Headache au maumivu ya kichwa

Ninachojua ukiugua ugonjwa wa udhaifu wa mishipa ndani ya kichwa (mishipa kuziba, kuvimba, mishipa iponayo baada ya kupasuka nk) inatakiwa ukienda haja kubwa usitumie nguvu nyingi kusukuma choo ama la sivyo mishipa inaweza pasuka na ukapata mshituko wa damu - stroke. Hivyo mgonjwa hushauriwa kula chakula laini na kunywa soft drinks za kutosha ili kupata choo laini hata hivyo hutakiwi kusukuma choo kwa haraka.

Tendo la kujisaidia haja kubwa linaungana moja kwa moja na msukumo wa damu ndani ya mishipa ya damu, ikiwa ni pamoja na mishipa ya damu iliyopo kichwani. Jaribu kuangalia tofauti ya tiba uipatayo kama ukipata choo laini na choo ngumu. Kama choo ngumu inakuletea maumivu zaidi nashauri piga picha ya MRI ya kichwa ili kupima mishipa yako kichwani kama ipo sawa. Kama ni choo laini inakuponya basi nafikiri ni saikoloji na relaxation tu ambapo pressure/stress huondoka kichwani na kuondoa maumivu.

Hata hivyo si choo laini zote ni rahisi kutoa, choo laini km "muwasho" mara nyingi huwa haiishi, ukimaliza haja bado uhahisi unayo, yaani hujamaliza. Na huambata na feeling ya utamu. Hivyo utakua na hamu ya kundelea kuitoa lakini yenyewe inaminya. Hii itakupa maximum relaxation.

Ni kweli haja kubwa ni tiba.

Ni vizuri ukamwona doktari bingwa kwa ajili ya kuchunguza kichwa - mishipa na njia za fahamu, note: mimi si dokta. Najua kidogo tu kuhusu shit.
 
Haya mawili yanahusiana kwasababu moja ya maswali daktari analokuuliza ukimwambia unasumbuliwa na maumivu ya kichwa ni kama unapata haja kubwa na mara ngapi kwa siku au wiki
 
Ni vizuri ukamwona doktari bingwa kwa ajili ya kuchunguza kichwa - mishipa na njia za fahamu, note: mimi si dokta. Najua kidogo tu kuhusu shit.
Tom, good points noted, thanx. But you are funny buddy... :)
 
Last edited by a moderator:
Duhhh!!!...SteveD hii ya leo kali mpaka sina comment!
I hope u get satisfactory answers.
 
Na ukisikia hali ya kukata gogo, ukioga maji ya baridi tu,hali yote hiyo inakwisha, sasa kwenye kupunguza maumivu kwa kukata gogo, kumbuka usioge maji ya baridi, kabla ya kukata gogo.nadhani hii experience watu wengi wanaijua.
 
...Na ukisikia hali ya kukata gogo, ukioga maji ya baridi tu,hali yote hiyo inakwisha,

LOL....doh!!!

yaani kwanini mtu ujipe shida yote hiyo, unajizuia ili unyee humo humo tumboni?
Mimi namshauri Bro SteveD ale mapapai, angalau moja kila siku.
 
Wakuu,

Hii ilinisaidia sana. Nilipopimwa niliambiwa nikapumzike na kunywa maji kwa wingi. Nilipata kupumzika nahisi kama wiki mbili hivi na nikajiwekea ka-utamaduni ka kuwa nakunywa maji lita moja daily. Ilikuwa ngumu lakini niliweza (japo nimeacha nowadays kitu ambacho huenda kinasababisha tatizo la sasa!)

Nashukuru wote mlonipa mawazo kwani ilisaidia sana. Nawashauri wenzangu wanaosumbuliwa na kichwa kufanya jitihada kunywa maji (hata kwa kulazimisha).
 
kwa muda mrefu nimekuwa ni kisumbuliwa na kichwa cha utosini yaani maumivu yake nimekuwa nikiyasikia katikati ya utosi na ikafikia kipindi ni kawa na hisi imani za kishirikina baada ya kutumia madawa mengi bila kupata afueni kwa hiyo naomba msaada wa kufahamishwa ni dawa zipi nitumie ilikupata kinga ya dawa ya kichwa hiki
 
Dawa ya Maradhi ya kichwa jaribu kutumia hii hapa > Maumivu ya kichwa mgonjwa upakae Mafuta ya Kitunguu Saumu mahala panapouma kichwani,yatoondoka hayo Maumivu ya kichwa upesi. Halafu utakimeza kwa maji kitunguu Saumu punje moja ili uondowe chanzo cha Maumivu iwapo yapo ndani ya Mfuko wa kusaga chakula wa tumbo (Maida).

Na ingine hii hapa Dawa ya Maumivu ya Kichwa Utachemsha Kitunguu Maji Kilichochambuliwa pamoja na karafuu iliyosagwa na iliokandwa katika Mafuta ya zeituni,ataiacha mpaka ipoe kisha utaisafisha na atachukuwa mafuta ya zeti usugue mahala panapouma na utakunywa kiasi cha kijiko kabla ya kulala. Tiba hii huipa nguvu mishipa.
 
mzee kimbilia kuokoka, wanataka kukuchukua msukule hapo..kwa wote matakaosoma hapa, ukiona kichwa kinagonga katikati kwenye utosi, ndio wanataka kukuchomoa hapo...watakuweka juu ya dari au nyuma ya mlango muda si mrefu...pole sana.
 
ikutishi, hakika yake hiyo ndiyo dalili mojawapo ya kuchukuliwa msukule, utawekwa kwenye dari ya mtu, au kwenye ofisi uwe unasolve madocument kila siku...kama huamini uliza watu ambao zamani walikuwa wachawi wa kuchukua misukule watu , watakwambia ukweli wake.
 
wadau naomba ushauri wenu. asubuhi ninapo amka huwa nina kuwa na maumivu ya kichwa, ningekuwa mtumiaji wa kilevi labda ningesema ni hangover lakini situmii, nimejaribu kutumia tiba ya glasi 4 za maji mara tu niamkapo lakini pia haijasaidia, malaria wala BP sina ni mwezi sasa tangu nipate tatizo hili. naomba ushauri plz.
 
wadau naomba ushauri wenu. asubuhi ninapo amka huwa nina kuwa na maumivu ya kichwa, ningekuwa mtumiaji wa kilevi labda ningesema ni hangover lakini situmii, nimejaribu kutumia tiba ya glasi 4 za maji mara tu niamkapo lakini pia haijasaidia, malaria wala BP sina ni mwezi sasa tangu nipate tatizo hili. naomba ushauri plz.

Yapo magonjwa mengi sana ambayo yanaweza kusababisha kichwa kuuma asubuhi tu. Kwa hiyo kupima kisukari malaria na Bp havitoshi kabisa. Kwanza tafuta Daktari ambaye atakusikiliza vya kutosha. Na kisha yeye ndio atapendekeza vipimo. Mara nyingi daktari kukuona na kukusikiliza na au kukupima yeye mwenyewe kunapelekea mpaka zaidi ya 80% ya kuutambua ugonjwa. Nina maana usiende kwenye maabara na kuomba wewe mwenye vipimo bali nenda kwa daktari na yeye ndio atajua nini cha kupima.
 
Yapo magonjwa mengi sana ambayo yanaweza kusababisha kichwa kuuma asubuhi tu. Kwa hiyo kupima kisukari malaria na Bp havitoshi kabisa. Kwanza tafuta Daktari ambaye atakusikiliza vya kutosha. Na kisha yeye ndio atapendekeza vipimo. Mara nyingi daktari kukuona na kukusikiliza na au kukupima yeye mwenyewe kunapelekea mpaka zaidi ya 80% ya kuutambua ugonjwa. Nina maana usiende kwenye maabara na kuomba wewe mwenye vipimo bali nenda kwa daktari na yeye ndio atajua nini cha kupima.[/QUOT] mkuu ahsante kwa ushauri nitaufanyia kazi.
 
kiukweli wakuu nimekuwa nikiumwa na kichwa sana kiasi cha kufikiri uwenda ni laana.Nimetumia dawa za malaria za kila aina lakini wapi! Dawa zenyewe ni sindano aina ya antmethor,metachelphin,Duo cotexin lakini bado kichwa kinauma balaa.Hivi zaidi ya malaria nini zaidi husababisha maumivu ya kichwa.Dozi ya typhoid ndo nimemaliza.Msaada wakulu.
 
pole terry,
nakushauri ukapime macho, yaweza kuwa ni ugonjwa wa macho nao husababisha
kichwa kuuma, pia ujaribu kipima na wingi wa damu..
 
Back
Top Bottom