Hebu naombeni mnipe maoni yenu juu ya hili

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,956
Habarini wadau.

Naombeni ushauri wenu kwenye hili bila kubagua nani atoe huo ushauri.

Najuwa wengi wetu especially wanaume tumepitia ile hali (situation) ambapo kuna mwanamke ulimpenda sana kwa moyo wako wote na yeye alilifahamu hilo.

Ila kwa kujua kuwa amependwa basi akatumia nafasi yake kucheza na hisia zako indirectly kwa maana ya kuwa hakuwa muwazi na hisia zake kwako na kujali jitihada zako za kumuonyesha mapenzi ya dhati.

Unapitia hii hali hadi unafika muda mateso ya kihisia na maumivu yanakushinda nguvu unakubali kuachia mtu unayempenda kimapenzi kupita mwanamke yoyote hapa ulimwenguni. Unamuacha na kuanza safari ya maumivu makali bila yeye na bila kujua hatima ya moyo wako eneo la mapenzi.

Unaamua kuwa sugu na kujikaza muda unakwenda na kichwa chako taratibu kinaanza kukubaliana na ukweli kuwa hautakuwa nae tena na unatakiwa kufungua kurasa mpya.

Unafanikiwa kuruhusu akili yako kuanza mahusiano na watu wapya na hatimae unakutana na binti mwingine tena mdogo kuliko yule aliyekuumiza ila huyu anakuja kivingine, anakupenda na kukujali. Unajitahidi kumpima na kuona hila ndani yake ila hola unakuta hakuna sababu ya kutokumuamini. Unaona si mbaya kukubaliana na ukweli kuwa amekuja mwingine ambaye anaweza kukupa ujasiri wa kupenda tena ingawa si kama mwanzo.

Unalianzisha na safari hii penzi linakuwa zuri na la amani na maisha yanaenda. Hatua zinapigwa na unaanza kuona maisha haya hapa katika sura ya utu uzima na unaweza sasa kujiita mtu mwenye maisha yake.

Ukiwa na utulivu wako na kila kitu kwenye utaratibu unashangaa ujumbe unaingia, ni yule kidudu mtu ambaye sasa humuoni tena special. Anakutafuta kwasababu anazozijua yeye ila moyoni hauna tena imani nae na unashangaa hata kwann akutafute baada ya muda mrefu kupita.

Mbali na maneno yake mbali mbali ya kinafiki na kujaribu kukurubuni anakuja na nia ya kutaka kutazamia kama anaweza kukurejesha mlipoishia na kutaka kutengeneza amani na wewe na kukuomba msamaha kuwa at least umsamehe ili awe na amani ya moyo kuwa aliyekukosea hadi huko aliko anaona baraka zake hazipatikani wala mambo hayamuendei vema eneo la mahusiano umeweza kumsamehe.

Guys hebu mnambie huu wakati au hii moment wewe kama yalikukuta ulifanya nini, ulisema nini, ulitamka nini, ulikuwa katika hali gani?

Haya yamenikuta aiseee hasira ni nyingi hapa, sijaongea kitu nimekaa kimya nisije nikakosea shabaha.
 
Mkuu bado huja move on?
Umepata wapi nguvu ya kuandika uzi mrefu hivi kumuhusu huyo Ex wako?
Ungekua huna mapenzi ama humpendi wala usingekuja kuomba ushauri humu..
Ungemlamba tofali maisha yaendelee....

Mapenzi hayashauriwi ila ni wazi utamrejeea
 
Back
Top Bottom