Jmushi1, Kama umenisoma vizuri na wewe mwenyewe ukajitazama na kujipima utanielewa lkn kama utapenda tu kuitazama picha hii kwa rangi zetu hutanielewa.Mkuu nimelipenda bandiko lako kasoro hapo tuu!Je unamaanisha mtoto auwawe?Ama ni vigezoi gani vitakavyo justify kuchoma nyumba za ibada kwasababu ya mtoto huyo?Tolorence ni jambo la maana sana kwa dini zote.
Vita vikianza kwasababu hiyo,basi lazima kuwepo upande wa kukiri udhaifu!Na apande huo ni huo wenye kuleta vita ama vurugu!
Kwanza kabisa naomba unielewe ya kwamba ifike wakati sisi wazazi, walimu, watu wazima na viongozi wetu wawe responsible na accountable ktk matukio haya maana sisi ndio chanzo na tunaowalea watoto hawa kiasi kwamba wamefikia kufanya mambo ya ajabu kabisa. Hii kusema ati mtoto kakojolea Kuruan mnachukulia kama jambo dogo sana tena kuna viongozi wamediriki hata kusema ati walikuwa wakicheza tu!...Huu mchezo gani jamani maana mimi sikuwahi kucheza wala kuona mchezo wa kukojolea vitabu vitakatifu wala kitabu cha shule acha mbali kumkojolea mtoto mwenzangu. Leo mnaita mchezo wa watoto! na umeanza lini mchezo huu nani alouvumbua maana sisi ktk makuzi yetu hatukuwahi kuucheza.
Tumecheza michezo mingi ya utoto lakini sijawahi kusikia mchezo wa aina hii hata siku moja katika makuzi yangu..Na hivyo huyu mtoto kafundishwa dharau hii na aidha wazazi wake, walimu wake au sehemu ya mafundisho ya dini. Haiwezekani kabisa ikawa wao wamebuni mchezo mpya ambao sii utamaduni wa Mtanzania halafu watu wanakuja hapa kutetea wakionyesha wazi kwao kukojolea Kuruan is not a big deal! yet mtu huyu huyu anadai kuwaheshimu Waislaam..Kesho mtoto mwingine atafanya hivyo hivyo. Hivi niulize kama ingekuwa kitendo cha kulawitiana baina ya hawa watoto wawili na mmoja akashitaki bado ingekuwa mnasema ulikuwa mchezo?.
Mkuu wangu nitarudia kusema hivi hakuna sababu yoyote inayoweza ku justify mauaji ama uchomaji moto wa makanisa lakini pamoja na kutokuwepo sababu ni muhimu sana sisi wenyewe kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kusababisha watu kukosa uvumilivu. Tufundishane UPENDO, tuheshimiane na kikubwa zaidi tuwafundishe watoto wetu watambue na kuheshimu imani na mali za wenzatu mbele ya haki zetu sisi wenyewe. Marekani wanasema kuua ni dhambi lakini ukiingia nyumba ya mtu pasipo idhini yake na akahofia maisha yake ana haki ya kukuua hata kama huna silaha. Hivyo acha kuingia nyumba za watu pasipo idhini, piga hodi na subiri ukaribishwe ndio ustaarabu utakao leta amani maana pasipo hivyo ile dhana tu ya kwamba umeingia ktk eneo la nyumba ya mtu tayari kunakuweka wewe hatiani na kumpa reason huyu mtu kukushambulia. Sasa mtu kisha kuuawa ndio tunataka kujenga sababu kuhalalisha tendo la kwanza kinyume cha sheria na kutothamini vya watu jamani?.. Ebu nenda Marekani halafu uichome bendera yao ya Taifa kule Alabama tuone kama kweli watakuacha!
Mwisho mkuu wangu unajua fika mimi Muislaam sijawahi na wala sintoweza kumkashifu YESU ama Ukirstu ni imani ya watu ambayo hainihusu kabisa na ndio maana niko upande mwingine.. na wala mwanangu kukojolea Biblia nikasema ni mchezo au jambo la kawaida tu - No its not! mwanangu hataweza wala kuthubutu maana namfundisha kuheshimu imani za watu wengine na hatakiwi ku cross the line.. Na kusema kweli sijawahi kusikia maisha yangu Muislaam akimkashifu Yesu ila wapo waislaam wanaopingana na tafsiri ya Biblia ktk mafundisho ya Kikristu..na hata kama ikitokea mtu kukashifu huwa tunasema hiyo ni -Blasphemy..
Sasa niwaulizeni nyie ni maneno gani au vitendo gani mtavi consider kama ni Blasphemy kwa dini ya kiislaam vikifanywa na mkristu au mtu mwingine yeyote? ningeomba Mkristu yeyote anipe jibu hapa maana kusema kweli sielewi what you Consider blasphemy in Islaam. Sielewi kwa nini matusi yote ya Uislaam huitwa ni right na freedom of expression isipokuwa ktk Ukristu neno au kitendo kile kile kitaitwa Blasphemy? Ndugu zangu tufundishane kupendana, tukatazane dharau na ushabiki wa kijinga sana ambao unaweza kuzua vita kubwa ambayo hapatakuwa na mshindi isipokuwa vilio, husda na visasi huku tukiwazika vipenzi wetu..