Hebu tushauriane kidogo

Kumwamini Mungu ni jambo jema sana. alifanya vizuri sana kumwombea mumewe.
 
mke aliambiwa hicho kipengele tu, hajui nani na kwa sababu gani walitaka kufanya hivyo,hakuambiwa mengineyo, na mhusika ndio anajua kwanini hakuweka mambo hadharani, labda mke angeshtuka/changanyikiwa nae aanze kuropoka alichoambiwa na ni kitu kizito kingemletea matatizo makubwa!
 
hii ingekuwa ni best option, ila wakati mwingine muhusika anaweza asiliweke maanani sana sababu yeye ndo anajua in and out ya hilo sakata.
 
maswali ni mengi inawezekana walimtisha wataangamiza familia nzima akaona ajitoe tu muhanga akafe mwenyewe hotelini.

.
 
nakubaliana nawe rafiki.....
kuna sehemu nimeandika hivyo.... ingawa mimi na wewe hatujui kama aliambiwa au hakuambiwa zaidi ya hilo.
Kwa sasa mke ana majonzi sana, ni ngumu sana kuanza kuongea na mtu vitu vya ndani, let alone mwandishi wa habari. alichokifanya kwa sasa ni kusema kuwa alikuwa aware na mauaji ya mumewe..... na nani? kivipi? kwa nini? labda akihojiwa na polisi anaweza kusema.
Namwonea huruma sasa mama mwenzangu. Naamini Mungu atampitisha salama katika hili
 
si kweli mkuu. ..msomi atleast anakuwa na uelewa wa mambo yanavyoenda duniani..naongea hili with experience

Toa yako nikupe yangu, umeshawahi kuona au kupata japo story tu ya familia iliyokutana na haya mambo na wote humo ndani ni wasomi?? Walifanya nini?? Sio hasa swala la kufuatiliwa na usalama wa taifa au polisi, mwanaume menyewe huwa anaishia kulia itakuwa mwanamke?? Hakuna uelewa kwenye kifo ndugu yangu ndiyo maana nakwambia omba Mungu tu haya mambo yasitokee kwenye familia yako
 
mi nadhani hili halina cha usomi wala nini.....
ni jinsi tu wanandoa mlivyo karibu na kuwasiliana katika mambo yenu.
Kuna wengi sana wana mambo mengi na mazito, lakini wanakaa na kutatua pamoja, mambo yanaenda......
 
Na mimi pia nilijiuliza maswali mengi na ya kwako yakiwemo, Nilifikiri hivi! Huenda kitendo chake cha kukaa Hotelini alihitaji faragha, lakini pia ninafikiri huenda kuna watu alitazamia kukutana nao mara baada ya kurudi kutoka Dodoma, inawezekana kuna watu walitaka kupata taarifa hivyo ili akutane nao alihitaji faragha na pia mazingira ambayo yatamuweka mbali na mke na familia.
 
tunajiuliza mengi sana na kujijibu na hakika hatutapata majibu ya kweli ya hayo maswali, sad!
 
ningekuwa mie hapo ingekuwa ndio mahali pa mwisho kupafikiria kusema nao lolote, ningewasikiliza wao wanakuja na lipi la kusema, unafikiri mpaka sasa baadhi ya polisi hawajui ukweli wa hili jambo? mume harudi hao watampa stress tu mama wa watu.
 
kama kauawa..na kama ilikua lazima auawe,unadhani wewe peke yako ungeweza kumlinda?
wauaji wana mengi..wangeweza kumuacha kwa muda ama wangewaua wote wawili..azma ikiwa ni kumuua mmoja,if u get in their way,nawe waweza uawa vilevile
ndo maana mimi nikasema ningemweka chini ya ulinzi watu hawaamini.
yaani hata job ningempeleka na kwenda kumfwata. akiwa job najua yupo na watu wengine......
hapa ambacho ningehakikisha tu ni asiwe peke yake
 
ningekuwa mie hapo ingekuwa ndio mahali pa mwisho kupafikiria kusema nao lolote, ningewasikiliza wao wanakuja na lipi la kusema, unafikiri mpaka sasa baadhi ya polisi hawajui ukweli wa hili jambo? mume harudi hao watampa stress tu mama wa watu.
hilo nalo ni janga jingine...... polisi wetu bwana!
 
kama kauawa..na kama ilikua lazima auawe,unadhani wewe peke yako ungeweza kumlinda?
wauaji wana mengi..wangeweza kumuacha kwa muda ama wangewaua wote wawili..azma ikiwa ni kumuua mmoja,if u get in their way,nawe waweza uawa vilevile
ukinisoma vizuri nimesema kabisa kuwa nisingezuia azma ya wauaji....... labda tu ningepunguza maswali mengine kichwani kwangu in case wauaji wataniacha hai
 
hawa ni polisi wa wapi? Tanzania hii? nilipo hawapatikani hao!
 
ukinisoma vizuri nimesema kabisa kuwa nisingezuia azma ya wauaji....... labda tu ningepunguza maswali mengine kichwani kwangu in case wauaji wataniacha hai

hapo ndio ninapoona labda baba aliamua abaki mwenyewe, akijua madhara ya hiyo ishu, wangekutwa wawili humo ndani kuna uwezekano mkubwa wote wangemalizwa, imagine hapo mama angebaki, familia jamani, ukute watoto bado wadogo!
 
yaani rafiki ni hatari......
lakini hapa tunajiaminisha kuwa baba aliuawa...... je ile stori ya kusema alijiua kama ni kweli, hatuoni kuwepo naye kungeweza kusaidia asijiue? naendelea tu kujiuliza
 
yaani rafiki ni hatari......
lakini hapa tunajiaminisha kuwa baba aliuawa...... je ile stori ya kusema alijiua kama ni kweli, hatuoni kuwepo naye kungeweza kusaidia asijiue? naendelea tu kujiuliza

tutajiuliza mpaka tushae, hebu twende na hiyo ya mke aliyosema mume wake alimwambia kuna watu wanataka kumuua, atleast alisema hayo, hizo mambo za tai ni mbwembwe tu za wauaji.
 
hilo ndo jambo la msingi dada yangu na kwa kweli inasikitisha mno.
yaani mdogo wangu imeniuma sana. kweli mawasiliano ndani ya nyumba ni muhimu sana kuliko chochote.
Ni vizuri wanandoa kujiweka kwenye mazingira ya kutoshindwa kumwambia mwenzako chochote, hata kama ni cha kipuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…