Headache au maumivu ya kichwa

Kama zi uchovu wa kazi (unahitaji kupumzika), Kapime malaria, ukiona huna jaribu kunywa maji kwa wingi kama lita unusu kwa saa utaona matokeo yake. May be ni dehydration hyoo mkuu.
 
Kamawewe ni mcha Mungu,unahaki ya kumuuliza juu ya tatizo lako.Msumbue sana kwa maombi,na tafuta wachungaji waombe uone muujiza!utaniambia.
 
Wengi wenu mnazungumza nadharia badala ya kutoa msaada. Kwa haraka hebu pima malaria(bs) pili pima widal test (typhoid) na pima pressure haya ndo maradhi ambayo yanaweza sababisha headache kwa muda mfupi kwa mtu ambaye alikuwa mzima siku tatu zilizopita, kama hivi haitakuwa sababu basi afanye uchunguzi zaidi. Watu wanasema eti akae afanye maombi Mungu anasema jisaidie nami nitakusaidia fanya maombi huku unafanya uchunguzi ili Mungu akuonyeshe nini sababu. Ugua pole
 
Hakikisha pia unapata choo laini kwa sababu ingine Maumivu ya kichwa hutokana na ukosefu wa kutopata haja kubwa jaribu uwe unakula Mboga za majani mapapai , matunda, ndizi, na vyakula vilaini ili uweze kupata haja kubwa kiwepesi. na hii dawa pia tumia itakusaidia Kwa Matatizo ya mfumo wa usagaji wa chakula tumboni kama vile kutosagika chakula,gesi tumboni,kutapika michango mkazo wa ghafla n.k. Tafuna kipande cha Tangawizi kila mara baada ya chakula.[/QUahsante sana nimetumia kile kitunguu swaum nikaona mabadiliko lakini bado nahisi kama ngoma inapigwa ndani ya kichwa
 
Leo nimeshindwa kwenda kazini kabisa naomba ushauri wenu.
Juzi J4 nilikwenda kucheki malaria hospital kutokana na kujisikia kizunguzungu na kichwa kuuma kwa mbele nikakuta ninavijidudu saba nikapewa dawa ya malaria iitwayo Coartem (artemether.lumefantrin). Nimeanza kutumia dawa hiyo siku hiyohiyo kwa kufuata maelekezo yote ya Dr lakini mpaka sasa dalili zilizonifanya nihisi naumwa bado zinaendelea. Naombeni ushauri wenu. asanteni
 
nunua chumvi yenye madini joto kila ukienda dukani. over
 
Kunywa maji mengi haswa muda wa asubuhi ( lita 1 ~ 2 siyo mbaya kwa interval ya dakika 15)ni dawa ya magonjwa mengi sugu na yasiyo sugu.
 
nunua chumvi yenye madini joto kila ukienda dukani. over
kwa siku anaenda dukani zaidi ya mara 3,atakuwa na chumvi kiasi gani ndani?mwambie atumie chumvi yenye madini joto,siyo kununua kila akienda dukani!
 
kuna mambo mengi yanachangia kuumwa na kichwa na kizunguzungu kwa muda mrefu bila kuacha kwanza kuna kuongezeka kwa damu au damu kuwa nzito, kuna kukaa kwa PC muda mrefu(tunatofautiana binadamu kwa uwezo wa kukaa kwa PC),kuna vinywaji kama Redbull, vitamulta ukiwa unatimia mara kwa mara kwa kiasi kikubwa husabisha hiyo kitu hasa red bull unashauriwa unywe ukiwa unahisi uchovu na si zaidi ya mbili.
Hizo ni sababu chache zinazoweza kusababisha kuumwa kwa kichwa pamoja na kizunguzungu kwa muda mrefu hasa ukiwa umekaa chini ukatulia/kupumzika na mara nyingi unakosa usingizi.
 
mmeshaambiwa dawa rasmi ya malaria ni mseto. Hizo kotem za nini? ALU ni nzuri. Labda wadudu hawajaisha
 
Maliza Kutumia hizo dawa kisha uende tena kwa Daktari ili akupime hiyo Malaria kama bado ipo au imekwisha. Kuhusu hayo maradhi yako ya kichwa hebu jaribu hizi Dawa zangu (Dawa ya Maradhi ya kichwa jaribu kutumia hii hapa > Maumivu ya kichwa mgonjwa jipake Mafuta ya Kitunguu Saumu mahala panapouma kichwani,yatoondoka hayo Maumivu ya kichwa upesi. Halafu utakimeza kwa maji kitunguu Saumu punje moja ili uondowe chanzo cha Maumivu iwapo yapo ndani ya Mfuko wa kusaga chakula wa tumbo (Maida).

Na ingine hii hapa Dawa ya Maumivu ya Kichwa
Utachemsha Kitunguu Maji Kilichochambuliwa pamoja na karafuu iliyosagwa na iliokandwa katika Mafuta ya zeituni,ataiacha mpaka ipoe kisha utaisafisha na atachukuwa mafuta ya zeti usugue mahala panapouma na utakunywa kiasi cha kijiko kabla ya kulala. Tiba hii huipa nguvu mishipa.




[h=2]Dawa ya kizunguzungu na hata kuumwa na kichwa[/h]Chukua Haba Sawda kwa kiingereza inaitwa (Nigella Sativa seed) kisha kaanga na utie kwenye kitamba cheupe na uwe unanusa kila mara. Pia inasaidia kwa kuumwa na kichwa.

Kizunguzungu husababishwa na mambo mengi mfano:
1-Upungufu wa damu mwilini
2-kukosa kulala kwa uzuri
3-Mafikra yakizidi
4-Kukosa kula vizuri

Tumia hizo Dawa kisha unipe FeedBack P.h.D. MziziMkavu
 
Mtu anayeumwa kichwa cha utosini kinasababishwa na nini? Na mtu anayekula udongo anakuwa na matatizo gani? Na nini madhara ya udongo anaokula?
 
Kuumwa kichwa kila siku,mtu akiinama anaenda moja kwa moja,na kuna wakati haoni mbali na kupata kizunguzungu,na kichwani kuchoma choma kwa ndani.Akilala kitandani anaona kama anazunguka.
 
Nakushauri hivi, Nenda hospitali kapime Malaria. ukisha pima kama hauna Malaria ndio tumia Dawa zangu hizi hapa .

Maumivu ya kichwa mgonjwa jipake Mafuta ya Kitunguu Saumu mahala panapouma kichwani,yatoondoka hayo Maumivu ya kichwa upesi. Halafu utakimeza kwa maji kitunguu Saumu punje moja ili uondowe chanzo cha Maumivu iwapo yapo ndani ya Mfuko wa kusaga chakula wa tumbo (Maida).

Na ingine hii hapa Dawa ya Maumivu ya Kichwa
Utachemsha Kitunguu Maji Kilichochambuliwa pamoja na karafuu iliyosagwa na iliokandwa katikaMafuta ya zeituni,ataiacha mpaka ipoe kisha utaisafisha na atachukuwa mafuta ya zaituni usugue mahala panapouma na utakunywa kiasi cha kijiko kabla ya kulala. Tiba hii huipa nguvu mishipa.




Dawa ya kizunguzungu na hata kuumwa na kichwa

Chukua Haba Sawda kwa kiingereza inaitwa (Nigella Sativa seed) kisha kaanga na utie kwenye kitamba cheupe na uwe unanusa kila mara. Pia inasaidia kwa kuumwa na kichwa.

Kizunguzungu husababishwa na mambo mengi mfano:
1-Upungufu wa damu mwilini
2-kukosa kulala kwa uzuri
3-Mafikra yakizidi
4-Kukosa kula vizuri

Tumia hizo Dawa kisha unipe FeedBack P.h.D. MziziMkavu
 
  • Thanks
Reactions: rom
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom