Hekaya za Abuuwasi na hadithi zingine

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,238
12,751
Wengi walisoma hizi hadithi zamani. Ngoja tujikumbushe humu. Pia unaweza kusioma ndani ya maktaba app na vingine zaidi ya 60. Tupm au namba 0715278384 ukitaka kuungwa.


HEKAYA ZA ABUNUWASI NA HADITHI ZINGINE

Bombay; London: Macmillan,1942.
pictuspublishers@gmail.com
Pictuss, 2021





YALIYOMO



kisa cha kwanza
Kisa cha pili
Kisa cha tatu
Kisa cha nne
Kisa cha tano
Kisa cha sita
Kisa cha saba
Kisa cha nane
Kisa cha tisa
Kisa cha kumi
Kisa cha kumi na moja
Kisa cha kumi na mbili
Sultani na mvuvi
Sultani na mkwewe
Mvuvi na jin
Kisa cha majuha wawili wanawake
Jogoo na sungura
Kisa cha paka kupenda mekoni
Kisa cha kuku na mwewe
Kisa cha majuha watatu
Simba na sungura
Fikirini na Hemedi
Kisa cha Wadigo
Kisa cha mtu na wanawe
Hadithi ya mtoto wa sultani na wa tajiri
Wezi stadi
Mtego wa panya huingia waliomo na wasiokuwamo
Mganga na mwanafunzi bubu
Kiburi si maungwan
Kisa cha maskini
Hadithi ya bibi mg'indo
Kwanini watu weupe huitwa wazungu
Kisa cha Ali na watoto wa nduguye
Kisa cha sungura na cheche
Wajinga ndiyo waliwao
Mbwa na paka
Njia ya kuvukia mwenye deni
Nyoka na jongoo
Kweli tatu
Ndoto
Mvivu kupita wote ndiye atakayekuwa mfalme
Kisa cha binti Matlai Shems
Muamini Mungu si mtovu
Kasa na kitatange
Hadithi ya chewa
Kisa cha kuku na kanga
Mtoto wa maskini
Mtu aliyesikia lugha za wanyama
Binti Hamadi
 
KISA CHA I

Abunuwasi alikuwa anapendwa sana na Harun Rashid. Hata ikawa Harun Radhid hawezi kushinda siku moja asimuone Abunuwasi.
Siku moja Abunuwasi akawa anataka kununua punda, na fedha hana. Akatoka akaenda nyumbani kwa Harun Radhid, na wakati si muda wa watu kwenda kwa Harun Rashid. Akafika mlangoni na kuwakuta mabawabu, akataka idhini ya kupanda juu. Mabawabu wakamwambia watu hawana ruhusa ya kwenda juu kwa muda huo. Akatokea bawabu mkubwa na kusema, nitakupa ruhusa upande lakini utakachopata tugawane sawasawa. Abunuwasi akasema, vema! Nimekubali.
Wakaandikiana shahada kwamba atakachopata wagawane sawasawa. Hati ya bawabau akachukua Abunuwasi, na hati ya Abunuwasi akachukua bawabu. Abunuwasi akapanda hata kwa Harun Rashid. Alipofika mbele ta Harun Rashid hakuamkia, akakaa kitako kimya. Harun Rashid adipendezwe na habari ile ya kunyamaza Abunuwasi na kukaa bila kuamkia. Akamuuliza, "Ya! Abunuwasi, una nini leo? Abunuwasi akasema, "nataka unipige fimbo mia moja. Basi Harun Rashid alimpenda Abunuwasi asiweze kumpiga. Akamwambia, "Huachi maneno haya Abunuwasi!"
Abunuwasi akajibu, "La! Lazima utanipiga."
Harun Rashid akatwaa fimbo na kumpiga, lakini kidogo kidogo. Akampiga hata zikatimia hamsini. Hapo Abunuwasi akatwaa hati ya bawabu na kumuonyesha Harun Rashid na kumwambia, "Yuko mwenzangu tumepatana kadiri nitakachopata kwako tugawane nusu kwa nusu. Na sasa mimi nimepata fimbo hamsini na yeye lazima apate hamsini."
Harun Rashid akaamrisha aende akaletwe mkubwa wa mabawabu. Akaletwa, kaamrisha achapwe fimbo hamsini. Akaambiwa hii ni adhabu yako, usirudie tena siku nyingine. Bawabu akajuta kufanya makubaliano na Abunuwasi.



KISA CHA II

Abunuwasi alijenga nyumba yake ya orofa moja. Ilipokuwa tayari, akatafuta mshitiri anunue asipate. Lakini kwa bahati akapata tajiri mmoja aliyekuwa tayari kununua, lakini Abunuwasi akamuuzia orofa ya juu tu, na ngazi yake akamuwekea nje, akitaka kupanda juu sharti apite kwa nje. Mambo yakawa hivi siku nyingi.
Hata siku moja akataka akataka kumalizia kuuza na sehemu ya chini kwa yule tajiri. Yule tajiri akakataa kununua . Abunuwasi akatafuta mshitiri mwingine asipate. Akafanya hila nyingine, akatafuta vibarua wengi sana, akaja nao pale nyumbani pake akamwita yule tajiri aliyekuwa juu, "Bwana, bwana!" Yule tajiri akaitika, "Naam!" Abunuwasi akamwambia, "Mimi nataka kuvunja nyumba yangu hii ya chini, wewe shikilia sana nyumba yako huko juu usije ukasema sikukuambia.
Yule tajiri akashindwa na hila za Abunuwasi, akainunua ile nyumba kwa bei aliyotaka Abunuwasi.





KISA CHA III
Siku moja Abunuwasi alipata dinari zake mia. Akaenda sokoni akanunua punda mzuri, akampanda. Akaenda naye mpaka nyumbani kwake. Hata siku moja akaja mtu kuazima punda wa Abunuwasi. Abunuwasi akamwambia, "Punda hayuko." Mara kidogo punda akalia.
Yule mtu akasema, "Punda si huyo analia na wewe wasema hayuko!" Abunuwasi akajibu, "Sasa wewe umekuja kuazima punda ams umekuja kuazima mlio? Kama umekuja kuazima mlio na mimi nitalia." Abunuwasi akalia, "Ho! Ho! Ho!" Kisha akamwambia, "Haya panda uende zako."



KISA CHA IV
Siku moja punda wa Abunuwasi alikuwa na kiu. Lakini Abunuwasi hakuwa na chombo cha kumuwekea maji. Akaenda kwa jirani yake, akamwambia, "Naomba uniazime sufuria nimnyweshee punda wangu maji." Alipopewa akaenda zake. Akakaa na sufuria ile kwa siku tatu. Siku ya nne, akatwaa ile sufuria , akatia na sufuria ndogo ndani yake na kumpelekea jirani yake.
Alipofika akamwambia, "Sufuria yako hii hapa." Jirani yale alipoitwaa akaona dani yake kuna sufuria ndogo. Akasema, "Hii sufuria ndogo si yangu." Abunuwasi akasema, "Mimi si mwizi, siwezi kuiba mali ya watu. Sufuria yako imezaa ikiwa kwangu, na hiyo ndogo ni mtoto wake." Yule mwenye sufuria akafurahi sana, akasema, "Nyumba ya Abunuwasi ina baraka sana, hata sufuria inazaa!"
Baada ya siku tatu Abunuwasi akaenda kuazima sufuria ileile, akapewa. Safari hii Abunuwasi akakaa nayo hata asiirudishe. Mwenye sufuria akaamua kwenda kwa Abunuwasi kuulizia sufuria yake
Abunuwasi akamwambia, "Sufuria yako imekufa."
Yule bwana akasema, "Shaba hufa?" Abunuwasi akajibu, "Haikuzaa?"
Yule bwana akajibu, "Ilizaa."
"Kila kitu kinachozaa hatima yake hufa." Akasema Abunuwasi.
Yule bwana akashindwa la kumjibu. Akawauliza wanazuoni habari hii nao wakamjibu vilevile.
Kinachozaa na kufa hakina budi. Abunuwasi akahodhi sufuria.



KISA CHA V
Abunuwasi alikuwa anachukiwa sana katika mji wa Baghdad. Siku moja watu wenye vyeo wakamfanyia fitina kwa Sultani, wakataka wamuue kwa hila.
Sultani akamwambia, Abunuwasi, "Nataka ujenge nyumba ya juu angani ikiwa inaelea, kama ukishindwa kuijenga utauwawa. Abunuwasi akasema, "Semaan wataan(nimesikia, nimekubali)."
Akaambiwa kuwa anatakiwa kuijenga nyumba hiyo ndani ya siku tatu. Abunuwasi akasema, "Inshallah." Akaenda nje ya mji na akatengeneza karatasi. Akaunga pamoja kwa wanga, akafabta portangi moja kubwa, akalifunga na kengele na kamba ndefu. Akangoja hata wakati wa upepo mwingi na kulirusha, likaruka juu sana kisha akaifunga kamba panapo mti.
Watu wa mjini wakaona kitu kipo angani na kusikia kengele zikilia. Walistaajabu sana maana hawakuwahi kuona kitu kama kile. Abunuwasi alipoona kazi yake imekamilika akatoka akaenda kwa kwa sultani. Akataka idhini ya kupanda juu ili akaonane na Sultani, akapata.
Alipomuona Sultani akamwambia, ile nyumba imekwisha jengwa maulana. Fungua dirisha utazame. Sultani akafungua dirisha na Abunuwasi akamuonyesha akimwambia, "unaona ileee? Unasikia vitu vinalia?" Sultani akajibu, "Naam, nasikia."
Abunuwasi akamwambia, "Hao ni mafundi wakitengeneza sakafu, na hivyo vinavyolia ni nyundo na misumari. Walakini bwana zimepungua mbao kidogo, nataka ufanye jamala inipatie mbao na watu wapeleke."
Sultan akasema, "watu hao watapita wapi?"
"Njia niliyopita mimi," akajibu Abunuwasi.
Basi sultani akatoa mbao na kuwapa watu. Akawaambia, "pelekeni mbao hizi, mfuateni Abunuwasi.
Abunuwasi akawachukua mpaka pale alipofunga kamba. Akwaambia, "njia ni hii, piteni."
Wakamjibu, "hatuwezi kupita juu ya kamba."
Abunuwasi akawaambia, "sharti mtapita."
Lakini wao wakasema hawawezi. Wakarudi kwa sultani na kumwaambia kuwa hawawezi kupita juu ya kamba.
Sultani akasema, "Kwa kweli hakuna mtu awezaye kupita juu ya kamba."
"Kumbe unajua! Mbona badi ukaniambia nijenge nyumba hewani?" Akasema Abunuwasi.
Sultani hakuweza kumjibu, akanyamaa kimya. Abunuwasi akaenda kukata ile kamba aliyofungia portangi nalo likaruka likaenda zake. Hiyo ndiyo asili ya maportangi.
 
KISA CHA VI
Hapo zamani alikuwako mwanamke mmoja mzee na mwanawe. Nao walikuwa ni madikini sana. Siku moja alitokea tajiri mmoja na kumwambia yule kijana kuwa akiweza kukaa ndani ya ziwa la barafu usiku kucha atampatia dinari elfu kumi.
Yule kijana kwa umaskini akajasirika kwenda kukaa katika ziwa la barafu usiku kucha. Na mama yake kwa uchungu wa mwana akawa akimgojea huku akimmulika. Kulipokucha yule kijana akamwambia tajiri, "nipe pesa yangu."
Tajiri akamjibu, "Sikupi! Mama yangu alikufanyizia moto usiku kucha."
Yule kijana akasema, "La, alikuwa ananimulika tu."
"La, uongo! Amekufanyizia moto." Akasisitiza yule tajiri.
Yule kijana alaenda kushtaki kwa Abunuwasi.
Abunuwasi akamwambia, "vema, nimekubali lakini utanipa kiasi gani utakapopata mali yako?"
"Nitakupa dinari elfu mbili," alijibu yule kijana.
"La, utanipatia dinari elfu tatu," akasema Abunuwasi.
Basi yule kijana akakubali. Abaunuwasi akamwambia, "nenda kadhtaki kwanza kwa sultani." Yule kijana akaenda kwa sultani. Akaeleza mabo yake yote. Alipo maliza sultani akasema, "tajiri yupo sahihi, wewe huna haki."
Yule kijana akarudi kwa Abunuwadi na kumwambia hukumu ya sultani. Abunuwasi akamwambia, "kwa fadhili ya Mungu, kesho utapata haki yako.
Abunuwasi akanunua mbuzi, mchele samli, bizari na vitu vyote vya karamu. Akamchinja mbuzi na kumchuna kisha nyama akaitia ndani ya sufuria. Na mchele pia akautia ndani ya sufuria. Akawasha moto lakini ukawa mbali na vyakula akaviweka mbali. Akawaalika watu kuja karamuni, sultani na mawaziri wake pia. Wakaja wakabarizi mlangoni pa Abunuwasi. Wakakaa hata jioni wasipate hata kahawa. Watu wakachukizwa sana. Wakaenda jikoni wakakuta moto uko mbali na vyakula viko mbali.
Sultani akamwambia Abunuwasi, "Abunuwas una wazimu?"
Abunuwasi akajibu, "kwanini maulana?"
"Tokea asubuhi tumekuja hapa. Hatujatia kitu tumboni na karamu hatuioni?"
Abunuwasi akajibu, "watu wanapika bwana, ila nyama haijaiva." Sultani akaenda akatazama jikoni, akaona nyama iko mbali, mchele mbali na moto uko mbali.
"Vyakula hivi havitaiva hata kwa miaka kumi." Akasema sultani.
Abunuwasi akasema, "vitaiva tu."
"Najua havitaiva, mimi nakwenda zangu, tena na watu nitawaambia waende zao."
Abunuwasi akamwambia, "Maulana usikasirike. Kumbuka yule kijana aliyelala usiku kucha katika ziwa la barafu alikuja kwako kushtaki. Nawe ukanena kuwa tajiri yuko sahihi, na kuwa kijana yule alipata moto kwa kumulikwa na mama yake! Atapataje moto naye alikuwa anammulika kwa uchungu wa mwana tu?. Basi tafadhali bwana, mpe yule kijana haki yake. Maana kama yeye alipata moto, na hivi vyakula vitaiva."
Sultani akasema, "ulisyosema ni kweli tupu." Kisha akamuagiza yule tajiri ampe yule kijana haki yake naye akampa. Baada ya hayo, Abunuwasi akaagiza vyakula vipapikwe, watu wakala karamu. Na Abunuwasi akapata haki yake.



KISA CHA VII
Siku moja Abunuwasi alikuwa mhitaji sana, basi akamwambia mkewe, "leo mhitaji sana mimi, nipe shauri."
Mkewe akamwambia, "mimi sina shauri, shauri kwako."
Abunuwasi akamwambia, "vema, mimi nitakwenda kwa sultani nitamwambia mke wangu amekufa na wewe nenda kwa mkewe na kumwambia mume wangu amekufa. Najua tutapata pesa ya kutumia."
Basi wakaondoka na kwenda kutekeleza huo mpango. Abunuwasi akaenda kwa sultani akamwambia, "mke wangu amekufa." Sultani akampatia sanda na fedha za maziko.
Na mkewe akaenda kwa mke wa sultani na kumwambia, "mume wangu amekufa." Naye akapewa fedha na sanda. Basi wakatoka na kwenda kutumia pesa zile.
Sultani alipoingia kwa mkewe akamwambia, "mke wa Abunuwasi amekufa." Mkewe naye akamwambia, "Abunuwasi amekufa.". Wote wakacheka.
Sultani akatuma watu kwenda kwa Abunuwasi kutazama. Wakaenda na wakamkuta mkewe anamuosha mumewe naye amevaa sanda. Akawaambia, "mume wangu amekufa." Walipotaka kumtia ndani ya sanda, Abunuwasi akapiga chafya na kusema, "Alhamdulilahi, Mungu kadiri, hukifanya hai kilichokufa, na kilicho hai kikafa."



KISA CHA VIII
Ilikuwa siku moja Abunuwasi alisema, "Pindi mwenyezi Mungu akinijalia kupata reale mia tisa tisini na tisa, sitazipokea mpaka zitimie elfu kabisa. Nami niwe kama watu." Watu wakamuona ana wazimu, apate reale elfu kadoro moja asipokee! Maneno haya yakaenea katika mji.
Hata tajiri mmoja akasema, "Ela nijaribu Abunuwasi, hivyo kweli akipata reale elfu kasoro moja ataacha?"
Akatwaa mfuko akatoa reale mia tisa tisini na tisa. Akaenda akaweka barazani pa abunuwasi. Alipotoka nje Abunuwasi akaona mfuko wa fedha. Akachukua ndani akahesabu akaona ni reale elfu kasoro moja
Akashukuru akanena, "Alhamdulilahi, Mwenyezi Mungu amesikia dua yangu niliomba anipe reale elfu.
Na sasa kanipa tisa mia na tisini na tisa, haidhuru, hii moja namkopesha Mungu, najua atanipa siku nyingine zitimie hesabu nitakayo."
Yule tajiri mwenye fedha akaja
kwa Abunuwasi akamwambia, "Umeona mfuko wa fedha hapa?" Akanena, "Naam."
"Zimo ngapi?"
Aka mwambia, "Reale elfu kasoro moja."
Akamwambia, "Basi nipe mwenyewe."
Abunuwasi akanena, "Kwa nini?"
Akasema, "Kwa kuwa ulisema pindi Mungu akupapo reale elfu kasoro moja hutazichukua sharti zitimie elfu."
Abunuwasi akasema, "La hii ni riziki yangu kwa Mungu, naliomba, amenipa. Basi kama amenipa reale tisa mia na tisini na tisa atashindwa kunipa moja?"
Yule taitri alipoona Abunuwas anafitini, akasema, "Twende zetu
kwa Harun Rashid."
Abunuwas akasema, "Kama ni hivyo, Mimi siwezi kwenda vivi hivi, na mimi nipe joho na kilemba na punda kama wewe. Tena ndipo twende barazani, maana sina nguo." Yule tajiri akakubali akampa punda, joho, na kilemba ili kumwazima kuendea mashtakani Wakaenda
Walipofika yule tajiri akasema maneno yake kumshitaki
Abunuwasi. Halafu Harun Rashid akamuuliza Abunuwasi habari
yake. Abunuwasi akasema, "Hawa Watu Wananionea sanaa mimi. Hivi ananisingizia habari za fedha hiyo, hakosi atasema na huyu Punda wake, na joho lake na kilemba chake."
Tajiri akasema, "Nipe basi! Si Vyangu?
Abunuwasi akasema, "Mnaona basi?"
Hata Harun Rashid akaona kweli wanamsingizia. Akaamuru
Achukue vyote abunuwasi.
 
KISA CHA IX
Siku moja Abunuwasi alikuwa anakata mti akawa amekaa kunako ncha ya tawi anakata shinan. Akapita mtu akamwambia, "Umekaa vibaya, hili tawi litakapoanguka na wewe utaanguka, maana umekaa nchani, unakata shinani." Abunuwasi akasema, "Sianguki, hii ndiyo namna ya kukata miti mimi kuanzia leo."
Yule mtu akaenda zake.
Abunuwasi akawa anakata ule
mti, ulipoanguka, na yeye akaanguka. Akaondoka
upesi akamkimbilia Yule mtu aliyemwambia utaanguka. Akamwambia, "Ee bwana, nataka uniambie na siku ya kufa kwangu."
Akamwambia, "Kwa nini?"
Akasema, "Sababu umeniambia, nitaanguka, na mimi nimeanguka kweli."
Akamwambia, "Nalikuonya umekaa vibaya, lakini siku ya kufa sijui."
Aka mwambia, "Sharti utaniambia."
Yule mtu akataka salama yake, akamwambia. "Siku utakapopanda punda wako akajikwaa mara tatu, hujafika unakokwenda. Siku hiyo ndiyo mauti yako.
Abunuwasi akakaa, siku moja akapanda punda wake akaenda shamba. Zamani za kurejea aka mpiga
sana punda wake akaenda shoti. Punda akajikwaa kwa kule kwenda mbio. Akaenda tena mbio tena, akajikwaa ya pili, Abunuwas akasema, "Kufa kwangu karibu sasa."
Akaenda mbele akajikwaa ya tatu. Abunuwas akashuka juu ya punda, akajifunika shuka, akajilaza twaaa kama mtu aliyekufa. Na yeye kulala huku asema kafa, maana aliambiwa punda akijikwaa mara tatu ndiyo kufa kwake.
Basi akalala namna ile siku tatu, watu mjini wanamtafuta.
Hata siku ya tatu akapita mtu mmoja akamuona Abunuwasi, akamwuliza, akamwambia, "ile njia ya kwenda mjini kwa Harun Rashid iko wapi hapa."
Abunuwas akaamka, akamwambia, "Mimi nafahamu nilipokua hai ukipita mwembe ule hata upandie pale; utakapofika mjini."
Yule akamwambia, "mbona unasema ulipokuwa hai?" akamwambia, "naam, sasa nimekufa mimi."
Akalala tena. Mara wakapita mabedui wamepanda ngamia. Walipofika pale alipokuwa Abunuwasi wale ngamia Wakashtuka, wakafanya machachari. Wale mabedui wakaudhika walipofahamu kama
Abunuwas ndiye aliyewashtua ngamia, Wakampiga
sana kwa bakora, na Abunuwas akanyamaza kimya, maana kafa. kisha Mabedui wakaenda zao.
Yule mtu aliyeuliza njia, alipofika barazani kwa Harun Rashid akawasikia watu wanaulizana habari ya Abunuwas. Yule mtu akasema, "Abunuwas yuko hapo kalala, asema kafa."
Harun Rashid akasema, "Mimi namjua Abunuwas mkienda kumwita tu haji. Chukueni baragumu mpaka alipo mkapige, kisha mwambieni Abunuwasi, Ondoka, amri ya kiyama imekwisha kuwako."
Wakaenda watu wakapiga baragumu. Wakamwambia,
"Abunuwas ondoka amri ya kiyama imekuwako."
Abunuwas akaondoka akajipangusa, akavaa nguo, akafuatana nao kwenda mjini.
Alipofika mjini watu wakamzunguka, wakamfanyizia mzaha, "Abunuwas kafufuka!"
Wengine wakamwuliza habari za ahera. Abunuwas akawaambia, "Ahera hakuna lolote. Watu wanatutisha tu kutuambia ahera hivi, ahera hivi, lakini hakuna lolote. Neno moja lipo, njaa, hapana kula huko."
Nayo kweli, maana alikaa siku tatu hakula. "
Tena neno la pii akawaambia, "Neno baya nililoona huko kuwa baya sana ni hili. Kuna Mabedui huko wamepanda ngamia, ukipambana na hao watakupiga sana."
Nayo kweli maana yeye ndiye waliyempiga
Harun Rashid akamwuliza habari za kufa kwake, Ilikwendaje? Akamweleza yote.
Haruni Rashidi akamwambia, "Mtu huyo amekusmbua sana."
Akanena, "La, hakunisumbua amenifaa sana. Sasa mimi najua habari zote za ahera."


KISA CHA X
Abunuwasi alikuwa anachukiwa sana na watu wa Baghdad kwa mambo yake ya kuudhi watu. Wakaenda wakamfitini kwa Harun Rashid, Harun Rashid akaamuru atupwe katika kisima, na ndani ya kisima hiki alikuwamo simba. Abunuwasi akafanya hekima, Alipofika chini kazi yake ikawa kumkunakuna yule simba asimle, hata mwisho wakazoeana.
Chakula cha Abunuwas ikawa nyama aliyokuwa akitupiwa simba kila siku.
Abunuwas akakaa mle kisimani jumla ya siku nyingi. Hata watu wakafanya kumsahau mjini. Siku moja ikatokea ibra kubwa katika mji. Walipoamka asubuhi wakaona umetokeza mkono wa mtu baharini, umenyosha vidole vitatu.
Watu wakastaajabu.Wakampa habari mfalme. Akatoka kwenda kutazama, yeye na mawaziri wake, wakauona mkono wa mtu kweli, umetokeza baharini umenyosha vidole vitatu. Wakatafuta kujua maana yake wasijue. Wakaitwa wanachuoni wote wakaulizwa maana yake asitambue mtu.
Walipoona wameshindwa kutambua maana yake, wakataka kuuondoa ule mkono. Wakaisha kufanyiza uganga na uganguzi mkono haukutoka. Hata mwisho watu wengine wakamkumbuka Abunuwasi, wakasema, "Angekuwapo Abunuwasi angetuambia maana yake mkono huu."
Wakampa habari Harun Rashid. Na yeye akaona kweli maneno yao.
Basi akatuma watu kwenda kumtazama Abunuwas kisimani.
Walipofika wakaita, "Abunuwas!" Akaitika, "Naam!"
Wakanena, "Mfalme anakutaka utoke."
Akanena, "Siwezi kutoka sina nguo."
Wakaenda kwa mfalme wakamwambia, "Abunuwasi kasema hawezi kutoka, hana nguo."
Mfalme akawapa shuka kwenda kumpa Abunuwasi. Abunuwasi alipopata shuka pa kuvaa chini akaipiga kilemba.
Wakamwambia, "Fanyaa sasa toka."
Akanena, "Siwezi kutoka sina nguo bado."
Wakamwambia, "Nguo hatukukupa sasa hivi?"
Akanena, "La, nimepiga kilemba." Wakampelekea nyingine akavaa. Halafu wakamwambia, "Sasa toka."
Akanena, "Nitatoka namna gani nami sina fulana, wala kanzu, wala joho?"
Wakatafuta vitu hivi waka mtupia, akavaa, akawaambia, "Sasa tayari nitupieni kamba," wakamtupia. Akaishika
ile kamba akawaambia, "Haya vuteni." Wale juu wakawa wanavuta, na, yeye akatwaa fimbo anamkuna yule simba, na huku anapandishwa juu.
Alipofika juu akapelekwa kwa Haruni Rashid Mfalme akamwambia habari za ule mkono wa mtu. Abunuwas akanena, "Nina njaa, nipeni chakula kwanza."Wakamfanyizia chakula Wakampa. Alipokwisha kula akawaambia, "Haya twendeni kunako mkono." Akatoka mfalme na jumla ya watu wakafuatana na Abunuwasi mpaka pwani. Abunuwasi akasimama kuukabili mkono. Na yeye akanyoosha mkono Wake akapunga kama vile anakaidi kitu. Mkono Ukafunga kidole kimoja Abunuwasi akapunga tena mkono, mkono ukafunga kidole cha pili. Halafu ukabaki mkono umenyosha kidole kimoja, Abunuwas akatikisa mkono ukaondoka. Watu wakastaajabu wakamuuliza Abunuwasi tafsiri yake. Abunuwas akanena, "Mkono ule umekuja kuuliza kama katika dunia ipo siri ya watu watatu? Mimi hupunga mkono, hunena la, hapana siri ya watu watatu. Vikabaki vidole viwili, maana yake, Je siri ya watu wawili ipo? Nikanena la, haipo.
Hapo kikabaki kimoja, maana yake, Ya mmoja je? nikanena, Naam siri ya mtu mmoja, ndiyo Maana mkono ukaondoka."
Watu wakamsifu Abunuwas kwa akili zake.
Harun Rashid akampa abunuwasi nyumba na zawadi nyingi. Akawa mtu mkubwa katika mji.
Hata baada ya siku kupita mfalme akaota ndoto kama katika nyumba aliyompa Abunuwasi, upande wa kushoto kuna makasiki ya fedha chini. Asubuhi akapeleka watu kwenda kuchimba nyumba ya Abunuwasi ghairi ya kumpa habari mwenyewe. Wakaichimba ile nyumba wasipate kitu. Habari hii ikamuudhii sana Abunuwasi. Akanena, "haidhuru nitalipa kisasi."
Akamwambia mkewe, "Mke wangu pika wali mzuri; kitoweo kuku."
Mkewe akapika wali akaisha. Akamwambia, "Haya sasa wewe toka nenda katembee." Abunuwasi akatwaa sahani na bakuli ya mchuzi akatia ndani ya sinia, akaweka chini ya meza, akafunika kwa kitambaa cheupe.
Kisha akafunga nyumba, na ufunguo akaweka juu ya mlango, akaenda zake. Njiani akakutana na vijana watatu. Akawaambia, "Najua ninyi vijana wa siku hizi jeuri sana, hivi nakuoneni mnakwenda upande wa nyumbani kwangu, msiende mkatwaa ufunguo ulio juu ya mlango, mkafungua nyumba, mkatazama chini ya meza, mkaona sahani ya wali kitoweo kuku, mkala na sahani na bakuli mkafunika ndani ya sinia bila kuosha."
Wale vijana wakaona ajabu maneno ya Abunuwas. Wakanena, "huyu anatutuma nini tukale huu wali?"
Wengine wakanena, "Kwanza wali wenyewe upo? Twendeni tukatazame."
Wakaenda wakafanyiza kama alivyosema Abunuwasi. Wakatwaa ufunguo juu ya mlango, wakafungua nyumba, wakatazama chini ya meza, wakaona upo wali kweli.
Wakautwaa wakala. Sahani wakazifunika ndani ya sinia bila kuosha, wakatoka wakaenda zao. Abunuwas akapima kiasi cha wale vijana kula wali hata kwisha akarudi kwake. Alipofungua nyumba akaona wamekula wali. Basi akachukua sahani na sinia zimefunikwa vile vile mpaka kwa Haruni Rashid, akanena, "kuna watu nawashtaki wamekula wali wangu."
Rashid kanena, "Wako wapi?"
Akanena, "Hawa nimewafunika ndani ya sahani."
Akaambiwa, "Funua tuwaone basi."
Akafunua, wakatoka inzi wakaruka. Akanena, "hawa ndio ninaowashitaki."
Sultani akamwambia Abunuwasi, "unashtaki hata inzi?"
Akanena, "wao ndio walionikosa, asiyenikosa siwezi kumshitaki nami nataka unihukumie kama sheria."
Sultani akamwambia, "nimekupa ruhusa kila utakapomwona nzi ametua mpige."
Akampa na hati ya mkono wake.
Abunuwasi akachonga rungu kubwa. Ikawa hupita madukani akiona inzi wametua juu ya tende huzipiga zile tende akazitawanya tawanya. Akikuta juu ya papa huwapiga akawaponda.
Na watu wakipiga kelele kwa ajili ya kuharibiwa vitu vyao. Abunuwas husema, "Mimi sipigi vitu nawapiga inzi."
Hata siku moja Abunuwas akamwambia mkewe, nitakwenda lipa kisasi cha kuchimbiwa nyumba yangu. Akaenda barazani kwa Sultani na fimbo yake. Akakaa karibu na Sultani. Hata mazungumzo yaliposhika sana, akaja inzi akamrukia Sultani kipajini. Abunuwasi akatwaa fimbo ke akampiga Sultani e fimbo ya kipajini, kisasi cha kuchimbiwa nyumba yake!
Watu wakamkamata Abunuwasi wakataka kumfunga.
Abunuwas akanena, "Kama mtanifunga, mwanifunga kwa kunionea, mimi sikumpiga
Sultani, nimepiga inzi aliyemtua Sultani. Na ruhusa ya kupiga inzi amenipa yeye mwenyewe nimpige nitakapomwona ametua. Na hii hati ya mkono wake." Ikatazamwa hati ikaonekana kweli akaachiwa Akaenda zake nyumbani kwake.
 
KISA CHA XI
Mtu mmoja alisafiri, naye alikuwa na ng’ombe jike mmoja. Kabla hajaondoka alimpeleka ng’ombe wake kwa mtu mmoja katika mji. Na yule mtu ana ng'ombe wake dume mmoja. Alipokuwa safarini yule mtu ng’ombe wake kazaa, wakatimia watoto saba. Aliporudi akaenda kwa yule mzee kuchukua ng’ombe wake. Naye anazo habari kuwa ng'ombe wake kazaa.
Alipofika akanena, "nataka ng’ombe wangu na watoto wake." Yule mzee akanena, "nenda zizini kamchukue ngo’mbe wako Yule yule uliyeniachia."
Yule mtu akanena, "itakuaje na ng’ombe wangu kazaa."
Akanena, "la, ng’ombe wangu dume ndiye aliyezaa. Wewe wako alipokuj, alikuja hana mtoto na sasa mchukue mwenyewe."
Yule mtu akaenda akisikitika, akafika kwa Abunuwasi. Akamueleza habari iliyompata. Abunuwasi akakubali kumsaidia. Abunuwasi akaingia ndani akatwaa nguo za kimaskini akavaa akaenda kwa yule mzee kwa masikitko sana, akasema "mzee nikopeshe rupia tatu , nikamfae baba yangu ndiyo kwanza amezaa."
Yule mzee akasema, "usifanye mzaha na mimi, kama amezaa mama yako nitakupa." Abunuwasi akasema, "la, hapana bwana baba yangu ndiye aliyezaa."
Yule mzee akanena, "sijapata kusikia kama mwanamume huzaa."
Abunuwasi akamwambia kama, "hujasikia leo ndio kwanza."
Basi mzee asikubali.
Abunuwasi akasema, "kama mwanamume hazai imekwendaje basi ukanyang’anya ng’ombe wa huyu kijana? Unasema ngo’ombe wako ndiye aliyezaa naye dume! Afadhali ungesema unataka uchungaji wako."
Yule mtu asiweze kumjibu Abunuwasi akawatoa wote saba akampa mwenyewe.



KISA CHA XII
Siku moja palikuwa palikuwa na tajiri akachinja mbuzi wake. Wakati wa kupika mbuzi huyu, akaja maskini mmoja na chakula chake akakaa upande unakoendea upepo akala chakula chake kwa kutowelea harufu ya mbuzi. Asubuhi Yule maskini akakutana na Yule tajiri akamwambia, "bwana umenifaa sana jana, nimetowelea harufu ya mbuzi wako hata nikashiba."
Tajiri akasema, "kumbe! Ndiyo maana mbuzi wangu hakuwa na ladha kwa sababu tamu yote umechukuwa wewe."
Akaenda akamshitaki kwa Haruni Rashid na yeye alikuwa anapendelea saba matajairi. Basi yule maskini akalazimishwa kutoa rupia thenashara. Maskini akaenda zake akilia, maana fedha hana. Akakutana na Abunuwasi, alipomuuliza akamueleza yote
Abunuwasi akamwambia maskini, "usilie."
Akatwaa Abunuwasi rupia zake thenashara akampa, akamwambia, "nakupa hizi nenda kalipe lakini usitoe mpaka nitakapokuja mimi."
Asubuhi wakakutana wote kwa sultani maskini akasema amekuja kulipa zile fedha lakini akasikitika sana akasema yeye hakula nyama, katowelea harufu tu. Mara akatokea Abunuwasi wakamweleza yalivyokuwa.
Kisha abunuwasi akamwuliza maskini, "unazo rupia thenashara?"
Akajibu, "ninazo."
Abunuwasi akazitwaa zile fedha akazishika, akamwita tajiri atwae fedha yake. Alipotaka kupokea, akamwambia, "ngoja."
Akazitupa chini akamwambia, "haya chukua huo mlio wa hizo rupia. Maana maskini naye hakula nyama amekula harufu tu." tajiri akashangaa kwa visa vya Abunuwasi, akashindwa,
Abunuwasi akamwachia maskini zile rupia akaenda zake
 
SULTANI NA MVUVI​

Alikuwako Sultani katika nchi ya Uajemi. Siku moja akaenda kutembea pwani pamoja na waziri wake. Wakamkuta mvuvi anatengeneza mishipi yake tayari kwenda baharini, na siku hiyo bahari imechafuka vikubwa na upepo unavuma mtindo mmoja. Sultani akamwita mvuvi, "ya" mvuvi akaitikia, "naam maulana."
Akanena, "palipo wanne na wanne hawakifu wanne?
Mvuvi akajibu hawakifu wanne."
Mvuvi akajibu, hawakifu wanne bwana."
Sultani akamuuliza, "unamtumikia mtu au unatumikia nafsi?"
Mvuvi akajibu, "naitumikia nafsi."
Sultani akanena, "ya mvuvi hallah! Hallah!"
Mvuvi akasema, "mimi mchokozi bwana namjua pweza alipo."
Sultani na waziri wakashika njia kurudi mjini. Njiani sultani akamuuliza waziri, "umefahamu maneno yale niliyosema mimi na mvuvi?"
Waziri akasema, "la sikufahamu."
Akamwambia, "wewe waziri mzima usifahamu maneno yale, akayafahamu mvuvi! Sharti unifahamishe."
Akamshika waziri hata asiwe na raha.
Waziri akaona hana njia ila amtafute yule mvuvi amuulize, akamwita kwake akamwambia, "nataka maana ya maneno yale uliyosema na sultani pwani?"
Mvuvi akamwambia, "sijui maana yake, mimi nilijiseme tu."
Waziri akamwambia, "tafadhali niambie nitakupa reale miteen."
Mvuvi akasema, "sijui." Akamwambia, "nitakupa reale hamsi mia."
Mvuvi akasema, "bwana wangu sijui fasiri yake."
Akamwambia, "nitakupa shamba langu la mahali fulani."
Akanena, "bwana sijui."
Hata mwisho akamwambia, "nitakupa hii nyumba yangu ninayokaa."
Mvuvi akamwambia, "niandikie hati ya mkono wako bwana," akamwandikia.
Akamwambia, "sasa nitakueleza, Sultani aliniambia palipo wanne na wanne hawakifu wanne.
Maana yake Sultani aliona ile dhoruba iliokuwako akaona ajabu kuniona mimi natengeneza nyavu kwenda baharini, ndipo akaniambia, 'wewe katika mwaka kuna miezi minne ya kaskazi ndio wakati wa uvuvi wa samaki kuna miezi minne ya maleleji ndio wakati wa bahari kuwa shwari, basi miezi hiii nane huwezi pata samaki wa kutosha kuweka miezi hii minne ya kusi?' Na mimi nikamwambia akiba ya miezi minane haitoshi kuwa akiba ya miezi hii minne ya kusi."
Waziri alipopata tafasiri hii akatoka akaenda kwa sultani. Akamwambia, "nimekwisha pata fasiri ya maneno yako na mvuvi." Sultani akamwambia umefahamu mwenyewe?"
Akanena, "naam."
Sultani akafurahi akampa zawadi. Baada ya siku si nyingi, sultani akapata habari kama mvuvi anakaa katika nyumba ya waziri. Maneno haya yakaenea katika mji hata sultani akataka kujua maana yake. Akamwita mvuvi akamuuliza, "amepataje kuwamo katika nyumba ya waziri?"
Akamwambia, "nyumba ni yangu sasa ya waziri."
Sultani akamuuliza, "imepataje kuwa yako."
Akanena, "bwana unafahamu siku ile pwani uliponiambia Hallah! Hallah!? Nalifahamu kuwa umeniambia usimpe rahisi. nami nikakwambia mimi mchokozi namjua pweza alipo maana yake mimi maskini najua njia ya kupata pesa, sitamwambia ila kwa kupata faida kubwa na sasa nimepata faida nakaa nyumba ya waziri."
Sultani alipoona kama waziri wake amemdanganya akakasirika sana akamwita akamwambia, "umenidanganya ya kuwa umetambua kwa akili zako kumbe umeambiwa! Basi sasa hufai wewe kuwa waziri. Umekuwa mwongo na mjinga. Huyu mvuvi ndiye atakayekuwa waziri wangu."
Mvuvi akawa waziri, akastarehe siku zake zote.
 
SULTANI NA MKWEWE​

Palikuwa na Sultani aliyekuwa na binti mmoja naye alikuwa akimpenda sana. Akampeleka chuoni akapata kuwa hodari sana katika elimu. Na katika mji ule alikuwako kijana mmoja wa kimaskini, lakini naye alikuwa amesoma vyema sana. Basi ikawa wakitokea watu wa kumposa yule mwanamke binti Sultani mtoto mwenyewe hukataa. Akamwambia baba yake, "Mimi sitaki kuolewa na mtu ila na Sefu," ndiye Yule mtoto wa maskini. Baba yake akamhoji sana, "kwa nini kutaka Sharti akuoe huyu?"
Akanena, "moyo wangu ndivyo ulivyopenda."
Sultani alipoona mwanawe ameshika,akakubali. Lakini akasema, "Sina budi kumtazama ili nijue kama ni kijana mwenye akili." Akamwita yule kijana, akamwambia, "nakwenda, kutazama watu mahali fulani, name sitaki kufatana na mtu ila wewe."
Yule kijana akanena, "vema."
Wakaondoka wakaenda. Njiani wakaona mpunga umepandwa, umekwisha ota, una kimo chema, tena umezungushiwa uzio. Yule kijana akamuuliza Sultani, "nini hiki?"
Sultani akanena, "si mpunga huu!"
"Na hiki kilichozungushiwa ni nini?"
Akamwambia, "si uzio huu?"
Kijana akasema, "hivyo?"
Wakaenda mbele wakakuta watu wanalinda ndege mnamo mpunga. Wanapiga kelele, "Hao! Hao! Hao!"
Sultani anapita kati ya makonde ya mpunga wao wamekazana tu "Hao! Hao! Hao!"
Yule kijana akamuuliza, "wanafanyaje hawa?"
Sultani akamwambia, "si watu hawa wanalinda ndege? Na hao wanaofukuzwa ni ndege."
Moyoni mwake mwake Sultani anamuona yule kijana kuwa mpumbavu. Maana maswali yote anayouliza ni ya kijinga. Wakazidi kwenda mbele.
Wakaona visima vingine viko kwa juu na vingine kwa chini. Wakaona watu wanakoga vile vya juu, na wengine wanateka maji ya kunywa hivi vya chini. Yule kijana akauliza, "nini hivi?"
Sultani akasema, "Si visima hivi?" "Na wale watu je?"
Sultani akanena, "wale wanakoga. na hawa wanateka maji ya kunywa."
Kijana akaitikia, "Eh-e-e." Wakaenda zao wakafika walikokuwa wakienda. wakakaribishwa vyema wakamletea sultani maziwa ndani ya kalasia. Akapokea yule kijana akayanywa kwanza kisha akampa Sultani. Halafu ikaja kahawa, naye kafanya vile vile. Sultani akaudhika na habari ile. Akaona kijana huyu mjinga, na bado hana adabu.
Hata walipokuwa wanarejea hawakuwa na mazungumzo mema. Maana Sultani alikuwa ameudhika sana. Akafika nyumbani kwake, binti yake akamwuliza, "je, baba umemuonaje mkweo?" Sultani akajibu, n"isikusikie tena unamtaja kijana yule. Kaniudhi namna gani! Mjinga na bado hana adabu."
Binti yake akamuuliza, "nini ujinga wake baba?"
Akamwambia, "kwanza tulikuta mpunga umezungushiwa uzio. Akauliza nini hiki?"
Basi binti yake akamwambia, "baba hujui kwa nini ameuliza?"
Akamwambia, "sijui." Akamwambia, "baba, mpunga ni majani tu, waweza kuanguka kwa upepo, na watu wanatwaa miti mikubwa wanazungusha. Ile miti ikianguka haitavunja mpunga?
Miti haina akili haiwezi kuzuia mpunga."
Sultani akaona kweli.
Akamwuliza ujinga wa pili, Sultani akanena, "Aliuliza watu waliokuwa wakilinda ndege, kwa kupiga kelele, 'Hao, Hao, Hao!''' Binti yake akamwambia, "waona ajabu huyo kuuliza? Alistaajabu kwa kuwa watu hawa wanamuona Sultani anapita nao wasinyamaze kidogo. Ndege hao watakula mpunga gani? Tena kule kusema Hao! Hao! Hao! Wakati Sultani anapita watu wengine hawatadhani ni ndege, watadhani hao ni Sultani na mkwewe."
Sultani akaona kweli.
Akamwuliza ujinga wa tatu, akamwambia habari ya vile visima, na watu kuoga juu na kunywa vya chini. Binti yake akanena, "Baba basi hayo si dhairi? Kuwaje watu kuoga vya juu na kunywa vya chini?
Yale maji wanayokoga ndiyo yanayokuja hivi visima vya chini."
Sultani akaona kweli. Binti yake akauliza, "nini tena?" Akamwambia, "sasa nikuelezee ukosefu wake wa adabu." Akamweleza habari ile ya kutangulia kunywa maziwa na kahawa. Binti yake akamwambia, "yeye kafanya hayo kwa akili yake. Wewe Sultani wanakuhasimu watu wengi. Aliona huyu kijana huenda wakatia sumu, au kitu cha dhara yoyote katika vitu hivi, ndipo akanywa yeye mbele." Sultani akaona yakuwa binti yake amesoma elimu vema, na yule kijana anamtaka kwa ajili ya akili zake. Akakubali kumwoza.
 
MVUVI NA JINI​

Alikuwako mvuvi mmoja maskini, naye mcha Mungu sana. Alikuwa na kawaida akienda kuvua mshipi wake hutupa mara tatu tu atakachovua ndio chake na asipopata huwa basi.
Siku moja akaenda kuvua akatupa mshipi wake majini, akavua mzoga wa punda. Akanena, "ya Rabi mambo gani tena haya? Sasa imebaki mishipi miwili tu. Akatupa mwingine akavua vigae vya nyungu! Akanena, "Hayo mambo gani tena! Sasa umebaki mshipi mmoja sijui nitavua nini?" Akatupa mshipi wa mwisho akavua chupa ya shaba, alipoona ya kuwa ni shaba akasema, "haidhuru nitakwenda uza hii shaba nitapata pesa za kutosha kununua chakula." Akatikisa, akasikia kinalia kitu ndani. Akasema, Ebu nijaribu kufungua nitazame kilichomo ndani.
Alipofungua akatokea jini mrefu, akasimama karibu yake, akamwambia, "ukitaka umekufa, usitake umekufa. Mimi nilifungwa na nabii Sulemani ndani ya chupa hii, nikatupwa baharini nimekaa baharini karne kadha wa kadha, Nikaweka nadhiri kama mtu akinivua kunitoa humu nitamjaza mema mengi. Hata nilipoona miaka imepindukia nikasema hapana, kwa ghadhabu zangu nikanena, 'mtu atakayenivua nitamuua' wala hapana vingine, basi na wewe ukitaka umekufa, usitake umekufa."
Binadamu akamwambia, "basi bwana mkubwa ijazi yako ya kukuvua ndiyo hii, kutaka kuniua mtu niliyakutendea mema?"
Jini akasema, "mimi sifahamu hayo, nataka uchague unataka kufa namna gani, lakini kufa huna budi."
Basi wakashindana hata wakasema twende tukashitakiane, wakashika safari kwenda zao mjini njiani wakamkuta ng’ombe, binadamu akamsimamisha na kumwuliza ng’ombe, "Ati bwana mtu akikutendea wema humlipa maovu?"
Ng’ombe akauliza, "kulikoni?" Akaelezwa kile kisa chote cha jini na binadamu, Ng’ombe akanena, "kweli mtu halipwi maovu kwa mema, lakini si ninyi binadamu. Binadamu astahili kutendewa hayo maana si kitu Mimi nawapeni maziwa ya kunywa, na nyama yangu mnakula, na ngozi yangu mwaifanya viatu, na nyingine mwaiwamba ngoma, basi huu wema?"
Jinni akasema, "Je! Binadamu unasikia, akamwambia nasikia lakini twende zetu." Wakaenda mbele wakakuta mnazi wakauliza kama walivyo muuliza Ng’ombe, Mnazi ukasema, "Binadamu astahili kutendewa kama hayo maana si kitu. Mimi mnazi nawafaa sana, nazi zangu wanapikia, kifuu wanakoka moto, makumbi wanafanya kamba, makuti wanaezekea, wakiwa na kiu nawapa maji, na ijazi yangu ni kunikata na kunifanya kizingiti!"
Jini akanena, "je binadamu unaskia? Akanena, Naskia lakini ushahidi ni mara tatu, twende mbele. Walipokwenda mbele wakakuta watu watatu, Yule binadamu akawauliza wale watu swali lile lile. Yule jini akasema, Maneno ni yale yale ya ng’ombe na mnazi, hawa binadamu haikosi watakupendelea wewe binadamu mwenzao.
Wale watu wakanena, "sisi hatuwezi kusema maana habari yenyewe hatusadiki. Ilikwendaje bwana mkubwa kama wewe kukaa ndani ya chupa hii?"
Jini akasema, "kama hamsadiki ngojeni niwaoneshe. Akaingia ndani ya chupa akasema nalikaa hivi.Wale wakafunga chupa hodari. Wakamwambia, kaitupe baharini akaenda akaitupa ukawa ndio mwisho wa uvuvi.
 
KISA CHA MAJUHA WAWILI WANAWAKE​



Hapo zamani za kale palikuwa na maskini katika mji mmoja. Maskini huyo alioa mke na akazaa naye mtoto mmoja wa kike. Alikuwa na ng’ombe mmoja jike na ndiyo ilikuwa rasilimali yake pekee. Na kazi yake ilikuwa ni kulima makonde uko nje ya mji.
Kila siku wakati wa kuingia mjini huchukua majani ya ukoka kama chakula cha ng’ombe wake. Bibi na mtoto hubaki nyumbani. Hata siku moja alipokuwa yule mtoto ametimia miaka saba umri wake, aliota ndoto usiku.
Na ndoto yake ilikuwa ameota kaolewa tena amezaa mtoto mwanamke mzuri sana. Asubuhi baba yake akaamka akaenda kondeni kwake. Yule mtoto alipoamka akaangua kilio akalia, "mama wee! Mama wee mtoto wangu yuko wapi?"
Hata mama mtu akasikia kilio akaenda chumbani akamwuliza, "je mwanangu walilia nini asubuhi yote hii?"
Mtoto akamjibu mama yake kuwa, "nimeota ndoto usiku mmenioza mume, kisha nikazaa mtoto mwanamke mzuri, sasa naamka simwoni, ndiyo maana nalia, umemchukua wewe mama." Akasema hivi na huku analia.
Mama mtoto aliposikia habari ya mtoto aliyezaliwa usiku na kumwona mwanaye analia, naye akaangua kilio akalia. Ikawa kelele moja kwa moja, hata majirani mtaani wakasikia vilio wakaja nao kusikiliza kuna nini? Mama mtu akawaelezea watu mambo yote ya ndoto, majirani wakacheka sana wakanena, "Haya mambo! Hatujapata kuona sisi watu kulia kwa sababu ya ndoto." Lakini wale wenyewe wamekazana kulia,
Jirani mmoja mzee alipoona hawa ni wapumbavu, na kelele zikazidi akataka kuwanyamazisha akaenda kumwambia yule mama, "bibi hapana maana kukaa kitako ukilia, kama mtoto aliyezaliwa usiku amekufa, iliyobaki ni kuweka matanga nakuondoa.
Lakini aliyekufa kwa kuwa ni mtoto mdogo fanyeni chakula tu mpate kuondoa msiba."
Yule mke wa maskini akasema, "hayo ni mashauri mazuri lakini nitafanyaje mume wangu hayupo, naye ndiye mwenye mashauri ya mapesa."
Yule jirani akamwambia, "huna hata kikuku ukachinja?"
Akajibu, "nyumbani hamna kitu ila ngombe wa bwana naye anampenda sana. Akaambiwa, "utafanyaje basi, nawe una sharti ya kuondoa msiba huu, usipoondoa itakua uchimvi utakufa wewe au mume wako."
Yule mwanamke aliposikia vile akafanyiza hofu, akaona afadhali amchinje huyu ng’ombe maana sina kitu kingine.Akaita watu akagiza wamchinje ng’ombe.
Watu wakachekelea sana wakajua leo ndio kufaidi. Wakamchukua ng’ombe wakamchinja, wakamchuna upesi upesi. Wakatwaa mguu wakaenda wakabadili kwa mchele, wakatwaa nyama nyingne wakabadili na vitakataka vingine vya kupikia, Mara upishi ukasimama ukapikwa wali hata ikipata saa saba chakula tayari
Akaitwa mwalimu kuja kusoma hitima. Watu wengi wakaja kula chakula ikawa tena kila aliiyesikia akaja na wote waliokuwa wakija wakapata chakula. Hata habari ikaenea mji mzima kwa maskini kuna hitima, na wakisifu chakula kwa wingi wakati huu wote mume yupo shamba analima hana habari za hitima nyumbani kwake, Kasikia kwa watu waliokuwa wakitoka mjini kwenda shamba lakini hakutia moyoni maana hali ya nyumbani kwake anaijua mwenyewe. Akakaa hata saa zake za desturi akang’oa ukoka wake, akashika safari taratiibu kwenda zake mjini.
Wakati huu kule nyumbani wale watu wamekwisha ondoka, maskini akafika nyumbani kwake mkewe akamlaki juu kwa juu, karibu bwana karibu. Yule maskini kimya akaongoza njia moja kwa moja mpaka zizini, akatua mzigo wake aingie ndani ya zizi ng’ombe hayumo!
Akashangaa, "ng’ombe wangu yuko wapi?"
Mara mkewe akaja akamwambia, "Mume wangu twende ndani nikakupe habari za mkasa ulionipata, na nikuelezee ng’ombe wako yupo wapi."
Yule maskini akasema, "siendi popote mpaka nimwone ng’ombe wangu kwanza, Mkewe akamwambia, Bwana twende ndani nikakueleze."
Lakini yule madjini akasisitiza, "nieleze hapa hapa." Yule mkewe tena akaona hana budi kumweleza mambo yaliyopita akamweleza yote. Maskini aliposikia kuwa ng’ombe wake amechinjwa kwa ajili ya ndoto, akaduwaa, asijue la kutenda, akaingia ndani akakaa kimya, mkewe akamletea chakula asiweze kula.
Hata usiku Yule maskini akamwambia mkewe, "tangu kuzaliwa sijapata kuona juha kama wewe. Ilikwendaje wewe kusikiliza maneno ya ndoto? Basi sasa nifanyizie mikate nataka nisafiri nataka niende mbali nitafute mtu mwingine aliye juha kama wewe. Nikimwona utakuwa mke wangu hivi hivi. La sikumwona nitakuacha."
Asubuhi mkewe akamtengenezea mikate akafunga akachukua na karatasi na bahasha na wino. Akaondoka akaenda zake msitu na nyika hata zikatimia siku saba akafika katika mji mmoja mkubwa. Na yeye kwa kuwa alikuwa na mashauri yake moyoni hakuingia mjini, akafika katika kibanda cha kizee mmoja mwanamke. Yule mwanamke hakukasirika akamkaribisha, akamfanyizia na chakula.
Yule mgeni akauliza sana habari za mjini, na habari za wakubwa wa mji, kizee mwanamke akamwambia, "mwanangu, je, una haja nao hata ukawauliza hivyo?"
Akanena, "naam, shughuli kubwa." Hata ilipofika usiku kizee akamwuliza, "je utakwenda mjini leo au utalala hapa leo?" Akanena, "Ningependa nilale hapa, asubuhi niingie mjini."
Yule kizee akamwambia, "karibu mwanangu, ipo nafasi tele hapa." Akapewa chumba cha pili katika kibanda chake. Yule mgeni akafurahi sana alipoingia chumbani kwake akafunga mlango wake akatoa karatasi zake, akakaa kitako akaandika barua zake, moja kwa Sultani, moja kwa binti Sultani moja kwa waziri, moja kwa mke wa waziri.
Akazifunga katika bahasha kila barua bahasha ya peke yake.
Asubuhi akamwuliza Yule kizee nyumba za watu hawa aliowaandikia barua ziko wapi?
Yule kizee akajibu, "Nyumba za watu hawa wote zipo pwani forodhani, ila nyumba ya Binti Sultani iko nje ya mji si mbali kwa kutoka hapa." Akauliza namna ilivyokaa, na alama zake akaambiwa zote, basi alipokwisha pata habari zote alizozitaka akaaga akasema, "kwa hapa mama sina budi kwenda mapema nikamuwahi kila mtu nyumbani kwake niwape barua zao."
Akaondoka akaenda akishika njia akaingia mjini akafika panapo ile nyumba ya binti Sultani. Akatazama huku na huko akaona tanuru ya chokaa na ile tanuru inaelekea penye dirisha la binti Sultani. Akachimba chini ya ile chokaa. Akangoja mpaka alipoona sasa ni sa tatu akajifukiza pale penye chokaa kwa kichwa chake, na huku anapiga kelele, "Eeh! Jamani nifaeni mwenzenu natoka, mbali mimi, shime jamaa." Mara akachungulia mtumishi dirishani akaona chokaa inatutumuka na kichwa cha mtu kinatokeza, akaenda akamwita bibi yake akamwambia tazama chini, "Kitu gani kile?"
Akachungulia chini akaona mtu anaotokeza penye chokaa na huku akipiga kelele. Mara binti sultani akamwita mtumishi mwana mume akamwambia, "Uledi nenda upesi ukamtazame mtu yule ana nini?"
Mara Uledi akaenda akamwuliza, "wewe ni shetani au binadamu?"
Yule mgeni akasema, "mimi ni mtu lakini natoka ahera nimetumwa kuja kuleta barua za watu hapa mjini. Je sasa mimi nipo wapi hapa?"
Uledi akamwambia, "hii nyumba inayokukabili ni nyumba ya binti Sultani." Yule mgeni akasema, "ooh! vema sana ninayo barua yake hapa."
Uledi akamshika mkono akatoka katika ile chokaa, akampeleka uani, akapewa maji akaoga, akapewa na chakula, na wakati wa kula akistaajabu. "Hivi ndiyo chakula cha ulimwenguni wa siku hizi?" Anafanya kasahau maana yake katoka ahera. Alipokiwsha wakampeleka kwa bibi, kufika tu yule mtu akamwamkia bibi, akatoa barua akampa, akamwambia, "barua yako hii yatoka ahera kwa mjomba wako, naye anakusalimu pamoja na bwana."
Binti sultani akafungua barua akasoma nayo imeandikwa hivi:
"Saalam mjomba, mimi huku ahera sijambo, na jamaa wote waliopo wazima ila mimi nina dhiki ya deni, nilikopa fedha za watu nami sina cha kuwalipa, basi tafadhali mpe huyu niliyemtuma rupia elfeeni aniletee nilipe deni za watu. Salaam Wakatabahu Mjomba wako."
Yule binti Sultani aliposoma ile barua alisikitika sana akaenda zake moja kwa moja mpaka chumbani akafungua bweta akatoa rupia elfeeni ndani ya mifuko miwili akaenda. Kwenye sanduku la nguo akatoa kanzu ya hudhurungi safi na kanzu melimeli iliyo safi, na kanzu ya doria iliyo safi. Akatoa na buraa Muskati moja, na kitambi cha debwani iliyo njema, na kofia nyeupe ya kazi nzuri.
Akatwaa na vitu vingine vidogo vidogo kama miski, na halundi akatafuta kileso kikubwa cha Hariri akafunga pamoja na vitu hivi vyote. Kisha akaandika barua kwa mjomba wake ahera akaandika hivi:
Salaam mjomba, waama baada ya salam barua yako imewasili. Nami nimefurahi kuniletea huyu mtu wa kunipasha habari ya kuwa wewe mzima, na vitu ulivyoagiza nimempa huyu mtu, nimempa rupia elfeeni, na nguo maana nasikia nguo adimu sana huko.
Salaam, mimi Binti Sultani.
Akampa bahasha Yule mtu wa ahera na barua hii. Akamwambia, "mchukulie mjomba mwambie bwana hukumkuta, ungepewa zaidi ya hivi." Binti Sultani akaendelea kusema, "je nikupe mtu akuchukulie mizigo?"
Yule maskini akanena, "itanilazimu kuchukua mwenyewe maana ahera haendi mtu ila aliyekufa. Basi kwa heri, bibi sina budi kwenda upesi maana jua linapanda na sisi watu wa ahera jua linaatuathiri."
Yule mgeni wa ahera alipotoka nje akaona haina haja ya kupeleka zile barua nyingine.
Akatazama huko na huko akaona mahali njia inapita kwenda vichakani akachagua njia hii, akashika njia kwenda zake. Njiani akapita akasema kimoyo moyo, "Ah! Kumbe majuha wapo wengi nikadhani ni mke wangu tu Kumbe hata katika watu wakubwa wamo majuha!"
Akashika njia akaendda zake upesi upesi, akaviisha vile vichaka akatokea katika mashamba. Alikua anakwenda hivi upesi kwa kuwa alishuku kuwa atafuatwa. Alipofika mle shambani akamkuta mzee mmoja analima, akamwambia, "eeh baba umepta habari za mjini leo?"
Yule baba akasema, "la! Sina habari, kumetokea nini?"
Yule mtu wa ahera akajibu, "imetoka amri kwa Sultani watafutwe vizee vya shamba wote wauawe iwe kafara ya nyumba moja ya Sultani inayojengwa, basi mimi kwa hisani yangu napenda uvae hii kanzu yangu, na mimi unipe nguo zako za kulimia unipe na jembe lako nilimie, na wewe panda juu ya mnazi huu utazame juu njia ya mjini utaona mtu anakuja."
Sasa turudi kwa binti Sultani baada ya kuondoka huyu mtu wa ahera mara bwana mume wa binti sultani akarudi nyumbani, akamkuta mkewe ana majonzi akamwuliza, "je bibi una nini?"
Yule bibi asiseme neno akatwaa ile barua akampa mumewe akaisoma. Alipokwisha soma akamwuliza mkewe jinsi yalivyokwenda mambo haya, mkewe akaleza yote jinsi alivyokuja mtu wa ahera akaleta barua hii, na yakuwa amempa mjomba wake wa ahera haja aliyotaka na zawadi nyingine.
Yule mume akakasirika sana akamwuliza mkewe, "wewe una wazimu! Sasa niambie huyu mtu kaenda njia gani?" Akaambiwa kapita ile njia ya vichakani, mara akaagizwa atandikwe farasi akavaa nguo zake, joho, kilemba na upanga mkononi. Akapanda farasi ili kumfuata huyu mwizi mkubwa lakini akamwambia mkewe, "fahamu mimi namfuata huyu mtu maneno yake yakinielea vema utakuwa mke wangu lakini ukiwa ni upuuzi wako na wazimu nitakuacha."
Akatoka akaenda zake kwa kasi. Basi alipokuwa anakuja mbio, Yule mjumbe wa ahera akasema, "je sikukwambia miye?" Mara yule mpanda farasi akafika pale akamkuta Yule hasimu wake analima. Akadhani huyu ni baba shamba tu, akamuuliza, "hukumwona mtu anapita hapa na bahasha?"
Akamjibu, "sikumwona bwana lakini tazama huko juu mnazini, kuna mtu: huyo ndiye aliyekuja kutoka huko mjini, alipofika hapa akapanda juu ya mnazi, nilipomwuliza akasema anaogopa basi sijui kama ndiye unayemtafuta."
Yule bwana akamwuliza yule mtu kama anajua kupanda mnazi, yule akasema, "la bwana sijui." Yule mwarabu akawa ameshikwa na uchungu, akawa anataka kumwua yule aliyekuwa juu ya mnazi, basi akavua nguo zake kanzu na joho na kilemba na jambia akampa yule mgeni wa ahera amshikie pamoja na farasi. Yeye akapanda juu ya mnazi. Alipokuwa akipanda akawa anasema, "utanitambua leo mwizi mkubwa wewe, leo kutoka yangu au yako."
Na yule aliyekuwa juu akaona kuwa maneno ya yule mgeni wa ahera kuwa ya kweli. Akadhani huyu anakuja kuniua kwa habari ya amri iliyotoka. Basi naye akamwambia, "haya njoo nami nikuoneshe kazi kama sikukupiga na mundu wangu, yule mwarabu akawa anapanda tu, wala hatazami chini.
Yule mjumbe wa ahera kule chini akaenda akatwaa bahasha yake akafunga juu ya farasi. Akatwaa na zile nguo za mwarabu akazifunga juu ya farasi akampanda, Huyooo! Akaenda zake. Yule mkulima aliye juu ya mnazi akamwambia mwarabu, "Ela! Ebu tazama chini yuko wapi farasi wako?"
Akatehemu, kwenda juu hawezi, kushuka chini hawezi. Kisha akaona hana hila ila kushuka apate hakika ya maneno yale. Akamwambia yule mzee, "shuka chini tupate kuulizana vema. Yule mzee akakataa kushuka mpaka mwarabu alipomwapia kuwa hatamuua. Basi wakadhuka wote. Walipofika chini mwarabu akamwambia, "nipe habari ya yule habithi." Mkulima akampa habari yote tangu mwanzo, alivyokuja na aliyosema, na kumtisha kwa amri ya mfalme iliyoko mjini. Hata ikajiri kubadilishana nguo na yeye kupanda juu ya mnazi, hata kutokea yeye mwarabu.
Yule mwarabu aliposikia kisa hiki, badala ya kukasirika akacheka sana. Na yule mkulima naye akanwambia mwaarabu, "Ela na mimi nieleze ilivyokwenda huko mjini." Mwarabu akamweleza habari zote za barua ya ahera, na vitu alivyopewa. Wote wawili wakakauka kwa vicheko.
Yule mkulima akamuuliza mwarabu, "sasa ukienda nyumbani, Utakwenda kusemaje?"
Yule mwarabu akasema, "Sina la kusema ila nitakwenda kumwambia bibi kuwa nimemkuta yule mtu, nami niliposika habari za ahera moyo wangu ukaingia huzuni sana, hata sikuweza kustahimili nikampa farasi wangu na nguo zangu zote awachukulie watu wa ahera. Je! waonaje kizee?"
Kizee akasema, "Kwell maneno yako. Mana ukisema kuwa umenyang'anywa utachekwa sana. Mwarabu akarudi mjini na kikoi chake na Jambia lake mkononi. Kisha akafika kwa mkewe.
Mkewe akamuuliza, "jinsi gani bwana nguo zako na farasi viko wapi?"
Akamwambia, "kweli maneno yako bibi. Habari za ahera nilizosikia kwa yule mjumbe wa ahera zimenitia huzuni sana, hata nimempa farasi na vitu vyangu vyote kuongezea vile uilivyompa wewe."
"Bai sasa Bibi na tukae. Lakini pamoja na hayo akija mtu mwingine kutoka ahera usimpe kitu mpaka unishauri."
Sasa tumrejee yule mjumbe wa ahera. Baada ya kupata farasi akamwendesha kasi, akaenda mwendo Wa siku chache kuliko alivyokuja maana sasa kapanda farasi. Akafika hata kwa mkewe, amechoka kwa kwenda mbio. Akamfungua farasi mzigo wake akaimweka katika lile zizi la ng’ombe wake. Na mzigo akauweka ndani.

Alipokwisha pumzika na kula chakula akamweleza mkewe mambo yote ya safari yake. Akamwonyesha na fedha. Akanena Sasa na tukae kitako mke wangu nimekwisha muona aliye juha kuliko wewe. Lakini Pamoja na hayo ukitokea tena Upuzi wa ndoto wajibu uningoje unieleze tufanye shauri pamoja. Wakakaa raha mustarehe.
 
KISA CHA XI
Mtu mmoja alisafiri, naye alikuwa na ng’ombe jike mmoja. Kabla hajaondoka alimpeleka ng’ombe wake kwa mtu mmoja katika mji. Na yule mtu ana ng'ombe wake dume mmoja. Alipokuwa safarini yule mtu ng’ombe wake kazaa, wakatimia watoto saba. Aliporudi akaenda kwa yule mzee kuchukua ng’ombe wake. Naye anazo habari kuwa ng'ombe wake kazaa.
Alipofika akanena, "nataka ng’ombe wangu na watoto wake." Yule mzee akanena, "nenda zizini kamchukue ngo’mbe wako Yule yule uliyeniachia."
Yule mtu akanena, "itakuaje na ng’ombe wangu kazaa."
Akanena, "la, ng’ombe wangu dume ndiye aliyezaa. Wewe wako alipokuj, alikuja hana mtoto na sasa mchukue mwenyewe."
Yule mtu akaenda akisikitika, akafika kwa Abunuwasi. Akamueleza habari iliyompata. Abunuwasi akakubali kumsaidia. Abunuwasi akaingia ndani akatwaa nguo za kimaskini akavaa akaenda kwa yule mzee kwa masikitko sana, akasema "mzee nikopeshe rupia tatu , nikamfae baba yangu ndiyo kwanza amezaa."
Yule mzee akasema, "usifanye mzaha na mimi, kama amezaa mama yako nitakupa." Abunuwasi akasema, "la, hapana bwana baba yangu ndiye aliyezaa."
Yule mzee akanena, "sijapata kusikia kama mwanamume huzaa."
Abunuwasi akamwambia kama, "hujasikia leo ndio kwanza."
Basi mzee asikubali.
Abunuwasi akasema, "kama mwanamume hazai imekwendaje basi ukanyang’anya ng’ombe wa huyu kijana? Unasema ngo’ombe wako ndiye aliyezaa naye dume! Afadhali ungesema unataka uchungaji wako."
Yule mtu asiweze kumjibu Abunuwasi akawatoa wote saba akampa mwenyewe.



KISA CHA XII
Siku moja palikuwa palikuwa na tajiri akachinja mbuzi wake. Wakati wa kupika mbuzi huyu, akaja maskini mmoja na chakula chake akakaa upande unakoendea upepo akala chakula chake kwa kutowelea harufu ya mbuzi. Asubuhi Yule maskini akakutana na Yule tajiri akamwambia, "bwana umenifaa sana jana, nimetowelea harufu ya mbuzi wako hata nikashiba."
Tajiri akasema, "kumbe! Ndiyo maana mbuzi wangu hakuwa na ladha kwa sababu tamu yote umechukuwa wewe."
Akaenda akamshitaki kwa Haruni Rashid na yeye alikuwa anapendelea saba matajairi. Basi yule maskini akalazimishwa kutoa rupia thenashara. Maskini akaenda zake akilia, maana fedha hana. Akakutana na Abunuwasi, alipomuuliza akamueleza yote
Abunuwasi akamwambia maskini, "usilie."
Akatwaa Abunuwasi rupia zake thenashara akampa, akamwambia, "nakupa hizi nenda kalipe lakini usitoe mpaka nitakapokuja mimi."
Asubuhi wakakutana wote kwa sultani maskini akasema amekuja kulipa zile fedha lakini akasikitika sana akasema yeye hakula nyama, katowelea harufu tu. Mara akatokea Abunuwasi wakamweleza yalivyokuwa.
Kisha abunuwasi akamwuliza maskini, "unazo rupia thenashara?"
Akajibu, "ninazo."
Abunuwasi akazitwaa zile fedha akazishika, akamwita tajiri atwae fedha yake. Alipotaka kupokea, akamwambia, "ngoja."
Akazitupa chini akamwambia, "haya chukua huo mlio wa hizo rupia. Maana maskini naye hakula nyama amekula harufu tu." tajiri akashangaa kwa visa vya Abunuwasi, akashindwa,
Abunuwasi akamwachia maskini zile rupia akaenda zake
C c. ,
 
Wengi walisoma hizi hadithi zamani. Ngoja tujikumbushe humu. Pia unaweza kusioma ndani ya maktaba app na vingine zaidi ya 60. Tupm au namba 0715278384 ukitaka kuungwa.


HEKAYA ZA ABUNUWASI NA HADITHI ZINGINE

Bombay; London: Macmillan,1942.
pictuspublishers@gmail.com
Pictuss, 2021





YALIYOMO



kisa cha kwanza
Kisa cha pili
Kisa cha tatu
Kisa cha nne
Kisa cha tano
Kisa cha sita
Kisa cha saba
Kisa cha nane
Kisa cha tisa
Kisa cha kumi
Kisa cha kumi na moja
Kisa cha kumi na mbili
Sultani na mvuvi
Sultani na mkwewe
Mvuvi na jin
Kisa cha majuha wawili wanawake
Jogoo na sungura
Kisa cha paka kupenda mekoni
Kisa cha kuku na mwewe
Kisa cha majuha watatu
Simba na sungura
Fikirini na Hemedi
Kisa cha Wadigo
Kisa cha mtu na wanawe
Hadithi ya mtoto wa sultani na wa tajiri
Wezi stadi
Mtego wa panya huingia waliomo na wasiokuwamo
Mganga na mwanafunzi bubu
Kiburi si maungwan
Kisa cha maskini
Hadithi ya bibi mg'indo
Kwanini watu weupe huitwa wazungu
Kisa cha Ali na watoto wa nduguye
Kisa cha sungura na cheche
Wajinga ndiyo waliwao
Mbwa na paka
Njia ya kuvukia mwenye deni
Nyoka na jongoo
Kweli tatu
Ndoto
Mvivu kupita wote ndiye atakayekuwa mfalme
Kisa cha binti Matlai Shems
Muamini Mungu si mtovu
Kasa na kitatange
Hadithi ya chewa
Kisa cha kuku na kanga
Mtoto wa maskini
Mtu aliyesikia lugha za wanyama
Binti Hamadi
Txaessszem xfd s
 
W
Wengi walisoma hizi hadithi zamani. Ngoja tujikumbushe humu. Pia unaweza kusioma ndani ya maktaba app na vingine zaidi ya 60. Tupm au namba 0715278384 ukitaka kuungwa.


HEKAYA ZA ABUNUWASI NA HADITHI ZINGINE

Bombay; London: Macmillan,1942.
pictuspublishers@gmail.com
Pictuss, 2021





YALIYOMO



kisa cha kwanza
Kisa cha pili
Kisa cha tatu
Kisa cha nne
Kisa cha tano
Kisa cha sita
Kisa cha saba
Kisa cha nane
Kisa cha tisa
Kisa cha kumi
Kisa cha kumi na moja
Kisa cha kumi na mbili
Sultani na mvuvi
Sultani na mkwewe
Mvuvi na jin
Kisa cha majuha wawili wanawake
Jogoo na sungura
Kisa cha paka kupenda mekoni
Kisa cha kuku na mwewe
Kisa cha majuha watatu
Simba na sungura
Fikirini na Hemedi
Kisa cha Wadigo
Kisa cha mtu na wanawe
Hadithi ya mtoto wa sultani na wa tajiri
Wezi stadi
Mtego wa panya huingia waliomo na wasiokuwamo
Mganga na mwanafunzi bubu
Kiburi si maungwan
Kisa cha maskini
Hadithi ya bibi mg'indo
Kwanini watu weupe huitwa wazungu
Kisa cha Ali na watoto wa nduguye
Kisa cha sungura na cheche
Wajinga ndiyo waliwao
Mbwa na paka
Njia ya kuvukia mwenye deni
Nyoka na jongoo
Kweli tatu
Ndoto
Mvivu kupita wote ndiye atakayekuwa mfalme
Kisa cha binti Matlai Shems
Muamini Mungu si mtovu
Kasa na kitatange
Hadithi ya chewa
Kisa cha kuku na kanga
Mtoto wa maskini
Mtu aliyesikia lugha za wanyama
Binti Hamadi
Reee*
 
Back
Top Bottom