Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Nimesema juzi kuwa ukosefu wa hekima ni janga kubwa la kitaifa kwa kweli nilimaanisha hilo. Tangu habari za mauaji ya Kamanda Barlow yalipotokea mwitikio wa watu wengi umekuwa ni kutokujali, kuhalalisha na hata kushangilia ni kama mtu kusema "akome". Wengi wanahalalisha hili kwa sababu wanaamini ujumbe umetumwa kwa polisi na kuwa polisi 'wanaua watu na sasa kimewarudia'. Kauli hizi ndizo zinazothibitisha ukosefu wa hii hekima.Tumeshuhudia kosa la mtoto mmoja kwenda kuhukumiwa makanisa na wakristu; leo kosa la Kamuhanda anahukumiwa Barlow? Leo hii kosa la askari mmoja wanalaumiwa jeshi zima kiasi kwamba leo chochote kitakachompata polisi tunafurahia?
Ni lazima tujifunze kuwa na hekima ya kutofautisha kitu kinachoitwa "collective punishment" kwamba tunaadhibu wote kwa kosa la mmoja. Labda ni kwa sababu tunaamini (bila kufikiria sana) kuwa "samaki mmoja akioza wameoza wote". Ukweli ni kuwa samaki mmoja akioza siyo wote wameoza!
Kamanda Barlow ahukumiwe kwa matendo yake mwenyewe na si matendo ya wengine. Je alikuwa ni kamanda mzuri kwa polisi, je alisimamia haki na utawala wa kisheria kwa kadiri ya uwezo wake (yaani pamoja na mapungufu yake kama alivyoshughulikia hili la koswakoswa la afisa)? Je kuwa dhaifu kiutendaji adhabu yake ni mauti?
Tuna tofauti gani basi na wale ambao wanaona mtu anapigwa na watu kwa sababu kadaiwa ni 'kibaka' na wao bila kuuliza wanachukua jiwe na kurusha au wanauliza "lete petroli" halafu wanaondoka zao huku nyuma mtu anatiwa kiberiti? Tuna tofauti gani na jamii isiyoerevuka ambayo haitaki kutafuta ukweli inaishi kwa imani na hisia tu?
Mauaji ya Barlow kama yalaivyokuwa mauaji ya Mwangosi na ya wananchi wengine wengi yanapaswa kulaaniwa na siyo kuhalalishwa, yanastahili kupingwa na siyo kutetewa na yanahitaji kukataliwa na siyo kuzoeleka.
Ni wazi kuna mapungufu ya kiutendaji na mambo mengi ambayo hayajibu maswali yetu ndio maana wengine tulitaka maafisa wa juu wa jeshi hilo wang'olewe kwa sababu wameligeuza kuwa ni jeshi la kisiasa sasa. Inapofika watu wanaona jeshi la polisi ni la CCM au lisilo na ule ukaribu wa zamani na wananchi basi ni hatari kwa sababu hawatalipa ushirikiano na wakipata nafasi ya kuwatendea polisi wanawatendea! Mwema, Chagonja na wengine wajuu wanapaswa kuondolewa ili mabadiliko ya kweli ya jeshi yaletwe na watu wenye uwezo. Inapofika watu hawaoni huruma ya mtu kupoteza maisha yake tumefika pabaya.
Hivi mauaji haya yana tofauti gani ya Pro. Mwaikusa? yana tofauti gani na mauaji ya yule Mwanasheria miaka michache iliyopita pale Dar; yana tofauti gani na mauaji wananchi kule Arusha, au Songea? Well.. tofauti ni namna tu lakini ni kuwa wote wamepoteza maisha katika mazingira ambayo hayakupaswa kutokea; ni mazingira ambayo yanahitaji kuchunguzwa na kuondolewa ili isije ikafika mahali huko mbeleni tukasikia Waziri auawa, Mwenyekiti wa Chama cha siasa apigwa risasi au Mbunge auawa au hata iwe yale yale ya Afisa auawa au mwananchii auawa akidhwaniwa ni jambazi!
Hekima inatuita tulaani mauaji haya, kuyapinga na kutaka juhudi zote za kuwaleta kwenye haki zifanyike pasi ya huruma au upendeleo au husuda. Hii haina maana watu tunaridhika na utendaji wea jeshi la polisi. Ushahidi ni mwingi mno kuwa jeshi letu linahitaji mabadilikko ya mfumo (structural reform) ili kulifanya liwe la kisasa zaidi, likijali watu na likiwa linaelewa tunu ya kanuni za demokrasia. Mahitaji ya mabadiliko hayo hayalalishi unyama dhidi ya polisi au raia. Na pamoja na hilo mabadiliko ya msingi yatokee ndani ya jeshi la polisi ili lionekane kweli linajali raia.
Binafsi ninalaani vikali mauaji ya kinyama ya kamanda wa polisi na kutaka haki itendeke kuhakikishwa wahusika wanakutana na mkkono wa sheria. Huwezi kupinga mauaji ya Mwangosi na kutaka haki itendeke halafu ushangilie mauaji ya Kamanda.
Haki ni haki hata ya adui yako ni haki. Mwangosi alikuwa na haki ya kuishi kama vile Barlow alivyokuwa nayo na kama mamia wengine walivyokuwa nayo na ambayo ilikatishwa kinyama. Tusivumilie mauaji ya aina hii kwani yana chochea visasi. Itakuwaje kama polisi nao katika kujihami wanaanza kuua kama mbwa na wananchi wanarudishia kisasi kama wana wazimu?
Litakuwa ni taifa la damu. Damu ambayo isipokataliwa itaendelea kutiririka kama kijito kisichokoma.