaa, US$ ilikuwa weak na kuzifanya ela za nchi nyingine kuchukuwa advantage. Nchi zilizokuwa within a reach of US$ fractuation band zilikuwa at par with US$ au ziliipita US$...sasa kwasababu US$ ndio inaendesha uchumi wa dunia kwa kiasi kikubwa, nchi nyingi sasa zinaisaka US$ kwa hofu ya depression na hivyo kuisukuma US$ kuchukuwa dominant position, na ndio mana sweedish kroner sasa ina approach its original position (US$1 =7).

Huku ndiko kupanda kwa kroner ninakokuelewa mimi. Hii ya Tanzania haijanielea vema.
.

Nadhani wachumi wa sweeden walielewa kwamba in fact kroner haikupanda (kwa maana halisi ya kupanda) bali US$ iliteremka. Kama ela ya Tz ingekuwa within fractuation band ya US$ hali kama hii ingetokea (yani shilling ingeizidi US$), hii ilitokea Canada. Dola ya Canada iliizidi US$ kwa mara ya kwanza tangu 1979, hapa tunapoongea dola ya Canada tayari imeteremka sana kupita miaka ya karibuni. Hivyo kwa mantiki hii tofauti ya graph ya Tz shilling na Sweedish kroner ni "mchoro tu" unaotokana kroner kuwa within fractuation band ya US$, kamwe haiwezi kuwa graph itakayotumika katika exchange rate forecast.

Pia suala la sisi kuwa sehemu ya global economy, bado nahitaji maelezo ya kunisadikisha. Sisi uchumi wetu umedorora na maisha ya wananchi yameendelea kuwa magumu katika kipindi cha miaka karibu thelathini iliyopita. Katika kipindi hicho hicho uchumi wa dunia ulikuwa katika hali bora(boom). Sasa mbona hatukupata hiyo trickle-down effect ya misaada, watalii, na kuongeza mauzo nje?

Kama bado hujatofautisha kati ya shughuli za uchumi, kukua kwa uchumi, na maendeleo ya watu ni vigumu kuelewa global economic crisis inatuathiri vipi in short term na in long-term. Tusipojuwa concepts hizi ni rahisi kulazimisha inputs (idadi ya watalii) kuwa outputs (maendeleo ya watu). Kinacho trickle-down sio inputs kama misaada, idadi ya watalii, au mauzo ya nje, bali ni output zizokanazo na inputs hizo.
 
3) Tuache bajeti tegemezi, tuache kutegemea wafadhili

Interesting suggestion Waberoya.....nina hofu kwamba uwezekano wa kuacha utegemezi ni sawa na ule ulioongelewa kwenye bibilia unaohusu sindano na ngamia.

4)Tufungue viwanda vingi sisi wenyewe, tujifunze ku-export ready made material, na siyo rawa materials,

This is possible endapo tu tutampitisha ngamia kwenye tundu la sindano kwenye suggestion # 3 juu.

5) Wananchi wanunue bidhaa za ndani , zilizotengenezwa humu humu, baada ya point ya nne kufanyika. viwanda vya ndani vitengenezewe mazingira mazuri ya kushindana na vya nje, to my surprise serikali wanapigana usiku na mchana kuweka mazingira mazuri kwa wageni!

Kuwafanya wananchi wanunue bidhaa za ndani inawezekana kwa asilimia kubwa.

6) point ya 4,5 ikishafikiwa, tuhamasishe matumizi ya fdha yetu ambayo inacirculate humu humu, kiasi ambacho itaongeza thamani ya fedha nje ya nchi.

Yep, ikifanyika suggestion 3 & 4, then 5 & 6 is possible.....can 3 & 4 be done?....may be not in my lifetime.

When you talk about donors, katika nchi yenye kila sababu ya kuendelea yenye, maliasili za kumwaga, when you talk about them, you are confirming that, all these issues of inflation, or whatever may be Tanzania is not a country to talk about! we are exporting raw materials mkuu, thats wrong very very wrong.

Sitaki nianzishe mada nyingine nje ya hii. Ila kwa maoni yangu binafsi huwezi kusema Tanzania ni nchi tajiri kwa kuwa tuna mali asili, wakati hatuna uwezo wakuzifanya mali sili ziwe fedha....umasikini ni pamoja na kushindwa kutumia mali asili zetu ili zitutoe katika umasikini....bottom line? We are poor.
 
Very interesting exchange of ideas from Invincble ,Mgonjwa Ukimwi and Waberoya here.I just hope the personalities that be note the potential out there and take note that we can solve our own problems given the oppurtunity to do so.
 
Mkuu, swali lako la mwanzo halikugusia NET results ya kupanda kwa shilingi yetu. Wewe uliuliza kama ifuatavyo:

Hata hivyo kutumia NET results kama indicator ya kupanda kwa thamani ya Tz ni makosa kiufundi na kutoitendea haki Tz Shilling, kwa sababu Tz shilling inapanda na kushuka kutegemea na fractuations za US$ (you can't hold US$ constant and record net depreciation ya Tz shilling, kwa sababu thamani ya US$ haiko constant). Net results ingekuwa meaningful indicator endapo Tz shillings haiyumbi kufuatana na US$.

Wachumi wa Sweeden wako sahihi, na hii haikutokea Sweeden tu bali katika nchi kadhaa, US$ ilikuwa weak na kuzifanya ela za nchi nyingine kuchukuwa advantage. Nchi zilizokuwa within a reach of US$ fractuation band zilikuwa at par with US$ au ziliipita US$...sasa kwasababu US$ ndio inaendesha uchumi wa dunia kwa kiasi kikubwa, nchi nyingi sasa zinaisaka US$ kwa hofu ya depression na hivyo kuisukuma US$ kuchukuwa dominant position, na ndio mana sweedish kroner sasa ina approach its original position (US$1 =7).

.

Nadhani wachumi wa sweeden walielewa kwamba in fact kroner haikupanda (kwa maana halisi ya kupanda) bali US$ iliteremka. Kama ela ya Tz ingekuwa within fractuation band ya US$ hali kama hii ingetokea (yani shilling ingeizidi US$), hii ilitokea Canada. Dola ya Canada iliizidi US$ kwa mara ya kwanza tangu 1979, hapa tunapoongea dola ya Canada tayari imeteremka sana kupita miaka ya karibuni. Hivyo kwa mantiki hii tofauti ya graph ya Tz shilling na Sweedish kroner ni "mchoro tu" unaotokana kroner kuwa within fractuation band ya US$, kamwe haiwezi kuwa graph itakayotumika katika exchange rate forecast.

Kama bado hujatofautisha kati ya shughuli za uchumi, kukua kwa uchumi, na maendeleo ya watu ni vigumu kuelewa global economic crisis inatuathiri vipi in short term na in long-term. Tusipojuwa concepts hizi ni rahisi kulazimisha inputs (idadi ya watalii) kuwa outputs (maendeleo ya watu). Kinacho trickle-down sio inputs kama misaada, idadi ya watalii, au mauzo ya nje, bali ni output zizokanazo na inputs hizo.

Asante kwa maelezo yako mkuu. Ila bado: Swali langu la mwanzo kuhusu mwaka; na lile la pili la net hayana tofauti kubwa. Mwaka una miezi 12, na kupanda na kushuka kwa Tsh hupimwa kwa vipindi/miezi ndani ya mwaka. Hivi net result ni ndani ya mwaka. Na pia kuna net result ndani ya kipindi hicho cha miaka kuanzia ya themanini. Net result katika vipindi vya aina zote mbili ni minus ya kutisha. Naelewa kupanda au kushuka kwa dola versus other currency hutokana na aidha uimara wa sarafu husika au udhaifu wa ile nyingine(dola). Lakini kwetu hakuna tofauti. Pesa yetu inateremka tu, iwe shughuli za kiuchumi zimeongezeka au uchumi umekuwa kama ilivyokuwa enzi ya Mkapa: Mbona ilikuwa inateremka tu, ilhali Kenya hapo pesa yao ilikuwa inapanda versus dola. Hata Uganda sarafu yao inapanda ukilinganisha na dola au hata ya kwetu.

Katika miezi hiyo michache ambapo Tsh ilionyesha musuli versus dola, tayari mazungumzo dunia nzima yalikuwa juu ya hofu yao kama dola inaweza kubaki kama global currency. Huko India, kuna sehemu za kitalii walikuwa wanakataa kupokea dola ya kiamerika kwa sababu ya hofu hiyo. Hapa kwetu ndio tembo(BOT) akaamka toka usingizini kidogo na kuziuza kwenye soko dola fulani.

Maendeleo kadiri yangu ni people-centred. Sasa kama shughuli za kiuchumi na kukua kwa uchumi hakulengi kumwendeleza mwananchi, hizo ni nadharia nisizozielewa pia.
 
Mkuu, swali lako la mwanzo halikugusia NET results ya kupanda kwa shilingi yetu. Wewe uliuliza kama ifuatavyo:

Hata hivyo kutumia NET results kama indicator ya kupanda kwa thamani ya Tz ni makosa kiufundi na kutoitendea haki Tz Shilling, kwa sababu Tz shilling inapanda na kushuka kutegemea na fractuations za US$ (you can't hold US$ constant and record net depreciation ya Tz shilling, kwa sababu thamani ya US$ haiko constant). Net results ingekuwa meaningful indicator endapo Tz shillings haiyumbi kufuatana na US$.

Wachumi wa Sweeden wako sahihi, na hii haikutokea Sweeden tu bali katika nchi kadhaa, US$ ilikuwa weak na kuzifanya ela za nchi nyingine kuchukuwa advantage. Nchi zilizokuwa within a reach of US$ fractuation band zilikuwa at par with US$ au ziliipita US$...sasa kwasababu US$ ndio inaendesha uchumi wa dunia kwa kiasi kikubwa, nchi nyingi sasa zinaisaka US$ kwa hofu ya depression na hivyo kuisukuma US$ kuchukuwa dominant position, na ndio mana sweedish kroner sasa ina approach its original position (US$1 =7).

.

Nadhani wachumi wa sweeden walielewa kwamba in fact kroner haikupanda (kwa maana halisi ya kupanda) bali US$ iliteremka. Kama ela ya Tz ingekuwa within fractuation band ya US$ hali kama hii ingetokea (yani shilling ingeizidi US$), hii ilitokea Canada. Dola ya Canada iliizidi US$ kwa mara ya kwanza tangu 1979, hapa tunapoongea dola ya Canada tayari imeteremka sana kupita miaka ya karibuni. Hivyo kwa mantiki hii tofauti ya graph ya Tz shilling na Sweedish kroner ni "mchoro tu" unaotokana kroner kuwa within fractuation band ya US$, kamwe haiwezi kuwa graph itakayotumika katika exchange rate forecast.

Kama bado hujatofautisha kati ya shughuli za uchumi, kukua kwa uchumi, na maendeleo ya watu ni vigumu kuelewa global economic crisis inatuathiri vipi in short term na in long-term. Tusipojuwa concepts hizi ni rahisi kulazimisha inputs (idadi ya watalii) kuwa outputs (maendeleo ya watu). Kinacho trickle-down sio inputs kama misaada, idadi ya watalii, au mauzo ya nje, bali ni output zizokanazo na inputs hizo.

We mgonjwa, kabla hujaondoka kwenye hi topic, naomba kujua, hivi kuwa na fedha yenye thamani kuliko dola ina maana kuwa uchumi wako mzuri? Maana nimekuwa nikiona Lira pamoja na Yen zikiwa chini ya USD lakini sijasikia wala kusoma sehemu wanasema hela yao wanataka iwe juu ya dola.

Pili, huku ku-appreciate kwa shilingi unakosema, kuna maana gani kiuchumi? Mimi siyo mchumi ila huwaga naisikia na kusoma kuwa hela ikiwa na nguvu sana export inakuwa ghali! What is this?

Tatu, watu kama wahabeshi, wana hela yako inaitwa brill (sikumbuki) mbona ina thamani, I mean yetu ukifanisha na yao unahitaji TSHS nyingi kupata ile? Sisi tunashindwa vipi kuwafikia au, wamewezaje kubakia pale wakati nimepita kule sioni kama wako mbele yetu kwa namna yoyote?!

Natanguliza shukrani
 
Maswali yamekwenda chuo haya Mwanjelwa. Tuanze moja moja basi.

We mgonjwa, kabla hujaondoka kwenye hi topic, naomba kujua, hivi kuwa na fedha yenye thamani kuliko dola ina maana kuwa uchumi wako mzuri?

Fedha kuwa na thamani kuliko dola kamwe haina maana kwamba uchumi wa nchi umekuwa au unakuwa. Kwanini? Kwasababu thamani ya fedha ni kiashirio tu cha mwenendo wa shughuli za uchumi katika kipindi husika. Thamani ya fedha ya nchi, inaonyesha tu, kwa mfano, mtu anavyotembea kwa wakati husika, haionyeshi mtu huyo kafikia wapi. Uchumi mzuri unapimwa kwa kuangalia ongezeko la pato la taifa (GDP).

Pili, huku ku-appreciate kwa shilingi unakosema, kuna maana gani kiuchumi? Mimi siyo mchumi ila huwaga naisikia na kusoma kuwa hela ikiwa na nguvu sana export inakuwa ghali! What is this?

Pato la taifa (GDP) la uchumi uliowazi kama Tz linaundwa na factor kuu 4. Hizi ni national consumption, investment, government expenditure, na tofauti kati ya import na export). Shilingi yetu iki-appreciate (ikapanda thamani), manake wanunuzi wa pamba yetu waliokuwa wananunua kilo 100 kwa dola moja mwanzoni wanapata kilo 80 kwa dola moja sasa. Kwahiyo kama Tz tunauwezo wa kuendelea kuzalisha na kuuza kilo 100 baada ya appreciation, tunapata faida. Kwa kesi hii appreciation inasaidia uchumi.

Tatizo linakuja pale wauzaji wengi wa pamba wanapogongana na wauzaji wakibongo. Mfano kama shilingi yetu ime-appreciate wakati shilingi ya Uganda na Kenya bado iko constant, wanunuzi wa pamba wataacha kununua pamba yetu na badala yake watanunua pamba ya Kenya au Uganda, mana huko dola yao moja itaendelea kununua kilo 100, badala ya 80 Tz. Kwa kesi hii appreciation imefukuza wanunuzi wa exports zetu, na haisaidii uchumi. Ubaya wa appreciation unaweza pia kuja endapo wanunuzi wa pamba wamegundua bidhaa ya bei nafuu inayofanya kazi kama (au angalau) pamba yetu; kahawa ni mfano mzuri hapa..kugundulika kwa kahawa inayotengenezwa mahabara kunafanya wanunuzi wa kahawa yetu wanywe kahawa ya ya bei poa ya mahabara pale shilingi yetu inapo appreciate.

Tatu, watu kama wahabeshi, wana hela yako inaitwa brill (sikumbuki) mbona ina thamani, I mean yetu ukifanisha na yao unahitaji TSHS nyingi kupata ile? Sisi tunashindwa vipi kuwafikia au, wamewezaje kubakia pale wakati nimepita kule sioni kama wako mbele yetu kwa namna yoyote?!

Ikumbukwe kwamba sio mungu anayepanga thamani ya fedha. Zipo nchi ambazo kwa makusudi zimeamua kupanga thamani ya ela yao. Kama waswahili wanavyosema kupanga ni kuchagua, nchi inapopanga thamani ya ela lazima ikubali hasara za uamuzi huu. Thamani ya fedha ni sawa tu na bei za bidhaa mbalimbali, katika uchumi huru bei ya chungwa lazima iwiane na gharama za kuzalisha chungwa na utayari wa mnunuzi kununua kwa bei hiyo (demand na supply). Chungwa likiuzwa bei ambayo mnunuzi hayuko tayari kununua litaoza, na likiuzwa bei ya chini kuliko gharama la kulizalisha halitazalishwa. Kwa hiyo nchi inapopanga thamani ya ela yake ina risk efficiency katika makuzi ya uchumi wake. Kadhalika nchi inaopoachia soko lirekebishe bei linayakubali mawimbi ya supply na demand...mawimbi ambayo sio mazuri nyakati zote. Zipo nchi ambazo zinaacha soko ipange thamani ya fedha na kuingilia tu pale mawimbi ya supply na demand yanapoharibu shughuli za uchumi kwa muda mrefu kiasi cha kuhatarisha.

Hitimisho, (i) appreciation kiuchumi inatuonyesha mwenendo wa bihashara/shughuli za uchumi, sio kipimo cha kukuwa kwa uchumi (GDP ndio kipimo cha kukuwa kwa uchumi); (ii) appreciation yaweza kuwa mzuri na mbaya kutegemea na mambo mengi kama vile umuhimu wa exports kwa wanunuzi, ubora wa exports katika soko, uwingi wa wauzaji wa export hiyo, kuwapo au kutowapo kwa bidhaa mbadala (a substitute good?), uwezo wa nchi kuzalisha exports...nk. (iii) nchi inaweza kujipangia thamani ya fedha yake, ili mradi tu inakubali hasara zake.
 
Back
Top Bottom