Hekima inapoita: Mauaji ya Barlow yanahitaji kulaaniwa, kukataliwa na yanalia "haki"

Mkuu nimelipenda bandiko lako kasoro hapo tuu!Je unamaanisha mtoto auwawe?Ama ni vigezoi gani vitakavyo justify kuchoma nyumba za ibada kwasababu ya mtoto huyo?Tolorence ni jambo la maana sana kwa dini zote.

Vita vikianza kwasababu hiyo,basi lazima kuwepo upande wa kukiri udhaifu!Na apande huo ni huo wenye kuleta vita ama vurugu!
Jmushi1, Kama umenisoma vizuri na wewe mwenyewe ukajitazama na kujipima utanielewa lkn kama utapenda tu kuitazama picha hii kwa rangi zetu hutanielewa.

Kwanza kabisa naomba unielewe ya kwamba ifike wakati sisi wazazi, walimu, watu wazima na viongozi wetu wawe responsible na accountable ktk matukio haya maana sisi ndio chanzo na tunaowalea watoto hawa kiasi kwamba wamefikia kufanya mambo ya ajabu kabisa. Hii kusema ati mtoto kakojolea Kuruan mnachukulia kama jambo dogo sana tena kuna viongozi wamediriki hata kusema ati walikuwa wakicheza tu!...Huu mchezo gani jamani maana mimi sikuwahi kucheza wala kuona mchezo wa kukojolea vitabu vitakatifu wala kitabu cha shule acha mbali kumkojolea mtoto mwenzangu. Leo mnaita mchezo wa watoto! na umeanza lini mchezo huu nani alouvumbua maana sisi ktk makuzi yetu hatukuwahi kuucheza.

Tumecheza michezo mingi ya utoto lakini sijawahi kusikia mchezo wa aina hii hata siku moja katika makuzi yangu..Na hivyo huyu mtoto kafundishwa dharau hii na aidha wazazi wake, walimu wake au sehemu ya mafundisho ya dini. Haiwezekani kabisa ikawa wao wamebuni mchezo mpya ambao sii utamaduni wa Mtanzania halafu watu wanakuja hapa kutetea wakionyesha wazi kwao kukojolea Kuruan is not a big deal! yet mtu huyu huyu anadai kuwaheshimu Waislaam..Kesho mtoto mwingine atafanya hivyo hivyo. Hivi niulize kama ingekuwa kitendo cha kulawitiana baina ya hawa watoto wawili na mmoja akashitaki bado ingekuwa mnasema ulikuwa mchezo?.

Mkuu wangu nitarudia kusema hivi hakuna sababu yoyote inayoweza ku justify mauaji ama uchomaji moto wa makanisa lakini pamoja na kutokuwepo sababu ni muhimu sana sisi wenyewe kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kusababisha watu kukosa uvumilivu. Tufundishane UPENDO, tuheshimiane na kikubwa zaidi tuwafundishe watoto wetu watambue na kuheshimu imani na mali za wenzatu mbele ya haki zetu sisi wenyewe. Marekani wanasema kuua ni dhambi lakini ukiingia nyumba ya mtu pasipo idhini yake na akahofia maisha yake ana haki ya kukuua hata kama huna silaha. Hivyo acha kuingia nyumba za watu pasipo idhini, piga hodi na subiri ukaribishwe ndio ustaarabu utakao leta amani maana pasipo hivyo ile dhana tu ya kwamba umeingia ktk eneo la nyumba ya mtu tayari kunakuweka wewe hatiani na kumpa reason huyu mtu kukushambulia. Sasa mtu kisha kuuawa ndio tunataka kujenga sababu kuhalalisha tendo la kwanza kinyume cha sheria na kutothamini vya watu jamani?.. Ebu nenda Marekani halafu uichome bendera yao ya Taifa kule Alabama tuone kama kweli watakuacha!

Mwisho mkuu wangu unajua fika mimi Muislaam sijawahi na wala sintoweza kumkashifu YESU ama Ukirstu ni imani ya watu ambayo hainihusu kabisa na ndio maana niko upande mwingine.. na wala mwanangu kukojolea Biblia nikasema ni mchezo au jambo la kawaida tu - No its not! mwanangu hataweza wala kuthubutu maana namfundisha kuheshimu imani za watu wengine na hatakiwi ku cross the line.. Na kusema kweli sijawahi kusikia maisha yangu Muislaam akimkashifu Yesu ila wapo waislaam wanaopingana na tafsiri ya Biblia ktk mafundisho ya Kikristu..na hata kama ikitokea mtu kukashifu huwa tunasema hiyo ni -Blasphemy..

Sasa niwaulizeni nyie ni maneno gani au vitendo gani mtavi consider kama ni Blasphemy kwa dini ya kiislaam vikifanywa na mkristu au mtu mwingine yeyote? ningeomba Mkristu yeyote anipe jibu hapa maana kusema kweli sielewi what you Consider blasphemy in Islaam. Sielewi kwa nini matusi yote ya Uislaam huitwa ni right na freedom of expression isipokuwa ktk Ukristu neno au kitendo kile kile kitaitwa Blasphemy? Ndugu zangu tufundishane kupendana, tukatazane dharau na ushabiki wa kijinga sana ambao unaweza kuzua vita kubwa ambayo hapatakuwa na mshindi isipokuwa vilio, husda na visasi huku tukiwazika vipenzi wetu..
 
Ukiulizwa Barlow ameua nani na wapi utasema? kwa nini makosa ya KAMUHANDA, ANDENGENYE akiwa ARUSHA, Shilogile wa Moro abebeshwe kamanda Barlow?

waambie ukweli mkuu ntamaholo,je wanaweza kumtaja hata raia 1 mwema alieuwawa na barlow au polis wake?au kosa lake kuua mijambazi namiuaji ambayo inavamia nakuiba maliza watu nakuua raiawema?naamini ktk nafsiyangu barlow kauwawa na majambaz ambayo yameshirikiana na mapolis ambao nimajambazi kwakua barlow aliwabana nakuwadhibiti majambazi na mapolis tamaa,wakaamua kummaliza wakamuua,tangulia kamanda cc tuko nyuma yako twaja,sasa wakazi wa mwanza subirini mchipuko mpya waujambazi utakao nawiri upya nakwauhuru zaidi,kwa heri barlow,mwanza watakukumbuka daima kwa uchapakazi wako wahaki ulioleta utulivu na amani jijini mwanza.
 
Acheni watu waonyeshe hisia zao. Ukweli ni kwamba polisi wa tz ni waonevu na wababe sana. Na hii ni justification ya baadhi ya watu kutosikitika kwa kifo cha Barlow.

Hata kama raia hajaonewa yeye mwenyewe au ndugu yake au jirani, lakini dhuluma ni dhuluma tu. Inachukiza mbele ya wapenda haki wote. Na mbaya zaidi polisi mmoja anaweza kuwa amemtendea dhuluma raia mmoja. Raia wengi wanalalamika kitendo hicho; lakini hatusikii polisi wakilaani hiyo dhuluma iliyotendwa na polisi mwenzao. Hii pia ni justification nyingine ya raia kuwachukia polisi kwa ujumla wao.

Nilikuwepo.
 
Mzee Mwanakijiji mimi siongezi neno. Maana kuna watu wametoa maneno ya ajabu kabisa hadi unaanza kuhoji utu wao uko kwenye nini hasa!!

Na walivyomuuwa Daud Mwangosi mbona hatujaona wakisikitika na hata kuwakamata wale walioshiriki kumpiga hadi kufa nashangaa sana mkitoa mapovu kisa ati Kamanda wa mkoa mwacheni eande "HELL,kumbukeni Mshahara wa dhambi ni mauti"
 
Sipongezi mauaji ya kamanda, lakini kimsingi alijiweka matatizoni mwenyewe. Pili haki ichukue mkondo kwa wahusika, tatu, Polisi waache sinema tulizozoezeshwa. Nne malipo ni hapa hapa duniani, kuhesabiwa mbinguni
 
ipo haja ya kutizama kwa kina mmomonyoko wa maadili chanzo hasa ni nini? Maana isiwe yule ambaye anayefanya hivyo akaonekana kwamba ni shujaa,gangwe ama hodari sana katika eneo fulani.Mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu umekuwa ni chanzo kikubwa cha
1.Ongezeko la watoto wa mitaani.
2.Kuongezeka kwa matumizi ya dawa za kulevya.
3.Janga la ukimwi.
4.Umaskini/ufukara.
5.Kutokuaminiana katika masuala nyeti ya nchi.
6.Usaliti
7.Kutokuncha Mwenyezi Mungu.
8.Ukosefu wa ajira.
9.Uzembe/Kutokuwajibika
10.Lawama/kulalamikax2,kiburi,ufedhuri,ukorofi na majigambo.
11.Ubinafsi/rushwa.
 
retaliatory impulse ndio huko kuongozwa na hisia na vionjo. Ninaelewa vizuri sana suala la revenge. Lakini revenge ni kwa yule aliyetendewa ndiye anaweza kusema anataka kujirudishia haki yake. Sisi wengine tunafurahia mauaji ya Barlow kwa sababu katufanyia nini? Kwmaba kwa sababu "polisi wanafanya hivi na vile" basi polisi wote sasa wauawe? Mbona niliandika vizuri tu kwenye suala la Kamuhanda? Wapo watu wanaamini Kamuhanda angeuawa basi 'haki ingekuwa imetendeka" na kufurahia. Mimi bado nisingefurahia wala kuhalalisha. Hatuwezi kujenga na kutetea jamii ya 'dog eat dog'!

MMKJJ naona unajaribu kutwanga ngumi kwenye maji, kweli unashindwa kujua kuwa watu wanafurahia goli moja dhidi ya goli sita walizofungwa? au mwenzetu hujaona hizo goli sita? suala la kama Kamuhanda angeuwawa basi hapo bado watu wangefurahia kwani ingekuwa kama vile beki aliyesababisha tufungwe naye amefunga bao lake na kuleta unafuu wa majonzi ingawa bado wana magoli mengi, nasikitika mtu kumuua mwenzie bila sababu lakini kamwe simsikitikii mwuaji kama Kamuhanda kwenda kuua mwandishi asiye na kosa, Siwezi kusikitika kwa mtu kama kamanda Barlow aliyetetea askari mwenzie katika jaribio la hatari na kijinga kabisa la kutaka kumuua afisa wa uhamiaji kwa sababu ya ngono huku siku zote wakifanikiwa kuua then wanatangaza kuwa marehema alikuwa ni jambazi, Mwanakijiji rudi nyumbani ujionee jinsi mapolisi walivyo majambazi, imefikia hatua wanakukamata hakuna kuonana na nduguzo, wanafunga mawasiliano yako na ndugu wote then upande wa nduguzo wakikufuatilia wanaambiwa kesi yako si ya kutoka leo wala mwezi ujao lakini wakifanya chochote kwa haraka basi kesi itakwisha, fikiria wake zetu walivyowaoga wanaenda kukopa millioni kadhaa wanalipa hiyo rushwa then wewe unatolewa na kufahamu rushwa imetolewa wakati huna kosa hata moja ulilokosa je hao si majambazi?

Kutetea uozo huu ni sawa na kukaribisha mbwa msikitini
 
Mzee! hayo uliyoandika hapo ni kipimo cha busara ulizonazo lakini hasira zilivyotujaa kwa hii midude...... huwezi kuamini.... !!!!! acha tushangilie bana! zinzi lolote dawa yake za shingo tu! isitoshe hii midude inatuuwa kila siku!!!...hapa nilipo kila siku naomba lindege linalombeba yule mrafi anaishi magogoni lianguke afe kabisa!
 
pinda kasema liwalo na liwe usiku huo huo ulimboka katekwa,kateswa na kutelekezwa,wakamkamata kichaa tukaona vizuri tu,hilo likapita,morogoro polisi wakaua wakasema ni kitu kizito hilo nalo likapita,mwangosi akauawa na polisi wakasema ni kitu kizito kimetoka upande wa wafuasi wa chadema,picha zikawaumbua.Je,hapo polisi wana utu?sasa kama wao wanatudhihaki je sisi ndio tuwasikitikie?
bana eeee liwalo na liwe malipo ni hapa hapa duniani tulishachoka.....

Na sasa linakuwa kweli! (alipozomewa huko huko mwanza si alisema sasa lile liwalo linaanza kuwa)
 
Mi kwangu kinachonifurahisha ni kura moja imepotea. Usiniulize nimejuaje kwamba angepigia chama flani.
Labda kama hujui angepigia chama gani.
 
Unakumbuka HEKIMA sasa kwa sababu kauawa Askari Polisi? Walipouawa Raia na wengine kung!olewa kucha ulikuwa wapi?
 
Polisi wa bongo na sheria zao za guilty until proven innocent badala ya innocent until proven guilty. Wacha waonje mauti nao wametesa na Kuua sana. Rest I'n he'll kamanda.
 
Ku ua mtu ni mbaya ila kama saa saba usiku alikuwa na mke wa mtu na sio mara ya kwanza, nafikiri mwenye mke kafanya maamuzi mazuri ya kumtanguliza, ila alitakiwa na huyo mkewe auawe ili waende akhera wote
 
Ukiulizwa Barlow ameua nani na wapi utasema? kwa nini makosa ya KAMUHANDA, ANDENGENYE akiwa ARUSHA, Shilogile wa Moro abebeshwe kamanda Barlow?
hawa watu wanafanya kazi kwa amri hata Barlow angeamrishwa kuua angeua tu mbona watu wake waliona na walikuwepo kipindi wabunge wa chadema highenes walipokuwa wakipingwa usiku walipokuwa wanatoka kwenye kampeni za udiwani askari na wasifanye kitu kama wametumwa vile Ma RPC wanatumika kisiasa sana,kitendo hicho kwa marehemu Barlow ni sawa kabisa.
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom