Heko Kwa kikundi cha Mizengwe kwa kazi zao zenye maadili na zinazo fundisha na zenye Uhalisia

Kidenga

Senior Member
Apr 28, 2018
144
445
Kikundi hiki kina miaka mingi sana katika sanaa. Mpaka leo mwanaume hajawahi vaa magauni au nguo za ajabu ajabu.

Wamekua katika mazingira halisi kabisa na bado kazi zao hazichoshi kutazama. Katika kazi zao mwanaume amebakia kuwa mwanaume na mwanamke nae amebakia katika nafasi yake. Kwa anae fuatilia kazi zao nadhani atakubaliana na mimi kuwa kwenye michezo yao mingi wanachekesha lakini kunafunzo mwishoni.

Natamani hawa jamaa kazi zao zibadilishe maisha yao. Kama kuna sera nzuri kwenye kazi za sanaa zihakikishe wananufaika na kazi walizo zifanya na wanazo zifanya.

Ni tofauti kabisa na wanaovaa magauni na wanaume kuigiza kama wanawake.
Madhara ya kazi za aina hii ni makubwa kwa watoto wetu kwani wanazaliwa na kukuta mwanaume akiwa kwenye nafasi ya mke. Ndo wana zidi kuzoea hii hali na mwisho wa siku itakuwa kawaida kwao.

Unaweza tazama kazi hii ya mizengwe
Ni moja kati ya kazi nyingi wanazotoa kila wiki. Tuwatambue na kuwapa support. Makampuni ya biashara tumieni hawa jaama kwenye matangazo yenu. Wanayo nafasi ya kufikisha ujumbe. Kwenye warsha za Serikali waalikeni hawa kama mnavyo waalika wengine.

Mwisho naomba kusema kuwa sina uhusiano wowote na kundi hili bali ni mtizamo wangu kutokana na kazi zao nikilinganisha na makundi mengine ya uchekeshaji yanayorusha kazi zao katika TV mbalimbali
 
Mzee Sumaku mbali na uigizaji pia ni mweka sauti mzuri sana kwenye tamthilia za kituruki zinazotafsiriwa kwa kiswahili, hasa za azam two tv

Ametia sauti katika tamthilia iliyoitwa the city, na sauti yake ikarandana vyema na muhusika aliyeitwa Agah Karaçay
kumbe yupo vizuri
 
Back
Top Bottom