Anaandika Maulidi Kitenge kuhusu Miquissone

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,825
Maji Yamefika Ukingoni

Mfalme mfupi mara ya kwanza alikuja msimbazi akiwa na hasira nyingi za kuutafuta mkate alikuja akiwa binadamu aliyekamilika zaidi na mguu wake wa kushoto ,nakumbuka sana katika zama zile alikuwa juu ya moto alikuwa dhahabu alikuwa almasi,hakika nyakati hazirudi nyuma kwasababu hadithi ya mfalme mfupi kila siku inasogea mbele na maswali magumu yanakuwa mengi kuliko majibu rahisi chanzo ni maji kufika ukingoni.

Katika zama zile za mfalme mfupi bahari ilikuwa safi samaki walivuta hewa safi na upepo mkali ulitii miguu ya dhahabu ya mfalme mfupi,sasa nyakati zimekimbia bahari imejaa uchafu hakuna chochote kinachomtii mfalme mfupi kuanzia samaki mpaka upepo na sababu ya msingi sio kipaji ni matokeo tu ya muda kuamua kuchukua matukio bora yote kwenye kitabu kitakatifu cha mfalme mfupi.Daah ukweli na muda daima ushinda kila kitu.

Jua lilikuwa linazama kwa mbali jahazi lilikuwa linachomoza upande wa mashariki mwa bahari na angani makundi ya ndege yalikuwa yanatoa ishara ya utukufu na maji ya bahari yalikuwa yamefiki kabisa kwenye kingo na mfalme mfupi alikuwa ameshika begi kubwa kuashiri safari ya kurudi nyumbani imewadia,kumbukumbu zinasema lile jahazi lilikuwa limeandikwa MV Miquissone.
1704024096754.jpg
 
View attachment 2858493
Makala za michezo tumuachie EDO KUMWEMBE.
 
Back
Top Bottom