Hekaya za Abunuwasi

ABUNUASI NA KISA CHA MLIO WA PUNDA

JIRANI yake abunuasi alikua anataka punda kwa ajil ya kusafirisha mizigo yake,akamwendeaabunuasi akamwabia jiran naomba niazimishe punda wako,abunuas akamjibu mimi sina punda, jamaa akafadhaika sana akawa anatoka lkn kabla ajakwenda mbali akamsikia punda akilia toka kwa abunuasi akarudi haraka akamwambia abunuasi umesema huna punda lkn nimeskia mlio wake,abunuasi akamjibu kwan unataka punda au mlio? Akimaanisha yeye ana mlio tuu lkn hana punda.
 
KISA CHA ABUNUWASI NA MHINDI

Siku moja Abunuas kamkodishia muhindi moja vyumba kwenye ghorofa yake ila yeye anakaa chin muhind juu. Sasa abunuas akataka kuuza ile ghorofa muhind akakubal kununua juu tu na hivyo abunuas kumfanya muhind anunue yote akaanza kumfanyia vituko mara abomoe ngaz za kupandia muhind akajenga zake,abunuas akafanya vituko ving muhimd anunue ghorofa ya chin ikashindikana mwishowe akamwita muhind akamwambia nimewaita mafundi wabomoe ghorofa yangu ya chin shika yako ya juu usije ukasema sikukwambia.muhind hoi kwa presha
 
ABUNUWASI NA SULTAN

Abunuwasi alipokuwa na shida na Sultani. Kufika mlangoni kwa sultani wale mlinzi akakataa kumruhusu aingie kumwona. Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa abunuwasi akiingia kwa sulatani atapata anachotaka maana alipendwa sana na sultani. Mkwara aliompa ni kwamba aahidi kuwa atakachopata kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi akakubali na akaingia kwa sultani.

Kufika ndani sulatani anamuuliza sema shida yako abunuwasi maaana leo unaonyesha una huzuni. Abunawasi akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani akashangaa, kwa kosa gani?

Abunuwasi akasema nichape tu Seyidina wangu na akasisitiza kuwa haondoki mpaka achapwe. Sulatani akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu sana viboko mia. Walipomchapa mpaka viboko hamsini Abunuwasi akasema vimetosha maana mlinzi wa pale getini tumekubaliana kuwa nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu
 
ABUNUWASI NA SHEREHE YA MFALME

Kulikuwa na sherehe kubwa kwa mfalme na akaalika watu kibao matajiri, kwenye eneo hilo kulikuwa na maskini mmoja alikuwa na njaa sana ila ndio hivyo hakualikwa kwenye sherehe. Ndani alikuwa na kiporo chake cha wali akakichukua na kukaa nje akisikilizia harufu ya msosi toka kwa mfalme, akala kiporo chake kwa kusindikizia ile harufu nzuri ya chakula.

Alipomaliza akanywa maji akaenda kwa mfalme kumshukuru kwa kushiba! mfalme alikasirika sana akamkwida aeleze ni vipi amekula chakula chake wakati hakualikwa, kesi ikapelekwabarazani itolewe hukumu kesho yake. Maskini akaenda kwa abunuwasi kuomba msaada kwani alijua faini atayopewa hatoweza kulipa, abunuwasi akamwambia tulia kesho tutaenda wote. asubuhi wakaenda, maskini akaambiwa alipe faini, abunuwasi akaenda mbele ya mfalme akamuuliza 'ulimualika maskini?'

Akajibu hapana, sasa alikulaje chakula chako? akamwambia amekula harufu. abunuwasi kamjibu sawa, basi ngoja nikupe faini yako. Akatoa sarafu kadhaa mfukoni mwake akaziangusha chini zikazagaa kwa kelele nyingi, zilipotulia akazichukua na kuzirudisha mfukoni, kisha akamwambia mfalme' kama maskini alikula harufu akashiba, basi umelipwa faini kwa mlio wa sarafu uridhike!'
 
ABUNUWASI nyumba yake iliungua moto,akifikiria atafanyaje na yale majivu ya nyumba yake akapata jibu,akayapakia magunia kibao ya
majivu kwenye punda akafanya safari ya kwenda nchi ya mbali, kufika kule alikuwa na gunia moja lililokuwa na sugari. Akatangazia mji ule kuwa amekuja na biashara ya sukari nzuri sana, wakuu wa mji ule wakapikiwa chai yenye sukari wakaipenda sana. Abunuwas akafanya biashara nzuri ya kuuza na yale magunia yote ya majivu nakurejea kijiji kwake akiwa na ukwasi mkubwa wa fedha. Wanakijiji wakajiuliza huyu bwana imekuwaje kaondoka na yale majivu ya nyumba yake iliyoungua na kurejea na mihela mingi?!...wakajiongeza wenyewe kwa kuchoma majumba yao na miti ili wapate majivu mengi kwenda kufanya biashara alipotokea Abunuwasi.
 
ABUNUWASI nyumba yake iliungua moto,akifikiria atafanyaje na yale majivu ya nyumba yake akapata jibu,akayapakia magunia kibao ya
majivu kwenye punda akafanya safari ya kwenda nchi ya mbali, kufika kule alikuwa na gunia moja lililokuwa na sugari. Akatangazia mji ule kuwa amekuja na biashara ya sukari nzuri sana, wakuu wa mji ule wakapikiwa chai yenye sukari wakaipenda sana. Abunuwas akafanya biashara nzuri ya kuuza na yale magunia yote ya majivu nakurejea kijiji kwake akiwa na ukwasi mkubwa wa fedha. Wanakijiji wakajiuliza huyu bwana imekuwaje kaondoka na yale majivu ya nyumba yake iliyoungua na kurejea na mihela mingi?!...wakajiongeza wenyewe kwa kuchoma majumba yao na miti ili wapate majivu mengi kwenda kufanya biashara alipotokea Abunuwasi.
Hahahaha
 
Abunuasi Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto, Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda Kumnunulia Mtoto Juisi, Masaa 3 Yakapita Bila Abunuasi Kutokea Kinyozi Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?" Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia Tuingie Hapa Tunyolewe Bure."
Huyu Abunuasi wa kisasa. Na bila shaka ni dalali wa vyumba.
 
WAJINGA NDIO WALIWAO


Paliondokea mtu katika kisiwa cha Unguja, enzi za Seyid Majid Bin Said, naye akikaa mjini. Na mtu huyu alikuwa hana kazi maalum, kazi yake ilikuwa ni kuwafuata Waarabu wakubwa wakubwa, na kupata manufaa yake kwao. Na kazi zamani hizo ilikuwa watu kufunga bidhaa na kwenda bara kufanya biashara, na kulima vyakula na kuuza.

Na yeye alikuwa mtu mmoja asiyetaka kazi ya namna hii. Hata hatima akaonelea mji haumweki. Akatafuta kanzu yake njema akavaa, na kilemba chake cheupe, na msahafu wake kwapani, akashika njia kwenda pande za mashamba kutarazaki. Na kazi aliyoichagua ni kazi ya ualimu kusalisha watu. Lakini yeye hajui kusoma hata herufi moja. Alichagua kwenda shamba kwa Wahadimu kwa kuwa huko ndiko walikokuwa wajinga wasiojua kusoma, na hata dini ya Kiislamu ilikuwa haijaingia kwao bado.

Basi Mwalimu akawasili Unguja Ukuu. Wahaimu walipomwona mgeni wakamkaribisha sana. Hata waliposikia kuwa yeye ni mwalimu wakazidi kumkaribisha na kumheshimu. Na yeye mwenyewe ikawa mchana kutwa kufunua msahafu, kutazama tu, watu wanadhani anasoma! Akapewa nyumba bure na chakula kwao. Hatima akawaambia, Jengeni msikiti nikusalisheni. Wahadimu wakajenga msikiti. Hata wakati wa kusali ulipojiri mwadhini hapana, maana wale wenyeji hawajui.

Basi ikawa kazi ya mwenyewe Mwalimu kuadhini. Lakini naye vilevile hajui kitu. Akasimama akaadhini hivi:- Allah Akbar! Allah Akbar! Wajinga ndio waliwao, Wajinga ndio Waliwao. Allah Akbar ! Watu wakajaa msikitini. Huyu mwalimu kama nilivyosema hajui kusoma, si kukuambia kusalisha! Lakini watu wamekwisha kuwamo msikitini, ikawa hana hila ila kusalisha. Akaenda panapo Kibla, akasalisha hivi:- M, m, m,m ,m,m Wajinga ndio waliwao, Amin.

Ikawa kila akisema M,m,m ,m,m ,m ,m Wajinga ndio waliwao, Wajinga ndio Waliwao, Wahadimu huitikia Amin! Ikawa kila akiinama na kuinuka maneno ni hayo hayo. Na Wahadimu wakidhani asema Kiarabu, wakawa wamekazana tu, Amin! Zilipokwisha sala wakatoka nje. Wahadimu wakamsifu sana mwalimu wao jinsi anavyosalisha vizuri. Ikawa hivi hali ya mambo kwa siku nyingi kupita. Wakamfanyia mshahara mwema.

Siku moja akatoka Malimu wa kweli mjini anayejua kusoma na kusalisha ili kwenda kutembea shamba. Akafika Unguja Ukuu. Akapata habari kama mjini pana Mwalimu mmoja arifu sana, ndiye anayesalisha msikitini. Na huyu mwalimu mgeni asiende kumtazama, akangoja mpaka wakati w sala.

Wakati wa sala ulipojiri akamsikia mwadhini anaadhini. Lakini maneno yake yakamstusha sana. Allah akbar! Allah akbar! Wajinga ndio waliwao. Allah akbar! Yule mgeni asiseme neno, akaenda msikitini, akakuta watu wamejaa. Na mbele yao panapo kibla yuko mtu anayemjua tangu mjini, naye kumjua kwake hajui kitu. Basi akamsogelea kule kule mbele ili amsikilize vema. Na mwalimu alipomwona huyu mgeni akastuka sana maana naye amjua tangu mjini. Akawaza kuwa leo uongo wangu utabainika. Lakini mara akili zikamjia hivi:- M,m,m,m,m Mwalimu usinibaini, nikipata sita, tatu zangu, tatu zako, Wajinga ndio waliwao Amin! Na maneno haya wakisikiana wao wawili tu, maana walikaaa karibu karibu. Akashika kusalisha kwa maneno yale yale. M, m,m,m,m,m Mwalimu usinibaini, Wajinga ndio waliwao, nikipata nane, nne zangu na nne zako, Amin.

Akasalisha hivi mpaka mwisho, wakatoka. Walipotoka nje wale walimu wakaamkiana kwa vicheko sana. Watu walipowaona wanacheka,wakidhani wanacheka yao ya huku nje, maana wanajuana. Kumbe wanacheka yaleyale ya Msikitini: Mwalimu usinibaini, wajinga ndio waliwao, nikipata nane, nne zangu, nne zako. Wakakaa katika hali hii wakiwala wajinga, mpaka walipochoka, wakaja zao mjini na wingi wa mapesa.


Hadithi hii inatufundisha nini? na hali ya Tanzania tukiangalia hali halisi ya uwekezaji feki pamoja na mambo mengine. JE sisi pia sio miongoni mwa hao wajinga ndio waliawao?
 
Story ya zamani
IMG-20210420-WA0110.jpg
 
Habari ya sungura

Siku moja sungura alikwenda kula majani matamu
katika shamba la watu. Shamba lile lilikuwa lime-
jaa mimea ya kila namna, hasa michipukizi ya
miharagwe, minyanya, na ya mdewere. Baba yake
mzee akamwambia: Usiende kula mdewere leo.
Nimemwona mwenyewe anatembeatembea sha-
mbani. Ukila chochote atakuua.
Sungura akajibu : Hii si kitu. Hataweza kuniua
mimi. Nikimwona nitakwenda zangu mbio, nitaJi-
ficha. Najua mirm.
Baba yake akasema : Mimi mzee, wewe mtoto.
Akili ya nani? Kabla hujamwona umekwisha kufa.
Lakini sungura hakutaka kusikiliza. Alipenda
mno kula mdewere. Akaenda shambani, akala yote
aliyoweza. Matamu kabisa ! Mara akamwona mtu
mmoja bunduki mkononi. Sungura akajisemea :
Sasa mbio ! Sitaki kufa mimi : mbio nyumbani !
Lakini mtu yule akalenga, akapiga bunduki, risasi
ikampata sungura. Akafa.
Kosa lake mwenyewe. Sungura yule alikuwa
mjinga. Hasikii maneno ya baba.

1628320901410.png
 
Back
Top Bottom