Mkuu wangu nimekusikia sana lakini sidhani kama kweli uko tayari kwa vita na kama wewe upo tayari sidhani kama nyuma yako kuna watu watakufuata. Watanzania vuvuzela sana, rutunasema sana lakini inapofikia swala la vita sidhani kama mko tayari isipokuwa kwa sababu za kipumbavu kama hizi.Natamani kukuunga mkono Mkuu Mkandara, kwa matumaini kuwa ulitaka kusema tumefikishwa mahali pa kuchoka.
Nyongeza yangu ni hii: kwamba katika mazingira tuliyonayo sasa, pengine ni busara kuanza kujianda kwa vita ya wao kwa wao, kwa sababu vita si mbaya katika kila maana. Vita inaweza kuwa mapito ya jamii kuboresha nchi. Historia ya mataifa mengi inaonesha vita inao uwezo wa kuboresha nchi. Vita itaboresha Iraq, vita iliboresha Ujerumani, Vita iliboresha ufaransa. Vita iliboresha Marekani. Vita imeboresha Afrika ya Kusini.
Mawazo yaliyosababisha wewe kutoa mchango huu ninaoupatia nyongeza, kwangu yanafanana na mawazo ya mtu mwoga.
Now uwoga unayo nafasi katika kumlinda mtu, lakini mimi nionavyo, amani inayotokana na uwoga wa mmojawapo katika jamii si amani ya haki. Tunahitaji amani ambayo chimbuko lake ni heshima, na heshima katika jamii nyingi imejengwa kwa vita.
Hoja yangu haihusu kabisa nidhamu ya woga na huo Uwoga unazungumzia wewe hauwezi kulingana na UPENDO maana neno hili linatoka moyoni na sii hisia bali kuelewa thamani ya UTU wako na mwenzako. Ni rahisi sana kusema binadamu wote sawa lakini pasipo mapenzi hata ukipigana vita basi vita hivyo havitakwisha. Ni rahisi pia kwako kusema Iraq, Marekani na Ujarumani zilipitia vita na hivyo kuboresha maisha yao lakini ulichoshindwa kuelewa ni kwamba UZALENDO wao ndio ulowasukuma kupigana vita dhidi ya kundi jingine, hawakutengana wala kupigana vita pasipo azma inayowajenga wao kwanza. Haya nambie sisi tutaingia vitani kupigana ili iweje?..
Hakuna Vita vya wenyewe vilivyoweza kuwajenga wananchi wake - HAKUNA isipokuwa kuwakwaza zaidi na zaidi na kuwagawa zaidi na zaidi maana nafisini hakuna UPENDO..Hivyo unaanza kufundishana kupendana kisha Uzalendo unalinda ngome zenu na Udugu hivyo hata adui akiingia mnakuwa tayari kujilinda. Tazama leo hii Hata Malawi wanatusimamia kidete kwa kifua mbele kabisa nna sii wao ntu hata Rwanda ya Kagame wanatuona ssi mazuzu na wala hajakosea maana kisha fahamu Tanzania ya Nyerere haipo tena. Kuna makundi makundi yanaypopingana yenyewe na wameisha poteza dira.. wapo wapo tu duniani wakisubiri kama Sii Mungu basi riziki yao itatoka kwa matajiri... wale wenye ndoto ya ONE DAY YES!