YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,911
- 51,889
Dini zimekuwa zikijitahidi Sana kuwekeza kwenye miundombinu na majengo ya vyuo vikuu Tanzania kwa kupitia wafadhili wao wa ndani nje ya nchi ambao Mara nyingi wakishamaliza huwa hawaendelei kuchangia gharama za uendeshaji.
Dini Kama Waislamu,wakatoliki,walutheri, waanglikana na wasabato na moravian Wana vyuo vikuu vizuri vyenye miundombinu mizuri sana lakini hupata taabu kuajiriwa wahadhiri na maprofesa mahiri kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.
Ushauri wangu kwa serikali badala ya kufungia hivyo vyuo kwa kukosa wahadhiri wenye sifa serikali iwe inatoa wahadhiri na maprofesa na kuwapeleka kwenye hivyo vyuo kwa ajira ya kudumu .Hizo dini zimeshatoa mchango wake kwa kujenga miundo mbinu serikali nayo ichangie nguvu kazi hasa upande wa wahadhiri na maprofesa iajiri na iwapeleke kwenye hivyo vyuo.
Idadi ya wanaomaliza kidato Cha sita ni wengi kuliko uwezo wa vyuo vichache vilivyopo vyenye sifa.Sioni kwa Nini chuo kifungiwe kuendesha kozi kisa eti hakina wahadhiri wenye sifa na serikali ipo Kodi zipo iajiri wahadhiri ipeleke vyuo viendelee kudahili wanachuo.
Dini Zina mchango mkubwa kwa jamii kwa upande wa vyuo vikuu na serikali nayo inatakiwa kuwa na mchango mkubwa kwa jamii kwenye vyuo kwa kutoa wahadhiri na maprofesa