Kauli ya CDF kuwa ''Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi'' imekuja kwa wakati sahihi

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Jeshi ndio nchi, bila jeshi lenye nidhamu hakuna serikali/Taifa imara leo USA, UK, China...nk wanaringa kwa sababu ya majeshi yao imara.

Pia Tanzania yetu tunalala usingizi mtamu na amani nzuri kwa ajili ya jeshi letu bora na lenye nidhamu ya hali ya juu japo wachache wasio na maadili pia wanaweza kuwepo.

Nikirejea kauli ya CDf jana kwamba kuna baadhi ya watu wasio RAIA wa Tanzania wamepewa mamlaka/ vyeo ndani ya nchi yetu kauli inayohitaji jicho la tatu kudili nayo tuelewe kauli imetoka kwa MTU mzito sana kwenye ranki za vyombo vya ulinzi na usalama nchini mwetu.

Ni kweli tumejisahau sana AMANI yetu imetufanya tujione tupo salama wakati sio kweli kwa dunia hii ya sasa Na hapo hapo baadhi ya nchi ndio zimetumia mwanya huo kuingiza watu wao kwenye mifumo nyeti ya nchi yetu na kufanya nchi yetu kuwa uchi.

Tunakubaliana wote kuna watu wa nje wapo kihalali na wanafanya kazi zinazojulikana hata serikali inawatambua Ila ndani yao tukumbuke pia wapo maafisa vipenyo wanaofanya kazi kwa nchi zilizowatuma wakitumia kigezo cha kuwa RAIA wa Tanzania wakati sio kweli hawa ndio CDf anawataka.

Kwanini nasema Amani yetu inatuponza bahati nzuri nimewahi kufika nchi moja Jirani yetu ile nchi kwenye mambo ya usalama hawataki mchezo kabisa baada ya kufika nchi ile tukaenda kupiga picha eneo la benki baada ya muda walifika wanajeshi hatukuelewa hata wametoka wapi wanataka simu zetu wakague zile picha huku wakitishia kutulenga na risasi bahati nzuri kuna MTU aliingilia kati mambo yakawa vizuri.

Next time nimeenda nikawa napiga picha eneo la sokoni ghafla kuna MTU akaibuka ananikanya hurusiwi kupiga picha hapa hii ni tofaufi na hapa kwetu kabisa picha zinapigwa kila kona labda maeneo ya Ikulu tu.

Kumbe basi baada ya taarifa ya CDf ni kazi kwa vyombo vyote vya ulinzi kukaa pamoja na kuanda master plan kwa ajili ya kudili na hii ishu ni kuangalia ni wapi penye mapungufu Je ni Uhamiaji, je ni usalama wa Taifa, Je ni jeshi la polisi na kuja na suluhisho la kudumu.

Napendelea ikawa ni ishu ya kimya kimya na kuwa endelevu kila baada ya miezi kadhaa wanafanya data cleaning kama surprise tukumbuke baada ya kauli ya CDf wao pia watakua wameshtuka na kupanga mipango mengine hivyo jambo hili linahitaji watu wazalendo sana.

Ila tukumbuke vijana wetu wa usalama hawajalala wapo kazini 24/7 wanahitaji kuongeza nguvu tu na kutumia njia za kisasa zaidi nasema hili nikitambua kazi zao nzito kuna jamaa flani kutoka nchi X alijua vyombo vyetu vya usalama vimelala mwisho wa siku kilichomkuta hatokisahau naamini bado kuna vijana wengi tu wazalendo wenyekufanya kazi kwa uweledi mkubwa tu.

Roma ikisema imesema.

Pia soma > Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi
 
Back
Top Bottom