Headache au maumivu ya kichwa

kiukweli wakuu nimekuwa nikiumwa na kichwa sana kiasi cha kufikiri uwenda ni laana.Nimetumia dawa za malaria za kila aina lakini wapi! Dawa zenyewe ni sindano aina ya antmethor,metachelphin,Duo cotexin lakini bado kichwa kinauma balaa.Hivi zaidi ya malaria nini zaidi husababisha maumivu ya kichwa.Dozi ya typhoid ndo nimemaliza.Msaada wakulu.

Nenda hospital ukapime kila kitu.
 
thanx mkuu.macho nimeshapima pale CCBRT Na mawani wakanipa lakini macho yenyewe bado yanauma nimerudi kama mara tatu but still hawajaona cha maana.
 
Kwani hizo dawa za maralia ulikuwa unaandikiwa na daktari au na zenyewe ulikuwa uananunua kutoka maduka ya dawa na kubwia?

Pole mara nyingi maumivu ya kichwa wanasema huwa ni taarifa ya tatizo lililoko kwenye mwili wako, usipende kutumia dawa kabala ya uchunguzi na ushauri wa daktari.

Fanya tena uchunguzi wa afya yako naufate uchauri wa daktari, otherwise kunywa maji na upate mapumziko ya kutosha inaweza pia ikawa ni msongo.
 
kiukweli wakuu nimekuwa nikiumwa na kichwa sana kiasi cha kufikiri uwenda ni laana.Nimetumia dawa za malaria za kila aina lakini wapi! Dawa zenyewe ni sindano aina ya antmethor,metachelphin,Duo cotexin lakini bado kichwa kinauma balaa.Hivi zaidi ya malaria nini zaidi husababisha maumivu ya kichwa.Dozi ya typhoid ndo nimemaliza.Msaada wakulu.

Pole Manny Terry...usiwe na tabia ya kutumia dawa bila ushauri wa tabibu au daktari, hizo dawa zote ulizotumia kwa malaria hapo hakuna daktari atakayekupa dawa hovyo hivyo! Na maduka ya dawa sio substitute ya hospitali!

Maumivu ya kichwa yaweza sababishwa na vitu vingi, sio malaria tu. Dada Bliss ameshakushauri upime macho (ni sababu mojawapo), au check presha 9ni sababu nyingineyo lakini kama umri wako ni wa makamo). Kama ni cha muda mrefu jaribu kuangalia trend yake, ukiweza chora na graph ikinapoanza kama kinaanza taratibu na maumizi yanaongezeka mpaka yanakuwa unbearable. Yaweza kuwa 'Migraine'.
 
Atapka kidogo mafuta ya kitunguu thaumu mahala panapouma, maumivu yataondoka upesi halafu atameza kwa maji kidole kimoja cha kitunguu thaumu kitaondoa kabisa chanzo cha maumivu hayo iwapo yapo tumboni.
 
Wana jf naombeni hata kwa muhtasari kujua kwa nn niumwe kichwa sana?tena kinaacha..
 
Ujaeleweka mkuu! Kuna kichwa kinauma inpofika alasir ,usiku na asubuh.kinauma upand upi mkuu.damu ikiwa ndogo kichwa kitauma au jizoeshe kunywa maji itakusahdia
 
Kafuta, sijui una maana gani unaposema 'tena kinaacha......' Zaidi ya hapo swali bado halijajitosheleza kwasababu maumivu ya kichwa yanategemea ni sehemu gani kwa namna gani, nyakati gani na vitu gani vinakuza au kupooza hali hiyo.

Hata hivyo napenda uelewe kuwa maumivu ya kichwa si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa fulani. Ili kuweka sawa maelezo nina maana ya kuwa kitu kama homa si ugonjwa bali ni dalili ya tatizo flani (symptoms).
Maumivu ya kichwa yanategemea pia mambo mengi ili kupata picha halisi. Yanaweza kuwa ni kipanda uso (migraine), au shinikizo la damu (high blood pressure), yawezakutokana na macho (vision), maradhi kama tumour n.k sababu ni nyingi sana.

Ni hadi hapo utakapotupa maelezo kwa kina tunaweza kukushauri ufanye nini, kama ni ya muda mrefu ni vema ukapata ushauri wa vipimo hospitali
 
Wana jf naombeni hata kwa muhtasari kujua kwa nn niumwe kichwa sana?tena kinaacha..

kUNA KITABU NILIKISOMA ZAMANI HARAKA HARAKA Kimeandikwa na jamaa ambaye alikuwa na maradhi ya kuumwa na kichwa sana kule Urusi (soviet union siku hizo )


Baada ya kumaliza dawa nyingi na kuangaliwa na madaktari wengi kwa muda mrefu hakupata nafuu yoyote.

Mwisho alikutana na daktarii mmoja ambaye baada ya kumuuliza masuali mengi alimshauri anywe kila siku si chini ya lita moja ya maji ya kunywa .

Alifanya hivyo na baada ya wiki moja alipona .

nami nakushauri ungekunywa maji zaidi ya lita moja kila siku na ujiangalie . kwa uwezo wake Mungu nategemea utapona
 
Maji ndiyo dawa wakuu muda mwingine uchovu pia huchangia maumivu ya kichwa nimesikia kuwa hata matumizi ya computer yanachangia kwa kiasi je unapata muda wa kulala vzr
 
mmh! mi sio dktari! ila maelezo yako tu yenyewe yanaumwa! jaribu kuwa muwazi kinaumaje,wapi nk
 
Naunga mkono hoja dawa yake ni maji ajitahidi kunywa maji ya uvuguvugu sio imladi maji hapo ndo tunakosea manaMAJI YA BALIDI YANALETA UKUNGU tumbon hivyo hayafanyi kazi.
1.asubuh ukiamka kabla hujaweka kitu chochote tumia glasi 4 kama unashindwa anza talatibu mpaka zitimie.najua siku za kwanza utapata shida kwenda choon kadri siku zinavyoenda nayo kasi ya kwenda chooni itapungua
2.baada ya kunywa maji kama kaa saa au nusu saa kama unahala kisha unaluhusiwa kufanya shughuli nyingine
 
Wana jf naombeni hata kwa muhtasari kujua kwa nn niumwe kichwa sana?tena kinaacha..

MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA TIBA YA MAJI:

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1=miligramu 31.25.

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.

Pengine umeshageuza kichwa na kujisemea, "Wewe ni kichaa.....hicho ni kiasi kingi sana cha maji". Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, glasi 8 za maji zikigawanywa mara nane kwa siku (glasi 1 = ml 250 au robo lita).

Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:

  • Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75x2.2=aunsi 165.
  • Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2=aunsi 82.5.
  • Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8=aunsi 10.3.
  • Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1=miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3x31.25=miligramu 322.

Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.

Kila mmoja wetu sasa anaweza kutumia uzito wake kwa kutumia fomula hii na kujua ni kiasi gani cha maji anahitaji kwa siku.

Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.

Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokolo hii ni kazi rahisi?.

Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.

Watu wazee na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.

Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.

Kumbuka kuwa, kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.

Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.


  • Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.
  • Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).
  • Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.
  • Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.

Namna bora za kula chumvi:

  • Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.
  • Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.
  • Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.

Kumbuka chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.

Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).

Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.

Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye "multivitamins" zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.

Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.

Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau au ya zabibu au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa.

Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.

Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).

Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.

Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.

Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.

Bilashaka umewahi kusikia msemo, "Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji", hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.

Muda gani unywe maji:

  • Kitu cha kwanza kufanya mara uamkapo tu, ni kunywa glasi 2 za maji (ml 500) kwakuwa umetumia glasi 2 za maji kwa kulala mpaka asubuhi.
  • Kunywa glasi 1 robo saa au glasi 2 nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni, kisha hesabu masaa 2 au 2 na nusu kila baada ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni bila kunywa wala kula chochote, ndipo unywe glasi 1 ya maji.
  • Kunywa glasi 1 ya maji kila uendapo kulala.
  • Muda wowote uamkapo usiku kwenda bafuni, kunywa nusu glasi ya maji na kipande cha chumvi kisha rudi kulala.
  • Muda wowote unapopatwa na kiu kunywa maji.

Kwanini unywe maji robo lita, robo saa kabla ya kula, au nusu lita, nusu saa kabla ya kula?:

Wanyama wote hunywa maji halisi (plain water). Ikiwa
utawachunguza paka na mbwa, mara zote hunywa maji na kusubiri wastani wa nusu saa kabla ya kula. Ratiba inabadilika wanapokuwa wanatibiwa, hapa hunywa na kisha hula papo hapo ama baadaye.

Mfululizo huu ni mhimu ili kubaki na afya bora.

Unapokunywa maji na kusubiri nusu saa kabla ya kula, maji yanaenda tumboni na kuziamsha tezi kutoa kemikali (homoni) kuzifunika kuta za tumbo ili kuzirinda dhidi ya haidrokloriki asidi ambayo huzarishwa wakati chakula kinawekwa mdomoni.

Maji na kemikali hizo kisha huenda kwenye utumbo mdogo ambako kemikali hizi hukaa kusubiri chakula kitakachokuwa kinakuja baadaye. Maji hayo huru, yanauacha utumbo mdogo na kwenda
katika seli zote za mwili na kuzijaza (kuzinyweshea) maji
kama vile unavyonywesha bustani. Baada ya seli kuwa
zimenyeshewa, maji yanayobaki kisha yanasukumwa tena kwenda tumboni ili kunyeshea chakula kilichofika.


Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula, bali zinatoka katika MAJI ambayo yanaiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.

Tunatembea katika haidrojeni.

Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya.

Ikiwa haunywi maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula
chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe.


Kama mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita 'shinikizo la damu'(BP).

Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na 'kichwa kizito' au kichwa kuuma ambacho
kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.


Ikiwa unakunywa alikoholi (pombe) na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).

Watu wanaoishi katika nchi za baridi huweka alikoholi kwenye tenki zao za gesi ili kuvuta maji ndani ya gesi na hivyo kuifanya gesi isigande.

Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida kama vile kufunga choo (constipation).

kufunga choo au kupata choo kigumu sana kunatokea wakati mwili umekopa maji toka katika utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana kunakopelekea taka za mwili kusimama kwenye kuta za utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana (colon). Wakati mambo yako yanapokuwa na umajimaji, huteleza yenyewe chini bila kutumia nguvu yoyote.

Kila tunapopumuwa hewa nje (exhale) tunapoteza maji.

Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumuwa tu kila baada ya masaa 24!!.

kama mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthima) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuwaji.

Mapafu na Moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo kama mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart attack).

Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo kama unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa
maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukakamaa kwa mishipa (cramps).


Ndiyo maana wanasema; kamwe usiende kuogelea
mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa
itakakamaa.


Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng'enyaji
chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng'enyaji wa chakula.

Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng'enywa na vinawezeshwa na maji pekee, kama vile matunda na mboga za majani.

Vinywaji vingine (liquid beverages) kama vile
kahawa, chai, soda na juisi, siyo maji kwa mwili. Hivi ni
vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata radha ya
viongezi (additives) na siyo radha ya maji halisi, na hivyo
tumbo litaitowa haidrokloriki asidi. Mwili utakishughurikia
kinywaji hicho kama chakula.


Utafaidika na baadhi ya maji kama vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine).

Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.

Magonjwa mengine yanayoweza kuepukika kwa kunywa maji kabla ya kula ni pamoja na vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.

Kunywa maji masaa 2 au 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng'enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng'enyaji wa chakula.

kunywa maji ya kawaida katika joto la kawaida.

Magonjwa mengine yanayotibika au kukingika kwa kutumia tiba ya maji ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu(BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, vidonda vya tumbo, utipwatipwa, kuzeeka mapema, na magonjwa mengine mengi.

Tiba hii ni nzuri kwa wote, wagonjwa watapona na wazima watabaki na afya bora na kujirinda dhidi ya maradhi kwa maisha yao yote.

''Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko katika dawa yeyote utakayoandikiwa na muuguzi wako – dr.Batmanghelidj''.


ANGALIZO:

  • Ikiwa hauendi chooni walau mara tatu kwa siku,unapaswa kumwona daktari kabla ya kuanza tiba hii.
  • Figo zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, hii inamaanisha, kiasi cha maji unachokunywa lazima kiwe karibu sawa na unachotoa.
  • Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini mhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
  • Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia nusu ya uzito wako katika aunsi. lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha baada ya kuzoea vinywaji kama kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine.
  • Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza tiba, usiache kunywa maji kwakuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka za sumu zimeanza kuondoka mwilini, baada ya muda utarudi katika hali yako ya kawaida.
  • Tunashauri watu wenye matatizo ya figo, Ini na moyo, kutofuata tiba hii mpaka watakapopata ruhusa ya daktari na muongozo sahihi.
  • Usinywe maji zaidi ya lita 3.78 kwa siku.
  • Usinywe maji kuanzia lita moja kwa pamoja au ukiwa umekaa katika mkao mmoja iwe kusimama au kukaa.

Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.
 
Jf doctor nisaidieni kichwa kinaniuma tangu jumapili hadi leo hii nimetumia dawa lakini tatizo haliish kibaya zaidi mpaka masikio yanaanza kuuma!
 
Kama ukienda hospitali na kugundua huna tatizo toa damu nusu lita(changia benki ya damu) utashangaa hakitauma tena,mimi nilifanya hivyo baada ya kusumbuka sana.

Kwa ufumbuzi wa muda mfupi ukiwa kitandani au kwenye kochi weka miguu ukutani ukitengeneza herufi 'L' kwa dakika 10.
 
Fikicha (sugua) tangawizi kwa maji na weka kwenye paji la uso. pia hii ni dawa kwa maumivu ya jino na maumivu ya sikio kwa maumivu ya sikio dondoshea tone moja kwenye sikio.

Au hii hapa
Utapaka mafuta ya kitunguu thaumu mahala panapouma,maumivu yataondoka upesi halafu Utameza kwa maji kidole kimoja cha kitunguu thaumu kitaondoa kabisa chanzo cha maumivu hayo iwapo Tumboni
 
Hakikisha pia unapata choo laini kwa sababu ingine Maumivu ya kichwa hutokana na ukosefu wa kutopata haja kubwa jaribu uwe unakula Mboga za majani mapapai , matunda, ndizi, na vyakula vilaini ili uweze kupata haja kubwa kiwepesi.

na hii dawa pia tumia itakusaidia Kwa Matatizo ya mfumo wa usagaji wa chakula tumboni kama vile kutosagika chakula,gesi tumboni,kutapika michango mkazo wa ghafla n.k. Tafuna kipande cha Tangawizi kila mara baada ya chakula.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom