Hebu leo wakumbuke wahadhiri wa vyuo vikuu waliokufurahisha kwa jinsi ya umahiri wao wakufundisha na walivyokuwa 'fair'

Jamani, ni hulka ya wanadamu kutotangaza mema ya watu lakini wepesi sana kutangaza mabaya ya watu.

Hivi karibuni kuna madaktari kadhaa walitangazwa na wanafunzi wao kwa ubaya sana! Sijui kama tuhuma walizotangazwa kwazo zilikuwa na ukweli au la!

Huu uzi naomba tufanye kinyume, tuwaseme wakufunzi wetu wa vyuo vikuu kwa majina yao kwa namna walivyo 'committed', 'fair' na mahiri katika kutoa mashule na hata walivyo fair katika kutoa na ku'mark' mitihani yenu!

Kama hukujariwa kufika chuo kikuu ww muweke mwalimu aliyekufurahisha kwa umahiri wake wa kufundisha ktk kiwango cha juu kabisa cha cha elimu ulichofikia!

Tafadhari bandugu, muelezee kidogo kivipi alikufurahisha ili kama atajua basi atiwe moyo na hayo afanyayo! Kumbuka tukitaka kuwananga huwa walimu wetu kwa ubaya huwa hatuishii kutaja majina tu bali tunaelezea kwa kirefu hata kujaza gazeti. Leo eleza hata kwa mstari mmoja tu kumjurisha alivyougusa moyo wako!

Niishie hapo
Taja nawe wako hata kama uliishiia chekechea Mkuu
 
Masenge huwa ni wa CDM.....au alishaunga juhudi?

Ilikuwa mwanajuhudi enzi hizo baada ya kutoka ujeruman na degree zake, akaenda kijijini kwao wajumbe wakamfurumusha, hivi sasa hapendi kabisa kusikia siasa wala kukumbushiwa hayo makitu!
 
Ilikuwa mwanajuhudi enzi hizo baada ya kutoka ujeruman na degree zake, akaenda kijijini kwao wajumbe wakamfurumusha, hivi sasa hapendi kabisa kusikia siasa wala kukumbushiwa hayo makitu!
Bado yupo UDSM?Hajastaafu???
 
Prof. Nicholas N. T. A. Bangu
Alinifundisha Physical Chemistry SUA 1997. Ni hatari sana huyu mtaalamu. Na alishatangulia mbele za haki.
 
Back
Top Bottom