Hebu leo wakumbuke wahadhiri wa vyuo vikuu waliokufurahisha kwa jinsi ya umahiri wao wakufundisha na walivyokuwa 'fair'

Professor Victor Mlekwa na Marehemu Dr Mtanyata.
Wa kwanza yeye akiingia kufundisha ni kucheka tu mwanzo mwisho anafurahi tu, sasa Dr. Mtanyata yeye ni matusi tu ya nguoni, yeye anaweza kufundisha kama Mara kumi tu semester nzima.

Professor Galabawa, dah Mbaya alikua na nyodo sijapata kuona, kwenye Masters akanipa B+ bahati nzuri External Examiner akanipa A.

Professor Yohana Msanjila yeye ni mzee wa busara tu, alikua Katibu wa CCT chaplaincy UDSM.

Dr. Leornad Chamuriho, kwa kweli alikua kama mzazi, hakua na nyodo, ndio Permanent Secretary sijui wa Wizara gani huko.

Professor Mbunda, babu anachomekea utadhani anachomekea na Mwiko, nadhani yale mashati alikua anachomeka kwanza kwenye pensi ndani, kyupi, suruali then mkanda.
Hili jamaa mwisho hapo limenifurahisha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dr.Towo MD huyu jamaa ni genius ,Prof Malele fundi mmoja wa Pharmacognosy pamoja na Prof Nshimo kisha weka mzungu wa roho Dr Kalala hapa namwongeza Dr Kabati (jamaa ana lifestyle flani nilikuwa nalielewa sana) mwisho namweka bibie Prof Temu mama mmoja hivi ana roho ya peke yake .

Ngoja niweke na mwalimu wangu wa High school wa biology Mama Mbele popote ulipo ulinijengea confidence na uwezo wa kujieleza popote pale nitakapokuwa duniani na Madam Florida kuhakiki facta zangu kabla sijazungumza weka na Madam Florence wewe maza Mungu akubariki

hawa watu wengi ni wastaafu sasa kama sio kurudi kwa Muumba nawashukuru sana popote walipo.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Dr,towo yuko vzuri ktk anatomy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom