Kuna Binamu yangu alikuwa na binti kipindi hicho binti alikuwa mzuri sana. Akamuacha ile ya ghafla akaanza kutoka na muarabu koko fulani hivi, hadi akasilimu akawa anajifanya muislam.
Jamaa akamchezea chezea sana akamfuga miaka kadhaaa akatemana nae, demu akarudi mjini akawa anaendelea na maisha ya mjini haya ya kudanga hata haeleweki.
Akawa anafanya fanya biashara. Akapata mwanaume akamchukua aishi nae. Jamaa wakaanza tafuta mtoto walitafuta kwa shida sana. Kuna kipindi alibeba ujauzito hadi muda wa kujifungua unafika demu mambo hayasomeki, mtoto alifia tumboni na hakuwa ameumbika vema. Aliendelea lakini hakukuwa na mafanikio. Wakashindwana na mwamba akapiga chini, akaenda kwa mshikaji mwingine yale yale.
Demu alienda kanisani nasikia akaambiwa kuna mwanaume ulishawahi kuwa nae ulimuacha katika hali ya huzuni sana ndie amefunga uzao wako. Demu akaenda kwa waganga hola akijua mambo ya ushirikina, akarudi kanisani mchungaji akamwambia mtafute jamaa kwanza tuzungumze nae. Kuja kumtafuta yule ndugu yangu akachomoa kuonana nae akasema kwanza asimtafute kwa mambo ya kipuuzi.
Yule dada alitafuta ndugu wamuombee msamaha, sasa wakimcheki huyu binamu anawashangaa kuwa ni lini alishamfanya chochote ni yeye ndie aliondoka tena kwa dharau sasa leo anarudi anamletea hizo drama ni za nini kwan ni wapi alimwambia yeye hatazaa.
Binti alitia huruma sana yule. Mwisho jamaa akawa sasa anashangaa tu sasa unataka nifanyaje. Alisota sana yule dada hadi sasa yupo yupo tu anasali kwa mwamposa siku hizi na yupo na 39 kama sio 40. Amevurugwa plus anakisukari.
Huyu binamu yangu huwa anasema "malipo ni hapa hapa duniani" unamuacha mtu anaumia anasota nusu ya kuchanganyikiwa kwaajiri yako then unataka maisha yaendelee tu as if wewe ni last born wa MUNGU.