Hayati Magufuli angekuwepo SGR Dar-Moro na Bwawa la Mwl. Nyerere vingekuwa vinafanya kazi

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Nawaza tu, endapo Magufuli angekuwepo leo;

1. Train ya umeme ingekuwa inapiga kazi usiku na mchana na serikali ingianza kuingiza pesa za kutosha.

2. Bwawa la Mwl. Nyerere lingeanza kuzalisha umeme wa kutosha na leo hii stori za kukatika umeme zisingekuwepo.

3. Kalemani angekuwa Waziri wa Nishati na Nape Nnauye bado angekuwa Mbunge wa kawaida.

4. Magufuli angekuwepo January Makamba angeendelea kuwa Mbunge wa kawaida na Paul Makonda angeteuliwa kuwa Mbunge wa kuteuliwa na sasa angekuwa Waziri wa Miundombinu.

5. Magufuli angekuwepo Lissu bado angekuwa Ubelgiji na Wamasai wasingeondolewa Ngorongoro.

6. Magufuli angekuwepo Sabaya kwa sasa angekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma!
 
Ni kweli ndio maana hata stendi kuu ya mabasi ya Magufuli Bus terminal walitaka kumyumbisha mara bei ya ujenzi kupandishwa, mara kuongezwa muda akasema hapana kwa hatua iliyofikia ni lazima ianze akamwalika mpaka rais wa Malawi, Dkt. Chikwera.

1695374998604.png

1695375077786.png

1695375149821.png

1695375208690.png

Ufunguzi wa stendi tarehe: 24th Februari 2021

Zilitengwa jumla ya shilingi Bilioni 136 kwa ajili ya ujenzi wa stendi za kisasa mbalimbali 18 nchini kote
1. Dodoma-imekamilika
2. Dar Es Salaam-Imekamilika
3. Mwanza-Imekamilika
4. Mbeya-?
5. Arusha-?
6. Singida-Imekamilika
7. Tanga-Imekamilika
8. Korogwe-Imekamilika
9. Pwani (Kibaha)-stendi feki na chini ya kiwango hivyo JPM alimwagiza kwenda kuzindia lakini naye akataa kukizindua
 
Nawaza tu, endapo Magufuli angekuwepo leo;

1. Train ya umeme ingekuwa inapiga kazi usiku na mchana na serikali ingianza kuingiza pesa za kutosha.

2. Bwawa la Mwl. Nyerere lingeanza kuzalisha umeme wa kutosha na leo hii stori za kukatika umeme zisingekuwepo.

3. Kalemani angekuwa Waziri wa Nishati na Nape Nnauye bado angekuwa Mbunge wa kawaida.

4. Magufuli angekuwepo January Makamba angeendelea kuwa Mbunge wa kawaida na Paul Makonda angeteuliwa kuwa Mbunge wa kuteuliwa na sasa angekuwa Waziri wa Miundombinu.

5. Magufuli angekuwepo Lissu bado angekuwa Ubelgiji na Wamasai wasingeondolewa Ngorongoro.

6. Magufuli angekuwepo Sabaya kwa sasa angekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma!
Hata mie naamini hivyo
 
Asingeweza mana walipa Kodi walikuwa wamebaki ni machinga tu. Wafanyabiashara na walipa Kodi wakubwa walikuwa wameshasepa. Pesa angeitoa wapi Sasa. Ashukuru mungu tu kumpumzisha mana ingekuwa aibu
uko sahihi ijapokuwa watakuja kukupinga.
 
Asingeweza mana walipa Kodi walikuwa wamebaki ni machinga tu. Wafanyabiashara na walipa Kodi wakubwa walikuwa wameshasepa. Pesa angeitoa wapi Sasa. Ashukuru mungu tu kumpumzisha mana ingekuwa aibu
Hao walipa kodi wakubwa ni akina nani? Serikali zote zilizofanikiwa zimewekeza kwa middle class na lower class ndio maana Bakhressa bado anatafuta 200
 
Asingeweza mana walipa Kodi walikuwa wamebaki ni machinga tu. Wafanyabiashara na walipa Kodi wakubwa walikuwa wameshasepa. Pesa angeitoa wapi Sasa. Ashukuru mungu tu kumpumzisha mana ingekuwa aibu
Sio kweli tulikuwa na shehena ya kutosha ya madini na tulidhibiti Sana wizi
 
Ni kweli ndio maana hata stendi kuu ya mabasi ya Magufuli Bus terminal walitaka kumyumbisha mara bei ya ujenzi kupandishwa, mara kuongezwa muda akasema hapana kwa hatua iliyofikia ni lazima ianze akamwalika mpaka rais wa Malawi, Dkt. Chikwera.
View attachment 2758122
View attachment 2758140
View attachment 2758149
View attachment 2758152
Ufunguzi wa stendi tarehe: 24th Februari 2021

Zilitengwa jumla ya shilingi Bilioni 136 kwa ajili ya ujenzi wa stendi za kisasa mbalimbali 18 nchini kote
1. Dodoma-imekamilika
2. Dar Es Salaam-Imekamilika
3. Mwanza-Imekamilika
4. Mbeya-?
5. Arusha-?
6. Singida-Imekamilika
7. Tanga-Imekamilika
8. Korogwe-Imekamilika
9. Pwani (Kibaha)-stendi feki na chini ya kiwango hivyo JPM alimwagiza kwenda kuzindia lakini naye akataa kukizindua
Uko sawa kabisa
 
Kama tuu Hadi anakufa alishindwa kukamilisha ujenzi wa Kipande Cha Dar-Moro.kwa mujibu wa ratiba sembuse Bwawa ambalo hata hela hakuwa nazo?

Mwisho mtu aliyeshindwa kujenga madarasa na kuwapa Watoto madawati Hadi wanaingia shule kama mafungu ya nyanya unadhani angeweza lipi?
 
Yeye alikua anaamrisha "fanya hivi", "nataka hiki kinyanyike hivi ndani ya muda fulani", lakini sasa hivi utasikia "na hili nalo mkaliangalie" na utendaji ni tofauti hivyo hivyo, Tanzania tunahitaji kiongozi mwenye mrengo wa kidiktekta, jasiri mwenye meno makali ya kulalua yeyote yule, na katili ili tufanikiwe, lakini asiwe wa kutokea kwa wale wanaojiona miungu wa nchi hii kwa sababu wao ndio maadui namba moja wanao paswa kuangamizwa.
 
Ni Mwendawazimu,Juha,zwazwa,Tahira,mwehu,zumbukuku,kichaa,zezeta ndiyo atakaye kupinga ulichoandika mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: Avs
Back
Top Bottom